BUNGE MAALUMU LA KATIBA

Posted by Arusha by day and by night On 01:56 No comments

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE MAALUM
________
MAELEZO KUHUSU BUNGE MAALUM
MAELEZO KUHUSU BUNGE MAALUM
1.0 UTANGULIZI:
Bunge Maalum linatarajia kuanza vikao vyake tarehe 18 Februari, 2014 katika Ukumbi wa Bunge. Mkutano huo utajumuisha Wajumbe 629 ambao wanapatikana kwa mchanganuo ufuatao:-
(i) Wabunge wote wa Bunge la Jahmuri ya Muungano wa Tanzania 357;
(ii) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi 82;
(iii) Wajumbe wa Kuteuliwa kwa uwakilishi 201
640
Katika idadi hiyo unapunguza wafuatao:-
 Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ambao pia ni Wajumbe wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (6);
 Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa uteuzi wa Rais wa Zanzibar (1)
 Wabunge waliofariki hivi karibuni (2)
 nafasi mbili (2) za uteuzi wa Rais zilizo wazi (2)
Jumla ya Wajumbe waliopo kwa sasa 629
3
Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Namba 83 ya Mwaka 2013, Kifungu cha 24 (2) imetoa mamlaka kwa Katibu wa Bunge na Katibu wa Baraza la Wawakilishi kufanya maandalizi ya muhimu ya kuanza kwa Bunge Maalum.
Kifungu hicho cha 24 (2) kinasomeka “Bila kujali masharti ya Kifungu kidogo cha (1), Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katibu wa Baraza la Wawakilishi kabla ya Bunge Maalum kuitishwa, watafanya maandalizi muhimu kwa utekelezaji bora wa Shughuli za Bunge Maalum”.
Hivyo, nachukua fursa hii kuwajulisha maendeleo ya hatua za maandalizi kama ifuatavyo:-
(1) USAJILI
Tayari zoezi la usajili limeanza tangu leo asubuhi saa 3:00 na mpaka kufikia saa 8:00 mchana idadi ya Wajumbe zaidi ya 120 walikuwa wameshasajiliwa. Zoezi la usajili litaendelea mpaka kesho jioni.
Baada ya hapo, usajili utakuwa ukifanyika kulingana na mahitaji iwapo kuna Wajumbe ambao kwa sababu moja au nyingine watakuwa bado hawajajisajili mpaka tutakapokuwa tunafunga zoezi hilo kwa utaratibu huo hapo kesho jioni.
4
(2) RATIBA YA BUNGE MAALUM:
Ratiba ya Bunge Maalum itaanza na Mkutano wa maelekezo kwa Wajumbe (briefing) saa 4:00 asubuhi siku ya Jumanne tarehe 18 Februari, 2014 katika Ukumbi wa Bunge. Baada ya hapo, kikao cha kwanza kitaanza saa 8:00 mchana kwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa muda. Shughuli nyingine zitakazofanyika ni:-
2.1 Mwenyekiti wa muda kusimamia uandaaji na upitishwaji wa Kanuni;
2.2 Mwenyekiti wa muda kusimamia uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti;
Ratiba kamili imeambatishwa na taarifa hii.
5
(3) HITIMISHO:
Kama ilivyoainishwa kwa Kifungu cha 28 (3) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Namba 83 ya mwaka 2013 kwamba “…… muda ambao Bunge Maalum litajadili Rasimu ya Katiba hautazidi siku sabini (70) kuanzia tarehe ambayo Bunge Maalum lilipoitishwa”
Aidha, Kifungu cha 28 (4) kinazungumzia uwezekano wa kuongeza muda “Mwenyekiti wa Bunge Maalum baada ya kushauriana na Makamu Mwenyekiti anaweza; kwa ridhaa ya Rais baada ya kushauriana na Rais wa Zanzibar kuongeza muda uliotolewa chini ya Kifungu Kidogo cha (3) kwa kipindi kitakachofaa kukamilisha shughuli za Bunge Maalum”.

0 comments:

Post a Comment