NA MWANDISHI WETU,HAI
MVUTANO WA KISIASA KATIKA KIJIJI CHA LEMIRA KATI KILICHOPO KATIKA WILAYA YA HAI UMESAABABISHA UJENZI WA CHOO KIPYA CHA SHULE YA MSINGI YA KIJIJI HICHO KUTOKAMILIKA KWA MIAKA MIWILI SASA PAMOJA NA KWAMBA FEDHA ZA KUKIKAMILISHA CHOO HICHO KUWEMO KATIKA AKAUNTI YA BENKI YA KIJIJI HICHO
HAYO YAMEBAINIKA KUFUATIA ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA HAI BW NOVATUS MAKUNGA KATIKA KIJIJI HICHO NA BAADAYE KUKAGUA UJENZI WA CHOO CHA SHULE YA MSINGI LEMIRA KATI KILICHOANZA UJENZI MWEZI JUNI MWAKA 2010 LAKINI MPAKA SASA HAKIJAKAMILIKA PAMOJA NA KUWEPO KWA FEDHA ZA KUKAMILISHA CHOO HICHO
AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI HICHO CHA LEMERA KATI BW MAKUNGA AMEAGIZA UONGOZI WA KIJIJI HICHO UNAOSHIRIKIANA NA KIJIJI CHA JIRANI CHA KUHAKIKISHA UNAKAMILISHA UJENZI HUO KWA USHAURI WA KITAALAMU KUTOKA IDARA YA UJENZI YA HALMASHAURI YA HAI
KWA UPANDE WAKE MKAGUZI WA NDANI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI BI AGULINA NZOTA AMEELEZA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 10.1 ZA CHOO HICHO ZILIZOTOKANA NA LUZUKU YA SERIKALI NA MICHANGO YA JAMNII ZILIPATIKANA NA BAADHI YA FEDHA HIZO BADO ZIPO KATIKA AKAUNTI YA KIJIJI
NAO WANANCHI WA KIJIJI HICHO MABWANA DARESKO KWEKA,ANAUFOO MINISI NA LEWI MUNISI WAMEELEZA KUSHANGAZWA NA TAARIFA YA KWAMBA BADO KUNA WANANCHI WANADAIWA MICHANGO YA KILA KAYA YA SHILINGI ELFU TANO YA UJENZI WA CHOO HICHO
MHANDISI WA UJENZI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI AMEAHIDI KUSHIRIKIANA NA KAMATI YA UJENZI YA KIJIJI KUHAKIKISHA CHOO HICHO KINAKAMILIKA KATIKA MUDA ULIOTOLEWA NA MKUU WA WILAYA HIYO BW MAKUNGA
0 comments:
Post a Comment