MKUTANO WA KIMATAIFA WA BIASHARA HARAMU YA WANAYAMAPORI WAENDELEA NCHINI UINGEREZA

Posted by Arusha by day and by night On 05:10 No comments

Rais Jakaya Kikwete akiongoza Kikao cha Ujumbe wa Mawaziri na Wakuu wa Taasisi za Uhifadhi nchini kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wa Kimataifa wa Kuzuia Biashara Haramu ya Wanyamapori jijini London, Uingereza. (Picha na Pascal Shelutete, TANAPA)



Pascal Shelutete, TANAPA

Mkutano wa Kimataifa kuhusu Biashara Haramu ya Wanyamapori (Conference on Illegal Wildlife Trade) unafanyika katika ukumbi wa Lancaster House.
 
Mkutano huu utakaohudhuriwa na jumla ya mataifa 47 na Mashirika 13 ya Kimataifa umeitishwa na Serikali ya Uingereza kwa lengo la kujadiliwa na masuala maalum matatu kuhusiana na biashara haramu ya wanyamapori. 
Masuala maalum yanayojadiliwa pamoja na ni Jinsi ya Kuimarisha Usimamizi wa Sheria (LawEnforcement) na mchango wa mfumo mzima wa sheria za jinai (criminal justice system) katika kukabiliana na biashara hiyo.

Aidha, utajadili Jinsi ya kupunguza hitaji la bidhaa zinazotokana na wanyamapori (demand for wildlife products) na Jinsi ya kusaidia Maendeleo Endelevu kwa Jamii zilizoathiriwa na biashara hiyo haramu.

Mkutano huu utazungumzia wanyama aina ya tembo, faru na tiger.

Wanyama hawa wamechaguliwa kwa kuzingatia jinsi wanavyoshambuliwa zaidi na makundi ya wawindaji haramu kwa lengo la kuu pembe na ngozi zao.


0 comments:

Post a Comment