Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akipata ufafanuzi wa Ujenzi wa Barabara ya Machame kutoka kwa Kaimu Meneja wa Tanroads mkoani Kilimanjaro,Mhandisi Reginald Massawe(Kushoto) |
Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga na maofisa wa Tanroads wakishuhudia mifugo ikisagwa katika barabara ya Machame |
Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akitoa maelekezo ya barabara ya Machame,kulia ni mmoja ya wataalamu wa ujenzi katika wilaya ya Hai,Mhandisi Peace |
Mkuu wa wilaya ya Hai akiangalia moja ya eneo la barabara ya Machame ambalo lina kasoro katika ukarabati wake huku maofisa wa Tanroads mkoa wa Kilimanjaro wakitoa maelezo |
Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akipata maelezo kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya Mhandishi mshauri wa barabara ya Kwasadala hadi Masama,Crown Tech Consult Limited
Na Richard Mwangulube,Bomang’ombe
Mkuu wa wilaya Hai,Novatus
Makunga amewaagiza viongozi wa vijijji na vitongoji vinavyopitiwa na barabara
ya Machine Tools hadi Machame kuanza kutekeleza sheria ya barabara katika kudhibiti uswagaji wa mifugo hususani
ng’ombe katika barabara hiyo .
Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo baada ya kukagua
barabara hiyo ambayo ilikarabatiwa kwa kipande cha kilometa 7.9 na Wakala wa
barabara nchini,Tanroads na baadaye alikagua barabara nyingine ya Kwasadala
hadi Masama inayoendelea kujengwa na wakala huyo.
Akizungumza na viongozi mbalimbali wa vijiji vya kata ya
Machame Kaskazini ambapo barabara hiyo imepita,aliwaeleza kuwa ni vyema sasa wakaanza kusimamia sheria inayozuia
mifugo kutembezwa barabarani badala ya wao kama viongozi kuanza kulalamika.
Viongozi hao awali walimweleza mkuu huyo wa wilaya kwamba kwa
asili eneo la Machame siyo la ufugaji wa mifugo inayochungwa bali ufugaji wao
ni ule wa ndani,hata hivyo limezuka wimbi la wamiliki wa Mabucha kwenda
minadani na kununua ng’ombe ambao katika kuwasafirisha uamua kuwachunga
barabarani na hivyo kuchangia uharibifu.
Makunga amemwagiza Kaimu meneja wa wakala wa Barabara,Tanroads
mkoani Kilimanjaro Mhandisi Reginald Massawe kuandaa semina ya uelewa kwa
viongozi wa vjiji na vitongoji itakayolenga kuwaelimisha sheria ya hifadhi ya
barabara pamoja na mpango wa kuisimamia na kuwapa nakala ya sheria hiyo ili
waanze mara moja kuitekeleza.
Amewataka viongozi hao kutoa notisi kwa wamiliki wa mabucha
kuhusiana na kuanza utekelezaji wa sheria hiyo kwa lengo la kuwafahamisha
kwamba kuanzia sasa watalazimika kusafirisha mifugo yao kwa njia ya barabara na
ni marufuku kuswaga mifugo barabarani.
Kadhalika amewataka kushirikiana na wakala wa barabara kuwaondoa
wote waliovamia maeneo ya hifadhi za barabara wakiwemo wanaondesha kilimo cha
majani ya mifugo na wafanyabiashara wanaohifadhi mchanga wa ujenzi kwa kuwapa
notisi kama sheria inavyotaka mapema iwezekanavyo.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa wilaya amemtaka Mhandisi
Massawe kutuma wataalamu watakaoianisha mapungufu mbalimbali ambayo yamejitokza
katika ukarabati huo wa baabara yakiwemo ya baadhi ya maeneo kutokuwa na makalvati,mikondo
ya maji kutokuelekezwa kwa usahihi,baadhi ya maeneo lami kuanza kumeguka pamoja
na mahitaji ya kuweka alama za kuvuka
kwa waenda kwa miguu jirani ni makanisa,misikiti na shule.
Awali mhandsi Massawe ameeleza wakala wa barabara imetumia
kiasi cha shilingi milioni 1,005 kukarabati sehemu ya kilometa 7.95 ya barabara
hiyo yenye urefu wa kilometa 14.98.Amesema kazi zilzofanyika ni pamoja na
kuondoa tabaka la lami,kuvuruga msingi wa awali,kujenga msingi mpya nakuweka
tabaka jipya la lami nyepesi kwa upana wa barabara wa mita 9.0.
Amesema kuwa dosari mbalimbali zilzojitokeza ambazo
walizibaini katika ziara hiyo ya mkuu wa wilaya ambazo znahtaji fedha nyingi zitafanyiwa
kazi katika awamu ijayo ya kukarabati barabara hiyo ambayo itaingizwa katika
mwaka ujao wa fedha ambao unaanza mwezi Julai huku ndogo ndogo wakianza
kuzirekebisha mara moja.
Amesema kuwa katika mwaka ujao wa fedha kiasi cha shilingi
milioni 800 zimetengwa kwa kazi ya kupanua mabega ya barabara kila upande na
kujenga tabaka la lami nyepesi sehemu ya barabara yenye urefu wa kilometa 5.
Akiwa katika barabara
ya Kwasadala hadi Masama mkuu huyo wa wilaya amemtaka mkandarasi kushirikiana
na viongozi wa eneo hilo katika kuhakikisha ujenzi wa makalvati ya kupitisha
maji unakwenda kwa usahihi kwa lengo la kuepuesha madhara hasa nyakati za
masika.
Aidha amemkatmkandarasi hiyo kutatua tatizo la baadhi ya
maeneo kushindwa kupiika kutokana mvua znazonyesha sasa kwa kumwaga vifusi hasa
katika maeneo yenye miteremko mikali.
Mkandarasi mpya wa barabara hiyo kampuni ya Hari Singh and
Sons Limited ameahidi kurekebisha sehemu zote korofi katika kipindi hiki cha
mvua wakati kazi ya ujenzi huo ambayo imefikia asilimi tano ikiwa inaendelea.
Mkandarasi huyo alianza kazi mwezi Januari mwaka huu baada ya
kuvunjwa kwa mkataba wa mkandarasi wa awali katika barabara hiyo ambayo ni
ahadi ya rais Jakaya Kikwete.
Utekelezaji wa mradi huo upo katika hatua za awali
ambapo ujenzi wa njia yamchepuko ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa daraja la mto
Namwi pamoja na ujenzi wa tabaka la kwanza la mawe yaliyosagwa unaendelea
katika eneo lenye urefu wa kilometa 2
Ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa Kilometa 12.5 unatarajiwa
kukamilika mwezi Januari Mwakani.
0 comments:
Post a Comment