WILAYA YA HAI YAANZA OPERESHENI YA KUPAMBANA NA ULEVI WA KUPINDUKIA

Posted by Arusha by day and by night On 06:26 No comments

Eneo maarufu kwa utengenezaji wa pombe haramu ya Gongo ndani ya tindiga la Boloti,wilayani Hai,baada ya watengezaji wa pombe hiyo kutelekeza mitambo yao

Eneo ardhi oevu linalotumiwa kama maficho ya watengeneza pombe aina ya gongo wilayani Hai
Eneo la mji mdogo wa Hai maarufu kama Bomang'ombe ambalo hivi sasa linapanuka kwa kasi

Majengo makubwa na ya kisasa ynayojengwa kwa kasi katika mji wa Hai


KUANZA KWA MKAKATI WA KUPAMBANA NA UNYWAJI WA POMBE SAA ZA KAZI PAMOJA NA UUZAJI NA UTUMIAJI WA  POMBE KINYUME NA MASHARTI YA LESENI ZA VILEO WILAYANI HAI

Zoezi la  kutekeleza azimio la Kamati ya ushauri ya Mkoa(RCC) kuhusiana na kilio cha muda mrefu cha jamii katika mkoa wa Kilimanjaro kwa  kuathirika kwa kukithiri kwa unywaji wa pombe wa kupita kiasi ambao umesababisha hata nguvu kazi kubwa hususani ya vijana kuathirika lilianza wilayani Hai Disemba 30,2014.

Zoezi hilo lilitanguliwa na utekelezaji wa agizo la  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Leonidas Gama la kusambazwa katika maeneo yote kwa Waraka namba moja wa mwaka 2014 wa mkuu wa mkoa, ambao ulifafanua lengo la serikali kufanya operesheni ya kudhibiti ulevi wa kupindukia mkoani Kilimanjaro.

Waraka huo uliogiza mamlaka zote za usalama na uongozi wa serikali kuanza rasmi operesheni maalumu ya kudhibiti matumizi ya unywaji wa pombe unaokiuka sheria kwa kuanzia Disemba 15 ulisomwa katika nyumba zote za ibada,kwenye mikosanyiko na kusambazwa kwa Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali(NGO’s) katika mkoa wa Kilimanjaro kwa muda wa mwezi mzima Kuanzia Novemba 15,2014

Katika utekelezaji wa waraka huo,wilaya ya hai ilifanya mambo yafuatayo;
1.      Kuandaa mkakati wa kutekeleza agizo hilo ambapo taratibu za kuunda kikosi kazi chenye askari mgambo sita,wawili wakiwa waajiriwa wa halmashauri ya wilaya pamoja na askari polisi mmoja mwenye silaha umeshakamilika na wataapishwa na hakimu mfawidhi mapema wiki ijayo.Kikosi hiki kitafanya kazi hii kwa kipindi cha miezi sita mfululizo kabla ya kufanyika kwa tathimini ya zoezi zima.

Kadhalika  kitapambana na waaribifu wa mazingira,uzuiaji wa kuingiza mifugo katika mji mdogo wa Hai na uingizaji wa mifugo katika vyanzo vya maji na Chemichemi pamoja na kuendesha kilimo katika kingo za mito na vyanzo vya maji.

2.      Kuandaa mpango kazi ambao tayari umekamilika na utahusisha kata zote pamoja na eneo la mji mdogo wa Hai.Mpango kazi huo kwa uchache umelenga katika mambo yafuatayo;

Ø  Kukagua Grocery zote na kuangalia kama zinafuata sheria za kuuza pombe

Ø  Kukagua baa zote ambazo zinafunguliwa na kufungwa nje ya muda ulioanishwa kwenye leseni

Ø  Maduka yanayouza pombe mbalimbali vikiwemo viroba kinyume na leseni zao za biashara

Ø  Msakako mkali wa maeneo yote yanayotengeneza pombe feki ikiwemp pombe haramu ya gongo pamoja na kuwabaini waliopo katika mtandao wa pombe hizo na maenep yate kunakosambazwa

Ø  Askari wa kikosi cha usalama barabarani kuanza kuwapima madereva wote wa vyombo vya moto kwa kutumia kifaa maalumu endapo watakuwa wametumia aina yoyote ya ulevi.

Ø  Vijiji kutunga sheria ndogo ndogo kudhibiti matumizi yasiyokuwa sahihi ya baadhi ya pombe ambazo zinaharibu ustawi wa jamii husika kama sheria inavyowaruhusu

3.      Msako mkali ulianza tarehe 30/12/2014 katika maeneo yote ya wilaya.Katika msako huo wakuu wa idara wote pamoja na maofisa wengine walishiriki ambapo walijigawa katika makundi sita ili kusambaa katika wilaya nzima kwa wakati mmoja.makundi yote sita yalifuatana na askari wawili wawili wenye silaha kwa ajili ya ulinzi wakati wa zoezi hilo.

Mkuu wa wilaya ya Hai, Mheshimiwa Novatus Makunga na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Hai,Bwana Melkizedeck Humbe walikuwa wasimamizi wa zoezi zima

MATOKEO YA MSAKO HUO HADI KUFIKIA TAREHE 31 DISEMBA 2014 NI KAMA UFUATAVYO;

S/N
AINA YA BIASHARA
WENYE LESENI ZA BIDHAA ZA KAWAIDA LAKINI WANAUZA POMBE
WENYE LESENI LAKINI WANAUZA POMBE KINYUME NA MUDA WA KISHERIA
HAWANA LESENI WAKIUZA BIDHAA ZA KAWAIDA PAMOJA NA POMBE
HATUA ZILIZOCHUKULIWA
1
Maduka ya Kawaida
21

37
Wote wamepigwa faini ya Tshs 50,000/= kwa kila mmoja na kupewa onyo
2
Baa za pombe za viwandani(kigeni)

4
3
Wote wametozwa faini ya Tshs 50,000/= kwa kila mmoja na kupewa onyo kali
3
Baa za pombe za kienyeji

6

Wote wametozwa faini ya Tshs 50,000/= kwa kila mmoja na kupewa onyo kali
4.
Glosary
9 (Kufanya biashara ya baa badala ya Glosary)

17


Jumla
30
10
57


Mambo yaliyojitokeza katika zoezi hilo

1.      Wafanyabiashara wengi wanauza bidhaa za kawaida pamoja na pombe kinyumbe na masharti ya leseni zao

2.      Wapo wafanyabiashara wengi zaidi wanaofanya biashara zao bila ya kuwa na leseni wakati huo huo wanauza bidhaa za kawaida kwa kuchanganya na pombe.Hali hii imeipotezea mapato mengi halmashauri ya wilaya.

3.      Wafanyabiashara wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu kuendesha biashara kwa kuzingatia masharti ya leseni

4.      Jamii bado haina uelewa wa kuwepo kwa sheria inayosimamia muda maalumu wa kuanza  kuuza pombe na muda wa mwisho wa kuuza pombe ambao unatofautiana katika maeneo ya mijini na vijijini

0 comments:

Post a Comment