RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA KARAKANA (HANGA) YA NDEGE ZA SHIRIKA LA NDEGE LA PRECISION AIR

Posted by MK On 22:59 1 comment

Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la ndege la Precision Air Bw. Michael Shirima akimkabidhi zawadi Mh Rais Dk. Jakaya Kikwete mara baada ya kuzinduz rasmi karakana na ndege za shirika hili (Hanga) kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere leo jijini Dar es salaam, Karakana hiyo itakuwa ikihudumia ndege za shirika hilo la mashirika mengine pia lakini pia itapokea wanafunzi walio kwenye mafunzo ya Uinjini wa ndege kutoka katika vuo vya ndani.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe pamoja na wakuu mbalimbali wa shirika la ndege la Precision Air na wafanyakazi wa shirika hilo mara baada  ya uzinduzi wa (Hanga) hiyo
Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ndege la Precision Air Bw. Alfonce Kioko alipokuwa akitoa maelezo  wakati wakati Rais alipokuwa akikagua  Hanga hiyo, kulia ni Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe 
Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya shirika la ndege la Precision Air Bw. Michael Shirima katikati mara baada ya kuzindua Karakana ya ndege za shirika hilo, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ndege la Precision Air Bw. Alfonce Kioko
Rais Jakaya Kikwete akiweka mkasi mara baada ya kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Karakana na ndege za shirika la ndege la Precision Air leo kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es salaam kulia ni Bw Bw. Michael Shirima

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Precision Air Bw Michael Shirima wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere tayari kwa uziduzi wa Karakana wa ndege za  kampuni hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw Alfonce Kioko, katikati ni Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik
Mkurugenzi wa Hoteli ya Kibo Palace ya Arusha Bw Vicent Laswai naye amehudhuria katika uzinduzi huo kama mdau wa Utalii.Picha zaidi Bofya Hapa.

1 comments:

Post a Comment