NAFASI ZA KAZI
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA
HAI
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE
Ø
Awe
raia wa Tanzania na mwenye umri usiozidi miaka 45
Ø
Waombaji
wote waambatanishe vyeti vya kuzaliwa
Ø
Waombaji
waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza(detailed CV) yenye anuani na
namba ya simu za kuaminika na majina ya wadhamini(Referees) watatu wa
kuaminika.
Ø
Maombi
yaambatanishwe na vivuli vya vyeti vya taaluma,picha za Passport size
mbili,maelezo,nakala ya vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale
waliofika kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia
sifa za kazi husika.Viambatanishi hivyo vibanwe vizuri kuondoa uwezekano wa
kudondoka au kupotea.
Ø
Tesmonials,provisional
Results”Statement of result” hati ya matokeo ya kidato cha nne na sita(Form IV
and Form VI Result Slips) havitakubaliwa.
Ø
Waombaji
waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa
na mamlaka husika (TCU na NACTE)
Ø
Waombaji
ambao tayari ni watumishi wa umma na wamejipatia sifa za kuingia kutoka kada
tofauti na walizonazo,wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa
waajiri wao.
Ø
Waombaji
waliostaafishwa katika utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana
kibali cha katibu mkuu kiongozi
1.
KATIBU
MAHSUSI DARAJA LA III (NAFASI 4)
SIFA
ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV
waliohudhuria mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa hati ya tatu.Wawe
wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja
na wawe wamepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuwa na
serikali na kupata cheti katika program za Windows,Microsoft
Office,Internet,E-Mail na Publisher.
2.
MSAIDIZI WA
KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NAFASI 2)
SIFA
ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne
wenye cheti cha utunzaji kumbukumbu katika fani ya masjala.
3. MTENDAJI WA
KIJIJI DARAJA LA III (NAFASI 18)
SIFA
ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye elimu ya kidato cha
nne(IV) au sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya
fani zifuatazo: Utawala,Sheria,Elimu ya jamii,Usimamizi wa fedha,Maendeleo ya
jamii na sayanzi ya sanaa kutoka chuo cha serikali za Mitaa Hombolo,Dodoma au
Chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.
BARUA
ZITUMWE KUPITIA POSTA KWA ANUANI IFUATAYO:
MKURUGENZI
MTENDAJI,
HALMASHAURI
YA WILAYA
S.L.P
27
HAI
MWISHO
WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 11/02/2015
0 comments:
Post a Comment