WILAYA YA HAI
TAARIFA YA SENSA YA WATU NA MAKAZI, 2012
HADI TAREHE 03/09/2012
1.0 Utangulizi
Sensa ya Watu na Makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua na kusambaza takwimu za kidemografia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum. Kwa maana nyingine, Sensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi, hali yao ya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi.
Zoezi la Sensa ya watu na makazi ni zoezi la Kitaifa ambapo serikali ilitoa maagizo na maelekezo kwa Wilaya zote nchini kuhusu maandalizi hadi hitimisho la zoezi hili.
Wilaya ya Hai ni miongoni mwa wilaya za serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania zilizoshiriki zoezi hili.
2.0 Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi, 2012
2.1 Idadi ya EA
Wilaya hii ina maeneo ya kuhesabia (EAs) 430. Maeneo ya kuhesabia kwa kutumia dodoso refu yakiwa ni 145 na yakutumia dodoso fupi yakiwa ni 285.
2.2 Idadi ya wasimamizi na makarani
Katika kufanikisha zoezi hili Wilaya iliteua Wasimamizi 55, Makarani 290 wa dodoso refu, Makarani 285 wa dodoso fupi na Makarani wa akiba 14.
2.3 Mafunzo ya Sensa pamoja na vituo vya mafunzo (idadi ya walioanza, idadi ya waliohitimu na idadi ya makarani wa akiba)
Wasimamizi 55, Makarani wa dodoso refu 290 na Makarani wa akiba 14 walipatiwa mafunzo kuanzia tarehe 9 Agosti hadi 20 Agosti 2012 katika shule ya sekondari ya Hai day.Makarani wa dodoso fupi 285 walipatiwa mafunzo ya siku saba kuanzia tarehe 13 Agosti hadi 20 Agosti 2012.
Wakufunzi 15 walioteuliwa na Wilaya walitumika ipasavyo katika kuwafundisha walengwa kwa siku zote za mafunzo pia wakufunzi wa sensa ngazi ya Mkoa walifika eneo la mafunzo kuangalia maendeleo ya mafunzo na kusisitizia baadhi ya maeneo muhimu ili kufanikisha zoezi hili ipasavyo.
2.4 Mapokezi ya vifaa (tarehe, aina ya vifaa na idadi yake)
Wilaya ilipokea vifaa mbalimbali vya kufanyia zoezi la sensa tarehe 8 Agosti na 24 Agosti 2012 na kuvigawa kwa Wasimamizi na Makarani wa sensa kabla ya kuanza kwa zoezi hilo.
Orodha ya vifaa hivyo ni ifuatayo:-
| |||
NA | KIFAA | MAKISIO | VILIVYOPOKELEWA |
1 | SWMT 1:Dodoso la Jamii | 649 | 800 |
2 | SWMT 2:Dodoso Fupi | 30704 | 30704 |
3 | SWMT 3:Dodoso Refu | 13050 | 12902 |
4 | SWMT 4:Dodoso kwa ajili ya wasafiri/Waliolala Hotelini/Hospitalini | 649 | 100 |
5 | SWMT 5:Dodoso kwa ajili ya watu wasio na makazi maalum | 649 | 50 |
6 | EA Maps | 430 | 430 |
7 | Vitabu vya mageresho kwa Dodoso Refu | 359 | 359 |
8 | Vitabu vya mageresho kwa Dodoso Fupi | 285 | 285 |
9 | Training Manuals | 8 | 8 |
10 | RCC/DCC Hand book | 2 | 1 |
11 | Instruction manual to Junior Enumerators | 285 | 330 |
12 | Instruction manual to Senior Enumerators | 359 | 359 |
13 | Supervisors Hand book | 96 | 96 |
14 | Writing Boards | 644 | 644 |
15 | Special bags | 644 | 644 |
16 | Ordinary bags | 644 | 644 |
17 | Calender of National Events | 644 | 644 |
18 | Oath of Secrecy | 644 | 644 |
19 | Calculators | 644 | 644 |
20 | Boxes of Erasers | 649 | 644 |
21 | Boxes of Pencils 2HB | 1298 | 564 |
22 | Boxes of Sharpeners | 649 | |
23 | Boxes of Blue biros | 649 | 644 |
24 | Boxes of Red biros | 649 | |
25 | Marker pens- Black & Blue | 80 | 80 |
26 | Boxes of chalks | 1941 | 1800 |
27 | Note Books | 644 | 644 |
28 | Reflector Coats | 644 | 0 |
29 | Flip charts | 10 | 0 |
30 | Caps | 644 | 0 |
31 | Masking tape | 40 | 40 |
32 | Identity Cards | 644 | 654 |
33 | Stickers | | |
34 | Posters | | |
35 | Sisals Ropes | | 40 |
36 | Leaflets | | 1000 |
37 | Cellotapes | | 35 |
38 | Empty Boxes | 430 | 430 |
39 | Special Cards for Passengers(NIMEHESABIWA) | | 200 |
40 | Fomu za Udhibiti Ubora (Control Forms) | | |
| - SWMT 11 | | |
| - SWMT 12A | | 70 |
| - SWMT 12B | | 668 |
| - SWMT 13A | | 58 |
| - SWMT 13B | | 108 |
| - SWMT 13C | | 18 |
| - SWMT 13D | | |
| - SWMT 13E | | |
| - SWMT 14 | | 550 |
| - SWMT 15 | | 1300 |
| - SWMT 16A | | 462 |
| - SWMT 16B | | 100 |
| - SWMT 16C | | 9 |
| - SWMT 16D | | |
Aidha wilaya imeendelea kupokea vifaa vya nyongeza mara kwa mara ikiwa ni pamoja na madodoso marefu na mafupi,vifutio ,vichongeo na penseli kila vilipokuwa vikihitajika.
3.0 Utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi, 2012
3.1 Idadi ya makarani walioanza zoezi la kuhesabu watu
Idadi ya Makarani walioanza zoezi la kuhesabu watu katika wilaya ya Hai ni
makarani 578. Makarani 293 wakiwa ni wa dodoso refu na 285 wa dodoso
fupi.
3.2 Zoezi la kutambua maeneo ya kuhesabia watu pamoja na
changamoto za kusoma ramani
Zoezi la kutambua maeneo ya kuhesabia watu lilifanywa na makarani katika
maeneo yote ya wilaya kuanzia tarehe 22 Agosti hadi 24 Agosti 2012 na
kufanya utatuzi wa changamoto mbalimbali sehemu ambazo ramani za
maeneo husika zilionekana kutofautiana na uhalisia.
Changamoto zilizojitokeza wakati wa kutambua maeneo.
Wakati wa kutambua maeneo changamoto zifuatazo zilijitokeza.
(i)Baadhi ya maeneo kutoonekana kwenye ramani. Kwa mfano kuna eneo liliachwa bila kuwekwa kwenye ramani lililopo katikati ya EA Na 04010 na 04012 Katika kijiji cha Nshara kata ya Machame Kaskazini.
Utatuzi wa changamoto hiyo.
Kwa kuwa eneo eneo lililokuwa limeachwa lina kaya nyingi ilibidi kutumia karani wa akiba wa kata hiyo kuhesabu eneo hilo.
3.3 Maeneo yaliyohesabiwa usiku wa tarehe 25/08/2012 kuamkia tarehe 26/08/2012 pamoja na changamoto zilizojitokeza.
Maeneo yaliyohesabiwa usiku wa tarehe 25/08/2012 ni uwanja wa ndege KIA, Hospitali za Machame,Hai na vituo vya afya,nyumba za kulala wageni na Hoteli zilizopo kata za Hai mjini,KIA,Machame kusini,Machame Kaskazini na Masama kusini.
3.4 Idadi ya EA zilizokamilika kuhesabiwa hadi kufikia tarehe 03/09/2012
Hadi kufikia tarehe 03/09/2012 jumla ya EA 365 kati ya 430 zilikuwa
zimekamilika kuhesabiwa,bado EA 95.
4.0 Mafanikio ya Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi, 2012
4.1 Mahusiano na viongozi wa jamii (mfano wenyeviti wa vijiji na vitongoji)
Hali ya mahusiano na viongozi wa jamii wakati wa zoezi la sensa ni nzuri.Viongozi hawa walitoa ushirikiano wa kutosha kwa makarani wa sensa.
4.2 Kuhesabiwa kwa hiari na kutoa ushirikiano
Idadi kubwa ya wananchi walikubali kuhesabiwa kwa hiari na walitoa
ushirikiano wa kutosha wakati wa zoezi hili.
4.3 Ushirikiano kutoka kwa Serikali na vyombo vya dola pale.
Serikali na vyombo vya dola vilitoa ushirikiano mkubwa pale upinzani wa kuhesabiwa ulipojitokeza. Kwa mfano. Kuna wananchi walikataa kuhesabiwa kwa sababu za imani za dini ambapo serikali na vyombo vya dola vilishirikiana hadi wahusika wakakubali kuhesabiwa.
4.4 Makarani kufanyakazi katika hali ya amani na utulivu.
Katika wilaya yetu makarani wote wa sensa wamefanya kazi katika hali ya
amani na utulivu. Hakuna tukio lolote lililoripotiwa la kuvuruga amani
katika maeneo ya kuhesabia.
5.0 Mapungufu/matatizo yaliyojitokeza wakati wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi, 2012
5.1 Wakati wa mafunzo:-
(i) kuchelewa kwa vifaa vya mafunzo. Kwa mfano wakati wa mafunzo ya Wasimamizi,Makarani wa dodoso refu na Makarani wa akiba, vitabu vya miongozo kwa watu hao vilifika siku 5 baada ya kuaza kwa mafunzo jambo lililowaweka wakufunzi katika mazingira magumu wakati wa kufundisha.
5.2 Wakati wa zoezi la kuhesabu watu:-
(i) Uhaba wa vifaa.
Wakati wa zoezi la sensa palitokea uhaba mkubwa wa vifaa hasa
madodoso uliosababisha kupungua kwa kasi ya uhesabuji na
kuiongezea Wilaya gharama kubwa za kurudufisha madodoso
hayo pale yalipochelewa kufika.
(ii) Baadhi ya maeneo ya kuhesabia kuwa na idadi kubwa ya
kaya.
Baadhi ya maeneo ya kuhesabia yameonekana kuwa na idadi
kubwa ya kaya kuliko ilivyotarajiwa jambo lililofanya kazi kuwa
ngumu kwa makarani na wasimamizi wa maeneo hayo.Kwa
mfano baadhi ya maeneo ya kata za Hai mjini,Machame
Kaskazini,Masama kusini na Masama Mashariki hayajakamilika
kuhesabiwa kutokana na wingi wa kaya.
(iii)Baadhi ya vifaa kutopatikana kabisa.
Baadhi ya vifaa kama vile fulana,kofia na makoti maalum
(reflector Coats havikupatikana kabisa jambo lililosababisha
baadhi ya wanakaya kutowapokea makarani wa sensa kwa
kigezo kuwa makarani hao wanaonekana tofauti na vyombo vya
habari vinavyotangaza karani wa sensa anavyotakiwa
kuonekana.
6.0 Changamoto
6.1 Wakati wa zoezi Sensa ya Watu na Makazi, 2012
(i) Baadhi ya wananchi kukataa kuhesabiwa.
Baadhi ya wananchi walikataa kuhesabiwa hasa kwa kigezo cha imani za
dini jambo lilillosababisha kutumika kwa vyombo vya dola kama vile jeshi la
polisi na viongozi wa ngazi mbalimbali kuwashawishi wananchi hao ili
wahesabiwe.
6.2 Mikakati iliyotumika kutatua changamoto
(i)Viongozi wa serikali,viongozi wa dini na vyombo vya dola vilitumika
kuwashawishi wananchi wote waliogoma hadi wakahesabiwa.
(ii)Maeneo ambayo kaya zimeonekana kuwa nyingi makarani wa akiba
Wametumika japokuwa makarani hao hawatoshelezi upungufu.
(iii)Viongozi wa vitongoji na vijiji wamekuwa wakitumika kuwashawishi
wananchi pale changamoto y akutowatambua makarani kwa kutovaa
vazi maalum linapojitokeza.
7.0 Maoni/Mapendekezo
7.1 Kipindi kilichobaki.
Ni vema utaratibu uliowekwa wa kuwatumia makarani wa sensa katika zoezi la kuandikisha daftari la wakazi likatazamwa upya kwani baadhi ya makarani wanaanza kurudi vyuoni na baadhi ya shule binafsi zimeshaaza kufunguliwa.
7.2 Sensa ijayo
(i) Ngazi za Wilaya na Mikoa zinapaswa zishirikishwe ipasavyo katika maandalizi ya zoezi la sensa kuanzia mwanzo wa maandalizi ili kupata takwimu sahihi za idadi ya kaya na wakazi jambo ambalo litasaidia kufanya makisio sahihi ya maeneo ya kuhesabia,vifaa,fedha,Wasimamizi na Makarani wakati wa sensa.
(ii) Muda mfupi kabla ya zoezi la sensa kuanza wataalam wa ramani wapite kwenye maeneo ya kuhesabia kwa kushirikiana na viongozi wa Vijiji na Vitongoji ili kubaini mabadiliko yaliyotokea katika maeneo hayo na kurekebisha ramani husika.
0 comments:
Post a Comment