SHULE CHACHE ZAJITOKEZA KATIKA MGOMO WILAYANI HAI

Posted by MK On 08:12 No comments

Na Richard Mwangulube,Hai

Jeshi la Polisi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro limelazimika kumhoji katibu wa Chama cha Walimu,CWT wilayani Hai kwa tuhuma za kuwatisha na kuwatoa madarasani baadhi ya walimu wa shule za msingi na sekondari ambao wamepuuza mgomo ulioitishwa na chama hicho na kuingia madarasani na kuendelea kufundisha.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa katibu huyo wa CWT Hai Bw Dowanson Temu alikutwa akifanya hivyo katika Shule ya Msingi Hai ambapo alifanikiwa kuwatoa madarasani walimu wote kumi na wanne huku watatu wakikataa na baadaye anadaiwa kuelekea katika shule ya sekondari ya Boma na baadaye shule ya Msingi Uhuru ambapo walimu wote wa shule hizo  walikataa kufanya mgomo na kuendelea na ufundishaji

Mkuu wa wilaya ya Hai,Mhe. Novatus Makunga amethibitisha kuhojiwa kwa katibu huyo kutokana na tuhuma za malalamiko ya walimu ambao pia wamedai kwamba walitishiwa kuletewa kundi la wenzao kwa ajili ya kuwachapa fimbo wote ambao watabainika ni wasaliti.

Ameeleza kuwa jeshi la Polisi lilianza kuwahoji maofisa wa Elimu wa halmashauri ya wilaya ya Hai na baadaye ndipo ilipofany hivyo kwa katibu Temu na baadaye kumwachia huru wakati upelelezi zaidi wa tukio hilo ukiendelea

Mkuu huyo pia alizungukia baadhi ya shule wilayani humo na kuwaakikishia walimu usalama wao kwa kuwataka waendelee na kazi wakati serikali bado ipo katika majadiliano na walimu wote nchini

Akizungumzia hali ya mgomo,Mhe Makunga ameeleza kuwa shule tatu za sekondari kati ya shule zote 44 ndizo walimu wameingia katika mgomo na amezitaja kuwa ni pamoja na Harambee na Uduru zilizoko kata ya machame kaskazini  na Kia iliyopo kata ya kia.

Kwa upande wa shule za msingi ameeleza kuwa ni shule mbili za Kibao na Mtakuja ndizo ziulizoingia katika mgomo kati ya shule zote za msingi 119

0 comments:

Post a Comment