FIRST AFRICAN MOUNTAINS REGIONAL FORUM CALLS FOR MAINSTREAMING OF MOUNTAINS IN THE DEVELOPMENT AGENDA

Posted by Arusha by day and by night On 03:30 No comments

East African Community Headquarters, Arusha, Tanzania, 22 October 2014: The first African Mountains Regional Forum has started at Ngurdoto Mountain Lodge in Arusha, Tanzania. The three-day forum to take place from October 22-24 is to provide an opportunity for different sustainable mountain development stakeholders to enhance understanding of common conservation and development issues in the region.

The forum is organized by the Albertine Rift Conservation Society (ARCOS) and the Africa Mountain Partnership Champions Committee (AMPCC) in partnership with the East African Community (EAC), United Nations Environment Programme (UNEP), and other partners. Participants from African government institutions, academia, civil society, media and the private sector are in attendance.

Dr. Sam Kanyamibwa, the executive director of ARCOS, called the meeting “a celebration of the fragile mountain ecosystem.” 

Hon. Magessa Mulogo, the Arusha Regional Commissioner in a statement delivered by the District Commissioner Arumeru District, Mr. Deus Munasa, said Tanzania is well endowed with mid-range mountains including Mt. Kilimanjaro, Africa’s highest mountain, which attracts more than 35,000 climbers a year. 

“Mt. Kilimanjaro is also a home to some 1.5 million people with nearly three quarters depending on its rich nature resources for water, food and medicinal herbs,” he said.

He added, “Despite all these positive attributes, projections from various studies suggest that ice on Mount Kilimanjaro is receding and that if it continues at the present rate, the majority of the remaining glaciers on the mountain could vanish with dire consequences for the neighbouring communities.”

Hon. Jesca Eriyo, Deputy Secretary General (Productive and Social Sectors), East African Community, said the East African region has renown trans-boundary mountainous ecosystems including Africa’s highest mountain, Mt. Kilimanjaro at 5,400m at the border of Tanzania and Kenya, the Mt. Elgon, which bestride Kenya and Uganda; the Virunga shared by Rwanda, Uganda and Democratic Republic of Congo (DRC) amongst other national mountainous areas such as Mt. Kenya, Mt. Rwenzori in Uganda, Mt. Meru in Tanzania, Mt. Karisimbi in Rwanda.

“These ecosystems support employment and income for the communities drawing their livelihoods from the ecosystems and their services,” she said.

Hon. Eriyo revealed that the EAC, through the Lake Victoria Basin Commission (LVBC) is implementing a number of projects in the region’s mountain ecosystems. One such project is the Mt. Elgon Regional Ecosystem Conservation Programme (MERECP).

“The aim of the project is to promote sustainable use of shared natural resources benefiting livelihoods and mitigating and adapting to anticipated climate change impacts in the Mt. Elgon ecosystem by 2015,” said Hon.Eriyo. The MERECP is funded by the governments of the Royal Kingdom of Norway and Sweden.

Chapter 13 of Agenda 21 recognizes mountains as important sources of water, energy, minerals, forest and agricultural products and areas of recreation and “storehouses of biological diversity, home to endangered species and an essential part of the global ecosystem.”

Mountains cover 25 percent of the world’s land surface, and directly support 12 percent of the world’s population living within mountain regions, while about 40 per cent occupies watershed areas below. Mountains contribute an estimated 80% of downstream river flow, a main source of hydropower. 

Mountain people, who are among the poorest in the world, are key to maintaining these mountain ecosystems and the need for action to alleviate poverty in mountain regions.

Through their watershed function, mountains supply more than half of humanity with water for drinking, irrigation, industry, food and energy production. The degradation of mountain ecosystem services has severe consequences for livelihoods and environments of downstream regions.

Mr. Robert Wabunoha, the legal officer at United Nations Environment Programme (UNEP), noted that despite their importance throughout human history and their wealth of resources, mountains have only recently begun to attract the attention of political decision-makers and planners.

“At national level, most countries do not have specific policies, laws or institutions simply because they have not been recognized as unique ecosystems that might require special attention,” he said, and added, “this situation requires Africa’s immediate action and commitment in moving towards mountain governance and formulation of mountain specific laws, policies and institutions.

Their widespread and trans-boundary nature, also calls for regional cooperation in addressing this issues.” UNEP is supporting the preparation of the first African mountain atlas.

Experts at the forum are proposing policies and actions to protect and maintain fragile mountain ecosystems. These include promotion of sustainable use of mountains in order to ensure their global water supply function and to enhance their ability to moderate the impacts of climate change and natural hazards for the benefit of mankind.

They have also called for support of the concept of payment of ecosystem services (PES) for the benefit of mountain communities who provide these valuable ecosystem services to downstream users.

The African Mountains Regional Forum ends on Friday.

ENDS-

UJENZI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI,MADAWATI NA SHULE MAALUMU WILAYANI HAI

Posted by Arusha by day and by night On 05:13 No comments



HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI

MIKAKATI YA UJENZI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI, MADAWATI NA SHULE MBILI MAALUM ZA SEKONDARI

1.0    UTANGULIZI

Halmashauri ya Wilaya ya Hai inazo Shule 45 za sekondari – Shule za serikali ni 29 na Shule zisizo za serikali ni 16 tu zenye usajili.  Kati ya Shule 29 za Serikali ni shule mbili tu – Lyamungo (wavulana tu) na Machame (wasichana tu) – ndizo zenye kidato cha tano na sita.  Shule za sekondari 29 za serikali hadi mwezi Agosti 25, 2014 zilikuwa na jumla ya wanafunzi 11437 – wanafunzi 10019 wa shule za kutwa (Kidato cha I – IV) na wanafunzi 1418 wa shule mbili za Bweni (Kidato cha V – VI).

Aina ya Shule
Wavulana
Wasichana
Jumla
Kutwa (Kidato I – IV)
4686
5333
10019
Bweni (Kidato V – VI)
922
496
1418
Jumla
5608
5829
11437

Yapo maelekezo ya Mkoa na Taifa kuwa ifikapo mwishoni mwa mwaka 2014, kila Wilaya iwe imetekeleza yafuatayo:
v  Kujenga au kuimarisha maabara za masomo ya sayansi kwa shule zote za Serikali – Wilaya ya Hai zipo shule 29 tu. 
v  Kuteua shule mbili na kuendeleza miundombinu yake, ambazo zinatakiwa kuwa shule maalum na za mfano kwa masomo ya sayansi kwa wilaya – shule ya wasichana na shule ya wavulana.
v  Shule zote za Msingi na Sekondari zisiwe na upungufu wa madawati.

2.0      HALI YA MAABARA SHULENI NA MIKAKATI YA UJENZI WAKE

2.1      Hali ya Uwepo wa Maabara Katika Shule za Sekondari

Halmashauri ya wilaya ya Hai katika shule zake 29 za sekondari inao uhaba mkubwa wa maabara halisi ambapo ni shule nane (8) tu zenye maabara halisi na shule 19 zinatumia vyumba vilivyoboreshwa “Science Rooms” kufundishia masomo ya sayansi kwa vitendo (Science practicals).  Shule sita tu zilipewa “Mobile Laboratories” kwa ajili ya masomo ya Sayansi kwa vitendo (Kiambatisho “A”, “B” na “C”).  Pamoja na upungufu mkubwa wa maabara halisi za sayansi bado wanafunzi wa shule zetu wanasoma masomo ya Sayansi kwa vitendo (Science practicals) na hata kufanya mitihani yao ya mwisho ya kidato cha IV na cha VI kwa vitendo (Real Practicals) na sio “Alternative to Practicals”.  Hatua hii inastahili pongezi kwa Halmashauri, walimu na wanafunzi wetu.

2.2    Mikakati ya Uboreshaji na Ujenzi wa Maabara Shuleni 

Halmashauri ya Wilaya ya Hai katika kutafsiri maelekezo ya Mkoa na Taifa inapendekeza hatua za dharura zifuatazo zichukuliwe ili kujenga maabara mpya, kuboresha vyumba vya madarasa maalum (Science Rooms) na kukamilisha ujenzi wa maabara kwa baadhi ya shule unaoendelea:

Ø  Kila jamii ya shule ielekezwe kujenga maabara moja itakayotumika kwa masomo yote matatu “Multipurpose Laboratory” sawa na ramani iliyopendekezwa na kutolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (WEMU).  Maabara ya aina hii inaaminika kuwa ya gharama ndogo ukilinganisha na maabara ya vyumba vitatu tofauti.  “Multipurpose Laboratory” inakisiwa kutumia kiasi cha Tsh. 45,000,000.00 hadi kukamilika ikiunganishwa na nguvu kazi za wananchi (Kiambatisho “D”);
Ø  Kila jamii ya shule husika isiyo na maabara halisi wamelekezwa kuimarisha vyumba maalum vinavyotumika (science rooms) kwa kujenga miundombinu ya kimaabara ndani ya chumba husika ili kiwe na sifa ya “Multipurpose Laboratory” kwa kuanzia;
Ø  Kuhimiza na kuhamasisha jamii za shule kukamilisha ujenzi wa maabara unaoendelea katika baadhi ya shule kwa kuendesha harambee na michango ya hiari kwa wadau wote wa elimu katika maeneo yao;
Ø  Ofisi ya Mkuu wa Wilaya iunde “Task Forces” zitakazohusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama (W) na Watendaji wa Halmashauri zitakazofuatilia ikiwa Viongozi wa Kata na vijiji wanachangisha michango na ujenzi unasimamiwa ipasavyo siku hadi siku kwa kila shule husika;
Ø  Asilimia 30 za mapato ya ndani yaliyotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo zitatumika kujengea maabara;
Ø  Fedha za CDG kwa mwaka 2014/2015 za vijiji zinaelekezwa kuimarisha vyumba vya maabara.
3.0      UIMARISHAJI WA SHULE MBILI MAALUM ZA WILAYA

3.1      Sifa za Shule Mbili Maalum Zinazotakiwa

Maelekezo ya Mkoa juu ya kuteua shule mbili – wasichana na wavulana – ambazo zitakuwa maalum kwa wanafunzi maalum (wenye ufaulu wa juu ndani ya wilaya kwa Mtihani wa kuhitimu Darasa la VII), yametoa sifa zifuatazo kuzingatiwa:
*      Shule iwe na eneo la kutosha (sio chini ya ekari 5) ili kuruhusu upanuzi wa shule kwa kujenga miundombinu muhimu kwa shule yenye bweni/hosteli;
*      Kuwepo na shule nyingine jirani ili kuweza kuchukua wanafunzi wa Kata/vijiji husika ambao ufaulu wao hautafikia kiwango cha kuingia shule maalum ya jirani;
*      Shule iwe na mazingira ya kuwezesha upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii;
*      Shule zitakuwa ni za michepuo ya Sayansi – zitaweka mkazo zaidi katika masomo ya sayansi na Hisabati.

3.2.      Maamuzi ya Halmashauri ya Wilaya

Halmashauri ilipopitia sifa zilizoainishwa katika kipengele 3.1, imejiridhisha na shule mbili za sekondari – Kia na Mukwasa – kuwa zinastahili kuendelezwa na kuwa shule maalum kwa vigezo vilivyoainishwa:

3.2.1        Kia Sekondari – Shule Maalum ya Wavulana:
Ø  Inalo eneo la Ekari saba hivyo inaruhusu upanuzi wa shule;
Ø  Ipo karibu na Uwanja wa Kimataifa wa Ndege (KIA) ambao utakuwa kivutio kwa wanafunzi kupenda kujifunza sayansi;
Ø  Ni shule inayopokea wanafunzi wachache kila mwaka ambao ni rahisi kusomea katika shule tarajiwa ya Tambarare – Kijiji cha Mtakuja, Kata ya Kia.

3.2.2   Mukwasa Sekondari  -  Shule Maalum ya Wasichana:
Ø  Inalo eneo la Ekari 6.7 hivyo inaruhusu upanuzi wa shule;
Ø  Ipo katika kijiji cha Mungushi – kata ya Masama kusini, hivyo ni rahisi kufikika kutoka mji wa Bomang’ombe na kupata huduma muhimu za kijamii kwa urahisi;
Ø  Ni shule inayopokea wanafunzi wachache kila mwaka ambao ni rahisi kusomea katika shule jirani za Boma, Hai day na Lerai zilizopo katika Kata ya Hai Mjini.



3.3            Mikakati ya Kuimarisha Shule Mbili Maalum

Baada ya uteuzi wa shule mbili maalum kinachofuata ni kufanya tathmini na kutafuta namna bora na ya haraka ya kuziimarisha kwa miundombinu ya haraka ili zianze kupokea wanafunzi maalum wa kidato cha I, hapo Januari 2015.  Miundombinu inayohitajika kwa haraka kwa shule hizo ambayo haipo kwa sasa ni:
v  Mabweni yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kwa kuanzia kwa kila shule yenye thamani ya Tsh. 150,000,000.00 kila shule;
v  Maabara za masomo ya Sayansi – Multipurpose Laboratory yenye thamani ya Tsh. 45,000,000.00 kila shule;
v  Nyumba 2 – Mkuu wa Shule na Matron / Patron – kila shule, zenye thamani ya Tsh. 45,000,000.00 kila nyumba.

Katika kuhakikisha majengo haya yanajengwa kwa kila shule inahitajika jumla ya Tsh. 570,000,000.00.  Hivyo, mikakati iliyoamuliwa kutumika kwa ajili ya ujenzi na uimarishaji wa maabara ndio pia itumike katika zoezi hili la uimarishaji wa shule mbili maalum ambapo michango itokane na wananchi wote ndani ya Halmashauri na sio kwa kata husika tu.

4.0      MAPENDEKEZO YA UPATIKANAJI WA FEDHA ZA UJENZI

4.1      Makisio ya Awali ya Ujenzi wa Maabara na Shule Maalum

Katika kufanya makisio ya awali kwa kutumia viwango vya Mpango wa “MMES” imebainika kuwa jumla ya Tsh. 1,165,000,000.00 zinahitajika kukamilisha ujenzi wa maabara mpya na kuimarisha “Science rooms” zilizopo pamoja na kuongeza miundo mbinu muhimu kwa shule maalum sawa na mchanganuo ufuatao:
*      Ukamilishaji wa maabara ni Tsh. 685,000,000.00;
*      Ujenzi wa hosteli 4 katika shule mbili maalum ni Tsh. 300,000,000.00;
*      Ujenzi wa nyumba 4 za walimu katika shule mbili maalum ni Tsh. 180,000,000.00.

4.2      Njia za Kupata Fedha

Halmashauri ya Wilaya ya Hai, inakisiwa kuwa na jumla ya wakazi 210,533 – wanaume 102,457 na wanawake 108,076 – ambapo ni wakazi 96,355 (45.77%) – wanaume 45,876 na wanawake 50,479 – tu wenye uwezo wa kufanya kazi kwa bidii (Kiambatisho “C”).  Wengine ni watoto na wazee wanaokisiwa kutokuwa na uwezo wa kuchangia maendeleo ya maeneo yao.  Katika kupata fedha za ujenzi yafuatayo yameamuliwa:

Ø  Halmashauri ya Wilaya imependekeza kila mwananchi mwenye uwezo wa kufanya kazi atakiwe kuchangia kwa wastani wa Tsh. 12,000/= na wakuu wa Idara na Waheshimiwa madiwani wachangie kila mmoja jumla ya Tsh. 50,000/= ambapo jumla ya Tsh.  1,165,895,500.00 zitakusanywa kutoka kwa wakazi 96,355 na kutimiza lengo la ujenzi wa miundombinu hitajika

Ø  Waheshimiwa madiwani, Maafisa Tarafa, watendaji wa Kata na Vijiji, walezi wa Kata na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji kila mmoja kwa nafasi yake waelekezwe kuchukua hatua za makusudi kukusanya michango, kusimamia ujenzi na kuhakikisha maabara zinajengwa shuleni mapema iwezekenavyo;

Ø  Halmashauri iunde na kuanzisha Mfuko wa Elimu wa Wilaya ambao utahusika zaidi kutafuta wafadhili na wahisani pamoja na kuratibu na kusimamia utekelezaji wa mapema ili kufanikisha ujenzi wa maabara na shule maalum kwa haraka iwezekanavyo ikiwa ni pamoja na kuweka msukumo wa pekee katika ukamilishaji wa shule tano (5) za Kidato cha V – VI sawa na malengo ya wananchi ya awali ndani ya Halmashauri.

4.3     Utaratibu wa Kukusanya Michango ya Wananchi
4.3.1        Ujenzi wa miundombinu ya shule umegawanyika katika vipengele vitatu ambavyo ni kama ifuatavyo:
Ø  Ujenzi wa maabara  = Tsh. 685,000,000.00
Ø  Ujenzi wa shule mbili maalum za Wilaya = Tsh. 570,000,000.00
4.3.2            Inashauriwa michango kutoka kwa kila mwananchi mwenye uwezo wa kufanya kazi achangie jumla ya Tsh. 15,000.00 ambayo itachangwa kwa utaratibu na mgawanyo ufuatao:
Maelezo
Kata Husika (maabara)
Halmashauri (Shule 2  maalum)
Halmashauri (Shule za Kidato  V - VI)
Jumla
Kiasi cha Mchango kwa Mwananchi Mmoja
7,000.00
5,000.00
3,000.00
15,000.00
Asilimia (%)
46.67
33.33
20.00
100

4.3.3            Katika bajeti ya mwaka 2014/2015, Halmashauri imetenga fedha kuwezesha ujenzi wa maabara 8 za sayansi na ununuzi wa vifaa na madawa vya maabara katika shule 8 za sekondari:-  KIA, Kikafu, Sawe, Kyuu, Tumona, Nkuu, Lukani na Lemira  = Tsh. Tshs. 513,540,000.00.
4.3.4            Katika bajeti ya mwaka 2014/2015, Halmashauri imetenga fedha kuwezesha ujenzi wa hosteli 2 za wanafunzi katika shule 2 za sekondari:- KIA – 2 (O-level) = 200,000,000.00.

5.0   HALI YA MADAWATI KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
5.1   Shule za Msingi
Halmashauri ya wilaya ya Hai ina jumla ya shule 121 zikiwemo za binafsi 17 na 104 za serikali.  Katika shule za serikali, wapo jumla ya wanafunzi 14410 ambapo takwimu za madawati ni kama ifuatavyo kwa mwaka 2014:

MAHITAJI
YALIYOPO
UPUNGUFU
ASILIMIA
14,410
12,541
1,869
12.97%


5.1.1   Mikakati ya Kuondoa Upungufu

Katika kuhakikisha upungufu wa madawati katika Shule za Msingi unaondolewa, Halmashauri ya Wilaya imezielekeza Kamati za Shule kutekeleza yafuatayo:

*      kufanya ukarabati wa madawati 922 yaliyovunjika kwa kutumia kiasi cha 32% ya fedha za ukarabati kutoka katika “Capitation Grant”.
*      Kuhamasisha jamii, wadau wa Elimu hasa Taasisi /NGOs /CBOS katika kuchangia madawati halisi kwa kugharamia matengenezo ya madawati 947 mapya hasa kwa shule zenye upungufu mkubwa.

5.2   Shule za Sekondari
Katika shule za sekondari hakuna upungufu wowote wa madawati (viti na meza) ya wanafunzi kutokana na Sera ya Halmashauri iliyopo kwa mpango ufuatao:
*      Kuhakikisha wanafunzi wa Kidato cha I wanaleta kiti na meza kwa shule zinazopangiwa wanafunzi wengi kuliko idadi ya Kidato cha IV waliohitimu;
*      Wazazi kuchangia kiasi cha Tsh. 15,000/= kwa mwaka kwa kidato cha I kwa ajili ya kukarabati viti na meza vinavyokuwa vibovu au kuongeza idadi ndogo ya viti vinavyokuwa vinapungua.

6.0  CHANGAMOTO
Pamoja na juhudi za Halmashauri kuhimiza ujenzi wa maabara, shule mbili maalum za sekondari na matengenezo ya madawati kwa shule za msingi, bado changamoto zifuatazozinajitokeza mara kwa mara:
v  Mwamko hafifu kujitolea kuchangia maendeleo ya shule zao pamoja na ulipaji wa ada za uendeshaji wa shule;
v  Upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi na Hisabati kiasi cha walimu 69 kwa sasa – mahitaji ni walimu 177 lakini waliopo ni walimu 108;
v  Wanasiasa kutotaka kuhimiza michango ya ujenzi wa shule kwa hofu ya kupoteza kura kwa wananchi wao.

7.0      HITIMISHO
  
Katika kuboresha Elimu ya sekondari kufikia mapinduzi ya kisayansi katika elimu tunahitaji nguvu ya pamoja kama Halmashauri na Wilaya kufanikisha malengo ya Taifa katika Elimu ya Sekondari.

Ili mafanikio yapatikane ni lazima viongozi wa serikali na vyama vya siasa, wadau mbali mbali wa maendeleo pamoja na wananchi tushikamane licha ya changamoto ambazo zinajitokeza mara kwa mara na lazima tushinde.  Aidha, Halmashauri itaendelea kuzingatia Sheria, Taratibu na kanuni katika kusimamia utendaji kazi ili kufikia matarajio na malengo ya Taifa katika Elimu.

INAWEZEKANA KILA MMOJA ATIMIZE WAJIBU WAKE

Nawasilisha.

Humbe, M. O.
Mkurugenzi Mtendaji (W)
HAI

RAIS JK AKIZINDUA BUNGE MAALUMU LA KATIBA

Posted by Arusha by day and by night On 06:39 No comments


HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, WAKATI WA KULIHUTUBIA BUNGE MAALUM LA KATIBA, TAREHE 21 MACHI, 2014, DODOMA

Mheshimiwa Samuel Sitta, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba;
Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;
Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar;
Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mheshimiwa Anne Semamba Makinda; Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba ;
Mheshimiwa Rashid Othman Chande, Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar;
Viongozi Wakuu Wastaafu;
Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba;
Waheshimiwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;

Pongezi
Nakushukuru sana Mheshimiwa Mwenyekiti kwa kunipa fursa ya kuja kuzungumza na Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge letu Maalum la Katiba katika siku hii muhimu na ya kihistoria kwa nchi yetu. Nimekuja kuwatakia heri na naungana na Watanzania wenzetu wote kuwaombea baraka za Mwenyezi Mungu, ili muweze kuifanya kazi yenu kwa utulivu, hekima, umakini mkubwa na kuimaliza kwa salama na kwa mafanikio yanayoyatarajiwa na Watanzania.

Natoa pongezi nyingi kwako na kwa Makamu wako kwa kuchaguliwa kwenu kuongoza Bunge hili maalumu na la kihistoria. Ushindi mkubwa mliopata ni kielelezo tosha cha imani kubwa na matumaini waliyonayo Wajumbe wenzenu kwenu. Matumaini yao ndiyo matumaini ya Watanzania wote, kwamba mtaliongoza vizuri Bunge hili, ili liweze kutimiza kwa ufanisi mkubwa jukumu lake muhimu sana katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Niruhusu pia niwapongeze kwa dhati Wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba kwa bahati ya aina yake waliyopata ya kutunga Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Fursa hii hutokea mara chache sana katika historia ya nchi yo yote na watu wake. Mkifanikiwa kuipatia nchi yetu Katiba nzuri majina yenu yataandikwa kwa wino wa dhahabu, katika kumbukumbu za historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni matarajio ya Watanzania kuwa mtatunga Katiba itakayokubalika na wengi. Katiba inayotekelezeka. Katiba itakayoimarisha Muungano wetu kwa kuondoa changamoto zilizopo sasa. Katiba itakayoipa nchi yetu mfumo bora wa kuongoza na kuendesha mambo yetu. Katiba itakayoimarisha umoja, upendo, ushirikiano na mshikamano miongoni mwa wananchi wa Tanzania, licha ya tofauti zao za asili za upande wa Muungano na maeneo watokako, au tofauti za jinsia, rangi, kabila, dini na ufuasi wa vyama vya siasa. Katiba itakayodumisha amani, usalama na utulivu
nchini. Katiba itakayostawisha zaidi demokrasia, haki za binadamu, utawala wa sheria, utawala bora na kudhibiti maovu.Na, mwisho ingawaje siyo mwisho kwa umuhimu, Katiba itakayoweka
mazingira mazuri kwa uchumi wa nchi kukua, na wananchi wengi kunufaika sawia na maendeleo yatayopatikana.

Historia ya Katiba Nchini
Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wajumbe;
Hii itakuwa mara ya tatu tangu kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 26, 1964, kwa nchi yetu kuwa na mchakato wa kutunga Katiba mpya.Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1965 ilipotungwa Katiba ya Muda na mara ya pili ni mwaka 1977 ilipotungwa Katiba ya Kudumu tuliyonao sasa. Tofauti na mara mbili zilizopita, safari hii mchakato unahusisha watu wengi zaidi. Wananchi wameshiriki moja kwa moja kutoa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, na ndio
watakaofanya uamuzi wa mwisho kuhusu Katiba mpya kwa kura ya maoni.

Wananchi pia walipata nafasi ya kuchagua Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya yaliyojadili Rasimu ya Kwanza ya Katiba. Pia walipata nafasi ya kutoa maoni yao kupitia Mabaraza ya Katiba ya taasisi. Katika Bunge hili wapo wananchi 201 kutoka makundi mbalimbali.

Katika mchakato wa kutunga Katiba za mwaka 1965 na 1977 kulikuwapo Tume za Kuandaa Rasimu na Bunge Maalum la Katiba kama ilivyo katika mchakato huu. Hata hivyo, kwa Katiba zilizopita Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano pekee ndio waliounda Bunge Maalum. Safari hii Bunge Maalum linajumuisha Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wananchi 201 wanaotoka kwenye jamii, wakiwakilisha asasi na makundi mbalimbali ya Watanzania kutoka Zanzibar na
Tanzania Bara. Mchakato wa sasa utaishia kwenye kura ya maoni itakayoshirikisha wananchi wote wa Tanzania wanaoruhusiwa kupiga kura. Michakato iliyopita iliishia Bunge Maalum pekee.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Tangu kutungwa kwake, tarehe 25 Aprili, 1977, mpaka sasa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 imefanyiwa mabadiliko takriban mara 14. Mabadiliko hayo yalitokana na kufanyika au kutokea kwa mabadiliko muhimu ya kiuchumi, kisiasa na kijamii katika nyakati mbalimbali hapa nchini na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa ruksa yako naomba nitaje baadhi ya mabadiliko yaliyofanywa:-­‐‑

1. Mabadiliko ya 1979 yaliunda Mahakama ya Rufani ya Tanzania kufuatia kufa kwa Mahakama ya Rufani ya Afrika Mashariki baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977.
2. Mabadiliko ya mwaka 1980 yalifanyika baada ya kutungwa kwa Katiba ya Zanzibar, hivyo kulazimu Katiba hiyo kutambulika kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
3. Mabadiliko ya mwaka 1984 yaliweka utaratibu wa ukomo wa vipindi vya Urais ambao haukuwepo kabla ya hapo. Aidha, masuala ya Haki za Binadamu (Bill of Rights) yaliingizwa kwa mara ya kwanza katika Katiba. Vilevile, Mahakama ya Rufani ya Tanzania na mambo mengine ya
iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliongezwa katika Orodha yaMMambo ya Muungano.
4. Mwaka 1992, yalifanyika mabadiliko yaliyoanzisha Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa badala ya ule wa Chama kimoja uliokuwepo tangu 1965.Pia utaratibu wa uchaguzi wa Rais na Wabunge ulirekebishwa ili uendane na mfumo wa vyama vingi vya siasa. Vilevile utaratibu wa kuwa na viti
maalum vya wanawake katika Bunge ulianzishwa. Wakati ule ilikuwa asilimia 15 ya Wabunge wote. Aidha, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu Bunge lilipewa mamlaka ya kumwajibisha Rais na Waziri Mkuu kupitia kura ya kutokuwa na imani.
5. Mabadiliko ya mwaka 1994 yaliweka mfumo mpya wa kumpata Makamu wa Rais kupitia Mgombea Mwenza.
6. Mwaka 2000 na 2005, pamoja na mambo mengine yalifanyika mabadiliko yaliyopanua wigo wa Haki za Binadamu na kuongeza uwakilishi wawanawake.

Umuhimu wa Mabadiliko ya Katiba
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kufanyika kwa mabadiliko hayo kunathibitisha utayari wa Serikali kufanya mabadiliko kila ilipoonekana inafaa kufanya hivyo. Pamoja na kufanya yote hayo na Serikali kuwa na msimamo huo, kumekuwepo na madai yaliyokuwa yanajirudia ya kutaka Katiba ya Tanzania iandikwe upya. Wako watu walioimithilisha Katiba yetu na nguo yenye viraka vingi mno kiasi kwamba ingefaa kununua mpya badala ya kuendelea kuivaa.

Madai ya kutaka Katiba mpya yalipazwa sauti baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Wapo waliokuwa wanadai Katiba mpya kwa imani, eti kwamba, itawawezesha kuishinda CCM. Lakini, si hayo tu, hata katika mchakato wa Serikali zetu mbili kushughulikia kero za Muungano, imedhihirika kuwa baadhi ya changamoto zilikuwa zinahitaji mabadiliko ya Katiba ili kuzipatia ufumbuzi wa uhakika na wa kudumu.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kwa kutambua ukweli huo na baada ya kushauriana na kukubaliana na viongozi wenzangu wakuu wa Chama tawala na Serikali zetu mbili wakati ule, ndipo tarehe 31 Desemba, 2010, nikatangaza dhamira ya kuanzisha mchakato wa kutunga Katiba mpya. Nilieleza siku ile kuwa katika mchakato huo tutakuwa na ushirikishwaji mpana wa wananchi wa Tanzania kwa makundi yao ya jinsia, dini,
siasa na shughuli wazifanyazo kujipatia riziki na kwa maeneo wanayotoka katika pande zetu mbili za Muungano.

Mchakato wa Katiba Mpya
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Tarehe 16 Machi, 2011 Baraza la Mawaziri liliridhia kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya kuliongoza taifa katika mchakato wa kutunga Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tarehe 18 Novemba, 2011 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa mujibu wa Sheria hiyo, mchakato wa kutunga Katiba Mpya ulikuwa unaanza kwa kuunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Tume hiyo imepewa jukumu la kusikiliza maoni ya wananchi mmoja mmoja na kwa makundi yao ya maslahi, taasisi zao na kupitia Mabaraza ya Katiba. Mwishowe Tume imetakiwa kutengeneza Rasimu ya Katiba mpya itakayofikishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba kujadiliwa na Katiba mpya kutungwa. Mchakato wa Katiba utahitimishwa kwa wananchi kupiga kura ya maoni ya kuamua kama wanaikubali au kuikataa Katiba mpya.

Tarehe 6 Aprili, 2012 nilifanya uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuwaapisha tarehe 13 Aprili, 2012. Tume ilianza kazi tarehe 2 Mei, 2012 na kuikamilisha kwa mafanikio, hatua zote zilizoihusu na kukabidhi kwangu na kwa Rais wa Zanzibar, Taarifa ya Tume na Rasimu ya Katiba tarehe 30 Desemba, 2013.

Kitendo cha Mwenyekiti wa Tume, Mheshimiwa Joseph Warioba kuwasilisha Rasimu
hiyo mbele ya Bunge hili tukufu tarehe 18 Machi, 2014, kinahitimisha rasmi kazi ya
Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kazi inayofuatia ni ya Bunge hili kujadili, kuamua na
kutunga Katiba mpya. Baada ya hapo Katiba mpya itafikishwa kwa wananchi kwa
uamuzi wa mwisho kwa njia ya kupiga kura ya NDIYO au HAPANA.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Rasimu ya Katiba ilichapishwa kwenye gazeti la Serikali na magazeti mengine yanayosomwa na wananchi kama ilivyoagizwa katika Kifungu cha 20(2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Pamoja na hayo, Taarifa ya Tume na Rasimu ya Katiba viliwekwa wazi kwenye tovuti ya Tume kwa kila mtu kusoma. Inafurahisha kuona kuwa watu wengi wameisoma Taarifa ya Tume na Rasimu ya Katiba na kumekuwa na mjadala mpana kuhusu nyaraka zote hizo muhimu. Watu wengi wametoa maoni yao na wanaendelea kufanya hivyo. Kwa maoni yangu hili ni jambo jema sana na ni kielelezo thabiti kuwa demokrasia imestawi na inazidi kuota mizizi Tanzania. Pia, kwamba, Watanzania wako huru kushiriki na kutoa maoni yao kwa mambo yanayowahusu.

Pongezi kwa Tume
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kwa mara nyingine tena narudia kutoa pongezi za dhati kwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya uongozi wa Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba akisaidiwa na Mheshimiwa Jaji Augustino Ramadhani, kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya. Kazi yao haikuwa rahisi hasa ukizingatia ukubwa wa nchi yetu, wingi wa watu wake, utitiri wa taasisi na pigo la kumpoteza  Mjumbe mwenzao muhimu Dkt. Sengondo Mvungi aliyetangulia mbele ya haki katikati ya mchakato. Pamoja na hayo, kwa bidii kubwa Wajumbe wa Tume wameweza kutembelea mikoa yote nchini na kuwafikia watu 351,644 waliotoa maoni yao kwa mdomo na kwa maandishi.

Halikadhalika, walipokea na kuchambua maoni 772,211 kutoka kwa wananchi na taasisi mbalimbali. Baada ya kupokea maoni ya wananchi, kufanya utafiti na kwa kutumia maarifa na uzoefu wao, Wajumbe wakafanya kazi ngumu, kuliko yote, ya kutengeneza Rasimu ya Katiba iliyoko mbele ya Bunge hili. Ni kweli kwamba Wajumbe hawakuweza kuwafikia wananchi wote wa Tanzania, lakini
wameweza kuwafikia wananchi wengi, ambao kwa kiasi kikubwa wanawakilisha taswira na mitazamo mipana ya jamii yetu. Baadhi ya Masuala Yaliyojitokeza Katika Mjadala wa Mapendekezo ya Tume

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Tume imefanya kazi nzuri, yenye thamani kubwa na ya manufaa kwa taifa la Tanzania. Rasimu imeandikwa vizuri na kwa weledi wa hali juu. Tume imetoa mapendekezo ambayo kwa kiasi kikubwa yanahuisha na kuboresha Katiba ya nchi yetu, kwa namna ya pekee. Katiba inayopendekezwa, imejumuisha dhana na mambo kadhaa mapya yanayokwenda vyema na wakati tulionao na kuweka msingi mzuri kwa huko mbele tuendako. Kwa taratibu za kawaida za marekebisho ya Katiba tuliyonayo, isingekuwa rahisi kuingiza mambo mengi mapya kiasi hiki.

Wajumbe Wana Kazi Kubwa
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Waheshimiwa Wajumbe;
Rasimu ya Katiba ni kitabu kikubwa kilichosheheni mambo mengi. Kina kurasa 106, sura 17 na ibara 271. Wajumbe wa Bunge hili mnatakiwa kusoma na kuelewa vizuri kila kilichoandikwa ili muweze kufanya uamuzi ulio sahihi. Mnawajibika kuchambua kwa kina na umakini mkubwa kila kilichomo, sura kwa sura, ibara kwa ibara, sentensi kwa sentensi na hata neno kwa neno. Hamna budi
kujiridhisha kuhusu uandishi wa vifungu vya Rasimu ya Katiba na kufaa kwa dhana mbalimbali zilizoingizwa na kujengeka katika Rasimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kile ambacho Wajumbe mtaona kinastahili kuboreshwa au kurekebishwa au kufutwa msisite kufanya hivyo ili Watanzania wapate Katiba iliyo bora. Msipofanya hivyo kuna hatari ya kupata Katiba ambayo ni ngumu kuitekeleza. Aidha, tunaweza kuwa na Katiba ambayo itanung’unikiwa na watu wengi na kusababisha madai ya kutaka ifanyiwe marekebisho muda mfupi baada ya kupitishwa. Bunge hili linao wajibu maalum wa kuzuia balaa hilo lisitokee katika nchi yetu. Ngazi mbalimbali
zilizowekwa katika mchakato huu ni kama chujio la kuepusha hali hiyo isitokee. Kile ambacho hakikuonekana katika hatua moja kitaonekana katika hatua inayofuata na kurekebishwa. Nawaomba fursa mliyonayo muitumie vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Nimekwishaeleza kuwa moja ya jambo mnalotegemewa kufanya ninyi wenzetu mliopewa dhamana ya kutunga Katiba ya nchi yetu ni kujiridhisha na uandishi wake. Yapo maoni yaliyotolewa kuhusu uandishi ambayo naomba myatafakari na kuamua ipasavyo. Kwa mfano, kuna baadhi ya vifungu vya Katiba vinayopendekezwa vimekuwa na mambo mengi mno kuliko inavyostahili Katiba kuwa (too prescriptive). Pia kuna mawazo kwamba baadhi ya mambo hayangetakiwa kuwa katika Katiba bali yawe kwenye Sheria zinazotafsiri utekelezaji wa Katiba yenyewe. Yako mambo yaliyotajwa kwenye Katiba ambayo yanatakiwa kuelezwa wazi kuwa mtu hatakwenda mahakamani kuidai Serikali impatie (non justiciable). yaliyotajwa kwenye Katiba ni mazuri na yanavutia, lakini lazima yaendane na uwezo wa nchi na uchumi wake kuhimili. Simaanishi kwamba tuyatoe kwenye Katiba, bali yabakie kama dhamira pale uwezo wa nchi utakaporuhusu yatekelezwe.

Tusipofanya hivyo, kuna hatari ya Serikali kujikuta inalaumiwa au hata kufikishwa mahakamani kila wakati kwa madai ya jambo moja au jingine ambayo haina uwezo nayo. Ni muhimu sana mambo kama hayo muyatazame ili tusije kuwa na Katiba ambayo ni ngumu kutekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Yapo pia maoni kuwa baadhi ya vifungu vina upungufu katika uandishi wake, hivyo kuhitaji kufanyiwa marekebisho. Isipofanyika hivyo kunaweza kuwepo athari na nyingine zinaweza kuwa mbaya. Kwa mfano, Ibara ya 2 ya Rasimu inayotambulisha eneo na mipaka ya nchi yetu. Ibara hiyo inasomeka kuwa “Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni eneo lote la Tanganyika likijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar likijumuisha sehemu yake ya bahari”.
Maelezo hayo yameacha kutambua, kwa upande wa Tanzania Bara, sehemu yetu ya maziwa na mito ambayo ni kubwa sana. Kwa nini tuache kuitaja? Je hatutoi nafasi kwa nchi tunazopakana nazo siku moja wakaja kupora sehemu zetu hizo na sisi kukosa utetezi kwa kuwa hata Katiba yetu haikuyatambua maeneo hayo kuwa ni yetu? Hili ni jambo kubwa ambalo Bunge hili lazima mlirekebishe. Wakati ndiyo huu hakuna mwingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Jambo jingine kuhusu uandishi ni mgongano kati ya pendekezo la msingi la Tume la kuwa na muundo wa Serikali tatu na majukumu ya Serikali ya Muungano ambayo kimsingi ni majukumu ya Serikali za nchi washirika. Katika Rasimu hii malengo ya taifa yameainishwa na Serikali ya Muungano inatakiwa kuhakikisha kuwa malengo hayo yanatekelezwa na itoe taarifa Bungeni. Katika mfumo wa Serikali tatu unaopendekezwa na Tume masuala yahusuyo uchumi na maendeleo ya
jamii kama vile kukuza kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda, biashara, pembejeo, elimu,hifadhi ya jamii na kadhalika yako chini ya mamlaka ya Serikali za nchi washirika.

Mamlaka ya Serikali ya Muungano ni kwa mambo saba tu yafuatayo:-­‐‑ Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano, Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano, Uraia na Uhamiaji, Sarafu na Benki Kuu, Mambo ya Nje, Usajili wa Vyama vya Siasa,Ushuru wa Bidhaa na Mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano.Kwa Rasimu kupendekeza muundo wa Serikali tatu na kuipa Serikali yaMuungano majukumu ambayo haina mamlaka nayo, ni kuzusha utata na migongano
kati ya Serikali ya Muungano na nchi washirika. Mkichagua mfumo wa Serikali tatu,inawalazimu muyaondoe mambo hayo kwani Serikali ya Muungano haistahili kuyatekeleza na wala haina uwezo wa kuweka masharti kwa Serikali za nchi washirika kwa mambo yaliyo kwenye mamlaka ya nchi hizo. Lakini kama mtaamua tuendelee na muundo wa Serikali mbili, mambo haya mazuri yanatekelezeka na Serikali ya Muungano bila ya matatizo. Katika uandishi wa Rasimu Utumishi katika Serikali ya Muungano haumo katika Orodha ya Mambo ya Muungano. Ni lazima liwemo. Hayo ni baadhi tu ya masuala yahusuyo uandishi katika Rasimu. Naamini mkiisoma Rasimu kwa makini mnaweza kuyagundua mengineyo.

Dhana Mpya
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Katika Rasimu kuna dhana mpya na mambo mapya kadhaa yaliyoingizwa ambayo yanabadili utaratibu wa sasa wa uendeshaji wa nchi na mambo mbalimbali.Nawaomba mfanye uchambuzi wa kina kwa kila kinachopendekezwa na kujiridhisha kuhusu kufaa kwake na manufaa yake. Fanyeni hivyo ili tujihakikishie kuwepo kwa mambo mazuri na uendeshaji mzuri wa shughuli katika taifa letu changa. Mambo ni mengi na kwa ufinyu wa muda sitaweza kuyazungumzia yote. Niruhusuni nizungumzie baadhi ya dhana na mambo mapya yaliyomo katika Rasimu. Jambo la kwanza, kwa mfano, linahusu Ibara ya 128 (2)(d) inayoleta dhana ya “Mbunge kupoteza Ubunge iwapo atashindwa kufanya kazi za Mbunge kwa miezi sita mfululizo kutokana na maradhi au kizuizi ndani ya gereza”.

Watu hawana tatizo na Mbunge kuwa kizuizini ndani ya gereza kama amepatikana na hatia Mahakamani na kuhukumiwa kifungo. Lakini, isijekuwa yuko rumande kwa tuhuma akisubiri kesi kusikilizwa. Je akija kuonekana hana hatia na kuachiliwa? Naungana na wale wanaoshauri kuwa jambo hili lifafanuliwe vizuri na kutambua Mbunge kutiwa hatiani na kupata adhabu ya kifungo cha kipindi hicho. Ni bora ifanyike hivyo sasa ili kuondoa mikanganyiko. Hakuna haja ya kusubiri mpaka
jambo hili lije kufafanuliwa baadaye kwa Sheria itakayotungwa na Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kwa upande wa mtu kupoteza Ubunge kwa sababu ya “kuugua kwa miezi sita mfululizo” ni maoni ya watu wengi kuwa huu ni ukatili ambao haustahili kufanywa na Katiba. Kuugua ndiyo ubinadamu na wakati mwingine Mbunge anaweza kupata ajali akiwatumikia wananchi wa Jimbo lake. Anaweza kuugua kwa miezi sita au zaidi na kupona kabla ya kipindi chake cha Ubunge kufika mwisho.
Kwa nini awekewe ukomo wa miezi sita? Katiba ya mwaka 1977 tunayotumia sasa haina sharti hilo. Watu wanauliza hoja na haja ya kuwa na sharti hili kwenye Katiba mpya ni ipi? Wanasema kwa kweli anachostahili Mbunge huyu kufanyiwa ni kuuguzwa afya yake iimarike ili aendelee kutumikia watu wake, na siyo kupoteza uongozi wake. Tusiwatie watu kishawishi cha kukatiza matibabu ili kukwepa sharti hilo. Ni vyema jambo hili mkalitazama kwa makini, na muone kama linastahili kuwepo au hapana.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Katika Rasimu hii imeingizwa dhana mpya ya kuweka ukomo wa vipindi vitatu kwa Wabunge. Tena mapendekezo haya hayasemi vipindi vitatu mfululizo au la!. Jambo hilo limezua mjadala motomoto katika jamii. Ni vizuri mkajiridhisha juu ya sababu za msingi na manufaa ya kufanya hivyo hapa Tanzania. Mazoea yetu na ya kwingineko duniani ni kuweka ukomo kwa Wakuu wa Nchi kwa sababu nzuri na rahisi kuzielezea. Lakini, kuwawekea ukomo Wabunge ni jambo jipya na huenda Tanzania tukawa wa kwanza. Nashawishika kuungana na wale wanaopendekeza kuwa pengine ni mapema mno kuanzisha utaratibu huo hapa kwetu. Nachelea kuwa tutainyima nchi yetu fursa ya kupata watu wenye maarifa na uzoefu mzuri wa uongozi kwa nafasi ya Ubunge au kwa nafasi za uongozi wa Taifa bila ya sababu za msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Jambo lingine jipya linalopendekezwa na Tume ni utaratibu wa kumuondoa Mbunge katikati ya kipindi chake cha uongozi. Kwa hoja linaonekana kuwa jambo jema lakini naomba athari zake mzitafakari vizuri. Kuna hatari ya kuanzisha misuguano kwenye Majimbo na kuwaacha Wabunge wasifanye kazi zao kwa utulivu bali wawe wanajihami dhidi ya wapinzani wao kuwatengenezea fitna za kuwatoa. Utaratibu unaopendekezwa wa Chama chake kujaza nafasi ya Mbunge inapokuwa wazi katika mazingira hayo nao unaweza kuwa ndicho kichocheo kikubwa cha vuguvugu la kumuondoa Mbunge. Walioshindwa kwenye kura ya maoni wanaweza kufanya kazi ya kuwachimba wenzao mpaka waondoke. Jipeni muda wa kupima faida na hasa thamani inayoongezwa na kuanzisha utaratibu huo. Naomba tujiridhishe kama jambo hili jipya lina tija. Hivi kupewa nafasi kila miaka mitano kurudi kwa wananchi hakutoshi kumuondoa Mbunge ambaye watu wamemchoka?

Muundo wa Muungano
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Jambo lingine kubwa lililopendekezwa na Tume ambalo limevuta hisia za karibu watu wote nchini linahusu muundo wa Muungano wetu kuwa wa Serikali tatu badala ya mbili za sasa. Pendekezo hili limezua mjadala mkubwa tangu lilipotolewa katika Rasimu ya kwanza na kurudiwa katika Rasimu ya pili. Wakati mwingine mjadala umekuwa mkali na wa hisia kali kwa kila upande.Kwa kweli hili ndilo jambo kubwa kuliko yote katika Rasimu kwa sababu linapendekeza kuanzishwa kwa muundo na mfumo mpya wa kuendesha nchi yetu. Hii ndiyo agenda mama ya Bunge hili ambayo kila Mtanzania anasubiri kwa hamu uamuzi wenu utakuwa upi. Ombi langu kwenu ni kuwa watulivu mnapojadili suala hili. Epukeni jazba ili mfanye uamuzi ulio sahihi. Lazima mtambue uamuzi usiokuwa sahihi kwa jambo hili una hasara kubwa. Tunaweza kupoteza kitu tulichokijenga kwa gharama kubwa kwa nusu karne iliyopita. Tanzania inaweza kuwa nchi iliyojaa migogoro na matatizo mengi ambayo hatunayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wajumbe;
Kama alivyoeleza Mwenyekiti wa Tume Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba, mara kadhaa, mjadala au madai ya kutaka muundo wa Serikali tatu si jambo jipya. Ulikuwepo hata wakati wa mazungumzo ya kuunganisha nchi zetu mbili mwaka 1964. Ulikuwa kiini cha kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar mwaka 1984. Muundo huu uliwahi kupendekezwa na Tume ya Nyalali
mwaka 1992, ndiyo hoja ya G55 mwaka 1993 na umependekezwa pia na Tume ya Jaji Kisanga ya mwaka 1998. Lakini mara zote hizo mapendekezo hayo hayakukubaliwa.Waasisi wa taifa letu, yaani Mwalimu Julius Nyerere, aliyekuwa Rais waJamhuri ya Tanganyika wakati ule na Sheikh Abeid Amani Karume, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar wakati ule, waliamua kuchagua Muungano wa Serikali mbili tulionao sasa. Walitoa sababu mbili kuu: “ni muundo unaoihakikishia
Zanzibar kuwa haimezwi na Tanganyika; na pia unaiepusha Tanganyika kubeba mzigo mkubwa wa kugharamia Serikali ya Tanganyika na ile ya Muungano”.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Natambua kuwepo kwa rai ya kutaka Mwalimu Nyerere asitumiwe katika mjadala huu. Nionavyo mimi ni vigumu kuacha kujadili fikra za Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume katika jambo hili. Wao ndiyo wa mwanzo kujadili na kukubaliana kuwa mfumo wa Serikali mbili ndiyo bora kwa nchi yetu. Iweje leo tunapozungumzia kuubadili, mawazo yao yawe hayafai kutumika au hata kuzungumzwa. Hivi hasa mawazo ya nani pekee ndiyo bora zaidi kutumika?Tutakuwa hatuutendei haki mjadala huu na sisi wenyewe tunaoshiriki katika mchakato huu. Rai yangu kwenu ni kuwa mzitazame hoja zote kwa marefu na mapana yake ili mpime kama zipo sababu za kuubadili muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali mbili na kuleta wa Serikali tatu. Na, kama zipo mabadiliko hayo yaweje! Lazima mfanye uamuzi kwa utambuzi na hoja zenye mashiko. (you must make an informed decision).

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Tume imetoa sababu mbili kubwa za kupendekeza muundo wa Serikali tatu.Sababu ya kwanza ni kwamba ndiyo matakwa ya Watanzania wengi kote Zanzibar na Tanzania Bara. Inaeleza kuwa idadi kubwa ya Watanzania waliotoa maoni, yaani asilimia 60.2 wa kutoka Zanzibar wanaunga mkono muundo wa Serikali ya Mkataba,na asilimia 61.3 wa kutoka Tanzania Bara wanaunga mkono muundo wa Serikali tatu. Sababu ya pili ni kwamba muundo huo unatoa majawabu ya uhakika na
endelevu kwa changamoto za muundo wa sasa wa Serikali mbili zinazonung’unikiwa na watu wa pande zetu mbili za Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Sababu hizi mbili kuu zilizotolewa na Tume zimezua mjadala mkali katika jamii. Wapo wanaokubaliana na Tume na wapo wasiokubaliana nayo. Wapo wanaosema Tume imesema kweli kwamba Watanzania wengi wanaunga mkono muundo wa Serikali tatu, hivyo muundo wa Serikali tatu hauepukiki. Ndiyo matakwa ya wengi hivyo msemo wa Kiswahili usemao wengi wape uheshimiwe.Lakini wapo wanaodai kuwa takwimu za Tume hazionyeshi ukweli huo.Wanasema kuwa taarifa ya Tume imeonesha kuwa Watanzania waliotoa maoni yao kwa Tume kwa mdomo na maandishi walikuwa 351,664. Kati yao ni wananchi 47,820 au sawa na asilimia 13.6 ndiyo waliokerwa na muundo wa Muungano hivyo wakauzungumzia. Wananchi 303,844 au sawa na asilimia 86.4 muundo wa Muungano kwao halikuwa tatizo, ndiyo maana hawakuuzungumzia kabisa.
Wanahoji kuwa iweje leo asilimia 13.6 ya Watanzania wote waliotoa maoni wageuke kuwa ndiyo Watanzania walio wengi!

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Wanasema pia, kwamba mbona Taarifa ya Tume yenyewe, kuhusu takwimu (uk. 66 na 67), inaonesha kwamba kati ya hao watu 47,820 waliotoa maoni kuhusu Muungano, ni watu 17,280 tu ambao ni sawa na asilimia 37.2 ndiyo waliotaka 15 muundo wa Serikali tatu, asilimia 29.8 walitaka Serikali mbili, asilimia 25.3 walipendekeza Serikali ya Mkataba na asilimia 7.7 walipendekeza Serikali moja. Hii hoja ya Watanzania wengi kutaka Serikali tatu msingi wake upi?

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Takwimu za Tume (uk. 57) zinaonyesha, vilevile kuwa Tume ilipokea maoni 772,211. Kati ya hayo asilimia 10.4 tu ndiyo yaliyozungumzia muundo wa Muungano na asilimia 88.6 hayakuzungumzia Muungano bali mambo mengine. Hivyo basi wanahoji pia kwamba kama muundo wa Muungano ungekuwa ni jambo linalowakera Watanzania wengi, lingedhihirika kwenye idadi ya watu waliotoa
maoni na kwenye idadi ya maoni yaliyotolewa. Yote hayo hayakujitokeza.

Waliouzungumzia Muungano walikuwa asilimia 13.6 tu ya watu wote waliotoa maoni na maoni yanayohusu Muungano yalikuwa asilimia 10.4 ya maoni yote.Hivyo basi, wanauliza “usahihi wa hoja ya Watanzania wengi kutaka Serikali tatu uko wapi?”Changamoto za Muundo wa Serikali Mbili Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wajumbe; Kama nilivyokwishagusia awali, sababu ya pili ambayo Tume inatoa kuhusu kufaa kwa muundo wa Serikali tatu ni kwamba mfumo huu unajibu changamoto nyingi za muundo wa Serikali mbili. Tume imeainisha vizuri changamoto za muundo
wa Serikali mbili.

Kwa upande wa Zanzibar wanalalamikia kile kinachoitwa Tanzania Bara kuvaa koti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo kutumia mamlaka ya Serikali ya Muungano kujinufaisha yenyewe. Fursa hiyo Zanzibar hainayo. Aidha, wanasema mipaka na mamlaka ya Serikali ya Muungano kwa
mambo ya Muungano, na kwa mambo ya Tanzania Bara haijaainishwa vizuri ikaeleweka. Wazanzibari pia, wanazungumzia mkanganyiko kuhusu ugawanaji wa mapato, na jinsi ya kuchangia shughuli za Muungano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Vilevile, wanalalamikia Rais wa Zanzibar kuondolewa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Aidha, kuna malalamiko kuwa orodha ya mambo ya Muungano iliyoongezwa kutoka mambo 11 mwaka 1964 mpaka 22 mwaka 1992 imepunguza uhuru wa Zanzibar kwa mambo yake ya ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kwa upande wa Tanzania Bara, Tume inaeleza kuwepo kwa manung’uniko kuwa Muungano wa Serikali mbili umepoteza utambulisho wa kihistoria wa Tanganyika na fursa ya watu wa upande wa Tanzania Bara kutetea maslahi yao ndani ya Muungano. Wanasema Zanzibar sasa imekuwa nchi huru; ina bendera yake,wimbo wake wa taifa na Serikali yake. Aidha, wanasema Zanzibar imebadili Katiba na kujitambulisha kama nchi na kuchukua madaraka ya Bunge la Muungano, kwa vile Sheria zinazotungwa na Bunge lazima zipelekwe kwenye Baraza la Wawakilishi kupata kibali cha kutumika Zanzibar.

Wananchi wa Tanzania Bara pia wanalalamikia kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar wakati wenzao wa kutoka Zanzibar wanayo haki hiyo Tanzania Bara. Na wao vilevile wananung’unikia mkanganyiko kuhusu ugawaji wa mapato na jinsi ya kuchangia gharama za uendeshaji wa shughuli za Muungano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar. Hizi ndizo baadhi ya changamoto ambazo Tume inaona jawabu lake ili kuzitanzua ni kubadili muundo wa Muungano kuwa wa Serikali tatu badala ya mbili za sasa.

Faida za Muundo wa Serikali Tatu
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imefafanua kwamba mfumo wa Serikali tatu utagawanya vizuri madaraka kati ya mamlaka tatu za Muungano. Unawezesha Washirika wa Muungano kubaki na utambulisho wao wa kihistoria na kiutamaduni na hivyo, utawezesha kuondoa hisia za Zanzibar kumezwa na Muungano. Pia unawezesha kila upande wa Tanzania kuendesha mambo yake yasiyo ya Muungano kadri wanavyoona inafaa. Vile vile unaweza ukaleta ushindani wa kimaendeleo baina
ya washirika na hivyo kusaidia kukuza maendeleo ya nchi.

Faida za Muundo wa Serikali Mbili
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Pamoja na kuainisha changamoto za muundo wa Serikali mbili na kupendekeza kuwa muundo wa Serikali tatu ndio utakaosaidia kuzitatua, Tume haikuacha kutambua manufaa na mchango muhimu uliotolewa na muundo wa Serikali mbili kwa nchi yetu. Tume inasema kuwa muundo wa Serikali mbili unapunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za umma. Umesaidia kujenga uhusiano na ushirikiano mzuri katika hnyanja mbalimbali baina ya wananchi wa pande zetu mbili za Muungano. Umezuia mkubwa kummeza mdogo; na umedumisha Muungano mpaka kuufikisha hapa ulipo tangu kuasisiwa kwake takriban miaka 50 iliyopita (1964). Aidha, umesaidia kudumisha amani, umoja na
utulivu hapa nchini.

Changamoto za Muundo wa Serikali Tatu
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Pamoja na kuelezea ubora wa muundo wa Serikali tatu kama jawabu kwa changamoto za Serikali mbili, Tume inakiri kuwa hata muundo huu nao una changamoto zake. Kwanza kabisa, Taarifa ya Tume inaeleza kuwa kutakuwa na gharama kubwa za uendeshaji wa shughuli za umma. Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba alitutoa hofu kuhusu gharama ingawaje mwaka 1993, Mwalimu alikuwa na
mawazo tofauti. Alisema kwamba: “watu …wanaodhani kuwa gharama ya Serikali yo yote kati ya hizo ingekuwa ndogo, (Waulizeni Wazanzibari) na wala gharama ya Serikali ya Shirikisho isingekuwa ndogo hata bila gharama ya mambo yasiyo ya Shirikisho”.

Ni matumaini yangu kwamba katika mjadala wenu mtajipa nafasi ya kulitafakari suala hili kubwa na nyeti. Tume imesema pia kwamba, Muundo huu, unaweza kuibua tatizo la uchangiaji wa gharama za uendeshaji wa shughuli za umma baina ya nchi washirika. Vilevile, kuna uwezekano wa kuwepo sera zinazokinzana au kutofautiana juu ya masuala ya msingi ya nchi na kuzua mgogoro kati ya washirika wa Muungano na baina ya nchi washirika na Serikali ya Muungano. Aidha, upo uwezekano mkubwa kwa muundo huu kuleta tofauti za kimaendeleo baina ya pande mbili za Muungano kutokana na kila upande kuwa na sera na mipango tofauti.

Tume pia imeelezea hatari ya muundo wa Serikali tatu kukuza hisia za utaifa (nationalistic feelings) kwa nchi washirika, hivyo kuweza kudhoofisha Muungano. Muundo huu pia unaweza kuleta misuguano (paralysis and deadklocs in decision making) katika kufanya uamuzi juu ya masuala muhimu ya kitaifa. Changamoto hizo si tu zinaweza kuwa tishio kwa ustawi wa Muungano bali pia hata uhai wake. Kwa ajili hiyo kuchagua muundo wa Serikali tatu kuna maana ya kufanya kazi ya ziada ya kuzikabili changamoto hizi ili zisiue Muungano wenyewe. Changamoto ambazo si
ndogo hata kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Wanaounga mkono muundo wa Serikali mbili wanasema kuwa kwa mlolongo huu wa changamoto zilizoainishwa na Tume yenyewe, unadhihirisha kuwa muundo wa Serikali tatu hautapunguza matatizo ya Muungano wetu bali utayaongeza maradufu kuliko ilivyo sasa. Wanakiri kuwepo kwa changamoto katika muundo wa sasa wa Muungano. Hata hivyo, wanaamini zinaweza kushugulikiwa na kupatiwa ufumbuzi bila ya kuhitaji kuwa na Serikali ya tatu. Wanatoa mifano kadhaa ya jinsi
Serikali zetu zilivyoshughulikia changamoto za Muungano katika kipindi cha uhai wake na mafanikio yaliyopatikana.

Katika kushughulikia kero za Muungano, Serikali zetu mbili ziliunda Tume ya Shelukindo mwaka 1992 na Kamati ya Pamoja ya Serikali zetu mbili mwaka 1993.Mambo mengi yaliyoainishwa katika Tume ya Shelukindo na Kamati ya Pamoja yameshughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi. Kwa upande wa kero zilizoelezwa kwenye Tume ya Shelukindo, ilipofikia mwaka 2006 yalikuwa yamebakia mambo 13 kati ya 31. Kwa jumla, kwa kero zilizoibuliwa na Tume ya Shelukindo na Kamati ya
Pamoja, hivi sasa yamesalia mambo sita tu. Kimsingi ni mambo yahusuyo maslahi ya kiuchumi na yote yapo katika hatua nzuri za kuyamaliza. Mambo hayo ni:
1. Mgawanyo wa mapato:
(a) Hisa za SMZ zilizokuwa katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki
(b) Mgawanyo wa Mapato yatokanayo na faida ya Benki Kuu.
2. Utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi asili.
3. Ushirikiano wa Zanzibar na taasisi za nje.
4. Ajira kwa watumishi wa Zanzibar katika taasisi za Muungano.
5. Usajili wa vyombo vya moto.
6. Tume ya Pamoja ya Fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Serikali zetu mbili zimeamua kwa dhati kutumia fursa ya mchakato huu wa mabadiliko ya Katiba kuyamaliza yale yanayohitaji kuingizwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mambo hayo ni matatu yafuatayo:
1. Utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi asili.
2. Ushirikiano wa Zanzibar na taasisi za nje.
3. Tume ya Pamoja ya Fedha.

Matatu mengine yatamalizwa kwa kutumia taratibu za kiutawala. Hali kadhalika,katika kipindi cha mpito kinachopendekezwa na Tume yaani 2015 – 2018 ni nafasi nzuri ya kushughulikia masuala yenye migongano kati ya Katiba ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano. Mimi naishi kwa matumaini na kwa vile tunayo dhamira njema ya kuimarisha Muungano wetu, naamini tutaweza kuziondoa tofauti zilizopo.

Orodha ya Mambo ya Muungano
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kuhusu orodha ya mambo ya Muungano kuwa 22 badala ya 11 ya awali,napenda kuwahakikishia kuwa Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hazina kigugumizi wala upungufu wa dhamira ya kisiasa ya kuyapunguza yale yanayopunguzika. Napenda kwanza kabisa, ieleweke kuwa kilichoongeza orodha hiyo si hila za Serikali ya Muungano kutaka kupunguza madaraka ya
Zanzibar kwa mambo yake ya ndani. Na, wala siyo udhaifu wa viongozi wa Zanzibar katika kutetea maslahi ya nchi yao. La hasha. Pili, naomba ieleweke kuwa, kila kilichoongezwa katika Orodha ya Mambo ya Muungano kilikuwa na sababu inayoeleweka, inayoelezeka na iliyokubalika na pande
zote mbili za Muungano.

Hakuna hata jambo moja lililoingizwa kwenye Katiba kwa kificho. Taratibu stahiki za kikatiba na kisheria zilifuatwa. Hoja ziliwasilishwa Bungeni na kujadiliwa kwa uwazi na uamuzi ulifanywa na Bunge kwa kuzingatia kanuni ya theluthi mbili ya kura za kila upande wa Muungano. Kumbukumbu zipo katika Hansard za Bunge la Muungano, ambazo ziko wazi kwa kila mtu anayetaka kuzisoma asome. Nashauri mkazisome ili mpate kujua ukweli na undani wa kila kilichoongezwa na sababu za kufanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Nchi zetu mbili zilipoungana mwaka 1964 na kuzaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kulikuwa na mambo 11 kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano. Mambo hayo ni haya yafuatayo:
1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano,
2. Mambo ya Nje,
3. Ulinzi,
4. Polisi,
5. Hali ya Hatari,
6. Uraia,
7. Uhamiaji,
8. Biashara ya nje na mikopo,
9. Utumishi katika Serikali ya Muungano,
10. Kodi ya Mapato, Kodi ya Makampuni, Ushuru wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa,
11. Bandari, Mambo ya Anga, Posta na Simu.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kati ya mwaka 1965 na 1992 mambo ya Muungano yaliongezeka kutoka 11 hadi kufikia 22, kimsingi kutokana na mambo mbalimbali yaliyotokea nchini na kwenye ukanda wetu wa Afrika Mashariki. Pande zetu mbili za Muungano zilikubaliana kuwa mambo hayo yaongezwe katika Katiba na taratibu za kisheria na Kikatiba zilifuatwa. Kwa idhini yako naomba nitoe maelezo kwa ufupi kwa yale
yaliyoongezwa na kitu kilichosababisha mabadiliko hayo kufanywa.
1. Jambo la kwanza kuongezwa, yaani la 12 lilikuwa ni “sarafu, mabenki na fedha za kigeni”. Hii ilifanyika tarehe 10 Juni, 1965 kufuatia kuvunjika kwa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki (East African Currency Board) mwaka 1964. Kwa ajili hiyo, kila nchi mwanachama wa Jumuiya ililazimika kuwa na sarafu yake na mipango yake ya kusimamia mambo yake ya kibenki na fedha.
Serikali zetu mbili zilikubaliana masuala hayo yashughulikiwe na Serikali ya Muungano na Muswada husika wa Bunge uliidhinishwa kuwa Sheria na Mzee Abeid Amani Karume aliyekuwa akikaimu Urais tarehe 10 Juni, 1965.
2. Tarehe 11 Agosti, 1967 yaliongezwa mambo yafuatayo kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano:-­‐‑
(a) Leseni za Viwanda na Takwimu, (Jambo la 13)
(b) Elimu ya Juu, (Jambo la 14)
(c) Jambo la 15 lilikuwa ni mambo yote yaliyokuwa kwenye Nyongeza ya 10 ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nyongeza hiyo ilikuwa na mambo 27 ambayo Serikali ya Muungano ilipewa jukumu la uratibu.

Mambo hayo ni pamoja na Mahakama ya Rufani ya Afrika Mashariki,Utabiri wa Hali ya Hewa, Utafiti, Vipimo na Mizani, Huduma ya Usafiri wa Reli, Barabara, Usafiri wa Majini na kadhalika.
3. Tarehe 22 Julai, 1968 “rasilimali ya mafuta, petroli na gesi asilia” iliongezwa kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano na kuwa jambo la 16. Kimsingi Serikali ya Muungano ilipewa jukumu la kuagiza mafuta ya petroli na gesi asilia kwa ajili ya nchi nzima. Baada ya kupanga upya Orodha ya Mambo ya Muungano, suala la rasilimali ya mafuta likawa la 15.
4. Tarehe 22 Novemba, 1973 Baraza la Mitihani la Taifa liliongezwa na kuwa jambo la 16. Hii ilifuatia kuvunjika kwa Baraza la Mitihani la Afrika Mashariki mwaka 1971 na hivyo nchi yetu kulazimika kuunda Baraza la Mitihani la Taifa mwaka 1973.
5. Mwaka 1984 yalipofanyika mabadiliko makubwa katika Katiba ya mwaka 1977, Orodha ya Mambo ya Muungano ilipangwa upya. Mambo yaliyokuwemo kwenye Nyongeza ya 10 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuorodheshwa kama Jambo la 15 katika Orodha ya Mambo ya Muungano
yalipunguzwa na kubaki matano. Mambo hayo yalipewa namba kama ifatavyo:-­‐‑ Usafirishaji wa Anga kuwa Jambo la 17, Utafiti kuwa la 18, Utabiri wa Hali ya Hewa kuwa la 19 na Takwimu kuwa la 20 na Mahakama ya Rufani ya Tanzania ikawa jambo la 21.
6. Tarehe 17 Mei, 1992 likaongezwa jambo la “Uandikishaji wa Vyama vya Siasa”na kuwa jambo la 22. Hii ilifuatia kuanzishwa kwa Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa na hasa uamuzi kuwa vyama vitakuwa vya kitaifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Bila ya shaka maelezo haya yatasaidia kuelezea nini kimeongezwa na mazingira ya kuongezwa kwake ni yepi. Kulikuwepo na sababu za msingi na wala siyo hila ya namna yo yote ile iliyofanywa na mtu ye yote mwenye nia mbaya na Zanzibar. Kama tulivyoona mambo mengi yalihusu kilichokuwa kinatokea ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kila yalipotokea mabadiliko katika uendeshaji wa shughuli za Jumuiya ya Afrika Mashariki, huduma zilizokuwa zikitolewa na Jumuiya
zilikabidhiwa Serikali ya Muungano kubeba kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kiuchumi. Yale yaliyokuwa yanagusa sehemu zetu mbili za Muungano yaliingizwa katika Orodha ya Mambo ya Muungano. Mengineyo yaliachiwa kila upande kushughulikia ilivyoona inafaa. Kwa maana hii basi, mambo ambayo yalitokana na uamuzi wetu wenyewe ni mawili tu. Mambo hayo ni rasimali ya mafuta na gesi asilia (1968), na uandikishaji wa vyama vya siasa (1992).

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Ni msimamo wa Serikali zetu mbili, tangu mwanzo mpaka leo kwamba,iwapo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshajenga uwezo wake wa kufanya baadhi ya mambo katika Orodha ya Mambo ya Muungano ipewe uhuru wa kufanya hivyo. Lililo muhimu ni kuwa zisiondolewe tunu zenyewe za Muungano wetu.Ndiyo maana, mambo kama vile bandari, takwimu, kodi ya mapato, leseni za
biashara, utafiti na mengineyo, yanasimamiwa na kuendeshwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na kuwemo kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano. Imekuwa hivyo kwa miaka kadhaa sasa na imethibitika kuwa Zanzibar inayamudu. Ni makusudio yetu kutumia fursa ya mchakato huu sasa kuyaondoa rasmi mambo hayo na mengineyo tutakayokubaliana kutoka kwenye Orodha ya
Mambo ya Muungano.

Rasilimali ya Mafuta na Gesi Asilia
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kwa ajili hiyo tumekubaliana kuliondoa suala la rasilimali ya mafuta na gesi asilia lisiwe jambo la Muungano. Jambo hili tulishakubaliana tangu wakati wa Rais Amani Abeid Karume tuliondoe na hata alipokuja Rais Shein msimamo haukubadilika. Kilichotuchelewesha kutekeleza ni kuibuka kwa fikra za kuwa na mchakato huu wa Katiba mpya. Tuliona kuwasilisha Bungeni Muswada wa Sheria wa kuondoa jambo hili katikati ya mchakato huu, ingeweza kuzua matatizo yasiyokuwa ya lazima. Tungeulizwa haraka ni ya nini tungeweza kukosa majibu.

Hatimaye wakati wake wa kulimaliza suala hili sasa umefika. Misemo ya wahenga ya “subira yavuta heri” na “kawia ufike” imetuongoza vyema tumefika mahali tunaweza kufanya hivyo. Zipo sababu mbili zilizotushawishi kuamua kuitoa rasilimali hii kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano. Kwanza kwamba, siku hizi Serikali haiagizi mafuta. Kazi hiyo hufanywa na makampuni binafsi. Pili, kwamba,
rasilimali ya mafuta na gesi yakipatikana Zanzibar ni suala la kiuchumi ambalo lipo
kwenye mamlaka ya Zanzibar kama ilivyo karafuu, hiliki, mwani na kadhalika. Au
kama ilivyo dhahabu, gesi, pamba, kahawa na kadhalika kwa upande wa Tanzania
Bara. Hivyo, Zanzibar iachwe kumiliki rasilimali yake ya kiuchumi.
Zanzibar na Ushirikiano wa Kimataifa
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Jambo lingine muhimu ambalo Serikali zetu mbili zimelizungumza na
kukubaliana tulitafutie ufumbuzi ni kuhusu Zanzibar kupata fursa ya kujiunga na
mashirika ya kimataifa, kukopa na kupata misaada kutoka nchi za nje bila kizuizi.
Kwa sasa fursa hiyo ina vikwazo vya namna mbalimbali. Ni ukweli usiopingika
kuwa jambo hili limechangia kwa kiasi kikubwa kujenga hisia hasi kuhusu
Muungano kwa upande wa Zanzibar. Aidha, limechangia sana kuchafua hali ya
hewa ya kisiasa Zanzibar kwa nyakati mbalimbali. Hata zile kauli kwamba Tanzania
24
Bara imejificha kwenye koti la Serikali ya Muungano, na kutaka itoke ionekane ili
iache kunufaika isivyostahili, zinazochangiwa sana na mazingira haya iliyonayo
Zanzibar. Serikali zetu mbili zinaamini kuwa mambo haya yakipatiwa ufumbuzi
tutakuwa tumeondoa kizingiti kikubwa katika ustawi wa Muungano wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar tumekubaliana kuwa, tutumie fursa za mchakato huu kuyamaliza mambo
haya yaishe! Bahati nzuri dhana iliyopo katika Ibara ya 65(2) ya Rasimu inatoa
jawabu mwafaka kwa tatizo hili. Tukikubaliana, itaipa Zanzibar “uwezo na uhuru
wa kuanzisha uhusiano na ushirikiano na jumuiya au taasisi yo yote ya kikanda na
kimataifa kwa mambo yaliyo chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya nchi”
bila kizuizi. Ni maoni ya Serikali zetu mbili kuwa fursa hiyo inaweza kutolewa kwa
Zanzibar bila ya kulazimika kuwa na muundo wa Serikali tatu. Hatuuoni ulazima
huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kwa maoni yangu kitu kingine muhimu cha kufanya ni kuongeza msukumo,
utakaohakikisha kuwa Tume ya Pamoja ya Fedha inatimiza ipasavyo majukumu
yake. Wanaohusika na utekelezaji wa maamuzi yake wabanwe ipasavyo kutimiza
wajibu wao. Iwekwe mifumo na masharti katika sheria au Katiba ya kuwabana
watekelezaji kwa ajili hiyo. Hali kadhalika ihakikishwe kuwa, Akaunti ya Pamoja
inaanzishwa bila ajizi na kutumika na pande zote. Aidha, mfumo wa mawasiliano na
ushirikiano baina ya Serikali zetu mbili yaani Kamati ya Pamoja ya Serikali ya
Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, upewe nguvu ya kisheria na kama
hapana budi upewe nguvu ya Kikatiba. Tukifanya hivyo tutafanikiwa kuyaweka
mambo yote sawa hata bila ya kuhitaji kuunda Serikali ya tatu.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Waheshimiwa Wajumbe;
Katika mjadala kuhusu mapendekezo ya kuwa na muundo wa Muungano
wenye Serikali tatu, wananchi wametoa maoni na mapendekezo mengi mazuri
25
kuhusu changamoto za Serikali tatu zilizoainishwa na Tume na namna ya kuzitatua.
Tena yapo maoni ya watu wanaopenda muundo wa Serikali tatu na wasiopenda
muundo wa Serikali tatu. Nawaomba myatafakari kwa uzito unaostahili. Yapo
mambo muhimu ya kuyatafutia ufumbuzi. Kwanza, kwa mfano ni ile hoja kwamba
Serikali ya Muungano inayopendekezwa haikujengeka kwenye msingi imara. Haina
nguvu yake yenyewe za kusimama. Inategemea mno ihsani ya nchi washirika. Kwa
sababu hiyo inaweza kuanguka wakati wowote, na Muungano kusambaratika, iwapo
itakosa ihsani ya nchi washirika. Tena inaweza kuwa hivyo hata kama ni mmoja wa
washirika amefanya hivyo.
Pili, kwamba, haielekei Serikali hiyo ina chanzo cha uhakika cha mapato ya
kuiwezesha kusimama yenyewe na kutekeleza majukumu yake. Ushuru wa bidhaa
unaopendekezwa unatiliwa shaka kuwa hautatosheleza mahitaji. Pia, kwamba,
hakuna uhakika wa fedha hizo kupatikana kwa vile, Serikali ya Muungano haina
chombo chake chenyewe cha kukusanya mapato hayo. Itategemea vyombo vya nchi
washirika kuikusanyia na kuipelekea. Kuna hatari ya shughuli za Serikali ya
Muungano kusimama wakati wo wote au hata kusimama kabisa kwa sababu ya nchi
washirika kuchelewa au kushindwa kuwasilisha makusanyo ya kutoka kwao.
Bahati mbaya Serikali ya Muungano haina uwezo wala nyenzo za kuhakikisha
kuwa mapato yake yanawasilishwa. Serikali hiyo haina mamlaka ya kuzibana nchi
washirika kuwasilisha au kuziwajibisha zisipofanya hivyo. Katika mazingira hayo ni
rahisi kwa Serikali ya Muungano kukwama na kushindwa kutekeleza majukumu
yake. Huu ni muundo ambao inakuwa ni rahisi sana kwa Muungano kuvunjika.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Katika Rasimu ya Katiba, Serikali ya Muungano inapewa fursa ya kukopa
kama chanzo cha kujipatia mapato ya kuendesha shughuli zake. Lakini, kwa sababu
ya kukosa rasilimali zake yenyewe, huenda ikawa vigumu kwa Serikali hiyo
kukopesheka. Kwa jumla hii ni Serikali ambayo ukuu wake hauna nguvu iliyo thabiti,
na watu wengine wanaona kama vile ukuu huo haupo kabisa. Akitokea kiongozi ye
yote wa nchi washirika akatunisha misuli dhidi ya Rais wa Muungano au kupinga
26
maamuzi ya Serikali au chombo cha Muungano, Rais na Serikali yake watakuwa
hawana lo lote la kufanya. Kwa kweli uhai wa Muungano katika muundo wa Serikali
tatu ni wa mashaka makubwa.
Hofu hizi kuhusu udhaifu wa Serikali ya Muungano chini ya mfumo wa
Serikali tatu unaopendekezwa, zinawasumbua hata wale wanaopendelea mfumo wa
Serikali tatu kuwepo. Wao wangependa iwepo Serikali ya Muungano yenye nguvu
na inayoweza kusimama yenyewe kwa kujitegemea. Wanaona kilichopendekezwa
hakitoi matumaini hayo. Hii ina maana kuwa lazima mawazo bora zaidi yatolewe ili
kupata Serikali ya tatu yenye ukuu unaoonekana na inayoweza kusimama yenyewe
bila kuwa tegemezi na egemezi kwa nchi washirika. Pia inaweza kuwa nguzo ya
kutegemewa na nchi washirika. Bila ya shaka Bunge hili likiamua tufuate mfumo huo
linaweza kuonyesha njia ya kuondoa hofu hizo. Kwa waumini wa Serikali mbili
wanaona kuwa huu ni uthibitisho wa ubora wa muundo wa Serikali mbili.
Changamoto za Hisia za Utaifa
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Katika kuainisha changamoto za muundo wa Serikali tatu, Tume ya
Mabadiliko ya Katiba imeyataja mambo mengine mawili makubwa ambayo
ningependa Waheshimiwa Wajumbe muyape tafakuri stahiki. Mambo hayo ni mosi,
misuguano na mikwamo (deadlocks and paralysis) katika kujadili na kufanya uamuzi
kuhusu mambo muhimu ya Muungano. Na pili, ni kuibuka kwa hisia za utaifa
(nationalistic sentiments) wa zamani kwa nchi washirika. Nawaomba myatafakari kwa
makini sana mambo haya, kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kuhatarisha siyo
tu ustawi na uhai wa Muungano, bali hata usalama wa raia na mali zao. Naona hata
Tume haikuweza kupata ufumbuzi ulio mwafaka kabisa kwa changamoto hizi. Bila
ya shaka katika mijadala yenu Waheshimiwa Wajumbe mnaweza kusaidia.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Ni lazima lifanyike kila linalowezekana kuhakikisha kuwa maamuzi
hayakwami kwani yakikwama maana yake shughuli za Muungano zitakuwa
zimekwama. Kama hazitakwamuliwa kwa wakati ustawi wa Muungano utaathirika.
27
Ikishindikana kabisa kupatikana ufumbuzi Muungano unaweza kuvunjika. Kuibuka
na kukua kwa hisia za utaifa (nationalistic feelings) kwa nchi washirika, yaani
Utanganyika na Uzanzibari ni tishio kubwa sana kwa uhai wa Muungano. Hebu
fikiria, watu walioishi pamoja kidugu na kwa kushirikiana, kama watu wamoja na
raia wa nchi moja yaani Watanzania kwa miaka 50, kuja kujikuta uhusiano wao kuwa
ni kati ya Watanganyika na Wazanzibari na siyo kati ya Watanznaia. Kwa mujibu wa
sensa iliyopita takriban asilimia 90 ya Watanzania waliopo sasa wamezaliwa baada
ya mwaka 1964. Nchi wanayoijua ni Tanzania. Litakuwa ni jambo lenye mshtuko
mkubwa na athari zisizoweza kutabirika, watu hao watakapojikuta ni wageni
wanaotakiwa kutengenezewa utaratibu maalum wa kusafiri na kuishi wakiwa
upande wa Muungano ambao siyo kwao kwa asili. Wanakuwa wageni na fursa
walizokuwa wanazipata waendapo popote haiwi rahisi tena kuzipata.
Katika mazingira hayo ni rahisi sana chuki kupandikizwa na watu waliokuwa
ndugu mara moja watajikuta maadui. Aidha, watu wanaweza kujikuta wakilazimika
kurudi kwao kwa asili ama kwa kufukuzwa au kwa sababu ya mazingira kuwa
magumu kiasi cha kuona bora waondoke. Watu hao wanaweza kulazimika
kuondoka huku wakiacha nyuma kila kitu walichokichuma maishani.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Changamoto hizi kubwa mbili za mfumo wa Serikali tatu ambazo Tume
imeziona, ni za kweli. Si mambo ya kufikirika. Yale yaliyowakuta watu wenye asili
ya Tanzania Bara ya kuchomewa moto biashara zao Zanzibar mwaka 2012 na watu
wenye hisia kali za Uzanzibari, na kuwataka watu wa Bara waondoke Zanzibar,
huenda yakawa madogo. Matukio ya namna hii yanaweza kutokea pande zote mbili
na kusababisha maafa makubwa. Itaanza baina ya watu, baadaye itakuwa baina ya
Serikali zetu mbili na kuzifikisha nchi zetu mbili zilizokuwa ndugu na rafiki, kwa
nusu karne, ghafla kuwa maadui wasioombana chumvi na wasiotakiana heri. Umoja
wetu utatetereka na Muungano wetu unaweza kuvunjika. Kwa nini tufike huko?
Mheshimiwa Mwenyekiti;
28
Sisi viongozi tuliopewa dhamana ya kuamua kwa niaba ya wananchi wetu,
hatuna budi kuyapima mambo haya kwa umakini mkubwa ili tufanye uamuzi ulio
sahihi. Tusije tukajutia uamuzi wetu tutakapoona watu wanafukuzana, wanauana na
mali zao kuporwa. Na, tukifikia hatua hiyo Muungano kusambaratika halitakuwa
jambo la ajabu.
Kwa kweli, unapoyatafakari haya, ni rahisi kuelewa kwa nini wazee wetu
waasisi waliamua walivyoamua. Waliona mbali. Tusipuuze fikra zao na maono yao.
Kuna hatari ya nchi yetu na watu wake kupoteza kila kitu tulichokijenga kwa miaka
50. Badala ya kujenga tunaweza kujikuta tumebomoa hata msingi katika nchi
washirika. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1993 alituasa kuhusu
hatari hiyo: “Hamuwezi kutenda dhambi kubwa namna hiyo bila adhabu… na
adhabu nyingine zimo mle mle ndani ya kitendo hazisubiri.”
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Siku moja kiongozi mmoja wa juu wa madhehebu ya dini nchini aliniuliza:
“Hivi Serikali mbili zikiwa na matatizo jawabu ni kuongeza ya tatu? Si matatizo
ndiyo yatazidi? Je, matatizo yakizielemea hizo Serikali tatu si kila mtu atachukua
njia yake? Mtakuwa mmepoteza kila kitu. Mimi nawashauri msichoke kutafuta
majawabu kwa matatizo ya hizi mbili! Huko mnakotaka kwenda kuna hatari
nyingi”.
Pengine na ushauri huu wa mtu wa Mungu nao ni vyema kuupa nafasi na
kuutafakari.
Kazi Yenu Kubwa
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Mambo ya kuyasemea ni mengi mno lakini kwa sababu ya ufinyu wa muda,
nisingeweza kuyazungumzia yote. Naamini, mtayaona katika kuipitia Rasimu na
kwenye majadiliano yenu. Napenda kusisitiza kwenu kuwa kazi iliyo mbele yenu ni
29
kubwa sana. Ni kubwa kwa maana mbili. Kwanza, jukumu lenyewe la kutunga
Katiba ya nchi ni zito sana. Taswira ya nchi yetu itakuwaje na itaendeshwa vipi kwa
miaka mingi ijayo iko mikononi mwenu. Ipeni nchi yetu hatima njema. Pili, ni
kubwa kwa maana ya uzito wa mambo ya kujadili na kuyafanyia uamuzi. Kwa ajili
hiyo, ni muhimu sana kuisoma Rasimu na Taarifa ya Tume kwa makini na kuzielewa.
Jipeni muda wa kutafakari kila neno, kila sentensi, na kila dhana ili muweze kufanya
uamuzi ulio sahihi. Mkifanya hayo mtakuwa mmeisaidia nchi yetu na Watanzania
wote kupata Katiba nzuri.
Nimefarijika sana kusikia kuwa mtajigawa kwenye Kamati 12 wakati wa
kujadili Rasimu. Huu ni utaratibu mzuri kwani mkiwa katika vikundi vya watu
wachache, mtakuwa na mijadala ya kina zaidi. Watu wote wanaweza kupata fursa ya
kutoa maoni yao, kwa kila kifungu na kila jambo linaloibuliwa na kuzungumzwa.
Kwa kufanya hivyo, mtatimiza kwa ukamilifu jukumu lenu la kutunga Katiba. Wote
mtakuwa mmeshiriki kujadili kila sura na vipengele vyake vyote. Mkimaliza kazi
yenu mtapokea kwa haki sifa nzuri kama Katiba itakuwa nzuri, au lawama stahiki
iwapo itakuwa kinyume chake.
Pongezi kwa Mwenyekiti wa Muda
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Nitakuwa mwizi wa fadhila kama nitamaliza hotuba yangu bila ya kutambua
kazi nzuri iliyofanywa na Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, Spika wa Baraza la
Wawakilishi, alipokuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hili. Kazi yake haikuwa
rahisi hata kidogo, lakini kwa umahiri na ustadi mkubwa ameweza kufanikisha
mambo kwa kiasi ambacho anastahili pongezi zetu sote. Anastahili pongezi kwa
sababu yeye aliendesha Bunge hili bila ya kuwepo kwa kanuni. Tatizo hili hatakuwa
nalo Mwenyekiti wa Kudumu kaka yangu Mheshimiwa Samuel Sitta.
Napenda pia kuwapongeza Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge Maalum la
Katiba kwa hatua mliyofikia. Hata hivyo, mmechukua muda mwingi katika hatua ya
awali hivyo hamna budi kuongeza kasi. Naomba niwakumbushe kuwa mijadala
yenu hii inafuatiliwa kwa karibu sana na Watanzania. Wamewekeza sana matarajio
30
yao kwenu. Hamna budi, haiba na taswira ya uongozi muionyeshe wakati wote wa
kuendesha mijadala yenu kwa lugha na vitendo vyenu. Wakati wa semina na mjadala
wa kupitisha Kanuni za Bunge hili, baadhi ya wananchi wamekwazika sana na
mwenendo wa baadhi ya Wajumbe. Hawakutegemea kuyaona matendo
waliyoyaona mkifanya na kusikia maneno waliyoyasikia kutoka kwenye vinywa vya
baadhi yenu.
Ni matumaini yangu na ya Watanzania wote kuwa hali ile haitajirudia tena
katika awamu hii. Tusiwafikishe mahali Watanzania wakakata tamaa na Wajumbe
wao au na hata chombo hiki muhimu sana kwa mustakabali wao na wa nchi yao.
Tutoe hoja badala ya kupiga kelele (argue don’t shout) au kuzomea. Hakuna haja ya
kutumia lugha isiyokuwa ya staha katika kujieleza. Hakuna haja ya kukingiana
ngumi, kutishiana hili na lile au hata kugombana. Ni utovu wa uungwana
usiotegemewa kutoka kwenu. Tusiwaangushe wananchi wa Tanzania
wanaotutegemea sana.
Wekeni Maslahi ya Taifa Mbele
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Ombi langu la mwisho kwenu ni kuwasihi kuwa wakati wote muongozwe na
kujali maslahi mapana ya nchi yetu na watu wake badala ya kujali maslahi yenu
binafsi au ya makundi yenu. Naomba kaulimbiu yenu iwe “Tanzania Kwanza”.
Najua kila mmoja wenu amekuja na maoni yake au atakuwa nayo kwa kila jambo
litakalojadiliwa. Wengine wamepewa misimamo na vyama vyao au makundi yao. Si
jambo baya na ni hatua muhimu ya kuleta mafanikio, kama misimamo hiyo na
mawazo hayo ni ya kujenga.
Hata hivyo, mnachotegemewa kufanya ni kuwa tayari kuwianisha na
kuunganisha mawazo yenu mazuri na ya wenzenu, ili kupata msimamo wa pamoja
na uamuzi wa pamoja ulio bora. Kwa sababu hiyo, hamna budi kuwa tayari
kusikiliza mawazo ya wengine, hata kama ni tofauti na yenu mliyokuja nayo.
Tafuteni kilicho chema kwa yale yanayosemwa na watu wengine hata kama ni watu
31
usiokubaliana nao au huwapendi au hampendani. Kunaweza kuwepo kitu chenye
manufaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wajumbe;
Nawaomba muwe hodari wa kushawishi badala ya kulazimisha. Mkifanya
hivyo hamtalazimika kutumia muda mwingi wa kula njama za namna ya kuwazidi
maarifa wale mnaotofautiana nao kwa mawazo. Lazima pia mtafute namna ya
kushirikiana na kuwasiliana na makundi mengine. Msitafute kushindana, hili ni
jambo ambalo lazima wote mtoke hapa mkiwa washindi. Yaani lazima Watanzania
wote washinde kwani wao ndiyo wenye Katiba yao. Nawapongeza viongozi wa
vyama vya siasa na asasi mbalimbali kwa kutambua na kuthamini umuhimu wa
kuwa na taratibu za mawasiliano, mashauriano na ushirikiano. Daima muwe watu
wa kutafuta maridhiano. Mmefanya vizuri katika hatua ya awali. Mmejiwekea
taratibu nzuri za kufanya hayo, tafadhalini zitumieni. Jengeni madaraja imara zaidi
katika awamu hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Naomba nimalize kwa kuwaomba Watanzania wote tukiongozwa na viongozi
wetu wa dini tumuombe Mola wetu ajalie rehema zake ili mchakato wa kutunga
Katiba uende salama. Aliongoze Bunge hili na Wajumbe wake waweze kufanya
uamuzi ulio sahihi na wenye manufaa kwa taifa letu kwa kila watakaloliamua.
Baada ya kusema maneno yangu mengi hayo, nirudie kukushukuru
Mheshimiwa Mwenyekiti kwa kunipa fursa hii adhimu ya kulihutubia Bunge
Maalum la Katiba. Nawatakieni kila la heri na mafanikio mema. Katiba Mpya
Inawezekana, Timiza Wajibu Wako.
Mungu Ibariki Tanzania!
Mungu Libariki Bunge Maalumu la Katiba!
Asanteni sana kwa kunisikiliza!