MWENGE WA UHURU WAINGIA NYUMBANI "KILIMANJARO"

Posted by MK On 08:16 No comments


Na Mwandishi Wetu,Same

Miradi 51  yenye thamani ya shilingi bilioni  5.8 itazinduliwa wakati wa mbio za mwenge mkoani Kilimanjaro.

Mwenge huo umepokelewa Leo asubuhi na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Leonidis  Gama  kutoka mkoani Manyara katika mji wa Hedaru uliopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro

Mkuu wa mkoa Mhe Gama  amesema kati ya miradi hiyo, miradi 23 inatarajiwa kuzinduliwa   wakati wa mbio hizo  za mwenge wa uhuru huku miradi 20 itawekewa mawe ya msingi  na  miradi nane itatembelea  na wakimbiza mwenge kitaifa


Bwana Gama amefafanua kuwa  kati ya miradi hiyo 51, miradi 15 ni ya sekta ya elimu,miradi  nane ya afya, maji miradi miwili, kilimo na ufugaji miradi  sita

Aidha mkuu huyo wa mkoa  ameeleza kuwa miradi  miwili  ni ya miundo mbinu, hifadhi ya mazingira  miradi minne , biashara na ujasiriamali miradi  mitano pamoja na miradi ya utawala  na miradi mingine ya maendeleo

Mkuu huyo wa mkoa   amefafanua kuwa  serikali kuu imechangia kiasi cha shilingi   bilioni  3,607,631,886/ na mchango wa serikali za mitaa  ni shilingi   milioni  659,778250/  

Aidha nguvu za wananchi wamechangia kiasi cha shilingi 774,103,801/ na mashirika wahisani ya  kutoka mataifa mbalimbali  wamehangia kiasi cha shilingi  801,197,120/  Ameeleza Mkuu huyo wa Mkoa wa Kilimanjaro leo

Ukiwa Mkoani Kilimanjaro Mwenge wa Uhuru umeanza kwa kukimbizwa katika  Halmashauri ya Same na kesho utaendelea Mwanga ikifuatiwa na  Moshi Vijijini, Rombo,manispaa ya  Moshi, Hai na  Siha kabla ya kukabidhiwa kwa kwa Viongozi wa Mkoa wa Arusha mnamo Agosti 7, mwaka huu eneo la KIA. 

Mwenge wa Uhuru uliwashwa kwa mara ya kwanza Desemba 9 mwaka 1961,siku ya Uhuru wa Tanzania na kupandishwa katika kilele cha mlima Kilimanjaro



 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Leonidas Gama(Kulia) akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe Mbwilo
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Leonidas Gama(Kulia) akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe Mbwilo
 Viongozi mbalimbali wa halmashauri za wilaya na manispaa katika mkoa wa Kilimanjaro wakisubiri kupokea mwenge wa Uhuru kutoka mkoani Manyara
 Mkurugenzi wa halmashauri ya Hai,Bwana Humbe(Katikati) akiwa na katibu wa CCM mkoani Kilimanjaro Bwana Kazidi(Kulia}
 Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro kutoka kulia ni Mhe Novatus Makunga(Hai),Mhe Pallangyo(Rombo),Mhe Dkt Charles Mlingwa(Siha) na Herman Kapufi wa same
 Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaro kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoani Kilimanjaro Mama Nsilo Swai,Mhe Shaibu Ndemanga(DC-Mwanga),Mhe Novatus Makunga(DC-Hai) na Mhe Pallangyo ambaye ni DC-Rombo
 Mwenge eeh Mwenge Mbio mbio,mwenge tunaukimbiza mbio mbio......muda mfupi kabla ya makamanda wa mkoa wa Manyara hawajaukabidhi katika mkoa wa Kilimanjaro

0 comments:

Post a Comment