RC-KILIMANJARO AWAFARIJI WALIOPATWA NA MAAFA WILAYANI HAI

Posted by Arusha by day and by night On 02:05 No comments


Na Richard Mwangulube,Bomang'ombe

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Mhe Leonidas Gama,Mwanzoni mwa wiki hii alitembelea vijiji vitano vya ukanda wa tambarare vilivyokumbwa na maafa ya mvua kubwa na upepo mkali katika wilaya ya Hai kwa lengo la kuwafariji waliokumbwa na maafa hayo.

Mhe Gama aliwafariji wananchi wa vijiji hivyo vya Shirimgungani,Mijongweni,Kwatito,Ngosero na Kikavu Chini.

Mkuu huyo wa mkoa aliwahakikishia wananchi hao kuwa serikali ipo pamoja nao katika kuhakikisha kuwa wanajikimu kimaisha kwa kuwa na mahitaji ya msingi ya chakula ambacho kitawapa nguvu ya kujipanga upya kwa maisha.

Aliuagiza uongozi wa wilaya kuangalia uwezekano wa kuwa na mbegu fupi za mahindi zinazokomaa kwa muda mfupi ili wananchi hao ambao hivi sasa wanajiandaa kwa msimu wa kilimo wawe na uhakika wa kupata mavuno ya kutosha.

Alisema kutokana na mazingira yanayojitokeza ya mvua za sasa kuja kwa kasi lolote linaweza kutokea likiwemo la mvua hizo kukata kwa muda mfupi.

Aidha Mheshimiwa Gama aliutaka uongozi wa wilaya sasa kuwa na programu ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na nyumba imara ili kuepukana na maafa ya kila mwaka pale zinapojitokeza mvua kubwa zinazoambanatana na upepo

WILAYA YA HAI YAWEKA MIKAKATI YA KUSAIDIA WENYE HALI MBAYA ZAIDI KATIKA MAAFA

Posted by Arusha by day and by night On 12:53 1 comment

Bibi Aziza Mohammed katika pozi za kawaida kila anaposikia makundi mbalimbali yanatembelea eneo la maafa pamoja na mjukuu wake ambaye ana matatizo ya akili
Bibi Aziz Mohammed katika pozi jingine pamoja na mjukuu wake ndani choo  hapo wakiwa wamefunua mfuko wa saruji
ftt
Nyumba ya familia ya Bibi Aziza Mohammed baada ya kuezuliwa paa

Na Mwandishi Wetu,Hai

Baada ya maafa ya Mvua kubwa na upepo mkali iliyosababisha maafa katika maeneo mengi ya wilaya ya Hai,hali hiyo imeanza kutumia ndivyo sivyo na baadhi ya wananchi wakitegemea kunufaika na misaada mbalimbali.

Hali hiyo imekuwa ikitumiwa na mwanamama anayefahamika kwa jina la Aziza Mohammed ambaye kutokana na taharuki ya upepo na mvua hiyo alilazimika kukimbilia katika choo chake cha kisasa ambacho alijenga kikiwa imara kuliko hata nyumba ya kuishi siku chache kabla ya tukio.

Baada ya tufani hilo kutulia na makundi mbalimbali ya watu wakiwemo viongozi kuanza kutembelea tukio ndipo alipobaini kuwa kukaa kwake chooni kunaweza kumpatia misaada na kuamua kufanya hivyo kwa kila anapopewa taarifa ya ujio wa makundi hayo.

Tofauti na wenzake waliopata maafa ambao waliombewa makazi ama kukaribishwa kwa majirani,lakini  kwa Bibi Aziza ilikuwa ni patashika kukubali kufanya hivyo mpaka pale viongozi wa kata na kijiji pamoja na maofisa wa maendeleo ya jamii walipoenda kumshawishi na kukubali kuhama.

Hata hivyo hakuweza kuridhika baada ya kubaini kuwa atapatiwa msaada wa bati wa kutosheleza vyumba viwili ambavyo vitajengwa kwa kununuliwa tofali za kuchoma na wasamaria wema na hivyo kukubali kurudishwa na baadhi ya waandishi wa habari ili kwenda kupigwa picha kule chooni akichukuliwa kutoka kule alikopewa hifadhi.

Hatua hiyo ilijitokeza baada ya kutoridhika na vyumba viwili na kuwaeleza waandishi wa habari hao kuwa mkoa na wilaya umeshindwa kumsaidia na hivyo anamsubiri Waziri mkuu Mizengo Pinda

"Ni kweli ilikuwa ni patashika kumwamisha huyo mama kutokana na mtazamo wake kwamba akiishi hapo chooni baada ya nyumba yake kuezuliwa paa atapata misaada,lakini viongozi wa kitongoji,kijiji na wa maendeleo ya jamii walimwelimisha baadaye alikubali,lakini cha ajabu,leo waandishi wa habari hao wamemchukuwa na kumrudisha kule chooni ili kupata picha" alisema mmoja ya viongozi wa kitongoji

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ameeleza kuwa serikali wilayani humo kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mboye wameweka mazingira ya dharura ya kusaidia kaya ambazo makazi yao yapo katika hali mbaya yakiwemo ya Bibi Aziza na wengine wengi kwa kutenga fedha za kununua matofali ya kuchoma.

Makunga ameeleza kuwa pamoja na kuwepo kwa msaada wa mabati 200 kutoka kwa Mwenyekiti wa makampuni ya IPP kupitia Bonite Bottlers,lakini ni vigumu kuezeka katika nyumba nyingi kutokana na kukosa uimara ikiwemo aliyekuwa akiishi Bibi Aziza na hivyo wanajipanga kumnunulia tofali imara za kuchoma za vyumba viwili.

Lakini pia alisema kuwa msaada kama huo utapelekwa kwa mzee aliyemtaja kwa jina moja la mzee Omar wa kitongoji cha kijiweni ambaye hana msaada kabisa pamoja na mama mjane wa kijiji cha Kikavu Chini ambaye atapatiwa bati lakini kijiji kimekubali kufanya harambe ya kumsaidia kukamilisha nyumba yake.

Makunga ameeleza kutokana na uchache wa msaada hasa bati bado uchanganuzi unafanyika ili kuweza kuzigawa kwa wale ambao wana hali mbaya zaidi.

Aidha Makunga amefafanua kwamba serikali wilayani humo haijawahi kuwaleta waandishi wa habari kupiga picha jinsi wananchi wanavyoishi bali kama ilivyo kwa majukumu ya waandishi wa habari kufanyakazi bila ya mipaka wamekuwa wakija na wasamaria wema wanaoleta misaada kwa lengo la kutaka kujua hali hali ya maafa hayo

TAARIFA YA MAAFA YA MVUA NA UPEPO MKALI WILAYANI HAI - FEBRUARI 2014

Posted by Arusha by day and by night On 13:40 No comments

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akipokea Shehena ya Unga wa Sembe kutoka kwa viongozi wa Kiwanda cha vinywaji barid cha Bonite cha mjini Moshi
Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga[Kulia] akipokea msaada wa mabati kutoka kwa viongozi wa kiwanda cha Bonite Bottlers cha mjini Moshi
Viongozi mbalimbali wa wilaya ya Hai wakiwa katika maeneo ya maafa kuwafariji wananchi


Wafanyakazi wa kiwanda cha vinywaji baridi cha Bonite wakishusha shehena ya mabati katika kijiji cha Shirimgungani
Wafanyakazi wa kiwanda cha Bonite wakishusha shehena ya unga wa sembe


Nyumba iliyokumbwa na maafa katika kijiji cha Mijongweni


Nyumba ambayo imefumuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyoandamana na upepo
Moja ya majengo ya shule yaliyoezuliwa paa katika eneo la Modio



TAARIFA YA MAAFA YALIYOTOKANA NA MVUA ZILIZOAMBATANA NA UPEPO MKALI WILAYANI HAI.
Wilaya ya Hai kwa nyakati tofauti tofauti imekumbwa na upepo mkali uliombatana na mvua. Mvua hiyo na upepo huo ulisababisha maafa makubwa ikiwemo kuezua,kubomoa kuta za nyumba na kuharibu mashamba ya mazao mbalimbali. Kata nane katika Wilaya ya Hai ndizo zilizokumbwa na maafa hayo zikijumuisha jumla ya vijiji 25.Tathmini  iliyofanyika imeonesha kuwa madhara  mengi yaliyotokea ni ya kuezuliwa kwa mapaa, kubomolewa kwa kuta za nyumba na kuharibiwa kwa mazao haswa migomba.Hali hii imesababisha baadhi ya kaya kukosa mahali pa kulala na kujihifadhi kwa majirani. Maeneo na madhara yaliyotokea ni kama ilivyooneshwa katika Jedwali Namba I hapa chini:
Jedwali Na, I  

Kata
Kijiji
Tarehe ya
 Maafa
Aina ya madhara yaliyotokea
1.
Machame Kusini
Kwatito
06/02/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,
kubomoka kwa kuta za nyumba.


S/mgungani
06/02/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,
kubomoka kwa kuta za nyumba,
kuharibiwa kwa migomba
2.
Machame Weruweru
Mijongweni
06/02/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba, 
kubomoka kwa kuta za nyumba.
Kuharibiwa kwa mashamba ya mpunga 
na kung’oka kwa miti.


Ngosero
06/02/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,
kubomoka kwa kuta za nyumba.


Kikavuchini
17/01/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,
kubomoka kwa kuta za nyumba
3
Masama Rundugai
Chemka
07/02/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,
kubomoka kwa kuta za nyumba


Rundugai
07/02/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,
kubomoka kwa kuta za nyumba.


Chekimaji
07/02/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,
kubomoka kwa kuta za nyumba.


Kawaya
07/02/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,
kubomoka kwa kuta za nyumba.
4
Masama Kusini
Kwasadala
10/02/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,
kubomoka kwa kuta za nyumba,
kuanguka kwa miti na nguzo za umeme







Kware
10/02/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,
kubomoka kwa kuta za nyumba,
kuanguka kwa miti na kuharibiwa kwa 
mashamba ya migomba


Mungushi
10/02/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,
kubomoka kwa kta za nyumba na
kuanguka kwa kuta za nyumba,kuanguka
 kwa miti na vyakula kuharibika
5
Masama  Mashariki
Roo
10/02/2014

6
Masama Magharibi
Mashua
08/02/2014 mpaka  10/02/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,
baadhi ya nyumba kuangukiwa
na miti na migomba kuangushwa na 
kuharibiwa na upepo.


Lukani
08/02/2014 mpaka  10/02/2014
Migomba kuangushwa na kuharibiwa na 
upepo.


Kyuu
08/02/2014 mpaka  10/02/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,
kuanguka kwa miti na vyakula
kuharibika.Kuharibiwa kwa migomba.


Nkwansira
08/02/2014 mpaka  10/02/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,
baadhi ya nyumba kuangukiwa na miti
 na migomba kuangushwa na kuharibiwa na upepo.


Losaa
08/02/2014 mpaka  10/02/2014
 Migomba kuangushwa na kuharibiwa 
na upepo.
7
Hai Mjini
Lerai
17/01/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,
kung’oka kwa miti ya asili


Kilimambogo
17/01/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba
8
Masama Kati
Mbosho
10/02/2014
Kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,
baadhi ya nyumba kuangukiwa
 na miti na migomba kuangushwa na kuharibiwa na upepo.


Mroma
10/02/2014
Kuanguka kwa miti na kuharibiwa kwa 
mashamba ya migomba


Lemira Kati
10/02/2014
Kuanguka kwa miti na kuharibiwa kwa 
mashamba ya migomba


Isuki
10/02/2014
Kuanguka kwa miti na kuharibiwa kwa 
mashamba ya migomba


Ng’uni
10/02/2014
Kuanguka kwa miti na kuharibiwa kwa 
mashamba ya migomba

Jedwali namba II hapa chini tunaonesha idadi ya kaya, watu walioathirika, na vifaa vya ujenzi vinavyohitajika kuwasaidia wahanga hao na thamani yake


Jedwali Na. II

Kata
Kijiji
Kaya
Idadi ya watu
bati
Chakula
(KG)
/mwezi
Mbao
Tofali




Machame Kusini
Kwatito
43
181
480
2172
824
24,600



Shirimgungani
08
49
86
588
128





Machame Weruweru
Mijongweni
24
146
269
288
237




Ngosero
11
44
62
132
413






Kikavuchini
18
90
280
1180
384





Masama Rundugai
Chemka
3
20
68
432
150
600





Rundugai
3
16
88
193
116
1200





Chekimaji
5
26
11
312
65
300





Kawaya
2
6
11
24
11
180




Masama Kusini
Kwasadala
46
186
711
2232
219
2543










Kware
40
200
527
2400
378






Mungushi
10
58
92
696
115





Masama Mashariki
Mudio
15
52
336
624
505
331





Mbweera
1
3
6
36
12





Masama Magharibi
Mashua
8
27
152
324
206
296





Kyuu
6
30
55
360
24






Nkwansira
4
24
48
288
104





Hai Mjini
Lerai
3
17
32
204
56






Kilimambogo
5
27
48
324
39





Masama Kati
Mbosho
7
28
149
336
373
210



   JUMLA  KUU  YA  MAHITAJI
262
1,230
3,511
12,640
4,359
30,260




Mvua na upepo uliotokea umesababisha  uharibifu majengo ya shule nane za sekondari na msingi katika kata saba za Wilaya yetu.
 
Maafa haya pamoja na kwamba yamesababisha uharibifu mkubwa wa nyumba,mashamba ya mazao mbalimbali na barabara, yalisababisha pia kifo cha mwananchi mmoja mwendesha pikipiki, Ndg Gabriel Mboya (miaka 46) katika kijiji cha Mijongweni tarehe 7/2/2014 baada ya kusombwa  na maji wakati akijaribu kuvuka korongo lilolokuwa likitiririsha maji ya mvua.

Hatua zilizochukuliwa kukabiliana na maafa haya:
Uongozi wa Wilaya umetembelea maenaeo yaliyoathirika na kuwafariji wananchi na kushauri Serikali za vijiji kusaidiana na jamii katika kuwasaidia waathirika wa maafa .

  • Tathimini ya athari za maafa ilianza kufanyika na inaendelea.
  • Uongozi wa Wilaya umewakutanisha wadau mbalimbali na kuwafahamisha hali ilivyo pamoja na kuwaomba misaada kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa maafa.
  • Baadhi ya wadau wameanza kutoa misaada na tarehe 18/02/2014, msaada uliotolewa na Kampuni ya “Bonite Bottlers”  ambao ni unga kilo 2500 na maharagwe kilo 1000 umegawanywa kwa waathirika wa maafa katika kata za Machame Kusini na Machame Weruweru.Msaada wa bati 200 uliotolewa na “Bonite Bottlers”  utagawanya baada ya mhandisi kufanya uhakiki wa mahitaji ya mabati kwa waadhirika.
  • Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Kilimanjaro(KNCU) nayo kupitia mwenyekiti wake Ndugu Menald Swai kilitoa msaada wa shilingi milioni moja
  • Baadhi ya ndugu wa waathirika wa maafa wamejitolea misaada mbalimbali ikiwemo ya chakula na ukarabati wa nyumba zlizoharibiwa.
  • Msaada mwingine  ni wa tarehe 20/02/2014 ambao ni tani nne za unga wa mahindi toka kampuni ya MONOBAN ya jijini Arusha zilizokabidhiwa na Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Ndugu Godfrey Mollel pamoja na Shilingi milioni moja ya kununulia maharage.Msaada huo umeanza kusambazwa  katika kata za Masama Rundugai,Masama Mashariki,Masama Magharibi na Masama Kati.Aidha tarehe 21/2/2014 tutamalizia kutoa msaada katika kata ya Hai Mjini mitaa ya Lerai na Kilimambogo.
Mvua iliyoambatana na upepo mkali na kusababisha maafa imetokea baada ya kipindi kirefu cha ukame na wakati Wilaya ina upungufu wa chakula wastani tani 648 za wanga na tani 65 za protini  katika maeneo ya tambarare.Tathmini ya kina inaendelea kufanyika ilikupata takwimu halisi za hali  ya chakula hapa wilayani.

Aidha ,hali ya chakula kiwilaya  ni ya kuridhisha katika maeneo ya milimani hali inayojidhiirisha kwa bei ya vyakula masokoni ambayo haijapanda sana.Bei ya vyakula muhimu katika masoko yetu ni kama ifuatavyo:
  • Mahindi               Kg.  1               Tshs 400   - 550
  • Maharage             Kg.  1              Tshs  1000 - 1200
  • Mchele                 Kg.  1              Tshs  800  -  1350
  • Ndizi                    Mkungu           Tshs  5000 -10000
Tunapenda kuishukuru serikali kwa kuipati Wilaya  chakula cha msaada kiasi cha tani 201.8 ambazo tani 20.2 ni kwa ajili ya wananchi wa sio na uwezo kabisa na tani 181.6 ni za kuuza kwa Tshs 50 kwa kilo. Chakula  kilipokelewa na kusambazwa kwa wananchi

HITIMISHO
Kwa upande wa Maafa,bado misaada inahitajika zaidi kwa walioathirika ambao hivi sasa wengi wameanza matayarisho ya kilimo kutokana na mvua ambazo zimeanza kunyesha,hivyo tunatoa wito kwa wasamaria wema kujitolea kwa hali na mali kuwasaidia ndugu zenu wa wilaya ya Hai ambao wana mahitaji makubwa wa kibinadamu.

Novatus Makunga
Mkuu wa wilaya
20/2/2014