RAIS KIKWETE AKAMILISHA AHADI YA KUWASAIDIA WAFUGAJI WALIOPATA JANGA LA UKAME

Posted by MK On 12:43 No comments



Na Mwandishi Wetu,Monduli

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekamilisha mradi wa aina yake wa serikali katika histori ya Tanzania wa uwezeshaji wa mifugo kwa kaya za wafugaji waliopoteza mifugo yote kutokana na ukame wa msimu wa 2008/2009 na 2010/2012 katika wilaya tatu za Longido,Monduli na Ngorongoro mkoani Arusha.

Rais Kikwete alifanya uzinduzi huo katika wilaya ya Longido mnamo Februari 19  Mwaka huu na sasa anakamilisha kukamilisha ahadi yake katika wilaya nyingine za Monduli na Ngorongoro.

Mradi huo kwa wa wilaya zote hizo hizo tatu umelenga kutoa kifuta machozi cha ng’ombe 25,000 na mbuzi 14,000 kwa kaya 6127.Mradi huo unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 12.9.

serikali itakuwa itakuwa inagawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za mkoa wa arusha kama kifuta machozi cha kupoteza kiasi cha karibu mifugo 800,000 iliyopotea kutokana na ukame na athari zake.

Katika uzinduzi wa wilaya ya Monduli uliofanyika katika kijiji cha Makuyuni,Rais Kikwete amegawa ng’ombe 500 kwa kundi la kwanza la wananchi ikiwa ni mitamba minne na dume moja la kisasa kwa kaya 16 za mwanzo.
 Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Makuyuni,wakati anazinduampango kwa wilaya ya Monduli wa kugawa ng'ombe kama kifuta machozi cha kupoteza kiasi cha mifugo kutokana na ukame na athari zake.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mpango wa kugawa ng'ombe kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo kutokana na ukame na athari zake.Kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Kushoto kwake ni WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi
 Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi ng'ombe mmoja wa wakaazi wa Monduli walioathririka na ukame na kupoteza mifugo yao yote katika hafla iliyofanyika katika kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe kwa wananchi wa wilaya ya Monduli kama kifuta machozi cha kupoteza kutokana na ukame na athari zake.


Rais Jakaya Kikwete akiwapungia mkono na Wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli kabla ya kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe kwa wananchi wa wilaya ya Monduli waliopoteza mifugo kutokana na ukame na athari zake.(Picha zote kwa hisani ya Ikulu)

0 comments:

Post a Comment