HAI YAANZA KUTOA CHANJO YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Posted by Arusha by day and by night On 01:52 No comments

Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akizindua zoezi la utoaji wa chanjo kitaifa katika kata ya Mabogini,mjini Moshi
Uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa uliofanyika mjini Moshi Mwishoni mwa mwezi uliopita
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akitoa chanjo huko mjini Moshi
Mama Salma Kikwete akitoa chanjo kwa moja ya watoto mjini Moshi
Baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro waliohudhuria uzinduzi wa wiki ya chanjo mjini Moshi

Viongozi katika meza kuu siku ya uzinduzi wa chanjo huko Moshi




Na Richard Mwangulube,Hai

Wilaya ya Hai imeanza zoezi la utoaji wa chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi ambalo  kwa ajili ya majaribio ya kupata jinsi ya kutekeleza mpango wa kutoa chanjo hiyo nchini kote.

Mwenyekiti wa  kamati ya afya ya msingi ya wilaya ya wilaya hiyo,Novatus Makunga akifungua kikao cha kamati hiyo ameeleza kuwa chanjo hiyo inatolewa katika wilaya zote sita ikiwemo wilaya yake ambapo maandalizi yote yalishakamilishwa.

Makunga ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Hai ameeleza kuwa zoezi hilo linatoa chanjo kwa watoto wa kike wa umri wa miaka kati ya tisa na kumi na tatu ambao ameeleza kuwa kitaalamu ndiyo umri ambayo hutoaji wa chanjo hiyo unaweza kuwa na faida kubwa.

Amefafanua kwamba kutokana na asilimia kubwa ya maamukizi ya saratani hiyo hutokana na tendo la ndoa na kwa kawaida chanjo hutolewa kabla ya muhusika hajaambukizwa ugonjwa husika hivyo kwa wasichana wenye umri huwa wanakuwa hawajaanza tendo la kujamiana.

Makunga ameeleza kwa kuwa wilaya hiyo himo katika miongoni mwa wilaya ambazo sasa zitahusika katika kutengeneza mpango utakaotumika kwa nchi nzima chanjo hiyo itaenesdhwa kwa makundi mawili ya watto hao wa kike ambapo kundi moja ni lile la walioko shuleni na kundi la pili ni kwa watoto walioko mitaani.

Amefafanua kuwa kwa watoto walioko shuleni mfumo liowekwa ili kwa na uhakika zaidi ni kwa watoto wa darasa la nne tu na kwa wale ambao wapo mitaani ambao kwa bahati mbaya wamekosa kwenda shule watakaopewa chanjo ni wa miaka tisa tu.

Makunga ameeleza kuwa chanjo hiyo itatolewa mara mbili ambapo chanjo ya pili itakuwa baada ya miezi sita na hivyo kuwapa uhakika watoto hao kutokuwa katika hatari ya kuambukizwa saratani ya shingo ya uzazi ambayo matokea ya saratani hiyo uwapata wanawake baada ya kati ya miaka kumi mpaka ishirini.

Ameeleza kuwa jumla ya shule za serikali na binafsi zipatazo 123 za msingi ambapo pamoja na watoto wa mitaani ambapo makadiri ya watoto wataochanjwa watakuwa kati ya 2,500 mpaka 3,000.

Amesema kuwa tayari katika maandalizi ya awali wilaya ilishawashirikisha maofisa maendeleo ya jamii katika vijiji na wakuu wa shule kwa ajili ya kutengeneza rejesta pamoja na kuwaelimisha watu mbalimbali wenye ushawishi katika jamii.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa wito kwa jamii nzima kuhamasisha kufanyika kwa chanjo hiyo kutokana na kansa hiyo kwa kati ya kansa ambayo imekuwa ikisababisha vifo vya wanawake wengi  nchini na imekuwa ni vigumu kutibika inapofikia ama kubainika katika awamu ya juu zaidi.

Amesema kuwa familia zenye uwezo hutumia fedha nyingi kuwapeleka watoto wao wa kike kuchanja chanjo hiyo katika mahospitali binafsi ambayo ni ghali na hivyo ksisitiza kwa jamii kuipa umuhimu mkubwa kutokana na serikali kuitoa bure kwa lengo la kuokoa maisha ya watu wake

Awali mganga mkuu wa wilaya ya Hai,Dk Paul Chaote ameeleza kuwa katika Tanzania kila mwaka wanawake wapatao 670 wanapata tatizo ya saratini hiyo ikiwa ni ya pili baada ya saratani ya matiti

Amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi nne ambazo zinaongoza kwa saratani hiyo ya shingo ya kizazi

Wilaya ya Hai imeshika nafasi ya nne kitaifa kwa kutoa huduma kikamilifu na hivyo kuzawadiwa ngao na fedha shilingi milioni tano katika uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa kulikofanywa na mke wa rais,Mama Salma Kikwete mwishoni mwa mwezi uliopita katika eneo la Mabogini mjini Moshi.

Wilaya iliyoongoza ni Mufindi ikifuatiwa na Handeni na Kondoa

0 comments:

Post a Comment