MWENGE KUINGIA WILAYANI HAI KESHO

Posted by Arusha by day and by night On 07:47 No comments

Siku Mwenge ulipopokelewa mkoani Kilimanjaro,Jumapili iliyopita Agosti 17,2014 katika kijiji cha Mabilioni wilayani Same na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Chiku Galawa
Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Kilimanjaro wakisubiri mwenge katika kijiji cha Mabilioni wilayani Same,Kutoka kulia ni Shaibu Ndemanga(DC Mwanga),Novatus Makunga(DC Hai),Dr Charles Mlingwa(DC Siha),Elinas Pallangyo(DC Romboa na Dr Faisal Issa(RAS Kilimanjaro)

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama(kushoto),akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Mwanga,Shaibu Ndemanga na Novatus Makunga wa Hai
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akimakabidhi mwenge wa uhuru,mkuu wa wilaya ya Same,Herman Kapufi kwa ajili ya kukimbizwa wilayani Same mara tu baada ya kuingia mkoani Kilimanjaro
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Chiku Galawa akielekea katika eneo la makabidhiano tayari kuukabidhi mwenge huo kwa mkoa wa Kilimanjaro


Na Richard Mwangulube,Hai

Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa na kukimbizwa wilayani Hai,kesho Agosti 22,2014 ambapo utafungua,kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi sita yenye thamani ya jumla ya shilingi 674,675,231.38

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ameeleza kuwa Mwenge huo utapokelewa katika kijiji cha Shirinjoro maarufu kama Maili sita majira ya saa tatu asubuhi ukitokea katika wilayani moshi katika Manispaa ya Moshi

Makunga ameeleza miradi hiyo itakayopitiwa na mwenge wa uhuru imewezeshwa kwa fedha za Serikali kuu,Halmashauri ya wilaya,Wahisani pamoja na nguvu za wananchi.

Ameeleza kuwa baada ya kupokelewa utazindua rasmi bwalo la kulia chakula katika shule ya msingi ya Lambo Estates ambalo limejengwa kwa gharama ya shilingi 56,863,100.Bwalo hilo liliwekewa jiwe la msingi na mwenge mwaka juzi.

Mwenge huo baadaye utaweka jiwe la msingi katika ujenzi mpya wa madarasa matatu ya shule ya msingi ya Modio ambayo ilivunjwa yote kutokana na kupigwa na tetemeko la ardhi ya kusababisha majengo yote kuwa na nyufa.Madarasa hayo yatagharimu shilingi 64,334,800.

Mradi mwengine utakaowekewa jiwe la msingi ni wa Kituo cha Ukusanyaji na uhifadhi wa maziwa cha Uduru ambacho kinajengwa kwa gharama ya shilingi  82,730,046.Baada ya hapo mwenge huo utafungua maabara ya kisasa katika shule ya Sekondari Udoro iliyojengwa kwa gharama ya shilingi 85,378,900.

Makunga ameeleza kuwa mwenge huo pia ufungua huduma za X-Ray katika hospitali ya serikali ya wilaya ya Hai iliyojengwa kwa gharama ya shilingi 185,415,000 na baadaye kuzindua kituo kikuu cha mabasi cha mji wa Hai kilichogharimu shilingi 199,955,367/38

Mkuu huyo wa wilaya ametoa wito kwa wananchi kutjitokeza kwa wiki katika shughuli ya mwenge wilayani humo ambapo amefafanua kwamba kwa mwaka huu umebeba ujumbe usemao "Katiba ni Sheria kuu ya Nchi," na kuongeza kuwa ujumbe huo una kauli mbiu "Jitokeze kupiga kura ya maoni tupate katiba mpya,"

Ameeleza mbali ya ujumbe huo kadhalika umeambatana na kauli mbiu za kataa UKIMWI,Malaria, Rushwa na Dawa za Kulevya.

Makunga ameeleza kuwa maandalizi yote kwa ajili ya mapokezi na hatimaye kukimbizawa kwa mwenge wilayani Hai yamekamilika ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha viongozi wa kada zote na wananchi kwa ujumla wao.

0 comments:

Post a Comment