KANUNI ZA BUNGE MAALUMU LA KATIBA

Posted by Arusha by day and by night On 02:07 No comments

i
BUNGE MAALUM
____________
KANUNI ZA BUNGE MAALUM
ZA MWAKA 2014
____________
[Zimetungwa chini ya Kifungu cha 26(1) cha
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83]
ii
TANGAZO LA SERIKALI Na.67 la tarehe 11/03/2014
SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA
(SURA YA 83)
______
KANUNI
______
(Zimetungwa chini ya kifungu cha 26(1))
______
KANUNI ZA BUNGE MAALUM ZA MWAKA 2014
_________
SEHEMU YA KWANZA
UTANGULIZI
1. Jina.
2. Matumizi.
3. Tafsiri.
SEHEMU YA PILI
HAKI NA KINGA YA BUNGE MAALUM
4. Haki na kinga ya Bunge Maalum.
SEHEMU YA TATU
MKUTANO NA VIKAO VYA BUNGE MAALUM
5. Utaratibu wa ukaaji ndani ya Ukumbi wa Mkutano
wa Bunge Maalum na mahudhurio ya Wajumbe.
ISSN 0856-0100X
SPECIAL SUPPLEMENT
No. 3 11th March, 2014
to the Gazette of the United Republic of Tanzania No.14 Vol.95 dated 11th March, 2014
Printed by the Government Printer Dodoma, by Order of the Government
iii
6. Mkutano wa Bunge Maalum.
7. Shughuli za Mkutano wa Bunge Maalum.
8. Utaratibu wa kumchagua Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti.
9. Kiapo cha Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti.
10. Kiapo cha Mjumbe.
11. Wimbo wa Taifa.
12. Dua ndani ya Bunge Maalum.
13. Vikao vya Bunge Maalum.
14. Muda wa vikao vya Bunge Maalum.
15. Wajibu wa Mjumbe kuhudhuria vikao vya Bunge
Maalum.
SEHEMU YA NNE
UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA BUNGE MAALUM
(a) Viongozi wa Bunge Maalum
16. Mwenyekiti na mamlaka yake.
17. Majukumu ya Makamu Mwenyekiti.
18. Uadilifu kwa viongozi wa Bunge Maalum.
19. Kumwondoa Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti
madarakani.
20. Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum.
21. Kazi na majukumu ya Katibu wa Bunge Maalum.
22. Naibu Katibu na majukumu yake.
(b) Watumishi wa Bunge Maalum
23. Watumishi wa Bunge Maalum.
24. Mpambe wa Bunge Maalum na majukumu yake.
(c) Uendeshaji wa Shughuli
25. Shughuli za kila siku.
26. Upangaji wa muda wa kutekeleza shughuli.
(d) Mpangilio wa Shughuli
27. Mpangilio wa Shughuli za Bunge Maalum.
28. Taarifa ya Mwenyekiti.
Kanuni za Bunge Maalum
iv
29. Haki za Bunge Maalum.
(e) Uhalali wa Shughuli
30. Akidi ya vikao vya Bunge Maalum.
(f) Utaratibu wa Kuwasilisha Rasimu ya Katiba
31. Utaratibu wa kuwasilisha Rasimu ya Katiba.
32. Rasimu ya Katiba kupelekwa kwenye Kamati.
32A. Utaratibu wa majadiliano kwenye Kamati.
32B. Mambo yasiyoruhusiwa kwenye Kamati.
32C. Staha ndani ya Kamati.
32D. Mamlaka kuhusu amani na utulivu kwenye Kamati.
(g) Utaratibu wa Kuwasilisha, Kujadili na Kupitisha Hoja
33. Uwasilishaji wa Hoja ya Kamati.
34. Masharti kuhusu mapendekezo ya Kamati.
35. Utaratibu wa majadiliano wakati wa kujadili taarifa
ya Kamati.
36. Utaratibu wa kupiga kura Ibara kwa Ibara.
37. Utaratibu wa kufanya uamuzi.
38. Utaratibu wa kupiga kura.
39. Utaratibu wa kupiga kura na kupitisha masharti ya
Rasimu ya Mwisho ya Katiba.
40. Utaratibu wa kupitisha Rasimu ya Mwisho ya Katiba.
41. Hoja ya kuwasilisha Rasimu ya mwisho ya Katiba.
42. Masahihisho ya uchapaji.
43. Uwasilishaji wa Katiba inayopendekezwa kwa Rais
na Rais wa Zanzibar.
SEHEMU YA TANO
KANUNI ZA MAJADILIANO
44. Nyakati za Mjumbe kusema kwenye Bunge
Maalum.
45. Jinsi ya kupata nafasi ya kusema kwenye Bunge
Maalum.
46. Mambo yasiyoruhusiwa kwenye Bunge Maalum.
Kanuni za Bunge Maalum
v
46A. Wajibu wa Mjumbe kusema ukweli.
47. Muda wa kusema ndani ya Bunge Maalum.
48. Kusema zaidi ya mara moja.
49. Staha ndani ya Bunge Maalum.
50. Mamlaka ya Mwenyekiti kuhutubia wakati wa
majadiliano.
51. Haki ya kuomba na kupata ufafanuzi.
52. Taarifa kuhusu utaratibu na Mwongozo wa
Mwenyekiti.
53. Vikao vya mashauriano.
SEHEMU YA SITA
KAMATI ZA BUNGE MAALUM
54. Kamati.
55. Muundo wa Kamati.
56. Utaratibu wa vikao na akidi katika Kamati.
57. Vikao vya Kamati kufanyika kwa faragha.
58. Muundo na majukumu ya Kamati ya Uongozi.
59. Majukumu ya Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge
Maalum.
60. Majukumu ya Kamati ya Uandishi.
61. Majukumu ya Kamati ya Mashauriano.
62. Majukumu ya Kamati Namba Moja hadi Namba
Kumi na Mbili.
63. Upangaji wa ratiba ya utekelezaji wa kazi na
majukumu ya Bunge Maalum.
64. Utaratibu wa kufanya uamuzi katika Kamati.
65. Wajibu wa Mjumbe kuhudhuria vikao na ukomo wa
Kamati.
SEHEMU YA SABA
UTARATIBU WA KUTUNGA MASHARTI YA MPITO NA
MASHARTI YATOKANAYO
66. Utaratibu wa kutunga masharti ya mpito na
masharti yatokanayo.
Kanuni za Bunge Maalum
vi
SEHEMU YA NANE
AMANI NA UTULIVU BUNGENI
67. Mamlaka ya Mwenyekiti kusimamia utaratibu.
68. Adhabu zinazoweza kutolewa na Mwenyekiti kwa
ukiukwaji wa Kanuni.
69. Adhabu zinazoweza kutolewa na Bunge Maalum
kwa ukiukaji wa Kanuni.
70. Mamlaka kuhusu amani na utulivu katika Bunge
Maalum.
71. Masharti kwa Mjumbe aliyesimamishwa kuhudhuria
vikao.
72. Mamlaka ya msamaha wa Mwenyekiti.
73. Udhibiti wa fujo kwenye Bunge Maalum.
74. Wajibu wa Mjumbe kutunza amani na utulivu
kwenye Bunge Maalum.
SEHEMU YA TISA
WAGENI
75. Mgeni Rasmi.
76. Ruhusa ya Wageni kwenye Bunge Maalum.
77. Ruhusa kwa Waandishi wa Habari.
SEHEMU YA KUMI
USALAMA WA MAENEO YA BUNGE MAALUM
78. Utaratibu wa kuingia Maeneo ya Bunge Maalum.
79. Upekuzi.
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
MENGINEYO
80. Lugha Rasmi ndani ya Bunge Maalum.
81. Taarifa Rasmi za Bunge Maalum.
82. Mavazi yanayoruhusiwa.
83. Ufafanuzi kutoka Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
84. Nafasi ya Mjumbe kuwa wazi.
Kanuni za Bunge Maalum
vii
85. Kutengua Kanuni.
86. Matumizi ya Ukumbi wa Mkutano wa Bunge
Maalum.
87. Kufanya mabadiliko au marekebisho katika Kanuni.
_________
NYONGEZA
__________
Kanuni za Bunge Maalum

Kanuni za Bunge Maalum
1
SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA
(SURA YA 83)
_________
KANUNI ZA BUNGE MAALUM ZA MWAKA 2014
__________
[Zimetungwa Chini ya Kifungu cha 26(1)]
___________
SEHEMU YA KWANZA
UTANGULIZI
1. Kanuni hizi zitaitwa Kanuni za Bunge Maalum za Mwaka
2014 na zitaanza kutumika baada ya kupitishwa na Bunge
Maalum.
2.-(1) Bila kuathiri masharti ya Sheria, Kanuni hizi zitatumika
kwa mambo yote yanayohusu utaratibu wa uendeshaji wa
shughuli za Bunge Maalum.
(2) Iwapo jambo au shughuli yoyote haikuwekewa masharti
katika Kanuni hizi, Mwenyekiti ataamua utaratibu wa kufuata
katika jambo au shughuli hiyo, kwa kuzingatia Sheria, sheria
nyingine za nchi, na uzoefu wa uendeshaji wa shughuli za
bunge au mabunge maalum ya nchi nyingine.
(3) Utaratibu utakaowekwa kwa mujibu wa fasili ya (2)
utatumika kama sehemu ya Kanuni hizi katika kuongoza
uendeshaji wa shughuli za Bunge Maalum.
3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama maelezo yanahitaji
vinginevyo-
“Akidi” maana yake ni idadi ya Wajumbe inayoruhusiwa kwa
madhumuni ya kuanza kikao cha Bunge Maalum, Kamati au
kufanya maamuzi ya Bunge Maalum au ya Kamati ya Bunge
Maalum;
Jina
Matumizi
Tafsiri
Kanuni za Bunge Maalum
2
“Bunge Maalum” maana yake ni Bunge Maalum la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania lililoundwa chini ya kifungu cha
22 cha Sheria;
“Gazeti” maana yake ni Gazeti la Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania;
“Hoja” maana yake ni pendekezo mahsusi lililotolewa na
Kamati au Mjumbe kwa ajili ya kupata uamuzi wa Bunge
Maalum kuhusu kurekebisha, kuboresha au kubadilisha
masharti ya Rasimu ya Katiba au jambo lolote linalotakiwa
kutolewa uamuzi na Kamati au Bunge Maalum;
“Kamati” maana yake ni Kamati yoyote ya Bunge Maalum
iliyoundwa kwa mujibu wa Kanuni hizi;
“Katiba inayopendekezwa” maana yake ni Rasimu ya Katiba
iliyopitishwa na Bunge Maalum kwa ajili ya kupigiwa kura ya
maoni;
“Katibu” maana yake ni Katibu au Naibu Katibu aliyetajwa
katika Kifungu cha 24(1) cha Sheria na inajumuisha mtumishi
mwingine yeyote wa Bunge Maalum aliyeidhinishwa
kutekeleza kazi za Katibu;
“Kikao” maana yake ni kikao cha siku moja cha Mkutano
wa Bunge Maalum na kinajumuisha kikao cha Kamati;
“Kitabu cha Maamuzi” maana yake ni kitabu cha
kumbukumbu ya maamuzi mbalimbali ya Mwenyekiti kuhusu
suala lolote la utaratibu katika Bunge Maalum;
“Maeneo ya Bunge Maalum” maana yake ni eneo lote la
ukumbi unaotumika kuendesha Mkutano wa Bunge Maalum,
ofisi, vyumba, maeneo ya mahojiano baina ya Wajumbe na
watu wengine, kumbi, bustani, viwanja na maeneo yote
mengine yanayotumiwa kuendesha shughuli za Bunge
Maalum au Kamati zake;
Kanuni za Bunge Maalum
3
“Mamlaka ya Bunge Maalum” maana yake ni mamlaka ya
Bunge Maalum kama yalivyotajwa katika kifungu cha 25 cha
Sheria;
“Maisha ya Bunge Maalum” maana yake ni muda wote
unaoanzia tarehe ambayo Bunge Maalum limeitishwa na Rais
likutane kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 22(4) cha
Sheria na kuishia tarehe ya kuvunjwa kwake kwa mujibu wa
masharti ya kifungu cha 28 cha Sheria;
“Mgeni” maana yake ni mtu yeyote ambaye si Mjumbe,
Katibu au mtumishi yeyote wa Bunge Maalum, na ambaye
hatekelezi kazi rasmi zinazohusu Bunge Maalum;
“Mgeni maalum” maana yake ni mgeni maalum aliyealikwa
kwenye Bunge Maalum kwa mujibu wa kanuni ya 75(3);
“Mgeni Rasmi” maana yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano
au Rais wa Zanzibar aliyealikwa na Mwenyekiti kulihutubia
Bunge Maalum;
“Maoni ya walio wachache” maana yake ni maoni
yaliyoandaliwa na Wajumbe wachache wa Kamati ambao
hawakuafiki maoni ya Wajumbe wa Kamati walio wengi;
“Mjumbe” maana yake ni Mjumbe kwa mujibu wa masharti
ya kifungu cha 22 cha Sheria;
“Mkutano wa Bunge Maalum” maana yake ni mfululizo wa
vikao vya Bunge Maalum kuanzia kikao cha kwanza hadi
cha mwisho, vinavyopangwa kwa ajili ya Bunge Maalum
kujadili na kufanya uamuzi kuhusu jambo au hoja mahsusi
iliyowekwa kwenye Orodha ya Shughuli kwa kuzingatia ratiba
ya shughuli za Bunge Maalum iliyowekwa kwa mujibu wa
Kanuni hizi;
“Mpambe wa Bunge Maalum” maana yake ni mtumishi wa
Bunge Maalum anayetekeleza majukumu yaliyoainishwa
katika Kanuni ya 24 ya Kanuni hizi;
Kanuni za Bunge Maalum
4
Sura
ya 83
“Mwenyekiti” maana yake ni Mjumbe aliyechaguliwa kuwa
Mwenyekiti kwa mujibu wa kifungu cha 23 cha Sheria na
inamjumuisha Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum;
“Mwenyekiti wa Kamati” maana yake ni Mjumbe yeyote
aliyechaguliwa kuongoza Kamati au Kamati Ndogo ya
Kamati na anajumuisha Makamu Mwenyekiti wa Kamati;
“Mwenyekiti wa Muda” maana yake ni Mjumbe
aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Muda kwa mujibu wa
Kifungu cha 22A cha Sheria;
“Mwenyekiti wa Tume” maana yake ni Mwenyekiti wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba iliyoundwa chini ya kifungu cha 5
cha Sheria;
“Orodha ya Shughuli” maana yake ni Waraka mahsusi
unaoonyesha mpangilio wa Shughuli za Bunge Maalum katika
kila kikao cha Bunge Maalum;
“Rais” maana yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania;
“Rasimu ya Katiba” maana yake ni Rasimu ya Katiba ambayo
imetayarishwa na Tume chini ya Sheria;
“Rasimu ya mwisho ya Katiba” maana yake ni Rasimu ya
Katiba iliyoandaliwa na Kamati ya Uandishi ili iwasilishwe
kwenye Bunge Maalum;
“Sekretarieti” maana yake ni watumishi wa Bunge Maalum
waliochaguliwa kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 24(5)
na (6) cha Sheria;
“Sheria” maana yake ni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba;
“Taarifa Rasmi” maana yake ni taarifa za majadiliano ya
Bunge Maalum zilizotajwa kwenye Kanuni hizi na zinajumuisha
taarifa za majadiliano ya Kamati;
Kanuni za Bunge Maalum
5
Haki na
kinga ya
Bunge
Maalum
“Tume” maana yake ni Tume ya Mabadiliko ya Katiba
iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 5 cha Sheria kwa
madhumuni ya kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi
kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba;
“Wajumbe wenye mahitaji maalum” maana yake ni
Wajumbe wenye ulemavu, wazee, wagonjwa, wanawake
wajawazito ambao wanahitaji huduma maalum;
“Wimbo wa Taifa” maana yake ni Wimbo wa Taifa wa Jamhuri
ya Muungano.
SEHEMU YA PILI
HAKI NA KINGA YA BUNGE MAALUM
4.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo na maoni katika
mijadala ya Bunge Maalum na maoni ya Mjumbe
hayatahojiwa mahakamani au sehemu yoyote nje ya Bunge
Maalum.
(2) Bila kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi, kila Mjumbe
atatekeleza majukumu yake kwa uhuru, na hatashurutishwa,
hatashinikizwa wala kupokea maelekezo kutoka kwa mtu au
chombo chochote.
(3) Bila kuathiri masharti ya Sheria au sheria nyingine yeyote,
Mjumbe yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai
mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au
kulifanya ndani ya Bunge Maalum linalohusiana na utekelezaji
wa mamlaka ya Bunge Maalum.
(4) Mjumbe yeyote hatashitakiwa wala kufunguliwa shauri
la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema
au alilolifanya katika kutekeleza uamuzi wowote wa Bunge
Maalum au wa Kamati yoyote ya Bunge Maalum.
(5) Mjumbe yeyote hatakamatwa kwa sababu ya shauri
lolote la madai, isipokuwa kwa kosa la jinai, ambapo
Mwenyekiti ataarifiwa kuhusu kukamatwa huko na sababu
zake.
Kanuni za Bunge Maalum
6
(6) Mjumbe yeyote atakuwa na haki ya kupatiwa taarifa au
nyaraka kwa ajili ya kumwezesha kutekeleza majukumu yake
kwa mujibu wa Sheria na Kanuni hizi.
(7) Mjumbe yeyote atakayehitaji kupata taarifa au nyaraka
chini ya fasili ya (6) atawasilisha maombi yake kwa maandishi
kwa Katibu akiainisha taarifa au nyaraka anazozihitaji na
Katibu atachukua hatua za upatikanaji wa taarifa au nyaraka
hizo.
SEHEMU YA TATU
MKUTANO NA VIKAO VYA BUNGE MAALUM
5.-(1) Mara baada ya kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge
Maalum, kila Mjumbe atakaa mahala pake, kwa mujibu wa
utaratibu maalum wa ukaaji wa Wajumbe ndani ya Ukumbi
wa Mkutano utakaokuwa umewekwa na Katibu.
(2) Bila kuathiri masharti ya fasili ya (1), kila Mjumbe atatakiwa
kuweka saini au kwa Mjumbe mwenye mahitaji maalum
kuweka alama ya dole gumba kwenye karatasi ya
mahudhurio itakayoandaliwa kwa madhumuni hayo.
(3) Wapambe wa Bunge Maalum, watumishi wa Bunge
Maalum, wasaidizi wa Wajumbe wenye mahitaji maalum na
waandishi wa habari watakaa sehemu ambazo zimetengwa
kwa ajili yao.
(4) Wageni mashuhuri, Mabalozi na Viongozi wengine
watakaa sehemu maalum kama itakavyopangwa na Katibu.
(5) Wageni wengine watatengewa sehemu maalum ya
kukaa.
6.-(1) Mkutano wa Bunge Maalum utaanza tarehe, siku na
mahali ambapo Rais ataagiza kwa mujibu wa masharti ya
kifungu cha 22(4) cha Sheria.
(2) Bila kuathiri masharti ya Sheria na masharti ya Kanuni hizi
kuhusu kuanza na kukoma kwa Mkutano wa Bunge Maalum,
Utaratibu
wa ukaaji
ndani ya
Ukumbi wa
Mkutano
wa Bunge
Maalum na
mahudhurio
ya
Wajumbe
Mkutano
wa Bunge
Maalum
Kanuni za Bunge Maalum
7
vikao vya Bunge Maalum vitaendelea kwa muda wowote
ambao utahitajika kwa ajili ya kutekeleza na kukamilisha
shughuli zote za Mkutano wa Bunge Maalum.
7.-(1) Shughuli za Mkutano wa Bunge Maalum zitakuwa kama
ifuatavyo:
(a) kusomwa kwa Tangazo la Rais la kuitisha Bunge Maalum;
(b) uchaguzi wa Mwenyekiti wa muda;
(c) kuandaa na kupitisha Kanuni za Bunge Maalum;
(d) uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti;
(e) kiapo cha Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti;
(f) kiapo cha Wajumbe;
(g) hotuba ya ufunguzi ya Mgeni Rasmi;
(h) uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba;
(i) kujadili taarifa na hoja za Kamati;
(j) kupitisha Rasimu ya Mwisho ya Katiba; na
(k) shughuli nyingine yoyote ambayo Bunge Maalum litaona
inafaa kufanywa au kutekelezwa kwa wakati huo.
(2) Kutakuwa na vikao mbalimbali kwa lengo la kukamilisha
shughuli za Mkutano wa Bunge Maalum.
(3) Mwanzoni mwa Mkutano wa Bunge Maalum, Katibu wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano au Katibu wa Baraza la
Wawakilishi, atasoma Tangazo la Rais la kuliitisha Bunge
Maalum.
(4) Mara baada ya Tangazo la Rais kusomwa kwa mujibu
wa fasili ya (3), Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na
Katibu wa Baraza la Wawakilishi kwa pamoja watasimamia
uchaguzi wa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum kwa
utaratibu watakaoona unafaa.
(5) Baada ya Mwenyekiti wa Muda kupatikana, Bunge
Maalum litafanya shughuli ya kuandaa na kupitisha Kanuni
za Bunge Maalum zinazoweka utaratibu wa kuendesha
shughuli zake.
(6) Bila kujali masharti ya fasili ya (7), Kanuni zilizopitishwa
kwa mujibu wa fasili ya (5) zitaanza kutumika mara moja
Shughuli za
Mkutano wa
Bunge
Maalum
T.L.S
Na. 31
la tarehe
14/02/2014
Kanuni za Bunge Maalum
8
kuendesha Shughuli za Bunge Maalum, baada ya nakala
zake kugawanywa kwa Wajumbe.
(7) Kanuni za Bunge Maalum zitachapishwa kwenye Gazeti.
8.-(1) Kutakuwa na uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti utakaofanyika katika Mkutano wa Bunge
Maalum, mara baada ya Bunge Maalum kuandaa na
kupitisha Kanuni zake.
(2) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watachaguliwa
kutoka miongoni mwa Wajumbe kwa kuzingatia masharti ya
kifungu cha 23(4) cha Sheria na Kanuni zilizoainishwa katika
Nyongeza ya Kanuni hizi.
(3) Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti
utafanyika na kuendeshwa kwa mujibu wa masharti ya
kifungu cha 23 cha Sheria, masharti ya Kanuni hizi na kwa
kuzingatia Kanuni za uchaguzi zilizowekwa na Nyongeza ya
Kanuni hizi.
(4) Endapo itatokea kuwa nafasi ya Mwenyekiti au Makamu
Mwenyekiti iwazi, uchaguzi utaitishwa kwa ajili ya kumchagua
Mjumbe wa kuziba nafasi hiyo, na Mjumbe huyo atatoka
upande wa Jamhuri ya Muungano alikokuwa ametokea
mtangulizi wake.
9.-(1) Mjumbe yeyote aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti au
Makamu Mwenyekiti, kabla ya kushika madaraka yake,
ataapa mbele ya Katibu kiapo cha ujumbe na kiapo cha
Mwenyekiti.
(2) Kiapo cha Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kitakuwa
katika sehemu mbili kama ifuatavyo:
(a) Kiapo cha Mjumbe:
“Mimi………………………….………………………….……
niliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum, naapa/
Utaratibu
wa
kumchagua
Mwenyekiti
na
Makamu
Mwenyekiti
Kiapo cha
Mwenyekiti
na
Makamu
Mwenyekiti
Kanuni za Bunge Maalum
9
nathibitisha kwamba nitakuwa mwaminifu na mtiifu kwa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kadri ya uwezo
na ufahamu wangu, nitatimiza wajibu wangu na kufanya kazi
zinazonihusu bila ya upendeleo. Ewe Mwenyezi Mungu
nisaidie.”
(b) Kiapo cha Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti:
“Mimi……………………………….……………………………
niliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa
Bunge Maalum, naapa/nathibitisha kwamba nitakuwa
mwaminifu na mtiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na kwa kadri ya uwezo na ufahamu wangu, nitatimiza wajibu
wangu na kufanya kazi zinazonihusu bila ya upendeleo. Ewe
Mwenyezi Mungu nisaidie”.
(3) Wakati wa kuapa au kula yamini, Mwenyekiti au Makamu
Mwenyekiti anayeamini kuwa kuna Mungu, atashika kitabu
kitakatifu kinachotambuliwa na imani ya dini yake.
(4) Iwapo Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti haamini kuwa
kuna Mungu, basi hatashika kitabu chochote kitakatifu wala
kutamka maneno “Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie”, bali
atainua juu mkono wake wa kulia na kutamka maneno ya
kiapo kwa mujibu wa kanuni hii.
(5) Iwapo Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti-
(a) anamwamini Mungu lakini katika imani yake hatumii
kitabu kitakatifu; au
(b) anamwamini Mungu na anatumia kitabu kitakatifu lakini
kutokana na imani ya dini yake hawezi kushika kitabu hicho,
basi, wakati wa kuapa au kula yamini atainua juu mkono
wake wa kulia na kutamka maneno ya kiapo kwa mujibu wa
fasili ya (2)(a) na (b).
10.-(1) Kila Mjumbe ataapa au kula yamini mbele ya
Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti kwa kutamka maneno
yafuatayo:
Kiapo
cha
Mjumbe
Kanuni za Bunge Maalum
10
“Mimi ……………………… niliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa
Bunge Maalum, naapa/nathibitisha kwamba nitakuwa
mwaminifu na mtiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na kwa kadri ya uwezo na ufahamu wangu, nitatimiza wajibu
wangu na kufanya kazi zinazonihusu bila ya upendeleo, na
bila ya kukiuka Sheria za nchi. Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.”
(2) Wakati wa kuapa au kula yamini, Mjumbe anayeamini
kuwa kuna Mungu, atashika kitabu kitakatifu
kinachotambuliwa na imani ya dini yake:
Isipokuwa kama Mjumbe atakuwa katika mazingira
yanayomzuia kushika kitabu kitakatifu, hatashika kitabu hicho
na badala yake atainua mkono wake wa kulia juu na
kutamka maneno ya kiapo kwa mujibu wa kanuni hii.
(3) Iwapo Mjumbe haamini kuwa kuna Mungu, basi hatashika
kitabu chochote kitakatifu wala kutamka maneno “Ewe
Mwenyezi Mungu nisaidie”, bali atainua mkono wake wa kulia
juu na kutamka maneno ya kiapo kwa mujibu wa kanuni hii.
(4) Utaratibu wa kuapa au kula yamini unaweza kufanyika
kwa mujibu wa Orodha ya majina ya Wajumbe iliyoandaliwa
kwa ajili hiyo.
11.-(1) Baada ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kushika
madaraka yao na Wajumbe kuapishwa, Wimbo wa Taifa
utaimbwa kuashiria kuanza rasmi kwa shughuli za Bunge
Maalum, na pia baada ya Kikao cha mwisho cha Mkutano
wa Bunge Maalum, kuashiria kukamilika kwa Shughuli za
Bunge Maalum.
(2) Wakati Wimbo wa Taifa unaimbwa, kila Mjumbe na mtu
yeyote mwenye uwezo wa kusimama aliyepo ndani ya
Ukumbi wa Mkutano wa Bunge Maalum, atasimama mahali
alipo kwa staha na utulivu, kama ilivyo mila na desturi ya
kutoa heshima kwa Wimbo wa Taifa unapoimbwa.
Wimbo
wa Taifa
Kanuni za Bunge Maalum
11
12.-(1) Kutakuwa na dua ya kuiombea Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na kuliombea Bunge Maalum kila siku kabla ya
kuanza Kikao cha Bunge Maalum, na dua ya kushukuru kila
siku kabla ya kuahirisha kikao hicho.
(2) Dua iliyoainishwa katika fasili ya (1) itasomwa na
Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti au Mjumbe mwingine
yeyote atakayekuwa anaongoza Kikao cha Bunge Maalum
na itakuwa na maneno yafuatayo:
(a) dua ya kuiombea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Bunge Maalum:
“Ewe MWENYEZI MUNGU Mtukufu, Muumba Mbingu na Dunia,
umeweka Mataifa katika Dunia, ili haki yako itendeke.
Twakuomba uibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
idumishe uhuru, umoja, haki na amani.
Utujaalie hekima na busara, sisi Wajumbe wa Bunge hili
Maalum ili tuwe na uwezo wa kujadili kwa dhati mambo
yatakayoletwa mbele yetu leo, na kufanya maamuzi sahihi
kwa manufaa ya watu wote na ustawi wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Amin.”
(b) dua ya kushukuru:
“Ewe MWENYEZI MUNGU Mtukufu, Muumba Mbingu na Dunia,
tunashukuru kwa kutuongoza katika kikao hiki tukaweza
kujadili kwa dhati mambo yaliyoletwa mbele yetu leo, na
kufanya maamuzi sahihi kwa manufaa ya watu wote na
ustawi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunakuomba
tunapotoka katika ukumbi huu utupe ulinzi wako na utujalie
Baraka zako. Amin.”
(3) Wakati dua ya kuiombea Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na kuliombea Bunge Maalum na dua ya kushukuru
itakapokuwa inasomwa, kila Mjumbe mwenye uwezo wa
kusimama aliye ndani ya ukumbi wa Mkutano wa Bunge
Maalum atasimama kwa staha na utulivu mahali alipo kama
ilivyo mila na desturi ya kutoa heshima kwa dua.
Dua
ndani
ya Bunge
Maalum
Kanuni za Bunge Maalum
12
13.-(1) Isipokuwa kama itaelekezwa vinginevyo, kila kikao cha
Bunge Maalum kitafanyika katika ukumbi wa Mkutano wa
Bunge Maalum ulioandaliwa kwa ajili hiyo.
(2) Bila kuathiri masharti ya Sheria na masharti ya Kanuni hizi,
kila kikao cha Bunge Maalum, kitaanza siku, tarehe na wakati
utakaowekwa na Bunge Maalum.
14.-(1) Kila siku kuanzia Jumatatu mpaka Alhamisi, vikao vya
Mkutano wa Bunge Maalum, vitaanza saa tatu asubuhi hadi
saa saba mchana ambapo Mwenyekiti atasitisha shughuli
yoyote itakayokuwa inafanyika hadi saa kumi jioni, isipokuwa
kama Bunge Maalum litaamua vinginevyo.
(2) Bila kujali masharti ya fasili ya (1), Mwenyekiti akiona
inafaa, Bunge Maalum linaweza kuendelea kukutana kwa
muda usiozidi dakika thelathini, au kuahirishwa wakati
wowote kabla ya saa saba mchana, baada ya kuwahoji
Wajumbe.
(3) Bila kujali masharti ya fasili ya (1), Bunge Maalum kwa siku
ya Ijumaa litakutana kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa
sita mchana ambapo Mwenyekiti ataahirisha shughuli za siku
hiyo hadi saa kumi jioni.
(4) Hoja ya kubadilisha nyakati za vikao inaweza kutolewa
na Mjumbe yeyote na itaamuliwa kwa kulihoji Bunge Maalum
na haitahitaji kutolewa taarifa.
(5) Bunge Maalum litakaporejea saa kumi jioni litaendelea
kukutana hadi saa mbili usiku, wakati ambapo Mwenyekiti
atasitisha shughuli na kuliahirisha hadi siku inayofuata au siku
nyingine atakayoitaja.
(6) Endapo shughuli zilizopangwa kwa siku hiyo zimemalizika
kabla ya saa mbili usiku, Mwenyekiti ataliahirisha Bunge
Maalum bila kuhoji, lakini iwapo zimesalia dakika kumi kabla
ya kufikia muda wa kuliahirisha, na Bunge Maalum bado
halijamaliza shughuli zake, Mwenyekiti anaweza kuongeza
Vikao
vya Bunge
Maalum
Muda wa
vikao vya
Bunge
Maalum
Kanuni za Bunge Maalum
13
muda usiozidi dakika thelathini, bila kulihoji Bunge Maalum,
ili kukamilisha shughuli zilizobaki.
(7) Iwapo muda wa kuahirisha shughuli za Bunge Maalum
umefika na Mwenyekiti atakuwa analihoji au yupo karibu
kulihoji Bunge Maalum, Mwenyekiti basi hatasitisha shughuli
hadi hoja iwe imeamuliwa, na baada ya hoja kuamuliwa,
Mwenyekiti ataliahirisha Bunge Maalum hadi siku inayofuata
au siku nyingine atakayoitaja.
(8) Majadiliano yoyote ya Bunge Maalum yaliyositishwa na
Mwenyekiti kwa mujibu wa masharti ya Kanuni hii,
yataendelea wakati Bunge Maalum litakaporejea, na
yataanzia pale yalipositishwa, na Mjumbe yeyote ambaye
maelezo yake yalikatizwa na Mwenyekiti, atakuwa na haki
ya kuendelea na maelezo yake katika marudio ya mjadala
huo, na endapo Mjumbe hatoitumia haki yake hiyo, basi
atahesabiwa kuwa alikuwa amemaliza kutoa maelezo yake.
(9) Iwapo shughuli zilizopangwa kwa ajili ya kikao cha siku
hiyo hazijamalizika, na Mjumbe akatoa hoja ya kuahirisha
kikao kutokana na dharura, Mwenyekiti atalihoji Bunge
Maalum kuhusu hoja ya kuahirisha kikao hicho na baada ya
hoja hiyo kuafikiwa, atakiahirisha kikao hicho hadi kikao
kinachofuata ambacho, kama Bunge Maalum halikuamua
vinginevyo, kitakuwa ni siku itakayofuata, isipokuwa tu kama
itakuwa ni siku ya Jumapili.
15.-(1) Kila Mjumbe atakuwa na wajibu wa kuhudhuria vikao
vyote vya Bunge Maalum na vya Kamati aliyopangiwa na
atasaini binafsi karatasi ya mahudhurio iliyoandaliwa kwa
madhumuni hayo.
(1A) Kila baada ya kikao cha Bunge Maalum, Katibu wa
Bunge Maalum atakusanya karatasi ya mahudhurio kama
uthibitisho wa mahudhurio ya Wajumbe katika Bunge
Maalum kwa siku hiyo.
Wajibu wa
Mjumbe
kuhudhuria
vikao vya
Bunge
Maalum
Azimio la
Bunge
Maalum
la tarehe
05/08/2014
Kanuni za Bunge Maalum
14
(2) Mjumbe yeyote mwenye udhuru, atalazimika kutoa taarifa
ya maandishi kwa Mwenyekiti na nakala kwa Mwenyekiti wa
Kamati na Katibu kuhusu kutohudhuria kwake, na taarifa hiyo
itahifadhiwa na Kamati kwa ajili ya kumbukumbu.
(3) Bila kuathiri fasili ya (2), Mjumbe yeyote ambaye
hatahudhuria kikao chochote cha Bunge Maalum hatalipwa
posho ya kikao, na endapo atakuwa amelipwa posho ya
kujikimu na ikabainika kuwa hakuhudhuria kikao au vikao
husika, basi posho hiyo itakatwa kutoka katika malipo ya
Mjumbe huyo yanayofuata.
(4) Kwa kuzingatia kwamba, kuhudhuria vikao vya Bunge
Maalum na Kamati zake ni wajibu wa kwanza wa kila
Mjumbe, mtu au chombo cha sheria kitakachomkamata na
kumzuia Mjumbe yeyote kuhudhuria vikao vya Bunge Maalum
kitalazimika kutoa taarifa ya maandishi kwa Mwenyekiti
kuhusu kukamatwa na kuzuiliwa kwa Mjumbe huyo na
sababu zake.
SEHEMU YA NNE
UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA BUNGE MAALUM
(a) Viongozi wa Bunge Maalum
16.-(1) Mwenyekiti atakuwa ndiye kiongozi mkuu wa Bunge
Maalum, na majukumu yake yatakuwa ni:
(a) kuongoza Mkutano na vikao vya Bunge Maalum;
(b) kuongoza mwenendo na utaratibu wa majadiliano katika
Mkutano na vikao vya Bunge Maalum;
(c) kutoa uamuzi kuhusu masuala yote ya utaratibu katika
Mkutano na vikao vya Bunge Maalum;
(d) kusimamia amani na utulivu katika Mkutano na vikao vya
Bunge Maalum;
(e) kusimamia uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge
Maalum.
(2) Mwenyekiti atakuwa na madaraka na mamlaka ya
kutafsiri Kanuni hizi, na uamuzi wake kuhusu suala lolote la
utaratibu kwa mujibu wa Kanuni utakuwa wa mwisho.
Azimio
la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Mwenyekiti
na
mamlaka
yake
Kanuni za Bunge Maalum
15
(3) Bila kujali masharti ya fasili ya (2), Mjumbe asiyeridhika na
uamuzi wa Mwenyekiti uliotolewa atakuwa na haki ya
kuwasilisha kwa maandishi malalamiko yake kwa Katibu
ndani ya siku moja kuanzia tarehe ya uamuzi.
(4) Baada ya kupokea malalamiko chini ya fasili ya (3), Katibu
atawasilisha malalamiko kwenye Kamati ya Kanuni na Haki
za Bunge Maalum ambayo itasikiliza na kutoa uamuzi juu ya
malalamiko hayo ndani ya siku mbili.
(5) Mara baada ya uamuzi wa Kamati kuhusu malalamiko
yaliyowasilishwa chini ya fasili ya (4), Mwenyekiti wa Kamati
atatoa taarifa juu ya uamuzi huo ndani ya Bunge Maalum.
(6) Katika kutekeleza majukumu yake, Mwenyekiti
ataongozwa na Sheria pamoja na Kanuni hizi, na pale
ambapo Kanuni hazikutoa mwongozo, basi ataongozwa na
sheria nyingine za nchi pamoja na uzoefu wa nchi nyingine
katika uendeshaji bora wa shughuli za Bunge Maalum.
(7) Bila kuathiri masharti ya fasili ya (6), iwapo wakati wa
kufanya uamuzi, uzoefu wa nchi nyingine umetumika,
Mwenyekiti atataja nchi husika ambayo uzoefu huo
umepatikana.
(8) Mwenyekiti atawajibika kusimamia ipasavyo Kanuni zote
za Bunge Maalum, na katika kutekeleza wajibu huo, anaweza
kumtaka Mjumbe yeyote anayekiuka kanuni yoyote au
utaratibu uliowekwa na Kanuni hizi ajirekebishe mara moja.
(9) Wakati wowote ambapo Mwenyekiti hatakuwepo katika
Bunge Maalum, au kwa sababu nyingine yoyote hawezi
kutekeleza madaraka na majukumu ya Mwenyekiti,
madaraka na majukumu hayo yatatekelezwa na Makamu
Mwenyekiti.
(10) Nafasi ya Mwenyekiti itakuwa wazi endapo litatokea
tukio lolote kati ya matukio yafuatayo-
(a) atafariki;
Kanuni za Bunge Maalum
16
(b) atajiuzulu;
(c) atathibitishwa na Bodi ya Tiba kuwa amekosa uwezo wa
kutekeleza majukumu yake kwa sababu za kiafya;
(d) atatiwa hatiani kwa kosa ambalo adhabu yake ni kifungo
gerezani;
(e) atapoteza sifa ya kuteuliwa kuwa Mjumbe; au
(f) ataondolewa kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani
naye.
(11) Endapo nafasi ya Mwenyekiti itakuwa wazi kutokana
na sababu zilizoainishwa kwenye fasili ya (10), Makamu
Mwenyekiti ataendesha shughuli za Bunge Maalum kwa
kipindi kisichozidi siku mbili ili uchaguzi wa Mwenyekiti ufanyike
kwa mujibu wa Kanuni hizi.
17.-(1) Makamu Mwenyekiti atashika madaraka yake kwa
mujibu wa masharti ya Sheria na Kanuni hizi.
(2) Makamu Mwenyekiti atakuwa msaidizi wa Mwenyekiti
katika kuliongoza Bunge Maalum na atatekeleza majukumu
yake kwa mujibu wa masharti ya Kanuni hizi.
(3) Wakati wowote ambao Mwenyekiti hayupo katika Bunge
Maalum au kwa sababu nyingine yoyote hawezi kutekeleza
mamlaka na majukumu yake, basi mamlaka au majukumu
hayo yatatekelezwa na Makamu Mwenyekiti.
(4) Wakati wowote ambao Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti wote hawapo kwenye Bunge Maalum, au kwa
sababu nyingine yoyote hawawezi kutekeleza mamlaka na
majukumu yao, basi mamlaka na majukumu hayo
yatatekelezwa na Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa
Kamati mwenye sifa za kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa
Bunge Maalum.
(5) Nafasi ya Makamu Mwenyekiti itakuwa wazi endapo
litatokea tukio lolote kati ya matukio yafuatayo-
(a) atafariki;
(b) atajiuzulu;
Majukumu
ya
Makamu
Mwenyekiti
Kanuni za Bunge Maalum
17
(c) atathibitishwa na Bodi ya Tiba kuwa amekosa uwezo wa
kutekeleza majukumu yake kwa sababu za kiafya;
(d) atatiwa hatiani kwa kosa ambalo adhabu yake ni kifungo
gerezani;
(e) atapoteza sifa ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Bunge
Maalum; au
(f) ataondolewa kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani
naye.
(6) Endapo nafasi ya Makamu Mwenyekiti itakuwa wazi
kutokana na sababu zilizoainishwa kwenye fasili ya (5),
Mwenyekiti, kwa kipindi kisichozidi siku mbili ataitisha uchaguzi
wa Makamu Mwenyekiti kwa mujibu wa Kanuni hizi.
18.-(1) Kwa kuzingatia kiapo cha kazi yake kilichowekwa kwa
mujibu wa Sheria, na kwa madhumuni ya uendeshaji bora
wa shughuli za Bunge Maalum, Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti au Mjumbe yeyote atakayekuwa amechaguliwa
kutekeleza kazi na majukumu ya Mwenyekiti, ataendesha
shughuli za Bunge Maalum kwa kutoa uamuzi wa haki, uadilifu
na bila chuki wala upendeleo wowote, kwa kuongozwa na
Sheria, sheria nyingine za nchi, Kanuni hizi pamoja na uzoefu
wa nchi nyingine katika uendeshaji bora wa shughuli za Bunge
Maalum.
(2) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti hawatahudhuria
kikao cha kikundi chochote kinachowakilishwa katika Bunge
Maalum kinachojadili na kuweka msimamo juu ya suala lolote
linalojadiliwa au litakalojadiliwa na Bunge Maalum na
hawatafungwa na msimamo au makubaliano yaliyofikiwa
na kikao hicho.
19.-(1) Mjumbe yeyote anayetaka kuwasilisha taarifa ya hoja
ya kumwondoa Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti
madarakani, atawasilisha taarifa ya maandishi ya kusudio
hilo kwa Katibu akieleza sababu kamili ya kutaka kuleta hoja
hiyo.
(2) Taarifa kwa mujibu wa fasili ya (1) inapaswa kuungwa
mkono na kusainiwa na wajumbe wasiopungua theluthi moja
ya wajumbe wote wa Bunge Maalum.
Uadilifu
kwa
viongozi
wa Bunge
Maalum
Kumwondoa
Mwenyekiti
au
Makamu
Mwenyekiti
madarakani
Kanuni za Bunge Maalum
18
(3) Mara baada ya kupokea taarifa ya maandishi ya kusudio
hilo la kumwondoa Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti
iliyotimiza masharti ya fasili ya (1) na ya (2) ya kanuni hii, Katibu
atapeleka taarifa hiyo kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za
Bunge Maalum kwa ajili ya kuijadili.
(4) Endapo Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum
itaridhika kuwa zipo tuhuma mahsusi dhidi ya Mwenyekiti au
Makamu Mwenyekiti zinazohusu uvunjwaji wa masharti ya
Sheria au Kanuni hizi, basi Kamati hiyo itaidhinisha kuwa hoja
hiyo ipelekwe kwenye Bunge Maalum ili iamuliwe.
(5) Endapo hoja iliyowasilishwa chini ya fasili ya (1) itakuwa
ni ya kumwondoa Mwenyekiti madarakani, Makamu
Mwenyekiti atakalia kiti cha Mwenyekiti wakati wa kujadili
hoja hiyo na Mwenyekiti atakuwa na haki ya kujitetea wakati
wa mjadala.
(6) Endapo hoja iliyowasilishwa chini ya fasili ya (1) itakuwa
ni ya kumwondoa Makamu Mwenyekiti madarakani,
Mwenyekiti atakalia kiti wakati wa kujadili hoja hiyo na
Makamu Mwenyekiti atakuwa na haki ya kujitetea wakati
wa mjadala.
(7) Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti atakuwa
ameondolewa kwenye madaraka endapo zitapigwa kura
za siri kwa ajili hiyo na idadi ya kura zinazounga mkono azimio
la kumwondoa madarakani zitakuwa si chini ya zaidi ya nusu
ya idadi ya wajumbe wote wa Bunge Maalum.
(8) Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti anayetuhumiwa
anaweza kujiuzulu nafasi yake kwa kutoa maelezo ya kujiuzulu
ndani ya Bunge Maalum kabla ya uamuzi juu ya hoja ya
kumwondoa madarakani.
20. Katibu na Naibu Katibu kama walivyotajwa katika kifungu
cha 24 cha Sheria, kabla ya kushika madaraka yao, kila
mmoja wao ataapishwa na Rais kiapo kilichowekwa kwa
mujibu wa kifungu cha 24(7) cha Sheria.
Katibu na
Naibu
Katibu wa
Bunge
Maalum
Kanuni za Bunge Maalum
19
21.-(1) Katibu atahakikisha utekelezaji bora wa kazi na
majukumu ya Bunge Maalum, na kwa madhumuni hayo-
(a) atahudhuria au atawakilishwa na mtumishi yeyote wa
Bunge Maalum katika vikao vyote vya Bunge Maalum na
vikao vya Kamati yoyote ya Bunge Maalum;
(b) ataweka kumbukumbu zote zinazotakiwa ziwekwe kwa
mujibu wa Kanuni hizi;
(c) atatayarisha Taarifa Rasmi za majadiliano ya Bunge
Maalum kwa mujibu wa Kanuni hizi;
(d) atatayarisha kwa utaratibu wa siku hadi siku, kitabu cha
shughuli za Bunge Maalum na kukihifadhi ofisini kikiwa
kinaonesha yafuatayo:
(i) maagizo yoyote yaliyotolewa na Bunge Maalum;
(ii) shughuli zote zilizopangwa kufanywa siku yoyote ya
baadaye; na
(iii) taarifa zote za hoja zilizokubaliwa na Mwenyekiti.
(2) Katibu atahakikisha utekelezaji bora wa shughuli za Bunge
Maalum na kwa madhumuni hayo atatayarisha siku hadi siku,
Orodha ya Shughuli za Bunge Maalum kama
itakavyoelekezwa na Mwenyekiti.
(3) Katibu atatunza kumbukumbu za uamuzi wa Mwenyekiti
kuhusu masuala ya utaratibu katika Bunge Maalum, Kitabu
cha Maamuzi ya Mwenyekiti, Kitabu cha Shughuli, Taarifa
Rasmi za Majadiliano ya Bunge Maalum, nakala ya Rasimu
ya Katiba, na hati nyingine zilizowasilishwa katika Bunge
Maalum.
(4) Taarifa chini ya fasili ya (3) zitawekwa kwenye miundo au
mifumo inayofaa kwa watu wenye mahitaji maalum.
(5) Mwananchi yeyote anaweza kukagua kumbukumbu
zilizoainishwa katika fasili ya (3) wakati wowote unaofaa kwa
kufuata utaratibu utakaowekwa na Mwenyekiti.
Kazi na
majukumu
ya
Katibu
wa
Bunge
Maalum
Kanuni za Bunge Maalum
20
(6) Katibu atahakikisha kuwa ukumbi wa Mkutano wa Bunge
Maalum, kumbi za vikao vya Kamati za Bunge Maalum,
maeneo ya Bunge Maalum, huduma kwa Wajumbe na vifaa
vingine vinavyohusika na Shughuli za Bunge Maalum viko
katika hali nzuri na inayofaa kuliwezesha Bunge Maalum
kutekeleza kazi na majukumu yake ipasavyo.
22.-(1) Naibu Katibu atashika madaraka yake kwa mujibu wa
masharti ya Sheria na Kanuni hizi.
(2) Naibu Katibu atakuwa msaidizi wa Katibu katika
utekelezaji bora wa kazi na majukumu ya Bunge Maalum, na
katika utekelezaji wa kazi na majukumu ya Ofisi ya Katibu.
(3) Bila kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi, wakati
wowote ambao Katibu hatakuwepo au kwa sababu nyingine
yoyote hawezi kutekeleza madaraka na majukumu yake, basi
madaraka na majukumu hayo yatatekelezwa na Naibu
Katibu.
(4) Endapo wakati wowote Katibu na Naibu Katibu wote
hawapo kwenye Bunge Maalum, au kutokana na sababu
nyingine yoyote, hawawezi kutekeleza madaraka na
majukumu yao, basi madaraka na majukumu hayo
yatatekelezwa na mtumishi wa Bunge Maalum
atakayeteuliwa na Katibu kwa ajili hiyo.
(b) Watumishi wa Bunge Maalum
23.-(1) Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum,
watachagua watumishi kuunda Sekretarieti ya Bunge
Maalum, kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 24 cha
Sheria.
(2) Bunge Maalum litakuwa na watumishi kwa idadi na nafasi
za madaraka ambazo Katibu na Naibu Katibu wataona
inafaa kwa ajili ya utekelezaji bora wa kazi na majukumu ya
Bunge Maalum.
Naibu
Katibu
na
majukumu
yake
Watumishi
wa
Bunge
Maalum
Kanuni za Bunge Maalum
21
(3) Watumishi wa Bunge Maalum chini ya uongozi wa Katibu
na Naibu Katibu watatekeleza kazi na shughuli zote
zilizowekwa au zitakazokuwa ni muhimu kwa ajili ya
kuhakikisha utekelezaji bora wa shughuli za Bunge Maalum
kwa mujibu wa masharti ya Sheria na Kanuni hizi.
24.-(1) Kutakuwa na Mpambe wa Bunge Maalum ambaye
atatekeleza shughuli zifuatazo:
(a) kusimamia na kuratibu masuala yote ya ulinzi na usalama
wa mali, vifaa na Maeneo ya Bunge Maalum yanayotumika
kwa ajili ya kuendeshea shughuli za Bunge Maalum;
(b) kusimamia shughuli ya upekuzi wa Wajumbe wa Bunge
Maalum, wasaidizi wa Wajumbe wenye mahitaji maalum na
Watumishi wa Bunge Maalum pamoja na wageni
wanapoingia katika Maeneo ya Bunge Maalum na katika
ukumbi wa Mkutano wa Bunge Maalum;
(c) kuhakikisha utulivu na amani katika sehemu wanayokaa
wageni na atawawekea utaratibu maalum wa kuingia na
kutoka katika ukumbi wa Mkutano wa Bunge Maalum;
(d) kumtangulia Mwenyekiti wakati anapoingia na
anapotoka kwenye ukumbi wa Mkutano wa Bunge Maalum.
(2) Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake
chini ya fasili ya (1)(a) na (c) ya Kanuni hii, Mpambe wa Bunge
Maalum na wapambe wasaidizi watatekeleza majukumu yao
kwenye Mkutano wa Bunge Maalum.
(3) Mwenyekiti anaweza kutoa maagizo anayoona
yanastahili kutolewa kwa Mpambe wa Bunge Maalum au
msaidizi wake yeyote kwa mujibu wa Kanuni hizi na Mpambe
wa Bunge Maalum au msaidizi huyo atawajibika kutekeleza
maagizo hayo.
Mpambe
wa Bunge
Maalum
na
majukumu
yake
Kanuni za Bunge Maalum
22
(c) Uendeshaji wa Shughuli
25.-(1) Katibu ataandaa Orodha ya Shughuli za kila siku za
vikao vya Bunge Maalum, kwa mujibu wa maelekezo ya
Mwenyekiti baada ya kushauriana na Kamati ya Uongozi ya
Bunge Maalum na kugawa nakala kwa kila Mjumbe kabla
ya kikao husika.
(2) Nakala zitakazoandaliwa katika fasili ya (1) zitakuwa katika
miundo na mifumo inayozingatia mahitaji ya Wajumbe wenye
mahitaji maalum.
(3) Katibu, kwa maelekezo ya Mwenyekiti, baada ya
kushauriana na Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum,
anaweza kuandaa Nyongeza ya Orodha ya Shughuli, na
kugawa nakala kwa kila Mjumbe kabla au wakati wa kikao
husika.
(4) Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum iliyoundwa kwa
mujibu wa Kanuni hizi itamshauri Mwenyekiti kuhusu
uendeshaji bora wa shughuli za Bunge Maalum.
26.-(1) Mwenyekiti baada ya kushauriana na Kamati ya
Uongozi ya Bunge Maalum atapanga muda wa majadiliano
ya Bunge Maalum kwa kila jambo litakalowasilishwa kwenye
Bunge Maalum kwa ajili ya kujadiliwa na ambalo
halijawekewa muda na Kanuni hizi.
(2) Baada ya muda uliopangwa kwa mujibu wa fasili ya (1)
kuisha, Mwenyekiti baada ya kusitisha mjadala, ataliongoza
Bunge Maalum kupiga kura kwa ajili ya kupata uamuzi wa
Bunge Maalum kuhusiana na jambo hilo.
(d) Mpangilio wa Shughuli
27.-(1) Shughuli za Bunge Maalum zitaendeshwa kwa kufuata
mpangilio ufuatao:
(a) taarifa ya Mwenyekiti;
Shughuli
za kila
siku
Upangaji
wa
muda
wa
kutekeleza
shughuli
Mpangilio
wa
Shughuli
za Bunge
Maalum
Kanuni za Bunge Maalum
23
(b) mambo yanayohusu haki za Bunge Maalum ikiwa ni
pamoja na kuzifanyia marekebisho Kanuni za Bunge Maalum;
(c) taarifa au hoja za Kamati;
(d) mjadala wa taarifa au hoja za Kamati;
(e) shughuli yoyote ambayo Mwenyekiti ataona inafaa
kushughulikiwa kwa wakati huo.
(2) Shughuli za Bunge Maalum katika kila Kikao zitatekelezwa
kwa kufuata Orodha ya Shughuli za siku hiyo.
(3) Baada ya hoja yoyote kuwasilishwa na kujadiliwa, Bunge
Maalum linaweza kuamua kuipitisha hoja hiyo kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na Kanuni hizi, au kwamba, hoja hiyo
ipelekwe kwenye Kamati inayohusika ili ifanyiwe kazi na
kupata ushauri wa ziada kuhusu hoja hiyo kabla ya kuipitisha.
28. Wakati wa Kikao chochote cha Bunge Maalum,
Mwenyekiti anaweza kutoa taarifa yoyote kuhusu shughuli
za Bunge Maalum kadri atakavyoona inafaa.
29.-(1) Jambo lolote linalohusu haki za Bunge Maalum
litawasilishwa kwa kufuata mpangilio wa shughuli za Bunge
Maalum uliowekwa chini ya Kanuni ya 27(1) ya Kanuni hizi,
baada ya Mwenyekiti kuarifiwa mapema kuhusu jambo hilo.
(2) Endapo baada ya kupata taarifa mapema, Mwenyekiti
ataamua kwamba jambo hilo liwasilishwe kwenye Bunge
Maalum, basi atampa nafasi Mjumbe anayehusika
kuliwasilisha kwa kutoa maelezo mafupi kuhusu jambo
lenyewe na sababu zinazomfanya aamini kwamba linahusu
haki za Bunge Maalum zilizotajwa kwenye Sheria na Kanuni
hizi.
(3) Hoja inayohusu haki za Bunge Maalum zilizoainishwa katika
Sheria na Kanuni hizi itapewa kipaumbele katika mpangilio
wa shughuli nyingine zote zilizopangwa kwa kikao
kinachohusika.
(4) Iwapo wakati wa kikao chochote cha Bunge Maalum
jambo lolote linaloonekana linahusu haki za Bunge Maalum
Taarifa ya
Mwenyekiti
Haki za
Bunge
Maalum
Kanuni za Bunge Maalum
24
litajitokeza, shughuli zitasitishwa kwa madhumuni ya
kuliwezesha jambo hilo kuwasilishwa na kuamuliwa, isipokuwa
tu kama wakati huo kura inapigwa.
(e) Uhalali wa Shughuli
30.-(1) Akidi kwa kila Kikao cha Bunge Maalum, isipokuwa
wakati wa kupitisha uamuzi wa Bunge Maalum, itakuwa ni
nusu ya Wajumbe wote wa Bunge Maalum.
(2) Mjumbe yeyote aliyehudhuria anaweza kumjulisha
Mwenyekiti kwamba, Wajumbe waliopo ni pungufu ya akidi
inayohitajika kwa ajili ya shughuli inayoendelea.
(3) Endapo Mwenyekiti ataridhika kwamba idadi ya
Wajumbe walio ndani ya ukumbi wa Mkutano wa Bunge
Maalum ni pungufu ya akidi inayohitajika basi atasitisha
shughuli za Bunge Maalum kwa muda atakaoutaja na
atamwagiza Katibu kupiga kengele.
(4) Bunge Maalum litakaporejea baada ya muda uliotajwa
chini ya fasili ya (3) kukamilika, Mwenyekiti atahakiki kama
idadi ya Wajumbe waliopo inafikia akidi inayohitajika ili
kuwezesha shughuli inayohusika kuendelea.
(5) Endapo Mwenyekiti ataridhika kwamba bado idadi ya
Wajumbe waliomo ndani ya ukumbi wa Mkutano wa Bunge
Maalum haifikii akidi inayohitajika, basi ataahirisha shughuli
hadi muda mwingine atakaoutaja.
(6) Shughuli za Bunge Maalum pamoja na uamuzi wowote
wa Bunge Maalum hautakuwa batili kwa sababu tu kwamba
nafasi yoyote ya Mjumbe ipo wazi.
(f) Utaratibu wa Kuwasilisha Rasimu ya Katiba
31.-(1) Rasimu ya Katiba itawasilishwa katika Bunge Maalum
na Mwenyekiti wa Tume kwa mujibu wa kifungu cha 20(3)
cha Sheria na Kanuni hizi.
Akidi ya
vikao vya
Bunge
Maalum
Utaratibu
wa
kuwasilisha
Rasimu ya
Katiba
Sura ya 83
Kanuni za Bunge Maalum
25
(2) Wakati wa kuwasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge
Maalum, hakutakuwa na hoja kuhusu mwongozo, taarifa,
utaratibu au ufafanuzi juu ya Rasimu ya Katiba
inayowasilishwa.
(3) Baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa kwa mujibu wa
fasili ya (1), Mwenyekiti atatangaza majina ya Wajumbe wa
kila Kamati na kila Kamati itatekeleza majukumu yake kwa
mujibu wa masharti yaliyowekwa na Kanuni hizi.
32.-(1) Bila kuathiri majadiliano ya Sura ya Kwanza na Sura
ya Sita, kila Kamati itajadili Sura zote za Rasimu ya Katiba
pamoja na Sura mpya zitakazojitokeza kwa wakati mmoja.
(2) Isipokuwa kama Kamati ya Uongozi itaelekeza vinginevyo,
mjadala katika Kamati chini ya fasili ya (1) utafanyika kwa
muda usiozidi siku kumi na tano kwa utaratibu utakaowekwa
na Kamati husika kwa kuzingatia masharti ya kanuni hizi.
(3) Bila ya kuathiri utaratibu wa majadiliano ya Sura ya
Kwanza na ya Sita, wakati wa mjadala ndani ya Kamati,
Mjumbe yeyote anaweza kutoa mapendekezo ya
marekebisho, maboresho au mabadiliko yaliyomo katika Sura
za Rasimu ya Katiba zinazojadiliwa kwa utaratibu ufuatao:
(a) ikiwa ni marekebisho, maboresho au mabadiliko
yanayobadilisha jambo la msingi au yanayobadilisha
maudhui ya ibara, mapendekezo ya marekebisho
yatapelekwa kwa maandishi kwa Katibu wa Kamati siku moja
kabla ya mjadala wa ibara husika;
(b) ikiwa ni marekebisho madogo ambayo hayabadilishi
msingi au maana, mapendekezo ya marekebisho
yatawasilishwa na Mjumbe wakati wa mjadala ndani ya
Kamati baada ya kupata ruhusa ya Mwenyekiti wa Kamati.
Rasimu ya
Katiba
kupelekwa
kwenye
Kamati
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
25/04/2014
Kanuni za Bunge Maalum
26
(4) Mjumbe aliyepata nafasi ya kutoa mapendekezo kwa
mujibu wa fasili ya (3), atawasilisha mapendekezo hayo
mbele ya Kamati, na Wajumbe wengine wanaweza
kuchangia mapendekezo hayo.
(5) Mwenyekiti wa Kamati hataruhusu mapendekezo ya
marekebisho, maboresho au mabadiliko ya Sura za Rasimu
ya Katiba zinazojadiliwa yanayokiuka Sheria au masharti
yaliyowekwa na Kanuni hizi.
(6) Bila ya kuathiri utaratibu wa majadiliano ya Sura ya Kwanza
na ya Sita, Mjumbe yeyote au kundi lolote la Wajumbe
lililotajwa chini ya kifungu cha 22(1) cha Sheria ya Mabadiliko
ya Katiba linaweza kupendekeza Sura mpya kwenye Rasimu
ya Katiba.
(7) Isipokuwa kama Kamati ya Uongozi itaelekeza vinginevyo,
mapendekezo ya Sura mpya kwa mujibu wa fasili ya (6)
yatawasilishwa kwa Katibu ndani ya siku tano mara baada
ya mjadala wa Sura za Rasimu ya Katiba kuanza kwenye
Kamati, na Katibu atawasilisha mapendekezo hayo ya Sura
mpya kwenye Kamati ya Uongozi.
(8) Kamati ya Uongozi baada ya kuridhika kuwa
mapendekezo yaliyowasilishwa chini ya fasili ya (7) yanakidhi
kuwa Sura mpya au sehemu ya Sura ya Rasimu ya Katiba,
itaagiza mapendekezo hayo yajadiliwe na Kamati Namba
Moja hadi Namba Kumi na Mbili na hatimaye taarifa za
Kamati hizo kuwasilishwa kwenye Bunge Maalum kwa ajili ya
kujadiliwa.
(9) Baada ya mjadala wa Kamati, kwa muda usiozidi siku
tatu, kila Kamati itaandaa Taarifa kuhusu mambo
yaliyoafikiwa na Wajumbe walio wengi kwa ajili ya
kuwasilishwa kwenye Bunge Maalum.
(10) Endapo kutakuwa na Wajumbe ambao hawakuunga
mkono maoni ya Wajumbe walio wengi katika Kamati,
Wajumbe hao wanaweza kuandaa maoni yao yanayohusu
Sura ya 83
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Kanuni za Bunge Maalum
27
maeneo ambayo hawakukubaliana na Wajumbe walio
wengi, na watamchagua mmoja miongoni mwa Wajumbe
walio wachache kuwasilisha maoni hayo.
(10A) Taarifa ya Kamati inayojumuisha maoni ya wajumbe
walio wengi na walio wachache itaandikwa kwa kufuata
mwongozo utakaotolewa na Kamati ya Uongozi ya Bunge
Maalum.
(10B) Taarifa ya Kamati itakayoandikwa kwa kukiuka
mwongozo utakaotolewa kwa mujibu wa fasili ya (10A)
haitakubaliwa.
(11) Baada ya Kamati kuandaa taarifa yake, Mwenyekiti wa
Kamati inayohusika atamjulisha Mwenyekiti kwa maandishi
kuwa Kamati imekamilisha kazi yake.
32A. Bila kuathiri masharti ya Kanuni ya 57(2), utaratibu wa
majadiliano katika Kamati utakuwa kama ifuatavyo:
(a) Mjumbe yeyote hataanza kuzungumza hadi aitwe na
Mwenyekiti wa Kamati kwa jina lake na kumruhusu kusema,
na wakati wa kusema ataelekeza maneno yake kwa
Mwenyekiti wa Kamati;
(b) Mwenyekiti wa Kamati atahakikisha kuwa nafasi za
kuchangia zinatolewa kwa uwiano unaofaa baina ya
wajumbe wa aina zote na makundi yote yanayowakilishwa
katika Kamati husika;
(c) Mwenyekiti wa Kamati anaweza kutoa nafasi ya
kuchangia kwa Mjumbe yeyote iwapo ataona kuwa taaluma
au uzoefu wa tasnia fulani wa Mjumbe huyo utaboresha suala
linalojadiliwa na Kamati;
(d) Kila Mjumbe wa Kamati atatoa maelezo yake kwa
kutumia vyombo vilivyowekwa kwa madhumuni ya kutafsiri,
kukuza na kurekodi sauti;
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Utaratibu wa
majadiliano
kwenye
Kamati
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
04/04/2014
Kanuni za Bunge Maalum
28
(e) Mjumbe wa Kamati hataruhusiwa kuzungumzia suala
lililokuwa likijadiliwa baada ya Mwenyekiti wa Kamati
kuwahoji Wajumbe na suala hilo kutolewa uamuzi.
32B. Bila kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi yanayolinda
na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano, masharti ya
Kanuni ya 46 na 46A yanayohusu mambo yasiyoruhusiwa
katika Bunge Maalum, wajibu wa Mjumbe kusema ukweli na
mamlaka ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum kutoa adhabu
yatatumika pamoja na mabadiliko husika katika kuendesha
majadiliano ya Kamati.
32C. Masharti ya Kanuni ya 49(2) na (3) yanayohusu staha
ndani ya Bunge Maalum yatatumika kuendesha shughuli za
Kamati.
32D. Bila kuathiri masharti ya Kanuni ya 56(9), endapo Mjumbe
yeyote wa Kamati atavunja au atajaribu kuvunja utaratibu
au amani na utulivu kwenye Kamati au ataonesha tabia za
vurugu kwa kutumia nguvu na mabavu ndani ya ukumbi wa
Kikao cha Kamati, Mwenyekiti wa Kamati ataamuru Mpambe
wa Bunge Maalum amtoe mara moja Mjumbe huyo nje na
asihudhurie Kikao cha Kamati cha siku hiyo.
(g) Utaratibu wa Kuwasilisha, Kujadili na Kupitisha Hoja
33.-(1) Isipokuwa kama Kanuni hizi zimeelekeza vinginevyo,
hakuna mjadala wowote utakaoendeshwa kwenye Bunge
Maalum ila tu mjadala unaohusu shughuli iliyoingizwa kwenye
Kitabu cha Orodha ya Shughuli za Bunge Maalum na
kuwekwa kwenye Orodha ya Shughuli za kikao hicho.
Mambo
yasiyoruhusiwa
kwenye
Kamati
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Staha ndani
ya Kamati
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
04/04/2014
Mamlaka
kuhusu
amani na
utulivu
kwenye
Kamati
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
04/04/2014
Uwasilishaji
wa Hoja
Kanuni za Bunge Maalum
29
(2) Hoja ikishawekwa kwenye Orodha ya Shughuli, Mwenyekiti
wa kila Kamati kuanzia Kamati Namba Moja hadi Kamati
Namba Kumi na Mbili au Mjumbe mwingine wa Kamati
aliyeteuliwa kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Kamati yenye
maoni ya Wajumbe walio wengi, atawasilisha kwa muda
usiozidi dakika mia moja na ishirini taarifa hiyo na kutoa hoja
kwamba taarifa hiyo ijadiliwe kwenye Bunge Maalum.
(3) Hoja yoyote itakayowasilishwa katika Bunge Maalum kwa
mujibu wa kanuni hii itawekwa katika lugha ambayo
italiwezesha Bunge Maalum kufanya uamuzi ambao ni
bayana.
(4) Hoja ya taarifa ya Kamati itakuwa kama ifuatavyo:
“Kwamba, taarifa ya Kamati Namba ……… ya Bunge
Maalum kuhusu Sura……..ya Rasimu ya Katiba sasa isomwe
na ijadiliwe na Bunge Maalum. Naomba kutoa Hoja.”
(5) Maoni ya Wajumbe walio wachache kwa mujibu wa
kanuni ya 32(10), yatawasilishwa na mmoja wa Wajumbe
ambao hawakuunga mkono maoni ya Wajumbe walio wengi
katika Kamati kwa muda usiozidi dakika sitini.
(6) Baada ya Hoja za taarifa za Kamati Namba Moja hadi
Namba Kumi na Mbili kutolewa katika Bunge Maalum na
Mwenyekiti kuelekeza hoja hizo zijadiliwe, mjadala kuhusu
taarifa hizo utaanza kwa kuzingatia utaratibu utakaopangwa
na Mwenyekiti.
(7) Taarifa za Kamati zote zitajadiliwa kwa muda usiozidi siku
kumi na sita.
(8) Kila hoja itawekwa kwenye Orodha ya Shughuli ikiwa
kama ilivyowasilishwa au kama ilivyofanyiwa marekebisho au
mabadiliko.
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
25/04/2014
na tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Kanuni za Bunge Maalum
30
(9) Hoja ikishatolewa ili iamuliwe inaweza kubadilishwa kwa:
(a) kuondoa maneno fulani kwa ajili ya kuingiza maneno
mengine;
(b) kuondoa maneno fulani bila kuingiza maneno mengine;
na
(c) kuingiza au kuongeza maneno mapya.
34.-(1) Bila kuathiri masharti mengine yaliyowekwa na Kanuni
hizi, Bunge Maalum halitashughulikia pendekezo lolote la
Kamati au la Mjumbe ambalo linahusu jambo ambalo lipo
nje ya Mamlaka ya Bunge Maalum.
(2) Bila kuathiri masharti ya fasili ya (1), mapendekezo yoyote
ya marekebisho, maboresho au mabadiliko hayatakubaliwa
iwapo yanakwenda kinyume na Sheria au Kanuni hizi.
35.-(1) Kwa kuzingatia mamlaka ya Bunge Maalum ya kujadili
na kupitisha Rasimu ya Katiba yaliyowekwa na Sheria, msingi
wa majadiliano ya Bunge Maalum utakuwa ni taarifa za
Kamati.
(2) Baada ya kuitwa na Mwenyekiti kujadili hoja, Mjumbe
mwenye uwezo wa kusimama atasimama mahali pake na
kutoa maelezo yake kuhusu hoja hiyo kwa kuyaelekeza kwa
Mwenyekiti.
(3) Katika kujadili hoja za Kamati, kila Mjumbe atakayepata
nafasi ataelekeza maelezo yake kwenye hoja au jambo
mahsusi linalojadiliwa kwa wakati huo, na endapo Mjumbe
yeyote ataanza kujadili au kutoa maelezo ambayo
hayahusiani na hoja au jambo mahsusi linalojadiliwa kwa
wakati huo au anarudiarudia maelezo yaliyokwishatolewa
na Mjumbe au Wajumbe wengine, Mwenyekiti anaweza
kumwamuru Mjumbe huyo akatishe maelezo yake na kukaa
kwenye kiti chake.
(4) Mjumbe aliyeamriwa na Mwenyekiti kukatisha maelezo
yake na kukaa kwenye kiti chake kwa mujibu wa fasili ya (3),
Masharti
kuhusu
mapendekezo
ya Kamati
Utaratibu
wa
majadiliano
wakati wa
kujadili
taarifa ya
Kamati
Kanuni za Bunge Maalum
31
atatii amri ya Mwenyekiti bila ukaidi wowote, na iwapo
atakaidi, ataadhibiwa na Mwenyekiti papo hapo kwa mujibu
wa mamlaka aliyonayo ya kusimamia Kanuni hizi na pia
uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge Maalum.
(5) Wakati wa kujadili taarifa za Kamati, Mwenyekiti au
Makamu Mwenyekiti wa kila Kamati au Mjumbe mwingine
wa Kamati aliyeteuliwa kuwasilisha taarifa ya Kamati au kutoa
maelezo ya ufafanuzi, ndiye atakayewajibika kutoa maelezo
ya ufafanuzi na kujibu hoja mbalimbali zitakazotolewa na
Wajumbe wakati wa mjadala.
(6) Baada ya mjadala wa taarifa za Kamati kwa Sura zote
za Rasimu ya Katiba pamoja na Sura mpya kuhitimishwa,
Mwenyekiti ataielekeza Kamati ya Uandishi kufanyia kazi
taarifa za Kamati, maoni na mapendekezo yatokanayo na
mjadala wa Taarifa hizo kwa mujibu wa fasili ya (7).
(6A) Kabla ya kuielekeza Kamati ya Uandishi chini ya fasili ya
(6), Mwenyekiti atalihoji Bunge Maalum kuhusu taarifa hizo
ambazo zimehitimishwa ili taarifa za Kamati pamoja na maoni
na mapendekezo yatokanayo na taarifa za Kamati na
mjadala wa taarifa hizo yaelekezwe kwenye Kamati ya
Uandishi.
(7) Kamati ya Uandishi itaandika upya ibara za Sura za Rasimu
ya Katiba zilizojadiliwa na Bunge Maalum katika muda usiozidi
siku tano na hatimaye kutoa taarifa kwa Mwenyekiti baada
ya kukamilisha kazi hiyo.
(8) Baada ya kupata taarifa ya Kamati ya Uandishi kwa
mujibu wa fasili ya (7), Mwenyekiti ataagiza taarifa hiyo
iingizwe katika orodha ya shughuli za Bunge Maalum.
(9) Taarifa ya Kamati ya Uandishi yenye ibara za Sura za
Rasimu ya Katiba zilizoandikwa upya itawasilishwa kwenye
Bunge Maalum kwa ajili ya kupitishwa kwa kupigiwa kura
ibara kwa ibara kwa mujibu wa kanuni ya 36.
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Kanuni za Bunge Maalum
32
(10) Endapo Bunge Maalum litabaini kuwa ibara iliyoandikwa
upya haikuzingatia taarifa za Kamati au maoni na
mapendekezo yaliyotolewa wakati wa mjadala wa taarifa
za Kamati katika Bunge Maalum, basi Mwenyekiti ataielekeza
Kamati ya Uandishi kuandika upya ibara hiyo ipasavyo.
36.-(1) Bila kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi, ibara za
Sura za Rasimu ya Katiba zilizoandikwa upya zitapigiwa kura
ibara kwa ibara katika muda usiozidi siku saba:
Isipokuwa kama Kamati ya Uongozi itaelekeza vinginevyo,
masharti ya fasili ya (1) hayatazuia Bunge Maalum kupigia
kura Ibara zozote za Sura za Rasimu ya Katiba kwa utaratibu
utakaowekwa na Kamati ya Uongozi.
(2) Ibara za Sura za Rasimu ya Katiba zilizoandikwa upya
zitapigiwa kura na kupitishwa kwa kuungwa mkono kwa wingi
wa theluthi mbili ya idadi ya Wajumbe wote kutoka Tanzania
Bara na theluthi mbili ya idadi ya Wajumbe wote kutoka
Tanzania Zanzibar.
(3) Endapo baada ya ibara ya Rasimu ya Katiba iliyoandikwa
upya kupigiwa kura, theluthi mbili ya wajumbe wote kutoka
Tanzania Bara na theluthi mbili ya wajumbe wote kutoka
Tanzania Zanzibar haikufikiwa, basi ibara hiyo itapelekwa
kwenye Kamati ya Mashauriano ili kupata muafaka.
(4) Baada ya Kamati ya Mashauriano kukutana na kujadili
ibara inayobishaniwa, itapeleka taarifa ya matokeo ya
mashauriano yake kwenye Bunge Maalum kwa ajili ya
kujadiliwa, na ibara hiyo kama ilivyo au baada ya kuandikwa
upya kwa kuzingatia taarifa ya Kamati ya Mashauriano na
mjadala wa taarifa hiyo, itapigiwa kura kwa mara nyingine
tena, na endapo wingi wa kura kwa idadi ya theluthi mbili
kwa kila upande wa Muungano haitapatikana, basi ibara
hiyo itahesabiwa kuwa haikukubaliwa wala kupitishwa na
Bunge Maalum kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na
Sheria na Kanuni hizi.
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Utaratibu
wa kupiga
kura ibara
kwa ibara
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Kanuni za Bunge Maalum
33
(5) Bila ya kuathiri masharti ya fasili ya (3), Mwenyekiti
ataielekeza Kamati ya Uandishi kuziweka pamoja ibara za
Rasimu ambazo hazikukubaliwa au kupitishwa kwa
madhumuni ya kujadiliwa tena na kupatiwa ufumbuzi kabla
ya Bunge Maalum kupokea Rasimu ya Mwisho ya Katiba
inayopendekezwa.
37.-(1) Bila kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi, utaratibu
wa Bunge Maalum kufanya uamuzi utakuwa ni kwa
Mwenyekiti kulihoji Bunge Maalum na kupata uamuzi wa
Bunge Maalum utakaotokana na wingi wa idadi ya Wajumbe
kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Kanuni hizi:
Isipokuwa kwamba, ili ibara au Rasimu ya Katiba iweze
kupitishwa katika Bunge Maalum itahitaji kuungwa mkono
kwa wingi wa theluthi mbili ya idadi ya Wajumbe wote wa
Bunge Maalum kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya idadi
ya Wajumbe wote wa Bunge Maalum kutoka Tanzania
Zanzibar.
(2) Iwapo jambo lolote linahitaji kuamuliwa au kutekelezwa
na Bunge Maalum, basi jambo hilo halitahesabiwa kuwa
limeamuliwa au limetekelezwa ipasavyo, ila mpaka liwe
limeamuliwa au limetekelezwa na Bunge Maalum kwa
kuzingatia masharti na utaratibu uliowekwa na Sheria pamoja
na Kanuni hizi.
(3) Kwa madhumuni ya kanuni hii, utaratibu utakaotumika
kupata uamuzi baada ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum
kutoa swali la kulihoji Bunge Maalum utakuwa ni kwa kura ya
siri kwa Mjumbe anayetaka kupiga kura ya siri au kura ya
wazi kwa Mjumbe anayetaka kupiga kura ya wazi kwa
kuzingatia utaratibu ulioainishwa katika kanuni ya 38.
(4) Bila kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi, wakati wa
kupata uamuzi wa Bunge Maalum kuhusu kupitisha Rasimu
ya Katiba, Bunge Maalum litapiga kura, ambayo kwa
madhumuni ya Kanuni hii, itaitwa kura ya mwisho.
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Utaratibu
wa kufanya
uamuzi
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
27/03/2014
Kanuni za Bunge Maalum
34
38.-(1) Utaratibu wa kupiga kura ya wazi au ya siri
utaelekezwa na Mwenyekiti kwa kushauriana na Katibu.
(2) Wakati wa kupiga kura ya siri, kila Mjumbe atapiga kura
ya “Ndiyo” au “Hapana”, kwa kutumia karatasi ya kupigia
kura itakayokuwa imeandaliwa na Katibu kwa ajili hiyo.
(3) Upigaji kura ya siri utakuwa ni kwa Mjumbe baada ya
kupewa karatasi ya kupigia kura, kuweka alama ya vema
(“) kwenye moja ya kisanduku pembeni ya namba ya ibara
husika au pembeni ya maneno “Rasimu ya Mwisho ya Katiba”
sanjari na maneno “Ndiyo” au “Hapana”, kwa jinsi yeye
binafsi anavyoona inafaa.
(4) Mjumbe ambaye ataharibu karatasi yake ya kupigia kura
atairudisha karatasi hiyo iliyoharibika kwa Katibu na atapewa
karatasi nyingine ya kupigia kura.
(5) Mjumbe ambaye atakuwa na mahitaji maalum au
atakuwa anahitaji usaidizi katika zoezi la kupiga kura,
atapatiwa mahitaji hayo na usaidizi huo kwa utaratibu
ulioandaliwa na Katibu kwa ajili hiyo.
(6) Baada ya kila Mjumbe aliyehudhuria Kikao na kupiga
kura ya siri, kura hizo zitakusanywa na kuwekwa kwenye
masanduku ya kura na kupelekwa kwenye chumba maalum
kitakachokuwa kimeandaliwa kwa ajili ya kuhesabu kura
mbele ya mawakala walioteuliwa kwa ajili ya kusimamia kura
hizo.
(7) Kwa Mjumbe anayetaka kupiga kura ya wazi, utaratibu
utakaotumika utakuwa ni kwa kuitwa jina na Katibu na
Mjumbe kutamka kwa sauti maneno “Ndiyo” au “Hapana”
kuhusu ibara husika au Rasimu ya Mwisho ya Katiba.
(8) Baada ya kura za wazi na za siri kuhesabiwa, Mwenyekiti
atatangaza matokeo ya kura, na matokeo hayo yataingizwa
katika Taarifa Rasmi.
Utaratibu
wa
kupiga
kura
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
27/03/2014
Kanuni za Bunge Maalum
35
39.-(1) Bila kuathiri masharti mengine ya Kanuni hizi, utaratibu
utakaotumika kwa ajili ya Bunge Maalum kutumia mamlaka
yake ya kujadili na kupitisha masharti ya Rasimu ya Mwisho
ya Katiba utakuwa kama ifuatavyo:
(a) kujadili na kupigia kura marekebisho au mabadiliko ya
kuboresha Rasimu ya Katiba yaliyowasilishwa na Kamati; na
(b) kujadili na kupiga kura ya mwisho kwa ajili ya kupitisha
Rasimu ya Mwisho ya Katiba kwa ujumla wake.
(2) Endapo taarifa za Kamati hazitapendekeza marekebisho
yoyote ya kuboresha Rasimu ya Katiba, basi masharti ya Sura
inayohusika ya Rasimu ya Katiba yatapigiwa kura kama
yalivyo kwa mujibu wa Sheria na Kanuni hizi na kupitishwa.
(3) Kupiga kura kwa mujibu wa masharti ya Kanuni hii itakuwa
ni wajibu na haki ya msingi ya kila Mjumbe, na kila Mjumbe
atapiga kura kwa binafsi yake:
Isipokuwa kwamba, Mjumbe ambaye anahitaji usaidizi au
nyenzo maalum kwa ajili ya kupiga kura mwenyewe,
atapatiwa usaidizi au nyenzo hiyo kwa ajili ya kumwezesha
kupiga kura.
40.-(1) Baada ya Bunge Maalum kukamilisha shughuli ya
kujadili na kupitisha ibara zote za Rasimu ya Katiba kwa mujibu
wa masharti yaliyowekwa na Sheria na Kanuni hizi, Mwenyekiti
ataiagiza Kamati ya Uandishi kuandaa Rasimu ya Mwisho ya
Katiba kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum wakati wa
kupitisha mapendekezo ya Kamati Namba Moja hadi Namba
Kumi na Mbili.
(2) Baada ya Kamati ya Uandishi kukamilisha kazi yake kwa
mujibu wa masharti ya fasili ya (1), Mwenyekiti wa Kamati
hiyo atamtaarifu kwa maandishi Mwenyekiti kuhusu
kukamilika kwa kazi hiyo.
(3) Baada ya Mwenyekiti kupokea taarifa iliyowasilishwa kwa
mujibu wa fasili ya (2), ataagiza Rasimu ya Mwisho ya Katiba
Utaratibu
wa kupiga
kura na
kupitisha
masharti ya
Rasimu ya
Mwisho ya
Katiba
Utaratibu
wa kupitisha
Rasimu ya
Mwisho ya
Katiba
Kanuni za Bunge Maalum
36
iliyoandaliwa kwa mujibu wa masharti ya fasili ya (1) iwekwe
kwenye Orodha ya Shughuli kwa ajili ya kuwasilishwa kwenye
Bunge Maalum na kupitishwa kwa kuzingatia masharti ya
kanuni ya 39(1).
41.-(1) Hoja ya kuwasilisha Rasimu ya Mwisho ya Katiba katika
Bunge Maalum kwa mujibu wa fasili hii itakayowasilishwa na
Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi itakuwa katika maneno
yafuatayo:
“Kwamba Rasimu ya Mwisho ya Katiba kama ilivyopitishwa
ibara kwa ibara na Bunge Maalum, sasa ipitishwe kwa ujumla
wake”
(2) Baada ya hoja kutolewa kwa mujibu wa fasili ya (1), Rasimu
ya Mwisho ya Katiba itapitishwa na Bunge Maalum kwa
mujibu wa masharti ya Sheria pamoja na masharti ya Kanuni
hizi.
(3) Baada ya kupitisha Rasimu ya Mwisho ya Katiba kwa
mujibu wa fasili ya (2), Bunge Maalum litapitisha utangulizi
na jina la Katiba inayopendekezwa.
42. Mwenyekiti anaweza kumuagiza Katibu kuifanyia
masahihisho Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum, kwa
ajili ya kuondoa makosa ya uchapaji.
43.-(1) Katiba inayopendekezwa, kama ilivyopitishwa na
Bunge Maalum, itathibitishwa na Mwenyekiti, na ndani ya
siku saba, ataiwasilisha kwa Rais na kwa Rais wa Zanzibar.
(2) Bunge Maalum litaandaa shughuli maalum ya kitaifa
katika tarehe na siku ambayo Mwenyekiti atakabidhi kwa
Rais na Rais wa Zanzibar Katiba inayopendekezwa.
Hoja ya
kuwasilisha
Rasimu ya
Mwisho ya
Katiba
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
25/04/2014
Masahihisho
ya
uchapaji
Uwasilishaji
wa Katiba
inayopendekezwa
kwa Rais na
Rais wa
Zanzibar
Kanuni za Bunge Maalum
37
SEHEMU YA TANO
KANUNI ZA MAJADILIANO
44. Kwa idhini ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Mjumbe
yeyote mwenye uwezo wa kusimama anaweza kusimama
na kuchangia kwenye Bunge Maalum katika nyakati
zifuatazo:
(a) wakati wa kuchangia mjadala wa Hoja yoyote
iliyowasilishwa katika Bunge Maalum ambayo Kanuni
zinaruhusu ijadiliwe;
(b) wakati anawasilisha mabadiliko yoyote ya Hoja;
(c) wakati amesimama au kwa Mjumbe asiyeweza
kusimama, akiwa amekaa, kutaka kuzungumzia jambo lolote
linalohusu utaratibu;
(d) wakati amesimama au kwa Mjumbe asiyeweza
kusimama, akiwa amekaa, kuzungumzia jambo linalohusu
haki za Bunge Maalum.
45.-(1) Mjumbe yeyote akitaka kusema katika Bunge Maalum
anaweza-
(a) kumpelekea Mwenyekiti ombi kwa maandishi;
(b) kusimama kimya mahali pake; au
(c) kwa mtu mwenye mahitaji maalum, kukaa kimya mahali
pake huku akiinua juu kifaa kinachoonekana kwa urahisi na
Mwenyekiti kilichotayarishwa na Katibu kwa ajili hiyo.
(2) Mjumbe yeyote hataanza kuzungumza hadi aitwe na
Mwenyekiti kwa jina lake na kumruhusu kusema, na wakati
wa kusema ataelekeza maneno yake kwa Mwenyekiti.
(3) Mjumbe akimaliza kutoa maelezo yake atakaa kwenye
nafasi yake na hapo Mwenyekiti atamwita Mjumbe mwingine
aliyepeleka ombi la maandishi au kama Mwenyekiti
hakupata ombi lolote la maandishi, basi Mjumbe mwingine
yeyote anayetaka kujadili hoja, anaweza kusimama na
Nyakati za
Mjumbe
kusema
kwenye
Bunge
Maalum
Jinsi ya
kupata
nafasi ya
kusema
kwenye
Bunge
Maalum
Kanuni za Bunge Maalum
38
Mjumbe asiyeweza kusimama atainua kifaa maalum mahali
pake na kusubiri Mwenyekiti amwone.
(4) Iwapo Wajumbe wawili au zaidi watasimama wakati
mmoja, Mwenyekiti atamwita Mjumbe atakayemwona
kwanza.
(5) Endapo maombi ya kuchangia hoja fulani yatakuwa
mengi zaidi ya muda uliotengwa kwa hoja hiyo, Mwenyekiti
atatoa nafasi ya kwanza kwa Wajumbe ambao:
(a) hawajachangia katika hoja zilizotangulia kujadiliwa katika
Mkutano unaoendelea; au
(b) wamechangia mara chache katika hoja zilizotangulia
kujadiliwa.
(6) Bila kuathiri masharti ya fasili ya (5) Mwenyekiti atahakikisha
kuwa nafasi za kuchangia zinatolewa kwa uwiano unaofaa
baina ya Wajumbe wa aina zote na makundi yote
yanayowakilishwa katika Bunge Maalum.
(7) Masharti yaliyotangulia katika kanuni hii hayatamzuia
Mwenyekiti kutoa nafasi ya kuchangia kwa Mjumbe
mwingine yeyote iwapo ataona kuwa taaluma au uzoefu
wa tasnia fulani wa Mjumbe huyo utaboresha hoja
inayojadiliwa.
(8) Mwenyekiti ataandaa orodha ya wachangiaji katika
Bunge Maalum na kuisambaza orodha hiyo kwa wajumbe
wote wa Bunge Maalum.
(9) Kila Mjumbe atazungumzia jambo ambalo liko katika
mjadala tu na hatarudiarudia maneno yake au yale
yaliyokwisha kusemwa na Wajumbe wengine, na iwapo
itatolewa hoja ya kufanya mabadiliko katika hoja
inayojadiliwa, mjadala sharti uhusu hoja hiyo ya mabadiliko
mpaka imalizike, ndipo mjadala urudie kwenye hoja ya
msingi.
Kanuni za Bunge Maalum
39
(10) Kila Mjumbe atasema akiwa amesimama na atatoa
maelezo yake kwa kutumia vyombo vilivyowekwa kwa
madhumuni ya kutafsiri, kukuza na kurekodi sauti:
Isipokuwa, Mjumbe yeyote mwenye mahitaji maalum
anaweza kuzungumza akiwa amekaa.
(11) Endapo Mwenyekiti atasimama wakati Mjumbe yeyote
anatoa maelezo ndani ya Bunge Maalum, au amesimama
au amekaa mahali pake akisubiri kuanza kuzungumza,
Mjumbe huyo atakaa au ataendelea kukaa mahali pake na
Bunge Maalum litabaki kimya ili Mwenyekiti aweze kutoa
maelekezo au taarifa yake.
(12) Mjumbe hataruhusiwa kuzungumzia hoja iliyokuwa
ikijadiliwa baada ya Mwenyekiti kuwahoji Wajumbe na hoja
hiyo kutolewa uamuzi.
(13) Mjumbe yeyote anaweza kutoa maoni yake kwa
maandishi na kuyawasilisha kwa Katibu wakati ambapo hoja
husika inaendelea kujadiliwa, na maoni hayo yataingizwa
katika Taarifa Rasmi za Bunge Maalum.
(14) Mjumbe yeyote hataruhusiwa kutoa salamu, shukrani
au pongezi wakati wa kuchangia hoja au mjadala katika
Bunge Maalum na ikitokea hivyo, Mwenyekiti atamwamuru
Mjumbe huyo kukaa chini.
46.-(1) Bila kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi
yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano
katika Bunge Maalum, Mjumbe hataruhusiwa:
(a) kusema uongo ndani ya Bunge Maalum;
(b) kutoa taarifa zisizokuwa za ukweli ndani ya Bunge Maalum;
(c)kuzungumzia jambo lolote ambalo halipo kwenye
mjadala;
Mambo
yasiyoruhusiwa
kwenye
Bunge
Maalum
Kanuni za Bunge Maalum
40
(d) kuzungumzia jambo lolote ambalo limekwisha kutolewa
uamuzi;
(e) kutumia majina ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Rais wa Zanzibar na marais waasisi wa Taifa kwa
dhihaka au kwa madhumuni ya kutaka kushawishi Bunge
Maalum kuamua jambo lolote kwa namna fulani;
(f) kuzungumzia mwenendo wa Mwenyekiti au Makamu
Mwenyekiti; isipokuwa tu kama imetolewa hoja mahsusi ya
kumwondoa Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti
madarakani;
(g) kumsema vibaya au kutoa lugha ya matusi kwa
Mwenyekiti, au Makamu Mwenyekiti, au Mjumbe au kwa mtu
mwingine yeyote;
(h) kutumia lugha ya kuudhi, kubagua, kunyanyapaa au
inayodhalilisha watu wengine;
(i) kutoa kauli za dhihaka au zinazoshutumu mwenendo wa
Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti au Mjumbe au mtu
mwingine yeyote;
(j) kuzomea, kupiga kelele za aina yoyote zinazoweza
kuvuruga mjadala katika Bunge Maalum;
(k) kufanya jambo lolote ambalo linaathiri heshima ya Bunge
Maalum au mwenendo bora wa shughuli za Bunge Maalum;
(l) kufanya jambo lolote ambalo linakiuka masharti ya Sheria
na Kanuni hizi.
(2) Endapo Mjumbe yeyote atakiuka masharti ya fasili ya (1),
Mwenyekiti atamwamuru Mjumbe huyo atoke nje ya Bunge
Maalum na asihudhurie vikao vya Bunge Maalum visivyozidi
vitatu.
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Kanuni za Bunge Maalum
41
(3) Mjumbe aliyepewa adhabu kwa mujibu wa fasili ya (2)
hatalipwa posho yoyote ya vikao au ya kujikimu kwa kipindi
chote atakachokuwa anatumikia adhabu hiyo.
(4) Endapo posho ilishatolewa kwa Mjumbe anayetumikia
adhabu, basi posho hiyo itakatwa kutoka katika malipo ya
Mjumbe huyo yanayofuata.
46A.-(1) Mjumbe yeyote anapokuwa anasema kwenye
Bunge Maalum ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa
kauli au maelezo ya ukweli kuhusu jambo analolizungumzia.
(2) Mjumbe yeyote anapokuwa akisema ndani ya Bunge
Maalum hatachukuliwa kuwa anasema uongo iwapo
anafanya rejea ya andiko la kitabu au utafiti kuhusu jambo
fulani.
(3) Mjumbe mwingine yeyote anaweza kusimama au, iwapo
ni Mjumbe mwenye mahitaji maalum, kukaa mahali pake
huku akiinua juu kifaa kinachoonekana kwa urahisi na
Mwenyekiti kilichotayarishwa na Katibu kwa ajili hiyo na
kutamka “kuhusu utaratibu” na baada ya kuruhusiwa na
Mwenyekiti, ataeleza kwamba, Mjumbe aliyekuwa anasema
kabla yake ametoa maelezo ya uongo kuhusu jambo au
suala alilokuwa analisema kwenye Bunge Maalum.
(4) Mjumbe anayetoa madai kwa mujibu wa fasili ya (3) ya
Kanuni hii atakuwa na wajibu wa kutoa na kuthibitisha ukweli
kuhusu jambo au suala hilo kwa kiwango cha kuliridhisha
Bunge Maalum.
(5) Bila ya kuathiri masharti ya fasili zilizotangulia za kanuni
hii, Mwenyekiti au Mjumbe yeyote, baada ya kutoa maelezo
mafupi kwa muda usiozidi dakika tatu kuhusu ushahidi
unaotilia mashaka ya dhahiri kuhusu ukweli wa kauli au
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Wajibu wa
Mjumbe
kusema
ukweli
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Kanuni za Bunge Maalum
42
maelezo kuhusu jambo au suala ambalo Mjumbe amelisema
ndani ya Bunge Maalum, anaweza kumdai Mjumbe huyo
atoe uthibitisho wa ukweli wa kauli au maelezo yake na kama
atashindwa kufanya hivyo, afute kauli au usemi au maelezo
yake hayo.
(6) Mjumbe aliyetakiwa kuthibitisha ukweli wa kauli au
maelezo yake aliyoyatoa katika Bunge Maalum, atawajibika
kutoa uthibitisho huo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge
Maalum, papo hapo au katika muda atakaopewa na
Mwenyekiti kwa ajili ya kufanya hivyo.
(7) Endapo Mjumbe aliyetakiwa kuthibitisha kauli au maelezo
yake aliyoyatoa katika Bunge Maalum atashindwa kufanya
hivyo, anaweza kujirekebisha kwa kufuta kauli au maelezo
yake papo hapo au katika muda atakaokuwa amepewa
na Mwenyekiti kwa ajili ya kuthibitisha kauli au usemi au
maelezo yake.
(8) Endapo hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa, Mjumbe
aliyetakiwa kutoa uthibitisho wa ukweli wa kauli au maelezo
yake aliyoyatoa katika Bunge Maalum atakataa au
atashindwa kutoa uthibitisho huo kwa kiwango cha
kuliridhisha Bunge Maalum na kama atakataa kujirekebisha
kwa kufuta kauli au maelezo yake, basi Mwenyekiti
atamwadhibu kwa kumsimamisha Mjumbe huyo asihudhurie
vikao vya Bunge Maalum visivyozidi vitatu.
(9) Mjumbe yeyote aliyepewa adhabu kwa mujibu wa fasili
ya (8) hatalipwa posho yoyote ya vikao au ya kujikimu kwa
kipindi chote atakachokuwa anatumikia adhabu hiyo.
Azimio la Bunge Maalum la tarehe 05/08/2014
(10) Endapo posho ilishatolewa kwa Mjumbe anayetumikia
adhabu, basi posho hiyo itakatwa kutoka katika malipo ya
Mjumbe huyo yanayofuata.
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Kanuni za Bunge Maalum
43
47. Isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo kwenye Kanuni
hizi au Mwenyekiti ameelekeza vinginevyo:
(a) Mwenyekiti baada ya kushauriana na Mwenyekiti wa
Tume watapanga muda unaofaa kwa ajili ya Mwenyekiti wa
Tume kuwasilisha Rasimu ya Katiba katika Bunge Maalum;
(b) Mwenyekiti wa Kamati au Mjumbe yeyote anayewasilisha
hoja ya taarifa ya Kamati ya maoni ya walio wengi,
atawasilisha taarifa kwa muda usiozidi dakika mia moja na
ishirini;
(c) baada ya kuwasilisha hoja ya taarifa ya Kamati chini ya
aya ya (b) Mjumbe anayewakilisha wajumbe wa Kamati
walioandaa maoni ya walio wachache atawasilisha maoni
ya walio wachache kwa muda usiozidi “dakika sitini;
(d) kila Mjumbe anayejadili hoja, ataruhusiwa kusema kwa
muda usiozidi dakika kumi:
Isipokuwa Mjumbe anayetumia maandishi ya nukta nundu
anaweza kutumia muda usiozidi dakika kumi na tano.
48.-(1) Isipokuwa tu kwa idhini ya Mwenyekiti, Mjumbe yeyote
hataruhusiwa kusema zaidi ya mara moja kuhusu hoja ila tu
kama:
(a) anatumia haki yake ya kujibu;
(b) anasema kuhusu utaratibu; au
(c) anaomba mwongozo wa Mwenyekiti;
(d) kupata ufafanuzi wa jambo mahsusi linalohusu hoja
inayojadiliwa ndani ya Bunge Maalum,
na itakuwa ni marufuku kutumia fursa hiyo kuzungumzia jambo
lolote ambalo lipo nje ya hoja inayojadiliwa.
(2) Mjumbe ambaye amezungumza kuhusu hoja anaweza
Muda wa
kusema
ndani ya
Bunge
Maalum
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Kusema
zaidi ya
mara
moja
Kanuni za Bunge Maalum
44
kuzungumza tena kuhusu hoja ya kufanya mabadiliko katika
hoja aliyoisemea.
(3) Wakati wa kujibu, mtoa hoja atapaswa kutumia dakika
zisizozidi tano kujibu mambo yale tu yaliyozungumzwa na
Wajumbe waliochangia hoja yake na hataruhusiwa kutoa
maelezo yoyote mapya, isipokuwa kama maelezo hayo ni
ya lazima kwa madhumuni ya kufafanua jambo lililochangiwa
na Wajumbe.
(4) Mjumbe yeyote hataruhusiwa kusema ndani ya Bunge
Maalum kuhusu jambo ambalo Mwenyekiti amekwishawahoji
Wajumbe na kura ya uamuzi kupigwa kuhusu jambo hilo.
49.-(1) Wakati wa Vikao vya Bunge Maalum, Mwenyekiti
anapokuwa anaingia au kutoka katika ukumbi wa Mkutano
wa Bunge Maalum, Wajumbe na wageni wote wanaoweza
kusimama waliopo kwenye ukumbi huo, watasimama kwa
utulivu mahali pao na kubaki kimya hadi Mwenyekiti
atakapokuwa ameketi katika kiti chake au atakapokuwa
ametoka kwenye ukumbi wa Mkutano wa Bunge Maalum.
(2) Mjumbe aliyepo ndani ya ukumbi wa Mkutano wa Bunge
Maalum wakati wa mjadala atatakiwa:
(a) kuingia au kutoka kwenye ukumbi wa Mkutano wa Bunge
Maalum kwa staha na atainamisha kichwa kuelekeza kwa
Mwenyekiti kwa heshima kila mara Mjumbe huyo
atakapokuwa akienda au kutoka mahali pake;
(b) kutulia na kukaa kwa heshima mahali pake, na
hatatangatanga kwenye ukumbi wa Mkutano wa Bunge
Maalum;
(c) kutopita kati ya kiti cha Mwenyekiti na Mjumbe
anayesema.
(3) Mtumishi wa Bunge Maalum, msaidizi wa Mjumbe
mwenye mahitaji maalum na mgeni yeyote aliyepo kwenye
Staha
ndani ya
Bunge
Maalum
Kanuni za Bunge Maalum
45
ukumbi wa Mkutano wa Bunge Maalum wakati wa mjadala
atatakiwa:
(a) kuingia au kutoka kwenye ukumbi wa Mkutano wa Bunge
Maalum kwa staha na atainamisha kichwa kuelekeza kwa
Mwenyekiti kwa heshima, kila mara anapotoka au
anapokwenda kukaa mahali pake;
(b) kutulia na kukaa kwa heshima mahali pake, na
hatatangatanga kwenye ukumbi wa Mkutano wa Bunge
Maalum;
(c) kutopiga picha, kutopiga au kupokea simu.
50.-(1) Mwenyekiti anaweza kulihutubia Bunge Maalum
wakati wowote na kwa ajili hiyo, anaweza kumkatiza Mjumbe
yeyote anayezungumza.
(2) Endapo Mwenyekiti atasimama wakati wa mjadala, na
kuanza kuzungumza, Mjumbe yeyote ambaye atakuwa
anazungumza wakati huo au ambaye atakuwa amesimama
mahali pake akisubiri kuanza kuzungumza, ataketi mahali
pake, na Bunge Maalum litabaki kimya ili Mwenyekiti aweze
kutoa maelekezo au taarifa yake.
51.-(1) Bila kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi, Mjumbe
yeyote atakuwa na haki ya kuomba na kupata ufafanuzi wa
jambo lolote mahsusi linalohusu hoja inayojadiliwa ndani ya
Bunge Maalum.
(2) Katika kutumia haki ya kuomba na kupata ufafanuzi kwa
mujibu wa masharti ya fasili ya (1), Mjumbe atalazimika
kufuata utaratibu wa jinsi ya kupata nafasi ya kuitumia haki
hiyo uliowekwa na Kanuni hizi, na muda wa kusema utakuwa
ni dakika mbili.
(3) Haki ya Mjumbe kuomba na kupata ufafanuzi kwa mujibu
wa masharti ya kanuni hii itapewa kipaumbele cha kwanza
dhidi ya haki ya Mjumbe ya kusema Bungeni.
Mamlaka ya
Mwenyekiti
kuhutubia
wakati wa
majadiliano
Haki ya
kuomba na
kupata
ufafanuzi
Kanuni za Bunge Maalum
46
(4) Mjumbe yeyote anayekusudia kuomba na kupata
ufafanuzi kwa mujibu wa kanuni hii, atasimama mahali alipo
au kwa Mjumbe mwenye mahitaji maalum asiyeweza
kusimama, kuinua kifaa maalum na kusema “kuhusu
ufafanuzi”, akielekeza maneno hayo kwa Mwenyekiti.
(5) Baada ya kuitwa na Mwenyekiti kwa jina na kuruhusiwa
kusema, Mjumbe aliyesimama au aliyeinua kifaa maalum kwa
ajili ya kuomba na kupata ufafanuzi ataeleza kwa kifupi
jambo hilo mahsusi analoliombea ufafanuzi, na wakati wa
kusema ataelekeza maneno yake kwa Mwenyekiti.
(6) Baada ya kuhitimisha maelezo yake, Mjumbe mhusika
atakaa mahali pake, na kama kuna Mjumbe mwingine
aliyesimama au aliyeonesha kifaa maalum kwa ajili ya
kuomba na kupata ufafanuzi wa jambo lingine, Mwenyekiti
atamwita jina na kumruhusu kusema; na kama hakuna
Mjumbe mwingine, Mwenyekiti atatoa ufafanuzi ulioombwa
na Mjumbe kabla ya kuruhusu mjadala wa hoja kuendelea.
(7) Endapo Wajumbe wawili au zaidi watasimama wakati
mmoja kuhusu jambo la ufafanuzi, Mwenyekiti atamwita
Mjumbe atakayekuwa amemwona kwanza, na atafuatiwa
na yule mwingine; na iwapo idadi ya Wajumbe waliosimama
au waliokaa na kuonyesha kifaa maalum cha Wajumbe
wenye mahitaji maalum itakuwa ni zaidi ya wawili, basi
Mwenyekiti atawaita kwa mpangilio atakaouona unafaa.
(8) Bila kuathiri masharti yaliyotangulia ya kanuni hii, jambo
lolote la ufafanuzi litashughulikiwa kwanza na Mwenyekiti
kabla ya kuruhusu mjadala wa hoja inayohusiana na jambo
linaloombewa ufafanuzi kuendelea.
52.-(1) Mjumbe yeyote atakuwa na haki ya kuhoji kuhusu
jambo lolote la utaratibu katika Bunge Maalum.
(2) Mjumbe anayetaka kuhoji kuhusu jambo la utaratibu
anaweza kusimama au, iwapo ni Mjumbe mwenye mahitaji
maalum, kukaa wakati wowote na kusema maneno “kuhusu
utaratibu”, ambapo Mjumbe yeyote ambaye wakati huo
Taarifa
kuhusu
utaratibu
na
Mwongozo
wa
Mwenyekiti
Kanuni za Bunge Maalum
47
atakuwa anasema atanyamaza na kukaa chini au
ataendelea kukaa chini na Mwenyekiti atamtaka Mjumbe
aliyeomba kuhusu utaratibu ataje kanuni au sehemu ya
Kanuni iliyokiukwa.
(3) Mjumbe aliyeomba utaratibu chini ya fasili ya (2),
atalazimika kutaja Kanuni iliyokiukwa na muda wa kusema
hautazidi dakika tano.
(4) Baada ya kutaja kanuni iliyokiukwa na kutoa maelezo
yanayohusu ukiukwaji wa kanuni husika, Mjumbe aliyeomba
utaratibu, atakaa au ataendelea kukaa mahali pake kusubiri
uamuzi wa Mwenyekiti.
(5) Mwenyekiti anaweza kutoa uamuzi papo hapo au
baadaye, kwa kadri atakavyoona inafaa na atatakiwa kutoa
sababu za uamuzi huo.
(6) Katika kufikia uamuzi chini ya kanuni hii, Mwenyekiti
anaweza kuitaka Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum
au Kamati nyingine yoyote ya Bunge Maalum impe ushauri
kuhusu jambo husika.
(7) Mjumbe aliyekuwa anazungumza wakati jambo la
utaratibu lilipohojiwa anaweza kuendelea na maelezo yake
baada ya Mwenyekiti kutoa uamuzi juu ya jambo hilo au
baada ya kuahirisha uamuzi juu ya jambo hilo.
(8) Mjumbe anaweza kusimama wakati wowote ambapo
hakuna Mjumbe mwingine anayesema na kuomba
“Mwongozo wa Mwenyekiti” kuhusu jambo ambalo limetokea
katika Bunge Maalum mapema, ili Mwenyekiti atoe ufafanuzi
kama jambo hili linaruhusiwa au haliruhusiwi kwa mujibu wa
Kanuni na taratibu za Bunge Maalum na majibu ya
Mwenyekiti yatatolewa papo hapo au baadaye, kadri
atakavyoona inafaa.
(9) Uamuzi wa Mwenyekiti kuhusu suala lolote la utaratibu
katika Bunge Maalum utakuwa ni wa mwisho.
Kanuni za Bunge Maalum
48
53.-(1) Kwa kuzingatia hali na mazingira ya mjadala
unavyoendelea ndani ya Bunge Maalum, Mwenyekiti
atasitisha shughuli za Bunge Maalum na kuelekeza mjadala
husika uendeshwe katika kikao cha mashauriano cha Bunge
Maalum ambacho kitafanyika kwa faragha.
(2) Mwenyekiti anaweza kutoa taarifa fupi katika Bunge
Maalum kuhusu majadiliano na uamuzi uliofanywa na kikao
cha mashauriano cha Bunge Maalum kama atakavyoona
inafaa.
SEHEMU YA SITA
KAMATI ZA BUNGE MAALUM
54.-(1) Bila kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hizi, Bunge
Maalum linaweza kuunda Kamati za namna mbalimbali, kwa
kadri litakavyoona inafaa kwa ajili ya utekelezaji bora wa
kazi na mamlaka yake.
(2) Bila kujali masharti ya fasili ya (1), kutakuwa na Kamati
zifuatazo:
(a) Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum;
(b) Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum;
(c) Kamati ya Uandishi;
(d) Kamati Namba Moja;
(e) Kamati Namba Mbili;
(f) Kamati Namba Tatu;
(g) Kamati Namba Nne;
(h) Kamati Namba Tano;
(i) Kamati Namba Sita;
Vikao vya
mashauriano
Kamati
Kanuni za Bunge Maalum
49
(j) Kamati Namba Saba;
(k) Kamati Namba Nane;
(l) Kamati Namba Tisa;
(m) Kamati Namba Kumi;
(n) Kamati Namba Kumi na Moja; na
(o) Kamati Namba Kumi na Mbili.
(3) Majukumu ya Kamati zilizoundwa kwa mujibu wa masharti
ya fasili ya (2) yatakuwa kama yalivyoainishwa katika Kanuni
hizi.
(4) Bila kuathiri masharti ya fasili ya (1) na ya (2), Mwenyekiti,
baada ya kushauriana na Kamati ya Uongozi anaweza
kuunda Kamati ya Mashauriano pale linapojitokeza suala
linalohitaji mashauriano.
(5) Uteuzi wa Wajumbe wa Kamati ya Mashauriano
itakayoanzishwa kwa mujibu wa fasili ya (4) utazingatia suala
husika na mazingira yake.
(6) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum
watakuwa wajumbe wa Kamati ya Mashauriano.
55.-(1) Kamati zitaundwa na Mwenyekiti kwa namna ambayo
itawezesha kila Mjumbe kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati
mojawapo.
(2) Wakati wa kufanya uteuzi wa Wajumbe wa Kamati,
Mwenyekiti atazingatia yafuatayo:
(a) kwa kadri inavyowezekana, idadi ya wajumbe inalingana
kwa kila Kamati, isipokuwa Kamati zilizotajwa katika kanuni
ya 54(2)(a) hadi (c);
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Muundo
wa
Kamati
Kanuni za Bunge Maalum
50
(b) uteuzi wa wajumbe katika kila Kamati utazingatia-
(i) uwiano wa Wajumbe kutoka pande zote za Muungano;
(ii) idadi ya kila aina ya Wajumbe ilivyo katika Bunge Maalum;
(iii) uwiano wa kijinsia;
(iv) wajumbe wenye mahitaji maalum;
(v) uwepo wa wajumbe wenye utaalam wa Sheria.
(3) Katibu atahakikisha kuwa Wajumbe wote wa Bunge
Maalum wanapewa orodha inayoonesha jinsi
walivyopangwa katika Kamati mbalimbali.
(4) Ujumbe katika Kamati utadumu kwa kipindi chote cha
maisha ya Bunge Maalum.
(5) Bila kuathiri masharti mengine ya Kanuni hizi, wajumbe
wa kila Kamati watamchagua Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti wa Kamati kutoka miongoni mwao ambao kwa
muda wote watakaokuwa Wajumbe, wataendelea kushika
nafasi hizo kwa kipindi chote cha maisha ya Bunge Maalum.
(6) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watachaguliwa kwa
misingi kwamba endapo Mwenyekiti atatoka upande mmoja
wa Jamhuri ya Muungano, Makamu Mwenyekiti atatoka
upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano.
(7) Kwa mujibu wa fasili ya (6), uchaguzi wa Mwenyekiti na
Makamu Mwenyekiti utazingatia uwiano wa kijinsia kwa
misingi kwamba endapo Mwenyekiti aliyechaguliwa ni
mwanaume, basi Makamu Mwenyekiti atachaguliwa
mwanamke au kinyume chake.
(8) Kutakuwa na sekretarieti ya kila Kamati itakayoundwa
na watumishi kutoka Bunge Maalum.
(9) Sekretarieti ya kila Kamati itakuwa na wataalam wa
masuala ya kibunge, Sheria, uandishi wa Sheria, utafiti na fani
zingine za utaalam kwa ajili ya kuiwezesha Kamati kutekeleza
ipasavyo majukumu yake, na itafanya kazi zake chini ya
usimamizi wa Katibu wa Bunge Maalum.
Kanuni za Bunge Maalum
51
(10) Bila ya kuathiri masharti ya fasili zilizotangulia za kanuni
hii, Katibu atateua mtumishi yeyote wa Bunge Maalum kuwa
Katibu wa Kamati ya Bunge Maalum, kwa ajili ya kutekeleza
majukumu yafuatayo:
(a) kutoa ushauri wa kitaalam kwa Kamati; na
(b) kuratibu shughuli za Kamati.
(11) Kwa ajili ya kutekeleza wajibu wake wa usimamizi kwa
mujibu wa fasili ya (8), Katibu atakuwa na haki ya kuingia
katika kikao chochote cha Kamati au Kamati Ndogo yoyote
ya Kamati na kutoa maelekezo au ushauri wa kiutendaji kwa
Katibu wa Kamati au mtumishi yeyote wa Sekretarieti ya
Kamati.
56.-(1) Masharti ya kanuni hii yanayoweka utaratibu wa
kuendesha Mkutano, vikao na shughuli za Kamati yatatumika
kwa Kamati zote za Bunge Maalum.
(2) Mwenyekiti wa Kamati ataongoza vikao vyote vya Kamati
na endapo hayupo kwenye kikao, Makamu Mwenyekiti wa
Kamati ataongoza shughuli za kikao hicho, na ikiwa
Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti hawapo, wajumbe
waliohudhuria watamchagua mmojawapo miongoni mwao
kuongoza kikao hicho.
(3) Kamati itakutana kila itakapoagizwa kukutana na
Mwenyekiti au Mwenyekiti wa Kamati baada ya kupata idhini
ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
(4) Vikao vya kawaida vya Kamati vitafanyika katika maeneo
ya Bunge Maalum yaliyoandaliwa kwa ajili hiyo.
(5) Kila Kamati itafanya vikao vyake kwa kuzingatia ratiba
ya shughuli za Bunge Maalum iliyowekwa kwa mujibu wa
Kanuni hizi.
(6) Akidi ya vikao vyote vya Kamati itakuwa nusu ya Wajumbe
Utaratibu
wa vikao
na akidi
katika
Kamati
Kanuni za Bunge Maalum
52
wote wa Kamati kutoka Tanzania Bara na nusu ya Wajumbe
wote wa Kamati kutoka Tanzania Zanzibar.
(7) Bila kuathiri masharti ya kanuni ya 57(1), Mwenyekiti kama
ataona inafaa, anaweza baada ya kushauriana na Katibu
kumwalika mtaalam yeyote ili kupata maoni na ushauri kwa
ajili ya kuboresha jambo ambalo litakuwa linajadiliwa na
Kamati za Bunge Maalum.
(8) Mtu yeyote atakayealikwa kutoa maoni na ushauri wa
jambo lolote kwenye Kamati kwa mujibu wa fasili ya (8)-
(a) atastahili haki na kinga zilizowekwa na Sheria na Kanuni
hizi kuhusiana na maoni na ushauri atakaoutoa kwenye
Kamati;
(b) atavaa vazi la heshima na pia atapaswa kuwa na
nidhamu na kutii maelekezo ya Mwenyekiti wa Kamati.
(9) Mwenyekiti wa Kamati yoyote ya Bunge Maalum atakuwa
na mamlaka ya kuhakikisha kuwepo kwa amani na usalama,
na pia nidhamu inayohitajika kwa ajili ya uendeshaji bora
wa kazi na shughuli za Kamati; na kwa ajili hiyo, Mwenyekiti
huyo kwa kushauriana na Mwenyekiti anaweza kuchukua
hatua za kinidhamu atakazoona zinafaa dhidi ya mjumbe
yeyote wa Kamati atakayevuruga au atakayejaribu kuvuruga
mwenendo bora wa kazi na shughuli za Kamati.
57.-(1) Vikao vyote vya Kamati vitafanyika kwa faragha na
mtu yeyote asiyekuwa mjumbe wa Kamati, mtumishi wa
Bunge Maalum au mtaalam aliyeitwa kwa mujibu wa Kanuni
hizi hataruhusiwa kukaa katika sehemu yoyote ya Ukumbi wa
mikutano ya Kamati wakati Kikao cha Kamati kinaendelea.
(2) Utaratibu utakaotumika katika kuendesha mjadala
kwenye Kikao cha faragha cha Kamati utaamuliwa na
Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Kamati kwa
kushauriana na wajumbe wa Kamati husika.
(3) Bila kuathiri masharti ya kanuni hii, Mwenyekiti wa Kamati
Vikao vya
Kamati
kufanyika
kwa
faragha
Kanuni za Bunge Maalum
53
au Mjumbe yeyote, kwa idhini ya Mwenyekiti atatoa taarifa
kwa vyombo vya habari kuhusu mambo yaliyojitokeza
kwenye kikao cha Kamati.
58.-(1) Kamati ya Uongozi itakuwa na Wajumbe wafuatao:
(a) Mwenyekiti ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati;
(b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa Makamu
Mwenyekiti wa Kamati;
(c) Wenyeviti wa Kamati za Bunge Maalum; na
(d) Wajumbe wasiozidi watano ambao watateuliwa na
Mwenyekiti kwa kuzingatia makundi yanayowakilishwa
kwenye Bunge Maalum.
(2) Katibu na Naibu Katibu watakuwa ni Katibu na Naibu
Katibu wa Kamati ya Uongozi.
(3) Majukumu ya Kamati ya Uongozi yatakuwa kama
ifuatavyo:
(a) kujadili na kuamua kuhusu mambo yote yanayohusu
uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge Maalum na Kamati
zake;
(b) kujadili na kupanga ratiba ya utekelezaji wa Shughuli za
Bunge Maalum; na
(c) kujadili na kufanya uamuzi kuhusu masuala yatakayohitaji
usuluhishi na maridhiano.
59.-(1) Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum
itatekeleza majukumu yafuatayo:
(a) kujadili mapendekezo ya kuzifanyia marekebisho au
mabadiliko Kanuni za Bunge Maalum yaliyopelekwa kwenye
Kamati hiyo na Mwenyekiti, na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti
wa Bunge Maalum;
Muundo na
majukumu
ya Kamati
ya Uongozi
Majukumu
ya Kamati
ya Kanuni
na Haki
za Bunge
Maalum
Kanuni za Bunge Maalum
54
(b) kujadili na kutoa taarifa ya ufafanuzi, mwongozo au
utaratibu kwa Mwenyekiti kuhusu jambo lolote la kikanuni
litakalopelekwa kwenye Kamati hiyo na Mwenyekiti;
(c) kupokea, kusikiliza na kutolea maamuzi rufaa ya Mjumbe
yeyote ambaye hakuridhika na uamuzi wa Mwenyekiti;
(d) kuchunguza kuhusu masuala yote ya haki, kinga na
madaraka ya Bunge Maalum yatakayopelekwa kwenye
Kamati hiyo na Katibu, na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti
baada ya taarifa hiyo kuwasilishwa katika Bunge Maalum;
(e) kujadili na kumshauri Mwenyekiti kuhusu utekelezaji bora
wa haki, kinga na madaraka ya Bunge Maalum; na
(f) kushughulikia suala lolote linalohusiana na nidhamu ya
Mjumbe yeyote lililopelekwa kwenye Kamati hiyo na
Mwenyekiti.
(2) Bila ya kujali masharti ya Kanuni hii, wajumbe wa Kamati
hii wanaweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa Kamati nyingine
zilizoundwa kwa mujibu wa Kanuni hizi.
60. Kamati ya Uandishi itatekeleza majukumu yafuatayo:
(a) kuandika upya ibara zote za Sura za Rasimu ya Katiba
zilizojadiliwa na Bunge Maalum;
(b) kuandaa Rasimu ya Mwisho ya Katiba kama ilivyopitishwa
na Bunge Maalum kutokana na uamuzi wa Bunge Maalum
kuhusu taarifa za Kamati Namba Moja hadi Namba Kumi na
Mbili za Bunge Maalum; na
(c) kuwasilisha mbele ya Bunge Maalum, Rasimu ya Mwisho
ya Katiba iliyotajwa katika aya ya (b) ili ipigiwe kura ya mwisho
na kupitishwa na Bunge Maalum kwa ujumla wake.
Majukumu
ya Kamati
ya Uandishi
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Kanuni za Bunge Maalum
55
61. Kamati ya Mashauriano itatekeleza majukumu yafuatayo:
(a) shughuli zinazohusu Mashauriano au mwafaka juu ya
mambo yanayobishaniwa na Wajumbe wa Bunge Maalum;
(b) kutoa taarifa katika Bunge Maalum kuhusu mwafaka
uliofikiwa juu ya mambo yaliyowasilishwa kwenye Kamati hiyo.
Majukumu ya Kamati Namba Moja hadi Namba Kumi na
Mbili
62.-(1) Majukumu ya Kamati Namba Moja hadi Namba Kumi
na Mbili yatakuwa ni:
(a) kujadili mambo yote yaliyomo katika sura zote za Rasimu
ya Katiba;
(b) kuandaa taarifa ya Kamati kuhusu mambo yaliyojadiliwa
na Kamati; na
(c) kuwasilisha kwenye Bunge Maalum taarifa ya Kamati
inayojumuisha mambo yaliyoafikiwa na wajumbe walio
wengi na maoni ya wajumbe wa Kamati walio wachache.
(2) Bila kuathiri mjadala wa Sura ya Kwanza na ya Sita,
utaratibu wa kujadili Rasimu ya Katiba utakuwa ni kwa kila
Kamati kujadili Sura zote za Rasimu ya Katiba na Sura mpya
zitakazojitokeza.
63.-(1) Katika kipindi cha siku saba baada ya Kanuni hizi
kupitishwa, Bunge Maalum kupitia Kamati ya Uongozi ya
Bunge Maalum itaandaa ratiba ya utekelezaji wa kazi na
majukumu ya Bunge Maalum na Kamati zake, kwa kuzingatia
muda uliowekwa na Sheria.
(2) Ratiba ya utekelezaji wa kazi na majukumu ya Bunge
Maalum iliyoandaliwa kwa mujibu wa fasili ya (1) ambayo
itaitwa “Ratiba ya Shughuli” itatekelezwa kama sehemu ya
Kanuni hizi.
Majukumu
ya
Kamati
ya
Mashauri
-ano
Majukumu
ya
Kamati
Namba
Kumi na
Mbili
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Upangaji
wa ratiba
ya
utekelezaji
wa kazi
na
majukumu
ya Bunge
Maalum
Sura 83
Kanuni za Bunge Maalum
56
(3) Endapo itatokea haja ya kuifanyia marekebisho,
pendekezo la kuifanyia marekebisho ratiba hiyo ya shughuli
litajadiliwa na kufanyiwa uamuzi na Kamati ya Uongozi ya
Bunge Maalum.
64.-(1) Mambo yote yatakayojadiliwa na Kamati
yataamuliwa kwa kuungwa mkono na theluthi mbili ya
Wajumbe wote wa Kamati kutoka Tanzania Bara na theluthi
mbili ya Wajumbe wote wa Kamati kutoka Tanzania Zanzibar.
Isipokuwa uamuzi hata kama haukufikia theluthi mbili suala
hilo litapelekwa kwenye Bunge Maalum.
(2) Mjumbe yeyote wa Kamati hataruhusiwa kuzungumzia
hadharani maoni ya Kamati kuhusu jambo lolote litakalokuwa
linashughulikiwa na Kamati kabla maoni hayo
hayajawasilishwa rasmi kwenye Bunge Maalum isipokuwa
kwa idhini ya Mwenyekiti wa Kamati.
(3) Kamati yoyote inaweza kuunda Kamati Ndogo kwa ajili
ya utekelezaji bora wa shughuli zake kadri itakavyoona
inafaa, na kila Kamati Ndogo itapangiwa kazi zake na Kamati
inayohusika.
(4) Kila Kamati itakuwa na jukumu la kujadili maudhui ya Sura
za Rasimu ya Katiba zilizopo kwenye mjadala wa wakati huo
na kuandaa taarifa ya Kamati itakayowasilishwa katika
Bunge Maalum.
(5) Bila ya kujali iwapo umepangwa muda maalum au la
kwa ajili ya Kamati kujadili maudhui ya Rasimu ya Katiba,
Mwenyekiti wa Kamati anaweza kuufupisha mjadala huo
endapo ataona unarefushwa bila sababu ya msingi wala
tija yoyote.
65.-(1) Utakuwa ni wajibu wa kwanza kwa kila Mjumbe wa
Kamati kuhudhuria vikao vya Kamati kwa wakati uliopangwa
na atasaini binafsi karatasi ya mahudhurio iliyoandaliwa kwa
madhumuni hayo.
Utaratibu
wa kufanya
uamuzi
katika
Kamati
Wajibu wa
Mjumbe
kuhudhuria
vikao na
ukomo wa
Kamati
Kanuni za Bunge Maalum
57
(1A) Kila baada ya kikao cha Kamati, Katibu wa Kamati
atawasilisha karatasi ya mahudhurio iliyosainiwa na wajumbe
wa Kamati kwa Katibu wa Bunge Maalum.
(1B) Mjumbe ambaye saini yake haitaonekana katika karatasi
ya mahudhurio bila sababu iliyokubalika na Mwenyekiti au
Mwenyekiti wa Kamati, Mjumbe hatalipwa posho yoyote ya
vikao na ya kujikimu, na endapo posho itakuwa ilishalipwa
kwa Mjumbe huyo, basi posho hiyo itakatwa kutoka katika
malipo ya Mjumbe yanayofuata.
(2) Mjumbe yeyote ambaye hatahudhuria vikao vitatu
mfululizo vya Kamati bila sababu zozote za msingi, atapewa
onyo na Mwenyekiti wa Kamati, na endapo ataendelea
mara mbili au zaidi kutohudhuria vikao vya Kamati baada
ya kupewa onyo, Mwenyekiti wa Kamati atalipeleka jina lake
kwa Mwenyekiti ili aliwasilishe katika Kamati ya Kanuni na Haki
za Bunge Maalum kupata ushauri wa hatua za kinidhamu
zinazofaa kuchukuliwa dhidi yake.
(3) Mjumbe ambaye jina lake litapelekwa kwenye Kamati
ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum kwa mujibu wa fasili ya
(2) anaweza kupewa adhabu au kuchukuliwa hatua yoyote
ya kinidhamu itakayopendekezwa na Kamati hiyo.
(4) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa fasili ya (2), Mjumbe
yeyote mwenye udhuru, atalazimika kutoa taarifa ya
maandishi kwa Mwenyekiti na nakala kwa Mwenyekiti wa
Kamati na Katibu kuhusu kutohudhuria kwake, na taarifa hiyo
itahifadhiwa na Kamati kwa ajili ya kumbukumbu.
(5) Kamati zilizoundwa kwa mujibu wa Kanuni hizi zitakoma
baada ya maisha ya Bunge Maalum kufikia ukomo wake.
Azimio la
Bunge
Maalum la
tarehe
05/08/2014
Kanuni za Bunge Maalum
58
SEHEMU YA SABA
UTARATIBU WA KUTUNGA MASHARTI YA MPITO NA MASHATI
YATOKANAYO
66.-(1) Mamlaka ya Bunge Maalum ya kutunga masharti ya
mpito na masharti yatokanayo yatatekelezwa kwa Bunge
Maalum kujadili na kupitisha masharti hayo kwa mujibu wa
masharti ya Kanuni hii.
(2) Baada ya Bunge Maalum kukamilisha kazi ya kupitisha
Katiba inayopendekezwa, Mwenyekiti au Mjumbe wa Kamati
ya Uandishi atawasilisha hoja ya kutunga masharti ya mpito
na masharti yatokanayo kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa
na Bunge Maalum kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na
Kanuni hizi.
(3) Kwa madhumuni ya kanuni hii, “masharti ya mpito” na
“masharti yatokanayo” maana yake ni masharti yaliyowekwa
katika Sura ya Kumi na Saba ya Rasimu ya Katiba.
(4) Utaratibu wa kutunga masharti ya mpito na masharti
yatokanayo utafuata utaratibu uliotumika kupitisha Sura
nyingine za Rasimu ya Katiba.
SEHEMU YA NANE
AMANI NA UTULIVU BUNGENI
67.-(1) Mwenyekiti atakuwa na mamlaka na wajibu wa
kuhakikisha kuwa, utaratibu bora unafuatwa katika Bunge
Maalum na uamuzi wa Mwenyekiti kuhusu jambo lolote la
utaratibu utakuwa ni wa mwisho.
(2) Mjumbe yeyote atakayekiuka utaratibu uliowekwa na
Kanuni hizi anaweza papo hapo kutakiwa na Mwenyekiti
afuate utaratibu, na vilevile Mjumbe mwingine yeyote
anaweza kusimamia na kumfahamisha Mwenyekiti kuhusu
ukiukwaji wa utaratibu na katika kufanya hivyo, atalazimika
kutaja Kanuni ya Bunge Maalum iliyoweka utaratibu
uliokiukwa.
Utaratibu
wa kutunga
masharti ya
mpito na
masharti
yatokanayo
Mamlaka
ya
Mwenyekiti
kusimamia
utaratibu
Kanuni za Bunge Maalum
59
68.-(1) Mjumbe yeyote atakayekiuka Kanuni yoyote ya Kanuni
hizi au atakayezungumzia jambo au mambo ambayo
hayaruhusiwi na Kanuni hizi, anaweza kuamriwa na
Mwenyekiti ajirekebishe mara moja na kama atakaidi,
Mwenyekiti atamwamuru akatishe maelezo yake na kukaa
mahali pake.
(2) Bila ya kujali masharti ya fasili ya (1), Mwenyekiti anaweza
kutoa onyo kwa Mjumbe yeyote aliyefanya kosa la kukiuka
utaratibu uliowekwa na Kanuni hizi, au kosa la kuvuruga
majadiliano kwenye Bunge Maalum au uendeshaji bora wa
Shughuli za Bunge Maalum.
(3) Endapo Mjumbe yeyote atatumia maneno au lugha
isiyotakiwa kwenye Bunge Maalum, yaani lugha ya matusi,
usafihi, uchokozi au lugha ya maudhi, na akitakiwa na
Mwenyekiti kujirekebisha kwa kufuta maneno au lugha hiyo
akikataa kufanya hivyo, Mwenyekiti anaweza kumwamuru
Mjumbe huyo atoke mara moja nje ya ukumbi wa Mkutano
wa Bunge Maalum na abaki huko nje kwa muda wote
uliosalia wa kikao cha siku hiyo.
(4) Baada ya kutumia madaraka yake chini ya fasili ya (3),
Mwenyekiti atawasilisha shauri husika kwenye Kamati ya
Kanuni na Haki za Bunge Maalum kwa ajili ya kutoa fursa kwa
Kamati hiyo kusikiliza shauri husika na kutoa kwa Mjumbe
husika haki ya kusikilizwa.
69.-(1) Mwenyekiti anaweza kutaja jina la Mjumbe yeyote
kwamba amedharau Mamlaka ya Mwenyekiti na kupeleka
jina hilo kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum
ikiwa:
(a) kwa maneno au vitendo, Mjumbe huyo anaonesha
dharau kwa mamlaka ya Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti
wa Bunge Maalum;
(b) Mjumbe huyo kwa makusudi atafanya kitendo chochote
cha kudharau Shughuli za Bunge Maalum au kuvuruga
mwenendo wa Shughuli za Bunge Maalum.
Adhabu
zinazoweza
kutolewa
na
Mwenyekiti
kwa
ukiukwaji
wa Kanuni
Adhabu
zinazoweza
kutolewa
na Bunge
Maalum
kwa
ukiukaji
wa Kanuni
Kanuni za Bunge Maalum
60
(2) Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum itajadili suala
hilo, na ikithibitika kuwa Mjumbe husika ametenda kosa,
inaweza kushauri kwamba:
(a) ikiwa ni kosa lake la kwanza, Mjumbe huyo asihudhurie
vikao vya Bunge Maalum visivyozidi vitatu; au
(b) ikiwa ni kosa lake la pili au zaidi, Mjumbe huyo asihudhurie
vikao vya Bunge Maalum visivyozidi vitano.
(3) Bunge Maalum linaweza kuzingatia ushauri mwingine
wowote utakaotolewa na Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge
Maalum kuhusu adhabu anayostahili kupewa Mjumbe
aliyetenda kosa kwa mujibu wa masharti ya kanuni hii.
(4) Bila ya kujali masharti ya fasili ya (4), Bunge Maalum
linaweza kumchukulia hatua nyingine za kinidhamu Mjumbe
yeyote aliyetenda kosa chini ya kanuni hii, kwa mujibu wa
mapendekezo ya Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge
Maalum.
(5) Adhabu yoyote itakayotolewa kwa Mjumbe aliyekiuka
masharti ya kanuni hii itatolewa kupitia Azimio la Bunge
Maalum ambalo litataja adhabu hiyo pamoja na sababu
zake.
(6) Mjumbe aliyeadhibiwa kwa mujibu wa masharti ya Kanuni
hii, atatoka mara moja katika ukumbi wa Mkutano wa Bunge
Maalum, baada ya adhabu yake kutolewa.
70. Endapo Mjumbe yeyote atavunja au atajaribu kuvunja
utaratibu au amani na utulivu kwenye Bunge Maalum au
ataonyesha tabia za vurugu kwa kutumia nguvu na mabavu
ndani ya ukumbi wa Mkutano wa Bunge Maalum, Mwenyekiti
ataamuru Mpambe wa Bunge Maalum amtoe mara moja
Mjumbe huyo nje na asihudhurie vikao vya Bunge Maalum
na Kamati zake kwa muda wa siku tatu.
Mamlaka
kuhusu
amani na
utulivu
katika
Bunge
Maalum
Kanuni za Bunge Maalum
61
71. Mjumbe aliyesimamishwa kuhudhuria vikao atatoka katika
ukumbi wa Mkutano wa Bunge Maalum na hataingia tena
katika sehemu yoyote ya ukumbi wa Mkutano wa Bunge
Maalum na maeneo ya Bunge Maalum na pia hatahudhuria
vikao vyovyote vya Kamati kwa muda wote atakapokuwa
amesimamishwa, na hatalipwa posho nyingine yoyote
isipokuwa posho ya kujikimu.
72. Bila kujali masharti yaliyowekwa na Sehemu hii, endapo
Mjumbe aliyeadhibiwa ataomba radhi kwa makosa
aliyoyafanya, Mwenyekiti anaweza kumsamehe baada ya
kuzingatia maoni ya Wajumbe kupitia Kamati ya Kanuni na
Haki za Bunge Maalum.
73.-(1) Kwa madhumuni ya kudhibiti fujo endapo itatokea
ndani ya ukumbi wa Bunge Maalum na iwapo Mwenyekiti
ataona kuwa kuna haja ya kutumia nguvu, basi anaweza
kuahirisha shughuli za Bunge Maalum bila ya hoja yoyote
kutolewa, au anaweza kusitisha kikao kwa muda
atakaoutaja, ili fujo hiyo iweze kudhibitiwa na Mpambe wa
Bunge Maalum.
(2) Baada ya utulivu kurudia, Mwenyekiti atalipeleka kwenye
Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum suala ambalo
lilisababisha kutokea kwa fujo ikiwa ni pamoja na jina la
Mjumbe au majina ya Wajumbe waliohusika na fujo hiyo ili
Kamati hiyo iweze kuzingatia suala hilo na kulishauri Bunge
Maalum hatua za kuchukua.
74. Kila Mjumbe atatakiwa kutunza amani na utulivu ndani
na nje ya ukumbi wa Mkutano wa Bunge Maalum na kutoa
taarifa pale anapoona amani hiyo inatoweka.
SEHEMU YA TISA
WAGENI
75.-(1) Mwenyekiti anaweza kumwalika Mgeni Rasmi
kulihutubia Bunge Maalum.
Masharti
kwa Mjumbe
aliyesimamishwa
kuhudhuria
vikao
Mamlaka ya
msamaha
wa
Mwenyekiti
Udhibiti wa
fujo kwenye
Bunge
Maalum
Wajibu wa
Mjumbe
kutunza
amani na
utulivu
kwenye
Bunge
Maalum
Mgeni
Rasmi
Kanuni za Bunge Maalum
62
(2) Endapo Mwenyekiti amemwalika Mgeni Rasmi kuhudhuria
na kulihutubia Bunge Maalum kwa mujibu wa fasili ya (1),
Katibu ataweka utaratibu utakaomwezesha Mgeni Rasmi
kuingia na kuhutubia Bunge Maalum.
(3) Bila kuathiri masharti ya fasili ya (1) na ya (2), Mwenyekiti
kwa kushauriana na Kamati ya Uongozi anaweza kumwalika
Mgeni maalum kuhudhuria vikao vya Bunge Maalum na
atakaa sehemu yoyote ndani ya ukumbi wa Bunge Maalum
kama atakavyoelekezwa na Mwenyekiti.
76.-(1) Wageni wanaweza kuruhusiwa kuingia kwenye ukumbi
wa Mkutano wa Bunge Maalum katika sehemu yoyote ya
ukumbi huo ambayo itatengwa kwa ajili hiyo na kwa
kuzingatia mahitaji ya Wageni wenye mahitaji maalum.
(2) Wageni wakiwa ndani ya ukumbi wa Mkutano wa Bunge
Maalum watalazimika kufuata na kuzingatia masharti
yafuatayo:
(a) watakaa kimya na kwa heshima inayostahili hadi
watakapotoka nje ya ukumbi huo;
(b) wanapaswa wawe wamevaa mavazi ya heshima;
(c) wataingia na kutoka ukumbini kwa staha;
(d) inapolazimu kuzungumza, wasizungumze kwa sauti ya juu;
(e) wasivute sigara au kiko wakati wowote wakiwa ndani ya
ukumbi wa Mkutano wa Bunge Maalum au mahali popote
nje ya ukumbi huo ambapo kuna sehemu ya kukaa Wageni;
(f) wasiingie na kamera wala kupiga picha;
(g) wasishangilie wala kuzomea wakiwa ndani ya ukumbi wa
Mkutano wa Bunge Maalum; na
(h) wasifanye jambo au kitendo chochote ambacho
kinaweza kuvuruga amani na utulivu ndani ya Bunge Maalum.
Ruhusa ya
Wageni
kwenye
Bunge
Maalum
Kanuni za Bunge Maalum
63
(3) Mwenyekiti anaweza kumwamuru Mgeni yeyote atoke
nje ya ukumbi wa Mkutano wa Bunge Maalum endapo
atavunja sharti lolote kati ya masharti yaliyotajwa katika fasili
ya (2) ya Kanuni hii.
77.-(1) Katibu anaweza kutoa ruhusa maalum au ya jumla
kwa mwakilishi wa chombo chochote cha habari kuhudhuria
Vikao vya Bunge Maalum.
(2) Ruhusa yoyote itakayotolewa na Katibu inaweza
kuwekewa masharti yafuatayo:
(a) chombo husika kitoe maombi rasmi kwa maandishi; na
(b) chombo husika kiteue Waandishi wenye sifa na maadili
ya kuweza kuandika habari za Bunge Maalum.
(3) Katibu anaweza wakati wowote kuondoa ruhusa aliyotoa
kwa mwakilishi wa chombo chochote cha habari, iwapo
chombo hicho kitatoa taarifa yoyote kuhusu Shughuli za
Bunge ambayo, kwa maoni ya Bunge Maalum, inapotosha
ukweli au vinginevyo inakiuka Kanuni, taratibu au haki za
Bunge Maalum.
SEHEMU YA KUMI
USALAMA WA MAENEO YA BUNGE MAALUM
78.-(1) Mwenyekiti ataweka utaratibu wa kutoa vitambulisho
kwa Wajumbe wa Bunge Maalum, watumishi wa Bunge
Maalum, watumishi wa Serikali na kwa mtu mwingine yeyote
anayeingia kwenye ukumbi wa Mkutano au Maeneo
mengine ya Bunge Maalum.
(2) Katibu atatoa vitambulisho vya aina tofauti kwa ajili ya
Wajumbe wa Bunge Maalum, watumishi wa Bunge Maalum,
watumishi wa Serikali, wasaidizi wa Wajumbe wenye mahitaji
maalum na Wageni wanaokaribishwa katika ukumbi wa
Mkutano na maeneo mengine ya Bunge Maalum.
Ruhusa
kwa
Waandishi
wa Habari
Utaratibu
wa
kuingia
Maeneo
ya Bunge
Maalum
Kanuni za Bunge Maalum
64
79.-(1) Kutakuwa na utaratibu wa kumpekua mtu yeyote
anayeingia katika maeneo ya Bunge Maalum kwa kuzingatia:
(a) staha na heshima; na
(b) tofauti ya jinsia.
(2) Endapo katika kufanya ukaguzi, Mjumbe au mtu yeyote
atapatikana na kifaa ambacho kwa asili yake ni cha hatari,
Mjumbe au mtu huyo atakiacha kifaa hicho kwa walinzi
waliopo mlangoni.
(3) Bila kujali fasili ya (2), Mjumbe au mtu mwenye mahitaji
maalum ataruhusiwa kuingia kwenye Maeneo ya Bunge
Maalum na kifaa kinachomsaidia katika mahitaji yake
maalum.
(4) Mjumbe au mtu yeyote atakayekataa kukaguliwa au
kukabidhi kitu chochote ambacho walinzi wataona kwamba
kinazuiliwa, hataruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi wa
Mkutano wa Bunge Maalum au maeneo mengine ya Bunge
Maalum.
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
MENGINEYO
80.-(1) Lugha rasmi itakayotumika kwenye majadiliano ya
Bunge Maalum ni Kiswahili.
(2) Bila kuathiri fasili ya (1), Mjumbe anaweza kutumia lugha
ya Kiingereza kwa madhumuni ya kufanya nukuu au
kufafanua jambo.
81.-(1) Taarifa Rasmi ya Majadiliano kwenye Bunge Maalum,
ikiwa katika lugha iliyotumiwa na msemaji, yakiwa ni maneno
halisi aliyotamka, itatayarishwa chini ya usimamizi wa Katibu.
(2) Kila Mjumbe aliyetoa hotuba katika Bunge Maalum
atapewa nakala ya hotuba yake mapema iwezekanavyo,
ili aweze kusahihisha makosa ya uchapaji, kama yatakuwepo,
Upekuzi
Lugha
Rasmi
ndani ya
Bunge
Maalum
Taarifa
Rasmi za
Bunge
Maalum
Kanuni za Bunge Maalum
65
lakini hataruhusiwa kubadilisha maana halisi ya maneno
aliyoyasema ndani ya Bunge Maalum.
(3) Mjumbe yeyote atakayefanya masahihisho kwa mujibu
wa fasili ya (2) atarejesha masahihisho hayo kwa Katibu ndani
ya kipindi cha saa ishirini na nne na asiporejesha itachukuliwa
kuwa taarifa hiyo ni sahihi na itaingizwa kwenye Taarifa Rasmi
za Bunge Maalum.
82.-(1) Mjumbe anayeingia kwenye ukumbi wa Mkutano wa
Bunge Maalum au ukumbi mwingine wowote ambao kikao
cha Kamati kinafanyika, atawajibika kuvaa mavazi nadhifu
na yenye kuhifadhi heshima yake, hadhi ya Bunge Maalum
na utamaduni wa nchi, na yasiwe na alama au rangi
inayoashiria chama chochote cha siasa.
(2) Vazi Rasmi kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti
litakuwa ni mojawapo ya mavazi yaliyoainishwa katika fasili
ya (3)(a)(b) ya Kanuni hii, bila ya au na joho lenye kuonesha
rangi za Bendera ya Taifa na Nembo ya Taifa lililoshonwa
maalum kwa ajili hiyo, ambalo litavaliwa juu ya vazi lake.
(3) Vazi rasmi la Katibu na Naibu Katibu na Makatibu Wasaidizi
wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge Maalum litakuwa kama
ifuatavyo:
(a) Kwa Makatibu wanaume:
(i) suti kamili ya kiafrika au suti ya safari, yenye ukosi au shingo
ya mviringo na mikono mirefu au mifupi ya rangi nyeusi au
bluu, bila ya au na joho maalum la Makatibu Mezani;
(ii) suti kamili ya kimagharibi ya rangi nyeusi au bluu na shati
jeupe na tai, bila ya au na joho maalum la Makatibu Mezani.
(b) Kwa Makatibu wanawake:
suti ya rangi nyeusi au ya bluu na shati jeupe na tai, bila ya
au na joho maalum la Makatibu Mezani.
Mavazi
yanayoruhusiwa
Kanuni za Bunge Maalum
66
(4) Mpambe wa Bunge Maalum na wasaidizi wake ndani ya
Ukumbi wa Mkutano wa Bunge Maalum watavaa mavazi
rasmi ambayo yataamuliwa na Mwenyekiti.
(5) Mwenyekiti anaweza kwa sababu maalum, kumruhusu
mtu yeyote anayehusika na Shughuli za Bunge Maalum kuvaa
vazi ambalo sio rasmi.
(6) Mjumbe yeyote anaweza kutoa taarifa kwenye Bunge
Maalum au kwenye Kamati iwapo Mjumbe mwingine wa
Bunge Maalum ataingia kwenye ukumbi wa Mkutano wa
Bunge Maalum au ukumbi wa Kamati akiwa amevaa vazi
linalovunja au kukiuka masharti ya Kanuni hii.
(7) Mwenyekiti au Mwenyekiti wa Kamati atakaporidhika
kuwa Mjumbe aliyetolewa taarifa kwa mujibu wa fasili ya (6)
ya Kanuni hii hajavaa vazi linaloruhusiwa, ataamuru Mjumbe
huyo atoke nje ya ukumbi wa Bunge Maalum au ukumbi wa
Kamati.
(8) Mjumbe aliyetolewa nje kwa mujibu wa fasili ya (7) ya
Kanuni hii, hataingia ndani ya ukumbi wa Mkutano wa Bunge
Maalum au ukumbi wa Kamati hadi pale atakapokuwa
amevaa vazi linaloruhusiwa.
(9) Kwa madhumuni ya fasili hii, mavazi yanayoruhusiwa ni:
(a) kwa wanawake:
(i) vazi lolote la heshima ambalo si la kubana mwili, lisiloonesha
maungo ambalo kwa mila na desturi za kitanzania hayapaswi
kuoneshwa na ni refu kuvuka magotini;
(ii) gauni la kitenge au blauzi inayovaliwa na kitenge au sketi
ya rangi yoyote;
(iii) suti ya kike;
(iv) vazi linalovaliwa wakati wa eda;
Kanuni za Bunge Maalum
67
(v) kilemba cha kadiri au mtandio;
(b) kwa wanaume:
(i) suti ya kiafrika au safari ya mikono mirefu au mifupi yenye
ukosi au shingo ya mviringo na yenye fulana au bila fulana
ya ndani, ya rangi moja, isiyokuwa na nakshi pamoja au bila
baraghashia;
(ii) suti ya kimagharibi, shati na tai, suruali ya aina yoyote
isipokuwa jeans;
(iii) vazi la kimwambao yaani kanzu nadhifu yenye mikono
mirefu, koti, baraghashia na viatu vya wazi;
(iv) vazi rasmi la kidini.
83.-(1) Bila ya kujali masharti ya kifungu cha 20(4) cha Sheria,
Bunge Maalum na Kamati yoyote ya Bunge Maalum inaweza
kuomba kupata maelezo ya ufafanuzi kutoka Tume ya
Mabadiliko ya Katiba kuhusu jambo lolote katika utekelezaji
wa majukumu na mamlaka ya Bunge Maalum.
(2) Ufafanuzi kwa mujibu wa fasili ya (1) unaweza kutolewa
na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Mjumbe yeyote wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
84.-(1) Endapo Mjumbe atafariki wakati Bunge likiwa katika
shughuli zake, Mwenyekiti ataahirisha Shughuli za Bunge kwa
siku hiyo kwa ajili ya maombolezo.
(2) Nafasi iliyoachwa wazi na Mjumbe kutokana na sababu
yoyote haitazuia Bunge Maalum kuendelea na utekelezaji
wa majukumu yake.
85.-(1) Kwa idhini ya Mwenyekiti, Kanuni yoyote inaweza
kutenguliwa kwa madhumuni mahsusi baada ya Mjumbe
yeyote kutoa hoja kwa ajili hiyo.
(2) Maelezo ya hoja ya kutaka kutengua Kanuni yoyote
Ufafanuzi
kutoka
Tume
ya
Mabadiliko
ya Katiba
Nafasi ya
Mjumbe
kuwa wazi
Kutengua
Kanuni
Kanuni za Bunge Maalum
68
itakuwa ni pamoja na maelezo kuhusu madhumuni ya kutaka
Kanuni hiyo itenguliwe.
(3) Kanuni hiyo itatenguliwa kwa madhumuni yaliyokusudiwa
tu na siyo kwa madhumuni mengine yoyote.
(4) Mazingira ambayo yanaweza kusababisha Kanuni
itenguliwe ni kama yafuatayo-
(a) kuahirisha kikao kabla ya muda uliopangwa kutokana
na sababu mbalimbali;
(b) kuongeza muda zaidi ya uliopangwa kwa ajili ya shughuli
za siku hiyo;
(c) kuongeza muda zaidi kwa ajili ya shughuli za Bunge
Maalum;
(d) kuongeza orodha ya shughuli yoyote ambayo haikuwepo
kwenye mpangilio wa shughuli za siku hiyo.
86. Ukumbi wa Mkutano wa Bunge Maalum hautatumika
kwa shughuli nyingine yoyote, isipokuwa kwa shughuli ya
uendeshaji wa Mkutano na Vikao vya Bunge Maalum na
Kamati zake, na pia shughuli nyingine za Bunge Maalum.
87.-(1) Bunge Maalum linaweza kuzifanyia mabadiliko au
marekebisho Kanuni hizi kwa Azimio litakalowasilishwa kwenye
Bunge Maalum na Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki
za Bunge Maalum.
(2) Endapo Mjumbe ataona kuna haja ya Kanuni fulani
kufanyiwa mabadiliko au marekebisho, anaweza kuwasilisha
mapendekezo yake pamoja na sababu zake kwa Mwenyekiti
wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum ili yafanyiwe
kazi na Kamati hiyo, na kama yataonekana yanafaa,
yatawasilishwa kwenye Bunge Maalum kwa mujibu wa fasili
ya (1).
Matumizi
ya Ukumbi
wa
Mkutano
wa Bunge
Maalum
Kufanya
mabadiliko
au
marekebisho
katika
Kanuni
Kanuni za Bunge Maalum
69
________
NYONGEZA
________
KANUNI ZA UCHAGUZI WA MWENYEKITI NA
MAKAMU MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM
[Chini ya Kanuni ya 8(2)]
___________
SEHEMU YA KWANZAUTANGULIZI
1. Kanuni hizi zitaitwa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti na
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
2. Kanuni hizi zitatumika katika mchakato wa Uchaguzi wa
Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti.
3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa pale ambapo maelezo
yatahitajika vinginevyo-
“mgombea” maana yake ni Mjumbe aliyejitokeza au
aliyependekezwa na Mjumbe mwingine au Wajumbe
wengine wa Bunge Maalum kuwa mgombea wa Uchaguzi
wa nafasi ya Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti;
“Msimamizi wa Uchaguzi” maana yake ni Katibu wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano na Katibu wa Baraza la Wawakilishi
ambao kwa mujibu wa Kanuni hizi, wamepewa mamlaka ya
kuendesha na kusimamia mchakato wa Uchaguzi wa
Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti;
“Mwenyekiti” maana yake ni Mjumbe aliyechaguliwa kuwa
Mwenyekiti kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 23(1) cha
Sheria;
“Mwenyekiti wa Muda” maana yake ni Mjumbe
aliyechaguliwa kwa mujibu wa kifungu cha 22A cha Sheria;
“nafasi” maana yake ni nafasi iliyo wazi ya Mwenyekiti au
Makamu Mwenyekiti;
Jina
Matumizi
Tafsiri
Kanuni za Bunge Maalum
70
“nafasi ya nasibu” maana yake ni nafasi iliyo wazi ya
Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti isiyotokana na kuundwa
upya kwa Bunge Maalum;
“siku ya uteuzi” maana yake ni siku ambayo imetangazwa
na msimamizi wa uchaguzi kwamba ni siku ya mwisho ya
kupokea majina ya wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti au
Makamu Mwenyekiti;
“uchaguzi” maana yake ni uchaguzi wa Mwenyekiti na
Makamu Mwenyekiti.
SEHEMU YA PILI
USIMAMIZI WA UCHAGUZI NA UWASILISHAJI WA JINA LA
MGOMBEA WA NAFASI YA MWENYEKITI NA MAKAMU
MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM
4. Uchaguzi wa Mwenyekiti utaendeshwa na kusimamiwa na
Mwenyekiti wa Muda kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa
na Kanuni za Bunge Maalum, pamoja na Nyongeza hii.
5.-(1) Baada ya Kanuni kupitishwa, Mwenyekiti wa Muda
atatoa tangazo la uchaguzi wa Mwenyekiti, na Mjumbe
mwenye sifa ya kugombea nafasi hiyo atawasilisha jina lake
kwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano au Katibu
wa Baraza la Wawakilishi.
(2) Kila mgombea wa uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti,
atatakiwa kujaza fomu iliyoandaliwa kwa ajili hiyo kwa mujibu
wa Kanuni hizi, ambayo itakuwa na majina ya Wajumbe ishirini
wa Bunge Maalum wanaounga mkono mgombea husika,
kwa idadi ya Wajumbe kumi kwa kila upande wa Jamhuri ya
Muungano.
(3) Fomu za Wagombea wa uchaguzi wa nafasi ya
Mwenyekiti kwa mujibu wa masharti ya fasili ya (2)
zitawasilishwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi, ofisini kwake,
kabla ya saa nne asubuhi ya siku ya uteuzi.
Uchaguzi
wa
Mwenyekiti
Kuwasilisha
jina la
mgombea
Kanuni za Bunge Maalum
71
(4) Baada ya kupokea fomu za wagombea kwa mujibu wa
masharti ya fasili ya (3), Katibu wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano na Katibu wa Baraza la Wawakilishi-
(a) wataandaa majina ya wagombea wote na kuyabandika
mahali pa wazi katika maeneo ya Bunge Maalum;
(b) wataandaa karatasi za kura zinazoonyesha majina ya
wagombea wote wa uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti,
waliotimiza masharti yaliyowekwa na Kanuni za Bunge
Maalum, pamoja na masharti ya Kanuni hizi, na wakati wa
kupiga kura, atatoa karatasi moja tu ya kura kwa kila Mjumbe.
SEHEMU YA TATU
UPIGAJI WA KURA
6. Baada ya uteuzi kufanyika, mgombea yoyote hataruhusiwa
kujitoa katika nafasi aliyoomba.
7.-(1) Kila mjumbe atatakiwa kupiga kura ya siri kwa kuweka
alama ya vema “(“)” kwenye kisanduku kilichopo pembeni
mwa jina la mgombea anayemtaka na kutumbukiza karatasi
hiyo katika sanduku maalum la kura lililoandaliwa kwa ajili
hiyo.
(2) Baada ya kuridhika kwamba Wajumbe wote wamepiga
kura na kutumbukiza karatasi zao za kupigia kura kwenye
masanduku ya kura, Katibu atayakusanya masanduku yote
na kuyapeleka kwenye chumba maalum cha kuhesabia
kura, na kura zitahesabiwa mbele ya Wawakilishi walioteuliwa
na wagombea, mmoja kwa kila mgombea.
(3) Mgombea atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa
Mwenyekiti kama atapata wingi wa kura za Wajumbe wote,
na iwapo hakutakuwa na mgombea aliyepata wingi wa kura,
uchaguzi utarudiwa:
Isipokuwa kwamba, ni wagombea wawili tu watakaokuwa
wamepata kura nyingi zaidi ndio watakaopigiwa kura, na
Kujitoa
katika
uchaguzi
Upigaji
wa
kura
Kanuni za Bunge Maalum
72
katika hatua hiyo, mgombea atakayepata kura nyingi zaidi
atatangazwa kuwa ndiye mshindi.
(4) Endapo wagombea wawili au zaidi watapata kura sawa,
basi wagombea hao tu ndio watakaopigiwa kura, na
mgombea atakayepata kura nyingi zaidi atatangazwa kuwa
ndiye mshindi.
(5) Iwapo wagombea wawili au zaidi watapata kura sawa
katika nafasi ya pili na yule wa kwanza hakupata zaidi ya
nusu ya kura zilizopigwa, basi wagombea hao wawili pamoja
na yule wa kwanza ndio watakaopigiwa kura, na mgombea
atakayepata kura nyingi zaidi atatangazwa kuwa ndiye
mshindi.
(6) Endapo awamu ya pili ya upigaji wa kura itashindwa
kumpata mshindi, basi Mwenyekiti wa muda atapiga kura
yake ya uamuzi ili mshindi apatikane.
(7) Endapo kutakuwa na mgombea mmoja tu, basi
mgombea huyo atapigiwa kura ya “Ndiyo” au “Hapana”,
na atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti
iwapo atapata kura za “Ndiyo” za idadi ya zaidi ya nusu ya
kura za Wajumbe wote.
8. Mara baada ya mshindi kupatikana, Msimamizi wa
Uchaguzi atamtangaza Mwenyekiti aliyechaguliwa, na
Mwenyekiti huyo Mteule ataapa viapo vilivyowekwa kwa
mujibu wa Sheria na Kanuni za Bunge Maalum.
9. Mara baada ya uchaguzi wa Mwenyekiti, Mwenyekiti wa
Muda atatoa tangazo la uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti
na utaratibu wa uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti utafuata
utaratibu wa uchaguzi wa Mwenyekiti kama ulivyoainishwa
katika Nyongeza hii.
Kutangaza
matokeo
ya
uchaguzi
Sura 83
Uchaguzi
wa
Makamu
Mwenyekiti
Kanuni za Bunge Maalum
73
FOMU YA KUGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI/MAKAMU
MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM
(Chini ya Kanuni 5(2) ya Nyongeza)
(Ijazwe na Mgombea)
A: MAELEZO BINAFSI YA MGOMBEA
Mimi………………………………………….…………….…naomba
kugombea nafasi ya Mwenyekiti/Makamu Mwenyekiti wa
Bunge Maalum.
1. Jina kamili: ....................................................................................
2. Umri:................................................................................................
3. Jinsi:................................................................................................
4. Anuani:……………………………………………….……...………
5. Kazi:…………………………………………………………...….……
B: ELIMU YA MGOMBEA
……………………………………………………………………………..…..……
………………………………………………………………………………..……..
………………………………………………………………………………..……..
C: UZOEFU
………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………..…..
…………………………………………………………………………………..…..
Kanuni za Bunge Maalum
74
D: UADILIFU
Je, umewahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote linalohusu kukosa
uaminifu na maadili?
Kama ndio (eleza aina ya kosa na adhabu iliyotolewa)
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
E: TAMKO LA MGOMBEA
Mimi………………………….……………….………..…….
nathibitisha kuwa maelezo yote yaliyopo hapo juu ni ya ukweli
Mbele ya Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano au
Katibu wa Baraza la Wawakilishi
Leo tarehe …………………
Saini ya Mgombea Saini ya Shahidi
…………………………. ....………………………
Ndiyo
Hapana
Kanuni za Bunge Maalum
75
MAOMBI HAYA YANAUNGWA MKONO NA WAJUMBE
WAFUATAO:
A: WAJUMBE KUTOKA TANZANIA BARA
B: WAJUMBE KUTOKA TANZANIA ZANZIBAR
Na. Jina Saini
1.
2.
3.
4.
5.
6.
7.
8.
9.
10.
Na. Jina Saini
1.
2.
3.
4.
5.
6.
7.
8.
9.
10.
Kanuni za Bunge Maalum
76
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE MAALUM
KIAPO CHA MJUMBE
(Chini ya Kifungu cha 23(7) Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,
Sura ya 83 na
kanuni ya 10(1) ya Kanuni za Bunge Maalum)
Mimi,……………...............................................................................,
niliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum, naapa/
nathibitisha kwamba nitakuwa mwaminifu na mtiifu kwa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kadri ya uwezo
na ufahamu wangu, nitatimiza wajibu wangu na kufanya kazi
zinazonihusu bila ya upendeleo.
Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie.
Ameapishwa na kuweka saini yake mbele yangu
…………………………………….….
MWENYEKITI
Tarehe……………Mwezi Machi, 2014
Kanuni za Bunge Maalum
77
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE MAALUM
KIAPO KWA MJUMBE ASIYEAMINI KUWEPO KWA MUNGU
(Chini ya Kifungu cha 23(7)) Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba, Sura ya 83 na
kanuni ya 10(3) ya Kanuni za Bunge Maalum)
__________
Mimi,………………………………………………………………………,
niliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum, natamka kwa
dhati/nathibitisha kwamba, nitakuwa mwaminifu na mtiifu
kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kadri ya
uwezo na ufahamu wangu, nitatimiza wajibu wangu na
kufanya kazi zinazonihusu bila ya upendeleo.
…………………………………………….
MJUMBE
Ameapishwa na kuweka saini yake mbele yangu
……………………………………………….….
MWENYEKITI
Tarehe……………Mwezi Machi, 2014
Kanuni za Bunge Maalum
78
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE MAALUM
KIAPO CHA MJUMBE AMBAYE NI MWENYEKITI AU MAKAMU
MWENYEKITI
(Chini ya Kifungu cha 23(7) Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,
Sura ya 83 na kanuni ya 9(1) ya Kanuni za Bunge Maalum)
Mimi,……………...............................................................................,
niliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum, naapa/
nathibitisha kwamba nitakuwa mwaminifu na mtiifu kwa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kadri ya uwezo
na ufahamu wangu, nitatimiza wajibu wangu na kufanya kazi
zinazonihusu bila ya upendeleo.
Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie.
……………………………………………
MJUMBE
Ameapishwa na kuweka saini yake mbele yangu
……………………………………………….….
KATIBU
Tarehe……………Mwezi Machi, 2014
Kanuni za Bunge Maalum
79
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE MAALUM
KIAPO CHA MWENYEKITI AU MAKAMU MWENYEKITI
(Chini ya Kifungu cha 23(7) Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,
Sura ya 83 na
kanuni ya 10(1) ya Kanuni za Bunge Maalum)
Mimi,……………...............................................................................,
niliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa
Bunge Maalum, naapa/nathibitisha kwamba nitakuwa
mwaminifu na mtiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na kwa kadri ya uwezo na ufahamu wangu, nitatimiza wajibu
wangu na kufanya kazi zinazonihusu bila ya upendeleo.
Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie.
…………………………………………….
MWENYEKITI/MAKAMU MWENYEKITI
Ameapishwa na kuweka saini yake mbele yangu
……………………………………………….….
KATIBU
Tarehe……………Mwezi Machi, 2014
Kanuni za Bunge Maalum
80
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE MAALUM
UCHAGUZI WA MWENYEKITI NA MAKAMU MWENYEKITI
__________________________
KARATASI YA KURA
__________
(Chini ya kifungu cha 23 cha Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba, Sura ya 83)
Weka alama ya (“) kwenye jina moja tu.
Kanuni hizi zimepitishwa kwa Azimio la Bunge Maalum la
tarehe 11 Machi, 2014
Dodoma,………………….., 2014 PANDU AMEIR KIFICHO
Mwenyekiti wa Muda wa
Bunge Maalum
NA. JINA ALAMA
1.
2.
3.
4.

0 comments:

Post a Comment