DC HAI,ALIKOTOKA NA ALIKOPITIA

Posted by MK On 15:27 No comments

2002-National Executive Committee Member, Daniel Ole Njoolay who is also Arusha’s Regional Commissioner congratulating Novatus Makunga (left) after being elected publicity secretary of the Party in Arusha region. The CCM regional conference was held in Arusha recently

DC WA HAI ATEMBELEA SOKO LA RUNDUGAI

Posted by MK On 20:52 No comments




Na Richard Mwangulube

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ameuagiza uongozi wa kata ya Masama Rundugai kuhakikisha wanakaa na wakala anayelisimamia soko na Rundugai kwa lengo la kutatua kero zilizoko ndani ya mamlaka yao wakati mipango ya uboreshaji wa soko ikisubiri mikakati  ya halmashauri ya wilaya.

Makunga ametoa agizo hilo baada ya kutembelea soko hilo ambalo hufanyika mara moja kwa wiki yaani kila jumatatu.

Baada ya kutembelea soko hilo na kukutana na maofisa mbalimbali wa kata ya Masama Rundugai na kijiji cha Rundugai,aliwataka viongozi hao kutatua tatizo la matumizi ya choo ambacho wananchi walidai kuwa kinafungwa muda wote na funguo hazifahamiki zinahifadhiwa wapi pamoja na ukosefu wa maji.

Wananchi wanaotumia soko hilo wameeleza kuwa wanalazimika kwenda kujisaidia maporini kandokando mya reli inayokatisha jirani na soko hilo na pia wamelalamikia huduma ya maji kwa madai ya kwamba wanatumia ya mwananchi jirani kwa kuwa soko hilo halina maji.

Makunga ameeeleza kero ya choo ambacho tayari kipo pamoja na kuvutwa kwa maji limo ndani ya uwezo wa uongozi wa kijiji na kata pamoja na wakala anayesimamia soko hilo huku akiongeza kuwa mipango ya kuliboresha soko hilo ikiwa jukumu la halmashauri ya wilaya ya Hai.

Ameeleza kuwa baadhi ya mikakati ambayo ni lazima ichukuliwe ni pamoja na kuondokana na utaratibu wa kupanga bidhaa chini ya ardhi pamoja na kujenga mazingira mazuri ya ufanyaji wa biashara na shughuli nyingine katika soko hilo.

Wananchi wa eneo hilo wameeleza kuwa soko hilo ni la muda mrefu sana ambapom pamoja na kulipa ushuru wa kati ya shilingi mia tatu na mia tano lakini hakuna uboreshaji wowote unaofanyika.

HAI VILLAGE LEADERSHIP SUSPENDED

Posted by MK On 09:10 No comments



 
Monday, 17 September 2012 08:33

By The Citizen Reporter,Moshi.

The entire leadership of Kwa Saadala, a sprawling village along the Arusha-Moshi highway, has been suspended over alleged embezzlement of  public funds and illegal sale of village assets.

The order was given over the weekend by the Hai District Commissioner, Mr Novatus Makunga, who said a probe team would be formed to investigate allegations that a public land meant for social and community services, such as schools, has been sold to individuals.Accused village leaders have been directed to step aside, as the probe into the scam gets underway. 

Those suspended include the Village chairman, Mr Ernest Munisi, Village Executive officer, Mr Claire Ramadhani and Masama South Ward Executive officer. A six-member team comprising officials from Moshi District Council, including the Land officer, Legal officer, Internal auditor, Personnel officer, Administrative officer and Supplies officer, will investiage the scam and has been given one week to complete the task.

Mr Makunga said that once the team completes its task, a meeting would be convened for all village stakeholders to discuss the findings of the report and what should be done to those proved guilty and have cases to answer. 

At last weekend's meeting, most residents alleged that the village chairman was behind the sale of the public land. One of them, Ms Judica Swai, claimed that open spaces close to the Msamadi Primary School had also been sold  without the school management and villagers’ consent.



VILLAGERS OPPOSE KIA EVICTION ORDER

Posted by MK On 09:07 No comments




Monday, 20 August 2012 22:41
 
By Zephania Ubwani,

The Citizen Bureau Chief Arusha. 

Nearly 1,000 families of villagers living around the Kilimanjaro International Airport (KIA) have opposed an eviction order and pleaded to the higher government authorities to assist them.The Kilimanjaro Airports Development Company (Kadco) says the villagers had trespassed on the land belonging to the airport and have to vacate.

But Mtakuja and Sanya Stesheni villagers in Hai District, Kilimanjaro Region claim that they are genuine residents of the area and were relocated there during the villagisation programme in the 1970s.


Their colleagues at Tindigani Village said they had been there since 1999 and could not see any justification for eviction from the lowland, which assures them of water supply. The other affected village is Chemka but there were no details.


During their recent meeting with Hai District leaders, the villagers, majority of them being livestock keepers, threatened to seek audience with the higher government authorities in Dodoma or Dar es Salaam over the dispute. They claimed that implementing the order would see 907 families comprising 6,349 people evicted. The move means they would also be forced to abandon 4,200 acres of farmland.


When contacted on the matter, the Hai District commissioner Novatus Makunga, said that the issue was ‘sensitive’ because the villages in dispute with the airport authority have land titles for their respective areas.

He pleaded to the villagers to be patient and not to send a delegation to Dodoma to see the Prime Minister Mizengo Pinda until a team formed by the district authorities to investigate the crisis completes its job.

The Hai District administrative officer, Mr Venance Mpotwa, heads a six-person team comprising at least two land officers and the district planning officer and it has been told to speed up the probe. 

However, the DC insisted that “The solution to the crisis would have to involve Kadco, a private firm that manages the airport, village officials and the traditional leaders, commonly known as Lwaigwanan,” said Mr Makunga.

He implored on the villagers to respect the boundaries of the airport, which is gearing up for construction of additional structures or further expansion.

The villagers claimed in the message to the Hai leaders that some of their relatives vacated the area voluntarily when construction of the airport began in 1969.It is estimated that the livestock keepers who will be affected by the eviction have a total of 42,763 head of cattle, 33,840 goats, 38,412 sheep and 14,414 donkeys.

The land dispute between KIA management and the adjacent villages first surfaced in 1989, prompting the government to order the two sides observe boundaries.

KADCO, which took over the management of the airport in 1998, has repeatedly warned against trespassing of their land because it would stifle expansion plans, including leasing part of it to potential investors.



WAHAMIAJI HARAMU WALIOTOROKA MOSHI WAKAMATWA HAI

Posted by MK On 03:04 No comments






Na Richard Mwangulube,Hai

Vyombo vya usalama wilayani Hai mkoani Kilimanjaro vimefanikiwa kuwanasa Wahabeshi wiwili ambao wanadhaniwa ni sehemu ya kundi la wahamiji haramu wanne waliofanikiwa kuwatoroka polisi usiku wa kuamkia ijumaa iliyopita katika eneo la Kilemapofu wilayani moshi.

Wahamiaji haramu hao kutoka Ethiopia walikamatwa jana saa mbili na nusu asubuhi wakiwa wamejificha katika kichaka kichopo katika eneo la Uzunguni katika mji wa Hai maarufu kama Bomang’ombe.

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga alithibitisha kwa njia ya simu kukamatwa kwa Wahabeshi hao ambapo ameeleza kuwa moja kati ya hao alikuwa na pasi ya kusafiria ya Ethiopia huku mwingine akiwa hana

Alisema kuwa katika maelezo ya awali Wahabeshi hao wamedai kuwa walitelekezwa katika eneo hilo la uzunguni na pikipiki zinazofahamika kwa jina maarufu kama bodaboda huku wakiwa hawaelewi uelekeo wa sehemu walipokuwa wameachwa.

“Tumekuwa na kampeni ya muda mrefu ya kuielimisha jamii kuhusiana na wimbi la sasa la wahamiaji haramu ama kuwepo na biashara haramu ya kusafisha watu kutoka Ethiopia na Somalia,hivyo wananchi walitupa taarifa kuhusiana na kuwatilia wasiwasi watu wawili na baadaye vyombo vya dola vilifanikiwa kuwatia mikononi lakini kikubwa kama wameanza kutumia pikipiki ni vyema tukawa macho zaidi,”alisema Makunga.

Aliwataja Wahabeshi hao kuwa ni pamoja na Tarekegn demeke[21] ambaye alikuwa na pasi ya kusafiria na Alem mituku[25] ambaye hakuwa na pasi ya kusafiria.

Makunga ameeleza kuwa vyombo vya dola wakiwemo polisi na maofisa wa uhamiaji wanaendelea kuwahoji kabla ya kuwachukulia hatua za kisheria zinazosimamia masuala ya uhamiaji.

Ameeleza kuwa kuna kila ushahidi kuwa wahabeshi hao ni sehemu ya kundi la wahamiaji sita waliokamatwa saa tisa usiku wa Septemba sita mwaka huu wilayani Moshi wakiwa wamebebwa na pikipiki tatu wakitokea wilayani Rombo huku lengo likiwa kufika Hai.

Ameeleza kuwa katika tukio hilo wahamiaji wanne walifanikiwa kutoroka huku polisi ikifanikiwa kuwatia mbaroni wawili na madeareva wa pikipiki hizo.

Makunga ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya ya Hai ameendelea kutoa wito kwa wananchi na viongozi wa vijiji kuhakikisha wanatoa taarifa za nyendo zozote za watu wasiofahamika kutokana na wahamiaji hao kubuni njia mpya ya kutumia usafiri wa pikipiki.

Mwishoni mwa wiki hii jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro lilifanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu kumi kutoka Ethiopia pamoja watu saba na pikipiki nne kwa tuhuma za kuwasafirisha wahamaiaji hao katika eneo la Kilemapofu na Mjohoroni wilayani Moshi

DC HAI AINGILIA KATI MALUMBANO YANAYOKWAMISHA KUKAMILIKA KWA CHOO CHA SHULE TANGU 2010

Posted by MK On 21:58 No comments









NA MWANDISHI WETU,HAI

MVUTANO WA KISIASA KATIKA KIJIJI CHA LEMIRA KATI KILICHOPO KATIKA WILAYA YA HAI UMESAABABISHA UJENZI WA CHOO KIPYA CHA SHULE YA MSINGI YA KIJIJI HICHO KUTOKAMILIKA KWA MIAKA MIWILI SASA PAMOJA NA KWAMBA FEDHA ZA KUKIKAMILISHA CHOO HICHO KUWEMO KATIKA AKAUNTI YA BENKI YA KIJIJI HICHO

HAYO YAMEBAINIKA KUFUATIA ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA HAI BW NOVATUS MAKUNGA KATIKA KIJIJI HICHO NA BAADAYE KUKAGUA UJENZI WA CHOO CHA SHULE YA MSINGI LEMIRA KATI KILICHOANZA UJENZI MWEZI JUNI MWAKA 2010 LAKINI MPAKA SASA HAKIJAKAMILIKA PAMOJA NA KUWEPO KWA FEDHA ZA KUKAMILISHA CHOO HICHO

AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI HICHO CHA LEMERA KATI BW MAKUNGA AMEAGIZA UONGOZI WA KIJIJI HICHO UNAOSHIRIKIANA NA KIJIJI CHA JIRANI CHA KUHAKIKISHA UNAKAMILISHA UJENZI HUO KWA USHAURI WA KITAALAMU KUTOKA IDARA YA UJENZI YA HALMASHAURI YA HAI

KWA UPANDE WAKE MKAGUZI WA NDANI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI BI AGULINA NZOTA AMEELEZA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 10.1 ZA CHOO HICHO ZILIZOTOKANA NA LUZUKU YA SERIKALI NA MICHANGO YA JAMNII ZILIPATIKANA NA BAADHI YA FEDHA HIZO BADO ZIPO KATIKA AKAUNTI YA KIJIJI

NAO WANANCHI WA KIJIJI HICHO MABWANA DARESKO KWEKA,ANAUFOO MINISI NA LEWI MUNISI WAMEELEZA KUSHANGAZWA NA TAARIFA YA KWAMBA BADO KUNA WANANCHI WANADAIWA MICHANGO YA KILA KAYA YA SHILINGI ELFU TANO YA UJENZI WA CHOO HICHO

MHANDISI WA UJENZI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI AMEAHIDI KUSHIRIKIANA NA KAMATI YA UJENZI YA KIJIJI KUHAKIKISHA CHOO HICHO KINAKAMILIKA KATIKA MUDA ULIOTOLEWA NA MKUU WA WILAYA HIYO BW MAKUNGA

PIGA KURA KUINUA VIVUTIO VYA UTALII TANZANIA

Posted by MK On 12:57 No comments


TUMIA FURUSA HII KUPIGIA KURA VIVUTUO VYA TANZANIA

Tumia fursa hii kupigia kura vivutio vya Tanzania ili viweze kuwa miongoni mwa maajabu saba ya asili ya bara la Afrika. Vivutio vya Tanzania vinavyoshindanishwa na vingine tisa (9) barani Afrika ni Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, na hifadhi ya Serengeti.
Tembelea sevennaturalwonders.org na upigekura yako.

MAENDELEO YA SENSA WILAYANI HAI

Posted by MK On 07:57 No comments


WILAYA YA HAI
TAARIFA YA SENSA YA WATU NA MAKAZI, 2012
HADI TAREHE 03/09/2012

1.0 Utangulizi

Sensa ya Watu na Makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua na kusambaza takwimu za kidemografia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum. Kwa maana nyingine, Sensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi, hali yao ya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi. 

Zoezi la  Sensa ya watu na makazi ni zoezi la Kitaifa ambapo serikali ilitoa maagizo na maelekezo kwa Wilaya zote nchini kuhusu maandalizi hadi hitimisho la zoezi hili.
Wilaya ya Hai ni miongoni mwa wilaya za serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania zilizoshiriki zoezi hili.

2.0 Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi, 2012
2.1 Idadi ya EA

Wilaya hii ina maeneo ya kuhesabia (EAs) 430. Maeneo ya kuhesabia kwa kutumia dodoso refu yakiwa ni 145 na yakutumia dodoso fupi yakiwa ni 285.

2.2 Idadi ya wasimamizi na makarani

Katika kufanikisha zoezi hili Wilaya iliteua Wasimamizi 55, Makarani 290 wa dodoso refu, Makarani 285 wa dodoso fupi na Makarani wa akiba 14.


2.3 Mafunzo ya Sensa pamoja na vituo vya mafunzo (idadi ya walioanza, idadi ya waliohitimu na idadi ya makarani wa akiba)

Wasimamizi 55, Makarani wa dodoso refu 290 na Makarani wa akiba 14 walipatiwa mafunzo kuanzia tarehe 9 Agosti hadi 20 Agosti 2012 katika shule ya sekondari ya Hai day.Makarani wa dodoso fupi 285 walipatiwa mafunzo ya siku saba kuanzia tarehe 13 Agosti hadi 20 Agosti 2012.

Wakufunzi 15 walioteuliwa na Wilaya walitumika ipasavyo katika kuwafundisha walengwa kwa siku zote za mafunzo pia wakufunzi wa sensa ngazi ya Mkoa walifika eneo la mafunzo kuangalia maendeleo ya mafunzo na kusisitizia  baadhi ya maeneo muhimu ili kufanikisha zoezi hili ipasavyo.

2.4 Mapokezi ya vifaa (tarehe, aina ya vifaa na idadi yake)

Wilaya ilipokea vifaa  mbalimbali vya kufanyia zoezi la sensa tarehe 8 Agosti na 24 Agosti 2012 na kuvigawa kwa Wasimamizi na Makarani wa sensa kabla ya kuanza  kwa zoezi hilo. 

Orodha ya vifaa hivyo ni ifuatayo:-


NA
KIFAA
MAKISIO
VILIVYOPOKELEWA
1
SWMT 1:Dodoso la Jamii
649
800
2
SWMT 2:Dodoso Fupi
30704
30704
3
SWMT 3:Dodoso Refu
13050
12902
4
SWMT 4:Dodoso kwa ajili ya wasafiri/Waliolala Hotelini/Hospitalini
649
100
5
SWMT 5:Dodoso kwa ajili ya watu wasio na makazi maalum
649
50
6
EA Maps
430
430
7
Vitabu vya mageresho kwa Dodoso Refu
359
359
8
Vitabu vya mageresho kwa Dodoso Fupi
285
285
9
Training Manuals
8
8
10
RCC/DCC Hand book
2
1
11
Instruction manual to Junior Enumerators
285
330
12
Instruction manual to Senior Enumerators
359
359
13
Supervisors Hand book
96
96
14
Writing Boards
644
644
15
Special bags
644
644
16
Ordinary bags
644
644
17
Calender of National Events
644
644
18
Oath of Secrecy
644
644
19
Calculators
644
644
20
Boxes of Erasers
649
644
21
Boxes of Pencils 2HB
1298
564
22
Boxes of Sharpeners
649

23
Boxes of Blue biros
649
644
24
Boxes of Red biros
649

25
Marker pens- Black & Blue
80
80
26
Boxes of chalks
1941
1800
27
Note Books
644
644
28
Reflector Coats
644
0
29
Flip charts
10
0
30
Caps
644
0
31
Masking tape
40
40
32
Identity Cards
644
654
33
Stickers


34
Posters


35
Sisals Ropes

40
36
Leaflets

1000
37
Cellotapes

35
38
Empty Boxes
430
430
39
Special Cards for Passengers(NIMEHESABIWA)

200
40
Fomu za Udhibiti Ubora (Control Forms)



    - SWMT 11



    - SWMT 12A

70

    - SWMT 12B

668

    - SWMT 13A

58

    - SWMT 13B

108

    - SWMT 13C

18

    - SWMT 13D



    - SWMT 13E



    - SWMT 14

550

    - SWMT 15

1300

    - SWMT 16A

462

    - SWMT 16B

100

    - SWMT 16C

9

    - SWMT 16D



Aidha wilaya imeendelea kupokea vifaa vya nyongeza mara kwa mara ikiwa ni pamoja na madodoso marefu na mafupi,vifutio ,vichongeo na penseli kila vilipokuwa vikihitajika.

3.0 Utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi, 2012

3.1 Idadi ya makarani walioanza zoezi la kuhesabu watu
Idadi ya Makarani walioanza zoezi la kuhesabu watu katika wilaya ya Hai ni
makarani 578. Makarani 293 wakiwa ni wa dodoso refu na 285 wa dodoso
fupi.

3.2 Zoezi la kutambua maeneo ya kuhesabia watu pamoja na
      changamoto za kusoma ramani
      
Zoezi la kutambua maeneo ya kuhesabia watu  lilifanywa na makarani katika   
maeneo yote ya wilaya kuanzia tarehe 22 Agosti hadi 24 Agosti 2012 na
kufanya utatuzi wa changamoto mbalimbali sehemu ambazo ramani za
maeneo husika zilionekana kutofautiana na uhalisia. 

  Changamoto zilizojitokeza wakati wa kutambua maeneo.
Wakati wa kutambua maeneo changamoto zifuatazo zilijitokeza.
 (i)Baadhi ya maeneo kutoonekana kwenye ramani. Kwa mfano kuna eneo liliachwa bila kuwekwa kwenye ramani lililopo katikati ya EA Na 04010 na 04012 Katika kijiji cha Nshara kata ya Machame Kaskazini.

Utatuzi wa changamoto hiyo.
Kwa kuwa eneo eneo lililokuwa limeachwa lina kaya nyingi ilibidi kutumia karani wa akiba wa kata hiyo kuhesabu eneo hilo.

3.3 Maeneo yaliyohesabiwa usiku wa tarehe 25/08/2012 kuamkia tarehe 26/08/2012 pamoja na changamoto zilizojitokeza.
      Maeneo yaliyohesabiwa  usiku wa tarehe 25/08/2012 ni uwanja wa ndege KIA, Hospitali za Machame,Hai na vituo vya afya,nyumba za kulala wageni na Hoteli zilizopo kata za Hai mjini,KIA,Machame kusini,Machame Kaskazini na Masama kusini.

3.4 Idadi ya EA zilizokamilika kuhesabiwa hadi kufikia tarehe 03/09/2012
 Hadi kufikia tarehe 03/09/2012 jumla ya EA 365 kati ya 430 zilikuwa
 zimekamilika kuhesabiwa,bado EA 95.

4.0       Mafanikio ya Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi, 2012
4.1 Mahusiano na viongozi wa  jamii (mfano wenyeviti wa vijiji na vitongoji)
      Hali ya mahusiano na viongozi wa jamii wakati wa zoezi la sensa ni nzuri.Viongozi hawa walitoa ushirikiano wa kutosha kwa makarani wa sensa.

4.2 Kuhesabiwa kwa hiari na kutoa ushirikiano
Idadi kubwa ya wananchi walikubali kuhesabiwa kwa hiari na walitoa    
 ushirikiano wa kutosha wakati wa zoezi hili.

4.3 Ushirikiano kutoka kwa Serikali na vyombo vya dola pale.
       Serikali na vyombo vya dola vilitoa ushirikiano mkubwa pale upinzani wa kuhesabiwa ulipojitokeza. Kwa mfano. Kuna wananchi walikataa kuhesabiwa kwa sababu za imani za dini ambapo serikali na vyombo vya dola vilishirikiana hadi wahusika wakakubali kuhesabiwa.

4.4 Makarani kufanyakazi katika hali ya amani na utulivu.
    Katika wilaya yetu makarani wote wa sensa wamefanya kazi katika hali ya   
    amani na utulivu. Hakuna tukio lolote lililoripotiwa la kuvuruga amani   
    katika maeneo ya kuhesabia.

5.0       Mapungufu/matatizo yaliyojitokeza wakati wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi, 2012
5.1       Wakati wa mafunzo:-
(i)        kuchelewa kwa vifaa vya mafunzo. Kwa mfano wakati wa mafunzo ya Wasimamizi,Makarani wa dodoso refu na Makarani wa akiba, vitabu vya miongozo kwa watu hao vilifika siku 5 baada ya kuaza kwa mafunzo jambo lililowaweka wakufunzi katika mazingira magumu wakati wa kufundisha.

5.2       Wakati wa zoezi la kuhesabu watu:-
                    (i) Uhaba wa vifaa.
                         Wakati wa zoezi la sensa palitokea uhaba mkubwa wa vifaa hasa     
                        madodoso uliosababisha kupungua   kwa kasi ya uhesabuji na
                        kuiongezea  Wilaya gharama  kubwa za kurudufisha madodoso
                        hayo pale yalipochelewa kufika.

        (ii) Baadhi ya maeneo ya kuhesabia kuwa na idadi kubwa ya
            kaya.
                       Baadhi ya maeneo ya kuhesabia yameonekana kuwa na idadi
                       kubwa ya kaya kuliko ilivyotarajiwa jambo lililofanya kazi kuwa   
                       ngumu kwa  makarani na wasimamizi wa maeneo hayo.Kwa
                       mfano baadhi ya maeneo ya kata za Hai mjini,Machame         
                       Kaskazini,Masama kusini na Masama  Mashariki hayajakamilika
                       kuhesabiwa kutokana na wingi wa kaya.
                
                   (iii)Baadhi ya vifaa kutopatikana kabisa.
                         Baadhi ya vifaa  kama vile fulana,kofia na makoti maalum
                         (reflector  Coats havikupatikana kabisa jambo lililosababisha   
                         baadhi ya wanakaya  kutowapokea makarani wa sensa kwa      
                        kigezo kuwa makarani hao  wanaonekana tofauti na vyombo vya
                        habari vinavyotangaza karani wa sensa anavyotakiwa
                        kuonekana.

6.0             Changamoto
6.1             Wakati wa zoezi Sensa ya Watu na Makazi, 2012

      (i)  Baadhi ya wananchi kukataa kuhesabiwa.
        Baadhi ya wananchi walikataa kuhesabiwa hasa kwa kigezo cha imani za  
        dini jambo lilillosababisha kutumika kwa vyombo vya dola kama vile jeshi la
        polisi na viongozi wa ngazi mbalimbali kuwashawishi wananchi hao ili
        wahesabiwe.
                
    6.2   Mikakati iliyotumika kutatua changamoto
           (i)Viongozi wa serikali,viongozi wa dini na vyombo vya dola vilitumika
             kuwashawishi wananchi wote waliogoma hadi wakahesabiwa.
         
           (ii)Maeneo ambayo kaya zimeonekana kuwa nyingi makarani wa akiba
            Wametumika japokuwa makarani hao hawatoshelezi upungufu.
          
            (iii)Viongozi wa vitongoji na vijiji wamekuwa wakitumika kuwashawishi
            wananchi pale changamoto y akutowatambua makarani kwa kutovaa
            vazi maalum linapojitokeza.

7.0       Maoni/Mapendekezo

7.1 Kipindi kilichobaki.
Ni vema utaratibu   uliowekwa wa  kuwatumia makarani wa sensa katika zoezi la kuandikisha daftari la wakazi likatazamwa upya kwani baadhi ya makarani wanaanza kurudi vyuoni na baadhi ya shule binafsi zimeshaaza kufunguliwa.

7.2 Sensa ijayo
(i) Ngazi za Wilaya na Mikoa zinapaswa zishirikishwe ipasavyo katika maandalizi ya  zoezi la sensa kuanzia mwanzo wa maandalizi ili kupata takwimu sahihi za idadi ya   kaya na wakazi jambo ambalo litasaidia kufanya makisio sahihi ya  maeneo ya kuhesabia,vifaa,fedha,Wasimamizi na Makarani wakati wa sensa.

(ii) Muda mfupi kabla ya zoezi la sensa kuanza wataalam wa ramani wapite kwenye maeneo ya kuhesabia kwa kushirikiana na viongozi wa  Vijiji na Vitongoji ili kubaini mabadiliko yaliyotokea katika maeneo hayo na kurekebisha ramani husika.