Na Mwandishi Wetu,Same
Miradi 51 yenye thamani ya shilingi bilioni 5.8 itazinduliwa wakati wa mbio za mwenge mkoani Kilimanjaro.
Mwenge huo umepokelewa Leo asubuhi na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Leonidis Gama kutoka mkoani Manyara katika mji wa Hedaru uliopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro
Mkuu wa mkoa Mhe Gama amesema kati ya miradi hiyo, miradi 23 inatarajiwa kuzinduliwa wakati wa mbio hizo za mwenge wa uhuru huku miradi 20 itawekewa mawe ya msingi na miradi nane itatembelea na wakimbiza mwenge kitaifa
Bwana Gama amefafanua kuwa kati ya miradi hiyo 51, miradi 15 ni ya sekta ya elimu,miradi nane ya afya, maji miradi miwili, kilimo na ufugaji miradi sita
Aidha mkuu huyo wa mkoa ameeleza kuwa miradi miwili ni ya miundo mbinu, hifadhi ya mazingira miradi minne , biashara na ujasiriamali miradi mitano pamoja na miradi ya utawala na miradi mingine ya maendeleo
Mkuu huyo wa mkoa amefafanua kuwa serikali kuu imechangia kiasi cha shilingi bilioni 3,607,631,886/ na mchango wa serikali za mitaa ni shilingi milioni 659,778250/
Aidha nguvu za wananchi wamechangia kiasi cha shilingi 774,103,801/ na mashirika wahisani ya kutoka mataifa mbalimbali wamehangia kiasi cha shilingi 801,197,120/ Ameeleza Mkuu huyo wa Mkoa wa Kilimanjaro leo
Ukiwa Mkoani Kilimanjaro Mwenge wa Uhuru umeanza kwa kukimbizwa katika Halmashauri ya Same na kesho utaendelea Mwanga ikifuatiwa na Moshi Vijijini, Rombo,manispaa ya Moshi, Hai na Siha kabla ya kukabidhiwa kwa kwa Viongozi wa Mkoa wa Arusha mnamo Agosti 7, mwaka huu eneo la KIA.
Mwenge wa Uhuru uliwashwa kwa mara ya kwanza Desemba 9 mwaka 1961,siku ya Uhuru wa Tanzania na kupandishwa katika kilele cha mlima Kilimanjaro
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Leonidas Gama(Kulia) akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe Mbwilo
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Leonidas Gama(Kulia) akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe Mbwilo
Viongozi mbalimbali wa halmashauri za wilaya na manispaa katika mkoa wa Kilimanjaro wakisubiri kupokea mwenge wa Uhuru kutoka mkoani Manyara
Mkurugenzi wa halmashauri ya Hai,Bwana Humbe(Katikati) akiwa na katibu wa CCM mkoani Kilimanjaro Bwana Kazidi(Kulia}
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro kutoka kulia ni Mhe Novatus Makunga(Hai),Mhe Pallangyo(Rombo),Mhe Dkt Charles Mlingwa(Siha) na Herman Kapufi wa same
Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaro kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoani Kilimanjaro Mama Nsilo Swai,Mhe Shaibu Ndemanga(DC-Mwanga),Mhe Novatus Makunga(DC-Hai) na Mhe Pallangyo ambaye ni DC-Rombo
Mwenge eeh Mwenge Mbio mbio,mwenge tunaukimbiza mbio mbio......muda mfupi kabla ya makamanda wa mkoa wa Manyara hawajaukabidhi katika mkoa wa Kilimanjaro