HAI YATENGA MAENEO 430 YA ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2012

Posted by MK On 20:55 No comments

Watanzania na wananchi wa wilaya ya Hai siku imekucha salama kabisa na shughuli za sensa zilianza vizuri kabisa jana usiku kwa makundi maalumu wakiwemo wasafiri na asubuhi hii zimeanza vizuri katika maeneo niliyoyapitia.

Wilaya yetu ya Hai imetenga maeneo ya kuhesabia 430 ambapo kati ya hayo,maeneo ya dodoso fupi yatakuwa 285 na dodoso refu 145.Tuna makarani wa sensa 622,Naomba wananchi wote kuwapa ushirikiano mkubwa

Tumeendelea kuwahimiza wananchi kujipanga kwa kuwa na takwimu sahihi za watu wote waliolala katika kaya zao usiku wa kuamkia leo ambazo ni pamoja na;Jina,umri,hali ya ndoa,kiwango cha elimu,uraia,cheti ama tangazo la kuzaliwa,hali ya ajira,mahali alip;ozaliwa na anapoishi,mahali anaposhinda kwa muda mrefu yaani anapotumia saa nyingi kufanya shughuli zake,hali ya ulemavu,mahali a;ipoishi kwa mwaka 2011 na kama ni mwanamke aeleze idadi ya watoto waliozaliwa wakiwa hai.

Haya ni baadhi tu ya maswali yaliyomo katika dodoso ambapo lile refu lina jumla ya maswali 62 na fupi lina maswali 37.

Mnamo saa mbili asubuhi hii nitakuwa live katika Boma FM kwa hiyo kwa wale wanaoisikiliza naomba mnitumie maswali yanayoitaji ufafanuzi na hata taarifa mbalimbali endapo kuna eneo ambalo mtaona kwamba haliendi sawa ama kunipigia simu moja kwa moja kwa nambari 0713682268

Wenu Novatus Makunga,Mkuu wa wilaya ya Hai

0 comments:

Post a Comment