MTUHUMIWA WA MAUAJI YA KUTISHA WILAYANI HAI ATIWA MBARONI

Posted by Arusha by day and by night On 06:38 1 comment

Majeneza yaliyohifadhi miili ya marehmu kabla ya mazishi
Miili ya marehemu ikiwasili katika kijiji cha Masama Roo kwa ajili ya mazishi
Sehemu ya waombolezaji wakati wa maziko huko kijiji cha Masama Roo
Waumini wakiwaombea dua marehemu
Safari ya kuelekea makaburini kwa ajili ya maziko



                                               Na Richard Mwangulube,Hai

Wananchi wa kijiji cha Roo wilayani Hai kwa kushirikiana na vyombo vya usalama wilayani humo vimefanikiwa kumtia mbaroni Yussuf Shahidi Hassan Njau(32) ambaye anatuhumiwa kuwaua kikatili kwa kuwakata mapanga wazazi wake ambao ni baba marehemu Shahidi Hassan Njau(60) na mama Minae Mohammed Swai

Mtuhumiwa huyo ambaye amekuwa akisakwa tangu Ijumaa iliyopita jioni alikamatwa eneo la jirani na shule ya Msingi Roo baada ya kujificha katika kichaka cha jirani na baadaye kutoka kwa lengo la kwenda kutafuta chakula

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga amesema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Bomang’ombe alikamatwa majira ya saa kumi na mbili za jioni jana.

Makunga amesema kuwa zoezi hilo liikuwa gumu kwani kwa siku mbili nzima jamii hasa kina mama waliogopa kwenda katika shughuli zao hasa mashambani kwa hofu na kufikia kupanga maandamano kuelekea ofisi ya wilaya.

Mkuu huyo wa wilaya ameushukuru uongozi wa Kijiji cha Roo chini ya uongozi wa mwenyekiti wa kijiji hicho Halfan Swai kwa kuwasimamia vyema askari mgambo na kikosi cha ulinzi shirikishi katika msako wa mtuhumiwa huyo.

Amesema kuwa bila umakini mkubwa,mtuhumiwa huyo angeishia kuuwawa na umati mkubwa wa wananchi wenye hasira ambao hawakuwa tayari kumwona mtuhumiwa huyo akiishi na jitihada kubwa zilifanyika kuhakikisha hilo halitokei baada ya kukamawa.

Mtuhumiwa huyo ijumaa iliyopita aliwauawa wazazi wake kwa kuwacharanga kwa mapanga  kisha kuchoma makazi yao kuchomwa  moto kabla ya moto huo kuja kuzimwa na majirani

Alisema mauaji hayo yalitokea juzi saa 12:30 jioni katika Kijiji cha Roo kilichoko Masama wilayani  Hai na habari zilizopatikana kijijini hapo na kuthibitishwa na Kamanda Boaz, zilieleza kuwa Shaibu alifikia  uamuzi huo baada ya kugombana na wazazi wake.

Awali baada ya tukio hilo Mwenyekiti wa  Kijiji Cha Roo Halfan Swai  alisema walibaini kuwapo ugomvi baada ya kukuta baadhi ya majirani  wakihangaika kuzima moto huku maiti za watu hao zikiwa zimelala chini zikivuja damu.

“Tulipofika  nyumbani kwa mzee Njau, tuliwakuta wananchi wakizima moto huku miili  ya  Minai na  Njau iliyokatwa kwa mapanga ikiwa imelazwa chini Njau alikuwa amepigwa panga kichwani  na ubongo ukiwa umesambaa chini. Tulihakikisha tumeuzima moto huo  kisha tuliipeleka  miili hiyo  hospitalini……., ”alisema Swai.

Kwa upande wake  Mkuu wa Wilaya ya Hai, Novatus Makunga, aliwataka wananchi kujifunza kuhusiana na tukio hilo huku akihimiza umma kutoendekeza tabia za kujichukulia sheria mkononi na badala yake watoe ushirikiano kwa  polisi kuhakikisha mtuhumiwa huyo anapatikana na kuburuzwa mahakamaniMarehemu hao walizikwa Jumamosi iliyopita katika kijiji cha Masama Roo.

1 comments:

wadamu tumekuwa wakatili kuliko wanyama, vitabu vya dini vinatuasa tuwaheshimu wazazi maana bila wao tusingalikuwako hapa duniani na tukkapewa ahadi na mwenyenzi Mungu ya kuwa tukitimiza hayo tutakuwa na maisha ya kheri na fanaka hapa dunian Eeeeenh nchi yangu na watu wangu watanzania ni nani aliyewaloga

Post a Comment