DC WA HAI ATEMBELEA SOKO LA RUNDUGAI

Posted by MK On 20:52 No comments




Na Richard Mwangulube

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ameuagiza uongozi wa kata ya Masama Rundugai kuhakikisha wanakaa na wakala anayelisimamia soko na Rundugai kwa lengo la kutatua kero zilizoko ndani ya mamlaka yao wakati mipango ya uboreshaji wa soko ikisubiri mikakati  ya halmashauri ya wilaya.

Makunga ametoa agizo hilo baada ya kutembelea soko hilo ambalo hufanyika mara moja kwa wiki yaani kila jumatatu.

Baada ya kutembelea soko hilo na kukutana na maofisa mbalimbali wa kata ya Masama Rundugai na kijiji cha Rundugai,aliwataka viongozi hao kutatua tatizo la matumizi ya choo ambacho wananchi walidai kuwa kinafungwa muda wote na funguo hazifahamiki zinahifadhiwa wapi pamoja na ukosefu wa maji.

Wananchi wanaotumia soko hilo wameeleza kuwa wanalazimika kwenda kujisaidia maporini kandokando mya reli inayokatisha jirani na soko hilo na pia wamelalamikia huduma ya maji kwa madai ya kwamba wanatumia ya mwananchi jirani kwa kuwa soko hilo halina maji.

Makunga ameeeleza kero ya choo ambacho tayari kipo pamoja na kuvutwa kwa maji limo ndani ya uwezo wa uongozi wa kijiji na kata pamoja na wakala anayesimamia soko hilo huku akiongeza kuwa mipango ya kuliboresha soko hilo ikiwa jukumu la halmashauri ya wilaya ya Hai.

Ameeleza kuwa baadhi ya mikakati ambayo ni lazima ichukuliwe ni pamoja na kuondokana na utaratibu wa kupanga bidhaa chini ya ardhi pamoja na kujenga mazingira mazuri ya ufanyaji wa biashara na shughuli nyingine katika soko hilo.

Wananchi wa eneo hilo wameeleza kuwa soko hilo ni la muda mrefu sana ambapom pamoja na kulipa ushuru wa kati ya shilingi mia tatu na mia tano lakini hakuna uboreshaji wowote unaofanyika.

0 comments:

Post a Comment