Naibu waziri wa maji Mheshimiwa Amos Makalla na Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa John Mnyika katika patashika ya kila mmoja kutetea kundi ambalo lilimzomea mwenzake
Mfuasi wa CCM akiwa na bango la kumshutumu Mbunge wa Jimbo hilo, John Mnyika. |
Mfuasi wa CHADEMA akifikisha ujumbe wa njia ya bango |
Polisi akilinda usalama mbele ya mashabiki wa CCM na Chadema |
Wafuasi wanawake wa CCM na Chadema wakichimbia mkwara |
Makalla akipata maelezo kutoka kwa mkandarasi kuhusu ujenzi wa Tanki jipya la maji eneo la Kibamba, Dares Salaam,wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji Dares Salaam na Pwani. |
Mkazi wa Kibamba, Chrisant Kibogoyo akiuliza swalikatika mkutanouliofanyika Kata ya Kibamba |
Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Kibwegere, Hellen Mshana akiuliza swali kwa waziri kwambanilini maji yatasambazwa katika shule hiyo na zinginezo |
Askari akimuondoa mfuasi wa Chadema aliyekuwa akilazimisha kumuuliza swali Waziri Makalla katika mkutano huo |
Wafuasi wa CCM na Chadema wakishindana kupeperusha bendera za vyama vyao wakiwakwenye magari eneo la Kibamba. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG |
Dar es Salaam,Jumatano Julai 16,2015.
Ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla jana iliingia dosari baada ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge na Diwani wa Kata ya Kimara, Paschal Manota (Chadema), kurushiana matusi mbele ya wananchi na nusura wakunjane mashati.
Ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla jana iliingia dosari baada ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge na Diwani wa Kata ya Kimara, Paschal Manota (Chadema), kurushiana matusi mbele ya wananchi na nusura wakunjane mashati.
Tukio hilo lilitokea jana wakati wa mkutano wa
wananchi wa Kata ya Saranga, Kimara uliofanyika Uwanja wa Shule ya
Sekondari ya Mavurunza ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya Makalla katika
ukaguzi wa miradi maji ya Dawasco.
Vurugu hizo zilitokea baada ya Makalla kuagiza
polisi kuwakamata wafuasi wa Chadema kwa madai kuwa walitaka kuvuruga
mkutano huo. Baada ya Makalla kutoa agizo hilo, Diwani Manota na Mbunge
wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika walisimama na kupinga uamuzi huo na
walirushiana maneno na Mwenyekiti Madenge aliyesema wawili hao waache
upumbavu.
“Unatetea nini? Acha upumbavu... Hatuwezi
kuendesha mkutano na watu wanaofanya vurugu,” alitusi Madenge huku
Manota akiwa na jazba kabla ya viongozi wengine wa kisiasa kuwatuliza.
Hata hivyo, kabla ya Makala kuzungumza, Mnyika
aliyekuwa ameongozana naye katika ziara hiyo alikuwa na wakati mgumu wa
kuzungumza kutokana na zomeazomea kutoka kwa wafuasi wa CCM.
Makalla alisema kosa kubwa lililosababisha kutokea kwa vurugu hizo ni maandalizi mabovu ya wafuasi wa vyama vyote.
“Wafuasi walikuwa na itikadi zao zaidi kuliko kuja
kusikiliza hoja za serikali kupitia ziara. Pia labda waliwakosa
uvumilivu kutokana na ahadi ya maji kuwapo kwa muda mrefu, lakini
kuvurugana wanasiasa ni kukosa uvumilivu,” alisema.
Kwa upande wake, Mnyika alipendekeza ziara zote za kiserikali zisiwe na uhusiano na vyama vya kisiasa.
“Kama ingekuwa ni mambo ya kuzungumzia ilani ya
chama, tangu mwaka 2005/10 ahadi ya maji ya asilimia 90 kwa Jiji la Dar
es Salaam haijatekelezwa,” alisema Mnyika.
Chanzo cha habari:Gazeti la Mwananchi
0 comments:
Post a Comment