NAFASI ZA AJIRA 15 KATIKA JIJI LA ARUSHA

Posted by bomang'ombe On 02:31 No comments

HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

1. Afisa usalama -  nafasi 2

Sifa za mwombaji
- Awe amehitimu elimu ya kidato cha nne au sita
- Awe mstaafu wa Jeshi la Polisi,Jeshi la Wananchi wa Tanzania au Jeshi la kujenga Taifa
- Mwenye uzoefu wa kutumia silaha za moto
- Umri usiozidi miaka 40 isipokuwa kwa wastaafu jeshi la polisi,JWTZ na awe amepitia mafuzo ya masuala ya usalama(security)
-Awe hajawahi kushtakiwa kwa kosa lolote la jinai ndani na nje ya kazi alizowahi kufanya
- Awe na vyeti sahihi vya elimu yake
- Awe na vyeti au barua ya kustawfu kwake na asiwe alifukuzwa kazi
- Aeleze ana mke au mume na watoto wangapi,wako wapi na wanafanya nini
-Awe raia wa Tanzania

2. Afisa mtendaji wa kata II - nafasi 12

Sifa za mwombaji
 -Awe na shahada ya moja ya fani zifuatazo; Uongozi wa utumishi,Rasilimali watu,Sosholojia,Sheria
na fani nyingine zinazofanana na hizo.
- Awe na cheti cha fomu IV na VI
- Wasifu wake (CV)
- Barua ya udhamini
- Passport size tatu

3. Afisa zmanunuzi msaidizi - Nafasi 3

Sifa za mwombaji
-Awe na stashahada ya manunuzi au ugavi
- Ama cheti cha kidato cha IV au VI
- Awe na passport size tatu
- Awe na barua ya udhamini

4 . Mtunza Bohari nafasi - 1

Sifa za mwombaji
- Awe na stashahada ya ugavi
- Ama cheti cha kidato cha IV na kidato cha VI
- Awe na passport size 3
- Awe na barua ya udhamini

Jinsi ya kuomba
Waombaji wote waliokidhi vigezo watume maombi yao kwa ;
Mkurugenzi wa Jiji
S.L.P 3013
Arusha

Mwisho wa kuomba ni siku kumi na nne baada ya kutolewa kwa tangazo hili.Tangazo hili limetolewa katika gazeti la Mwananchi la tarehe 25 Agosti 2014


0 comments:

Post a Comment