Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akiwaonyesha wananchi wa kijiji cha Sanya Stesheni Rejesta ya wakazi kama moja ya vitendea kazi vya wenyeviti wa vitongoji |
Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akimkabidhi rejesta ya wakazi mmoja ya wenyeviti wa kitongoji katika kijiji cha Sanya Stesheni |
Ofisa tawala wa wilaya ya Hai akikamkabidhi nakala ya taratibu za kazi za kamati za kudumu za halmashauri ya kijiji cha Sanya Stesheni mmoja kati ya wenyeviti wa kamati hizo |
Mmoja ya wazee wa kabila la Wamaasai akimtawaza Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga kwa miongoni mwa viongozi wa jamii hiyo maarufu kama Laigwanan kwa kumkabidhi rungu. |
Mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Sanya Stesheni baada ya kumkabidhi rungu kama ishara ya uongozi |
Ofisa mtendaji wa kijiji cha Sanya Stesheni,Edes Mtenga akisoma risala ya wananchi wa kijiji cha Sanya Stesheni kwa mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga |
kaimu Ofisa elimu wilayani Hai,Makarios Mapunda akisisitiza kuanza kwa msako mkali wa kudumu wa watoto wote watoro pamoja na wazazi wasiopeleka watoto shule katika kijiji cha Sanya Stesheni |
Afisa ustawi wa Jamii wilayani Hai Hegla Joseph akisisitiza sheria ya haki ya mtoto ya 2009 ya kuwapeleka watoto shule katika mkutano wa kijiji cha Sanya Stesheni |
Afisa wa Polisi jamii pamoja na dawati la watoto na jinsia wilayani Hai akisisitiza sheria ya haki ya mtoto ya 2009 ya kuwapeleka watoto shule katika mkutano wa kijiji cha Sanya Stesheni |
0 comments:
Post a Comment