Ujumbe wa Tanzania ambazo kwa mwezi mzima umeshiriki kikamilifu hadi usiku wa manane pale ilipobidi na kuhakikisha kwamba maslahi ya Tanzania katika majadiliano ya kidiplomasia ya nchi wanachama kuhusu Mkataba wa Kisheria wa Kudhibiti Bishaara ya Silaha duniani yalikuwa yamezingatiwa.
Hata hivyo mkutano huo ulioanza Julai Mbili na kumalizika Julai 27 umeshindwa kutoa Mkataba kutokana na wajumbe kutokukubaliana kuhusu baadhi ya vipengere ambavyo wengine walikuwa wanataka viwe sehemu ya mkataba, huku wengine wakikataa kata kata.
Mkataba huo kama ungepatikana ulitarajiwa kwamba ungeleta matumaini na unafuu kwa mamilioni ya watu ambao maisha yao kila siku yamo hatarini kutokana na matumizi mabaya ya silaha. Inaelezwa kwamba biashara ya silaha duniani inashika nafasi ya pili baada ya biashara ya madawa ya binadamu.
Kutoka kushoto mstari wa mbele ni Bw. Theobald Kazora kutoka Ofisi ya Rais, Brigedia Jenerali Dkt. Charles Muzanila kutoka JWTZ ambaye pia alikuwa kiongozi wa ujumbe, Kaimu Balozi, Dkt. Justin Seruhere ambaye pia alikuwa kiongozi wa ujumbe akisaidia na Brigedia Jenerali Muzanila na Bw. John Kinuno ambaye ni wakili kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kutoka kulia mstari wa nyuma ni Bw. Peter Macomara kutoka Taasisi ya Kiraia, Brigedia Jenerali Venance Mabeyo kutoka JWTZ na Kamishna Esaka Mugasa kutoka Jeshi la Polisi na Mwambata Jeshi katika Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Meja Wilbert Ibuge ambaye hayupo pichani
0 comments:
Post a Comment