WILAYA YA HAI YAWEKA MIKAKATI YA KUSAIDIA WENYE HALI MBAYA ZAIDI KATIKA MAAFA

Posted by Arusha by day and by night On 12:53 1 comment

Bibi Aziza Mohammed katika pozi za kawaida kila anaposikia makundi mbalimbali yanatembelea eneo la maafa pamoja na mjukuu wake ambaye ana matatizo ya akili
Bibi Aziz Mohammed katika pozi jingine pamoja na mjukuu wake ndani choo  hapo wakiwa wamefunua mfuko wa saruji
ftt
Nyumba ya familia ya Bibi Aziza Mohammed baada ya kuezuliwa paa

Na Mwandishi Wetu,Hai

Baada ya maafa ya Mvua kubwa na upepo mkali iliyosababisha maafa katika maeneo mengi ya wilaya ya Hai,hali hiyo imeanza kutumia ndivyo sivyo na baadhi ya wananchi wakitegemea kunufaika na misaada mbalimbali.

Hali hiyo imekuwa ikitumiwa na mwanamama anayefahamika kwa jina la Aziza Mohammed ambaye kutokana na taharuki ya upepo na mvua hiyo alilazimika kukimbilia katika choo chake cha kisasa ambacho alijenga kikiwa imara kuliko hata nyumba ya kuishi siku chache kabla ya tukio.

Baada ya tufani hilo kutulia na makundi mbalimbali ya watu wakiwemo viongozi kuanza kutembelea tukio ndipo alipobaini kuwa kukaa kwake chooni kunaweza kumpatia misaada na kuamua kufanya hivyo kwa kila anapopewa taarifa ya ujio wa makundi hayo.

Tofauti na wenzake waliopata maafa ambao waliombewa makazi ama kukaribishwa kwa majirani,lakini  kwa Bibi Aziza ilikuwa ni patashika kukubali kufanya hivyo mpaka pale viongozi wa kata na kijiji pamoja na maofisa wa maendeleo ya jamii walipoenda kumshawishi na kukubali kuhama.

Hata hivyo hakuweza kuridhika baada ya kubaini kuwa atapatiwa msaada wa bati wa kutosheleza vyumba viwili ambavyo vitajengwa kwa kununuliwa tofali za kuchoma na wasamaria wema na hivyo kukubali kurudishwa na baadhi ya waandishi wa habari ili kwenda kupigwa picha kule chooni akichukuliwa kutoka kule alikopewa hifadhi.

Hatua hiyo ilijitokeza baada ya kutoridhika na vyumba viwili na kuwaeleza waandishi wa habari hao kuwa mkoa na wilaya umeshindwa kumsaidia na hivyo anamsubiri Waziri mkuu Mizengo Pinda

"Ni kweli ilikuwa ni patashika kumwamisha huyo mama kutokana na mtazamo wake kwamba akiishi hapo chooni baada ya nyumba yake kuezuliwa paa atapata misaada,lakini viongozi wa kitongoji,kijiji na wa maendeleo ya jamii walimwelimisha baadaye alikubali,lakini cha ajabu,leo waandishi wa habari hao wamemchukuwa na kumrudisha kule chooni ili kupata picha" alisema mmoja ya viongozi wa kitongoji

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ameeleza kuwa serikali wilayani humo kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mboye wameweka mazingira ya dharura ya kusaidia kaya ambazo makazi yao yapo katika hali mbaya yakiwemo ya Bibi Aziza na wengine wengi kwa kutenga fedha za kununua matofali ya kuchoma.

Makunga ameeleza kuwa pamoja na kuwepo kwa msaada wa mabati 200 kutoka kwa Mwenyekiti wa makampuni ya IPP kupitia Bonite Bottlers,lakini ni vigumu kuezeka katika nyumba nyingi kutokana na kukosa uimara ikiwemo aliyekuwa akiishi Bibi Aziza na hivyo wanajipanga kumnunulia tofali imara za kuchoma za vyumba viwili.

Lakini pia alisema kuwa msaada kama huo utapelekwa kwa mzee aliyemtaja kwa jina moja la mzee Omar wa kitongoji cha kijiweni ambaye hana msaada kabisa pamoja na mama mjane wa kijiji cha Kikavu Chini ambaye atapatiwa bati lakini kijiji kimekubali kufanya harambe ya kumsaidia kukamilisha nyumba yake.

Makunga ameeleza kutokana na uchache wa msaada hasa bati bado uchanganuzi unafanyika ili kuweza kuzigawa kwa wale ambao wana hali mbaya zaidi.

Aidha Makunga amefafanua kwamba serikali wilayani humo haijawahi kuwaleta waandishi wa habari kupiga picha jinsi wananchi wanavyoishi bali kama ilivyo kwa majukumu ya waandishi wa habari kufanyakazi bila ya mipaka wamekuwa wakija na wasamaria wema wanaoleta misaada kwa lengo la kutaka kujua hali hali ya maafa hayo

1 comments:

Jamani tuwe serious kuwasaidia hawa walio kumbwa na maafa ya mvua na upepo mkali.Mwenye hata kuanzia 5000 na kuendelea ni msaada pia siyo mpaka uwe na mamilioni ya pesa,Nawapa pole sana kwa wale walio kumbwa na maafa hayo.Mungu awalinde na magonjwa ya mlipuko.

Post a Comment