TAARIFA YA UPANUZI WA SEKONDARI ZA KIDATO CHA TANO NA SITA WILAYANI HAI

Posted by Arusha by day and by night On 02:29 No comments

Moja ya jengo katika sekondari ya Hai Day
Baadhi ya majengo sekondari ya Hai Day
Majengo katika sekondari ya Hai Day
Majengo katika sekondari ya Harambee
Majengo ya sekondari ya Harambee
Majengo katika Sekondari ya Harambee
Jengo la hosteli katika sekondari ya  Lyasika
Moja ya darasa katika sekondari ya Lyasika
Kumekuwepo na mahitaji makubwa katika jamii kuhusiana na taarifa ya mradi wa ujenzi wa shule za sekondari za kidato cha tano na sita katika wilaya ya Hai.Shule hizo za sekondari ni pamoja na Hai Day, Harambee,Lemira, Lyasikika na Nkokashu

Mnano Mwaka 2009 serikali wilayani Hai ilianza mchakato huo wa kuwa na shule za sekondari zenye kidato cha tano na sita
za wananchi.

Hali hiyo ilitokana na ukweli kwamba wilaya ya Hai ina shule za sekondari 45 ambapo kati ya hizo 29 ni za serikali na 16 siyo za serikali.

Kati ya shule 29 za serikali ni shule mbili tu yaani ya Lyamungo kwa wavulana na Machame kwa wasichana ndizo zenye kidato cha tano na sita.

Kikao kilichobuni uanzishaji wa Kamati ya Harambee ya ya kuchangia upanuzi wa shule za sekondari za wananchi Wilayani Haikilichofanyika mnamo Oktoba,2009 ofisini kwa mkuu wa wilaya.

Waliohudhuria
1.Dkt. Norman Sigalla - Mkuu wa wilaya ambaye alikuwa Mwenyekiti
2.Peniel Shali Mjumbe
3.Kotima Sebere - Mjumbe
4.Elimeleck Kimaro -  Mjumbe
5.Amini Uronu - Mjumbe
6.Nicky Munuo - Mjumbe
7.Dr. Jonas SemuMjumbe
8.Dr. Edward Ulicky - Mjumbe 
9.Nicholous MtegaMkurugenzi
     Mtendaji wa wilaya ya Hai
 
SEKRETARIATI
  1. Restina Mwasha  -Afisa Maendeleo
         ya Jamii wa wilaya
  2. Azizi Nasoro    -  Afisa Elimu Ufundi (W) 
  3. Tabu Makanga  -Afisa Elimu Sekondari (W)

KAMATI YA HARAMBEE YA KUCHANGIA UPANUZI WA SHULE ZA SEKONDARI ZA KIDATO CHA TANO NA SITA ZA WANANCHI WILAYANI HAI

 Kikao hicho kiliunda kamati maalumu ya kuandaa harambee iliyokuwa na wajumbe wafuatao;
1. Peniel Shali - Mwenyekiti
2. Kotima Sebere - Makamu Mwenyekiti
3. Nicky Munuo - Mjumbe
4. Dr. James Semu - Mjumbe
5. August Suluo - Mjumbe
6. Elmeleck Kimaro - Mjumbe
7. Swalehe Kombo - Mjumbe
8. Adinani Mbowe - Mjumbe
9. Kunda Sawe - Mjumbe
10. Amini Uronu - Mjumbe
11. Naomi Kabaliki - Mjumbe
12. Sillah Uronu - Mjumbe
13. Shali Raymond(MB) - Mjumbe
14. Ment O. Mbowe

SEKRETARIATI
1. Dr Edward Ulicky
2. Zabdiel Moshi
3. Aziz Nassoro
4. Restina Mwasha
5. Tabu Makange

CHANGAMOTO
Kamati hiyo iliandaa harambe ambapo makundi mbalimbali yalitoa ahadi.
  • Makisio yalikuwa kukusanya shilingi bilioni 1.5 lakini ahadi      
          zilizojitokeza ni shilingi 482,098,500/. 
  • Taarifa ya ukaguzi inayoishia Julai 2012 inaonyesha jumla ya  
         shilingi 286,308,687.50 zilikusanywa.Jumla ya matumizi yote       
         yaliyofanyika ikiwa ni pamoja na gharama za benki ni shilingi
         281,109,775/= na kuwa na salio la shilingi 3,688,912.50 katika
         akaunti ya mfuko wa elimu
  • Majengo yaliyochangiwa na  mfuko hayajakamilika.
        Jengo la Hai Day Sekondary limejengwa kwa shilingi  
        312,002,150/=.Mkandarasi amelipwa shilingi 178,176,587/50            
        bado anadai shilingi 133,825,562/50
  • Bado hakujakuwa na mkakatiwa ufuatiliaji wa watu
        mbalimbali waliotoa ahadi kuanzia mwaka 2009.Hakujakuwa  
        na mpango wa wowote wa kuendeleza shughuli
        za kamati au upanuzi wa shule kwenda kidato cha tano na sita
  • Lengo la mfuko wa maendeleo ya elimu lilikuwa ni ujenzi wa
        madarasa mapya na mabweni na siyo kufanya ukarabati wa  
        majengo.Serikali hutoa fedha za ukarabati wa majengo   
        mashuleni
 
HALI YA UJUMLA WA MRADI
1.LYASIKIKA SEKONDARI
        Shule hii imepokea shilingi 15,000,000/= tu kati ya makisio ya shilingi 30,000,000/= ili kujenga bweni la wanafunzi 48.
        Jengo limefikia hatua ya upanuzi na limekwisha wekewa bati na baadhi ya madirisha yamewekewa fremu za chuma.Sakafu ya jengo haijakamilika bado ni upangaji wa mawe ndani ya msingi
2.HARAMBEE SEKONDARI
     Shule hii imepokea shilingi 15,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 3 na vyoo vya wanafunzi.
         Shule ilipokea kutoka mfuko wa maendeleo ya elimu wilaya,shilingi 15,477,542/= kutoka fedha za miradi ya maendeleo(CDG) na shilingi 10,000,000/= kutoka KNCU.Jengo ni la ghorofa na bado kazi kubwa hazijafanyika.
3.NKOKASHU SEKONDARI
        Shule hii imepokea shilingi 15,000,000/= kati ya shilingi 60,000,000/= za ukarabati wa madarasa mawili ya kidato cha tano.Ukarabati wa madarasa 2,Chumba cha matumizi ya maktaba na ofisi ndogo ya walimu pamoja na kujenga baraza na kubadilisha mabati chakavu eneo la paa la baraza na kubadilisha baadhi ya madirisha kuwa ya chuma kwa baadhi ya madarasa
4.LEMIRA SEKONDARI
      Shule hii imepokea shilingi 25,500,000/= kwa lengo la kumalizia ujenzi wa madarasa 3 na ujenzi wa hostel 2.Kulingana na makisio ya shilingi 75,000,000/=,Mfuko wa maendeleo ya elimu uliahidi kutoa asilimia 75 ya gharama zote kulingana na makisio ya ujenzi.Kazi ya ukamilishaji wa madarasa 3 imekamilika na yanaweza kutumika.

       Kazi zilizofanyika ni kuweka ceilingi board,vioo vya madirisha,ujenzi wa baraza yake na sakafu yake na kupiga rangi madarasa yote.Hostel ya wasichana bado ipo katika hatua za msingi na hakuna kazi inayoendelea.kuna vifaa kama tofali 100 na mchanga lori moja.
       Hosteli ya wavulana imefikia hatua ya lenta na hakuna kazi     
       inayoendelea.
5.HAI DAY SEKONDARI
      Mradi wa ujenzi wa vyumba 8 vya madarasa na matundu 16  ya vyoo jumla ya gharama shilingi 321,000,000.Kazi zote zipo katika hatua ya mwisho na mkandarasi amesalipwa shilingi 178,176,587.50

HITIMISHO
     Taarifa ya kina ya harambee hiyo ya upanuzi wa shule za sekondari kidato cha tano na sita wilayani Hai ilishasambazwa kwa waheshimiwa madiwani. 

    Wilaya imeandaa kikao cha wadau wa elimu ambacho kitafanyika katika wiki ya kwanza ya mwezi Ujao wa Juni ambapo taarifa ya mradi huu yenye kurasa zaidi ya mia moja itajadiliwa kwa kina pamoja na kuwasilisha mkakati wa kukamilisha shule hizo pamoja na maendeleo ya elimu kwa ujumla wake katika wilaya ya Hai 

Imetolewa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Hai,Mei 22,2014

MWISHO
 





























































 

0 comments:

Post a Comment