SERIKALI YAANZA UKARABATI WA BARABARA ZA HAI MJINI

Posted by Arusha by day and by night On 03:24 No comments



Na Mwandishi Wetu,Hai,Januari 13,2015

Wilaya ya Hai imeanza awamu ya pili ya ukarabati wa barabara za mji mdogo wa Hai wenye lengo la kuziimarisha zaidi kutokana na fedha za mfuko wa barabara zinazotolewa kwa halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro kwa  kila mwaka .

Ufafanuzi huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga baada ya baadhi ya wananchi kutoa malalamiko ya kwamba ukarabati huo ufanyika kwa kujimbua barabara na hivyo baadaye kusababisha adha kutimka kwa vumbi kwa wananchi wanaofanya shughuli zao pembezoni mwa barabara.

Makunga ameeleza kuwa ukarabati huo ambao umejionyesha katika taarifa ya matengenezo ya barabara wilayani Hai kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015 aliyoitoa kwa umma mwezi Agosti mwaka jana.

Amesema ukarabati unaoendelea sasa kwa waliofuatilia taarifa hiyo ni ule uliopangwa kufanyika kufanyika kati ya Mwezi Januari hadi Machi mwaka huu ambao unahusisha barabara za Hai mjini zenye jumla ya kilometa kumi na mbili.

Kwa mwaka huu wa fedha serikali kupitia Mfuko wa barabara umeitengea halmashauri ya wilaya kwa ajili ya ukarabarati wa barabara ikiwemo ujenzi wa madaraja pamoja na makalvati kiasi cha shilingi 1,026,434,000 

Ameeleza kuwa ukarabari huo wa  barabara hizo unafanyanyika ili  kuziimarisha ikiwemo ya kuweka mitalo ya kutolea maji barabarani kwa ajili ya maandalizi ya kuweka lami kwa awamu angalau kwa kila mwaka kwa kilometa zisizopungua moja kwa kutumia makusanya ya ndani ya wilaya.

“Katika vikao vilivyopita vya Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) pamoja na Bodi ya barabara ya mkoa lilipitishwa azimio kwa kila wilaya katika mkoa wa Kilimanjaro ipange utaratibu wa kujenga angalau kilometa moja ya lami kwa kila mwaka kupitia makusanyo ya mapato ya vyanzo vya ndani ya wilaya”alifafanua Makunga.

Makunga ametaja barabara ambayo ukarabati huo utakuwa wa kiwango cha juu ni inayoelekea  katika hospitali kuu ya serikali ya wilaya ikiunganishwa na barabara kuu ya Moshi hadi Arusha.

Ametaja maeneo mengine kuwa ni pamoja na Gezaulole,Kingerera,Dorcas na Bomani ambapo jumla ya gharama za ukarabati huo ni shilingi milioni 44 kwa barabara hizo za mji mdogo wa Hai.

Makunga amewataka wananchi kuondoa wasiwasi ya aina ya ukarabati huo ambapo ameeleza kuwa umelenga kufanyika tofauti na miaka ya nyuma kutokana na sasa eneo la kata ya Hai kupanda hadhi na kuwa mji mdogo 

Mji mdogo wa Hai ina kata tatu ambazo niBomang'ombe,Bondeni na Muungano zenye jumla ya kumi na saba
Taarifa ya awali iliyolewa na mkuu huyo wa Hai mwezi Agosti mwaka huu ambapo baadhi ya kazi zilishafanyika ni hii ifuatayo;


ACTION PLAN FOR MAINTENANCE OF DISTRICT ROADS BY ROAD FUND FINANCE YEAR 2014/2015
PACKAGING OF WORKS
SN
Road Name
Type of Maintenance
Length (Km)
Approved Budget (Tshs)
Implementation Period
1
Construction of Mnepo bridge
Bridge Construction
1No.
357,000,000
July-September
Total Package No.1
0
357,000,000
2
Shirinjoro-Lyamungo Sinde
Lyamungo Sinde-Mfoni
Shirinjoro-Lyamungo Sinde
Lyamungo Sinde-Kyalia
Elitira Mengi-Kyalia
Shirinjoro-Lyamungo Sinde
RM
RM
SI
RM
RM
PM
12
3
2
4
2
2
14,400,000
3,600,000
10,000,000
4,800,000
32,000,000
32,000,000
July-September
Total Package No.2
25
96,800,000
3
Kwasadala – Longoi
Bomang’ombe – Kikavuchini
Kwasadala – Longoi
Bomang’ombe - Kikavuchini
RM
RM
SI
PM
12.5
12
2
3
15,000,000
14,400,000
10,000,000
48,000,000
July-Septemba
 Total Package No.3
29.5
87,400,000
4
Sonu – Saawe
Kwasadala – Uswaa
Kwasadala –Uswaa
Sonu – Saawe
Lambo – Makoa
Bwani - Kyeeri
RM
RM
PM
PM
RM
RM
4
5.6
1
4
5
4
4,800,000
6,720,000
16,000,000
64,000,000
6,000,000
4,800,000
October-December
Total Package No.4
23.6
102,320,000
5
Kyuu – Lukani
Lukani – Mashua
Kwa Frank – Kyuu
Mbweera – Ufisi
Lukani – Mashua
Marukeni – Kyuu
Marukeni - Kyuu
RM
PM
RM
SI
SI
SI
RM
4
2.79
4
1.4
2
2
7
4,800,000
44,640,000
4,800,000
7,000,000
10,000,000
10,000,000
8,400,000
October- December
Total Package No.5
23.19
89,640,000
6
Marukeni - Kyuu
PM
5
80,000,000
January-March
Total Package No.6
5
80,000,000
7
Hai Town Roads
KIA – Mtakuja
Hai Town Roads
Construction of 1No.Vented Drift
PM
RM
PM
Construction
10
7.3
2
1No.
12,000,000
8,760,000
32,000,000
20,000,000
January-March
Total Package No.7
19.3
72,760,000
8
Shirinjoro – Mijongweni
Mferejini – Kimashuku – Kwatito
Shirinjoro – Mijongweni
Construction of 1No.Vented drift
1No.Bridege Repair-Weruweru
RM
RM
SI
Construction
Repair
5.17
7
0.83
1No.
1No.
6.204,000
8,400,000
4,150,000
20,000,000
10,000,000
April - June
Total Package No.8
13
48,754,000
9
Culvert Installation(No. 1 – No. 8)
52,270,000
July’13 – June’14
10
Supervision and Vehicle Maintenance(No.1 – No.8)
39,490,000
July’13 – June’14
GRAND TOTAL
138.59
1,026,434,000
Abbreviations
RM – Routine Maintenance
SI -    Spots Improvement
PM – Periodic Maintenance

MOSHI WAANZA MSAKO MKALI KWA WANAOUZA POMBE ZA KAZI

Posted by bomang'ombe On 11:44 No comments

Na Mwandishi Wetu,Moshi Halmashauri zote mbili katika wilaya ya Moshi zimeanza utekelezaji wa waraka namba moja wa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro unaohusu kudhibiti unywaji wa pombe usiozingatia sheria ya vileo nchini. Kaimu mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga amewaeleza waandishi wa habari mjini hapa kwamba halmashauri ya manispaa ya Moshi na halmashauri ya wilaya ya Moshi zote zilianza operesheni hiyo Desemba 15 ya mwezi uliopita. Ameeleza waraka huo uliagiza operesheni hiyo inayolenga kukomesha maduka ya kawaida kuuza pombe hususani viroba pamoja na baa kuuza vinywaji vikali saa za kazi ilitakiwa kuanza Desemba 15 mwaka jana. Makunga ameeleza kuwa operesheni hiyo ambayo itakuwa ya kudumu kama ile ya kudhibiti ukataji wa miti mkoani Kilimanjaro pia itazihusu pombe haramu ukiwemo ya gongo na zile feki zenye athali kubwa zaidi kwa binadamu. Amesema sheria ya muda ya kuuza pombe ipo wazi na ni sheria ambayo ilikuwepo tangu uongozi wa rais wa awamu ya kwanza ambapo kwa siku za mijini kwa katikati ya wiki ni kuanzia saa tisa mchana mpaka saa nne za usiku na kwa siku za mwisho wa wiki ni kuanzia saa sita mchana mpaka saa tano usiku. "Kadhalika ndani yake tunajumuisha mirungi pamoja na bangi ambavyo vimekuwa tatizo na janga kubwa katika jamii hususani kundi la vijana" alisisitiza. Amefafanua kwamba kwa upande wa manispaa ya Moshi imeanza kwa kuunda kamati maalumu ya kudhibiti unywaji wa pombe usiozingatia kanuni. Kamati hiyo pia inawaelimisha watumishi wote kuanzia ngazi ya mitaa kuhusu waraka huo pamoja na sheria nyingine za vileo,kutoa katangazo kwa jamii kuhusu kukemea unywaji wa pombe hovyo,kukagua na kuanisha maeneo yote yenye matatizo ya kupindukia ya ulevi. Ameyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na kituo kikuu cha mabasi na baa zinazozunguka kituo hicho pamoja na mitaa yenye baa nyingi ambapo tayari kumekuwepo na misako ya kustukiza. Makunga amesema zoezi hilo linafanywa kwa ushirikiano kati ya maofisa wa manispaa na jeshi la polisi kwa uratibu wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya. Ameeleza kuwa mpaka mwishoni mwa wiki katika manispaa jumla ya madereva 15 walibainika kuwa wamelewa na kupigwa faini,lita nne za gongo pamoja na watuhumiwa kumi walikamatwa na pia kukamatwa kwa mirungi kilo 25 na watuhumiwa 4 pamoja na bangi kilo 50 na watuhumiwa 6. Kwa yale makosa ya kawaida yanayoangukia katika masuala ya leseni watuhumiwa wametozwa faini ya kati ya shilingi 40,000 na 50,000 na kwa makosa ya kijinai kesi zao zipo polisi tayari kufikishwa mahakamani. Makunga ameeleza kuwa kwa upande wa halmashauri ya wilaya ya Moshi hadi kufikia mwishoni mwa wiki misako mikali imefanyika eneo la Himo na Njiapanda ambapo zaidi ya maduka arobaini yalibainika kukiuka leseni za biashara. Aidha katika operesheni hiyo jumla ya kilo 20 za mirungi na watuhumiwa husika 3 walikamatwa na kufikishwa polisi na jumla ya kilo 81 za bangi na watuhumiwa 11 walikamatwa. Makunga ameeleza kuwa operesheni kabambe itaanza katika wiki inayoanzia Jumatatu ijayo baada ya kumalizika kwa shughuli za sikukuu za mwishoni mwa mwaka za Krismasi na mwaka mpya.

WILAYA YA HAI YAANZA OPERESHENI YA KUPAMBANA NA ULEVI WA KUPINDUKIA

Posted by Arusha by day and by night On 06:26 No comments

Eneo maarufu kwa utengenezaji wa pombe haramu ya Gongo ndani ya tindiga la Boloti,wilayani Hai,baada ya watengezaji wa pombe hiyo kutelekeza mitambo yao

Eneo ardhi oevu linalotumiwa kama maficho ya watengeneza pombe aina ya gongo wilayani Hai
Eneo la mji mdogo wa Hai maarufu kama Bomang'ombe ambalo hivi sasa linapanuka kwa kasi

Majengo makubwa na ya kisasa ynayojengwa kwa kasi katika mji wa Hai


KUANZA KWA MKAKATI WA KUPAMBANA NA UNYWAJI WA POMBE SAA ZA KAZI PAMOJA NA UUZAJI NA UTUMIAJI WA  POMBE KINYUME NA MASHARTI YA LESENI ZA VILEO WILAYANI HAI

Zoezi la  kutekeleza azimio la Kamati ya ushauri ya Mkoa(RCC) kuhusiana na kilio cha muda mrefu cha jamii katika mkoa wa Kilimanjaro kwa  kuathirika kwa kukithiri kwa unywaji wa pombe wa kupita kiasi ambao umesababisha hata nguvu kazi kubwa hususani ya vijana kuathirika lilianza wilayani Hai Disemba 30,2014.

Zoezi hilo lilitanguliwa na utekelezaji wa agizo la  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Leonidas Gama la kusambazwa katika maeneo yote kwa Waraka namba moja wa mwaka 2014 wa mkuu wa mkoa, ambao ulifafanua lengo la serikali kufanya operesheni ya kudhibiti ulevi wa kupindukia mkoani Kilimanjaro.

Waraka huo uliogiza mamlaka zote za usalama na uongozi wa serikali kuanza rasmi operesheni maalumu ya kudhibiti matumizi ya unywaji wa pombe unaokiuka sheria kwa kuanzia Disemba 15 ulisomwa katika nyumba zote za ibada,kwenye mikosanyiko na kusambazwa kwa Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali(NGO’s) katika mkoa wa Kilimanjaro kwa muda wa mwezi mzima Kuanzia Novemba 15,2014

Katika utekelezaji wa waraka huo,wilaya ya hai ilifanya mambo yafuatayo;
1.      Kuandaa mkakati wa kutekeleza agizo hilo ambapo taratibu za kuunda kikosi kazi chenye askari mgambo sita,wawili wakiwa waajiriwa wa halmashauri ya wilaya pamoja na askari polisi mmoja mwenye silaha umeshakamilika na wataapishwa na hakimu mfawidhi mapema wiki ijayo.Kikosi hiki kitafanya kazi hii kwa kipindi cha miezi sita mfululizo kabla ya kufanyika kwa tathimini ya zoezi zima.

Kadhalika  kitapambana na waaribifu wa mazingira,uzuiaji wa kuingiza mifugo katika mji mdogo wa Hai na uingizaji wa mifugo katika vyanzo vya maji na Chemichemi pamoja na kuendesha kilimo katika kingo za mito na vyanzo vya maji.

2.      Kuandaa mpango kazi ambao tayari umekamilika na utahusisha kata zote pamoja na eneo la mji mdogo wa Hai.Mpango kazi huo kwa uchache umelenga katika mambo yafuatayo;

Ø  Kukagua Grocery zote na kuangalia kama zinafuata sheria za kuuza pombe

Ø  Kukagua baa zote ambazo zinafunguliwa na kufungwa nje ya muda ulioanishwa kwenye leseni

Ø  Maduka yanayouza pombe mbalimbali vikiwemo viroba kinyume na leseni zao za biashara

Ø  Msakako mkali wa maeneo yote yanayotengeneza pombe feki ikiwemp pombe haramu ya gongo pamoja na kuwabaini waliopo katika mtandao wa pombe hizo na maenep yate kunakosambazwa

Ø  Askari wa kikosi cha usalama barabarani kuanza kuwapima madereva wote wa vyombo vya moto kwa kutumia kifaa maalumu endapo watakuwa wametumia aina yoyote ya ulevi.

Ø  Vijiji kutunga sheria ndogo ndogo kudhibiti matumizi yasiyokuwa sahihi ya baadhi ya pombe ambazo zinaharibu ustawi wa jamii husika kama sheria inavyowaruhusu

3.      Msako mkali ulianza tarehe 30/12/2014 katika maeneo yote ya wilaya.Katika msako huo wakuu wa idara wote pamoja na maofisa wengine walishiriki ambapo walijigawa katika makundi sita ili kusambaa katika wilaya nzima kwa wakati mmoja.makundi yote sita yalifuatana na askari wawili wawili wenye silaha kwa ajili ya ulinzi wakati wa zoezi hilo.

Mkuu wa wilaya ya Hai, Mheshimiwa Novatus Makunga na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Hai,Bwana Melkizedeck Humbe walikuwa wasimamizi wa zoezi zima

MATOKEO YA MSAKO HUO HADI KUFIKIA TAREHE 31 DISEMBA 2014 NI KAMA UFUATAVYO;

S/N
AINA YA BIASHARA
WENYE LESENI ZA BIDHAA ZA KAWAIDA LAKINI WANAUZA POMBE
WENYE LESENI LAKINI WANAUZA POMBE KINYUME NA MUDA WA KISHERIA
HAWANA LESENI WAKIUZA BIDHAA ZA KAWAIDA PAMOJA NA POMBE
HATUA ZILIZOCHUKULIWA
1
Maduka ya Kawaida
21

37
Wote wamepigwa faini ya Tshs 50,000/= kwa kila mmoja na kupewa onyo
2
Baa za pombe za viwandani(kigeni)

4
3
Wote wametozwa faini ya Tshs 50,000/= kwa kila mmoja na kupewa onyo kali
3
Baa za pombe za kienyeji

6

Wote wametozwa faini ya Tshs 50,000/= kwa kila mmoja na kupewa onyo kali
4.
Glosary
9 (Kufanya biashara ya baa badala ya Glosary)

17


Jumla
30
10
57


Mambo yaliyojitokeza katika zoezi hilo

1.      Wafanyabiashara wengi wanauza bidhaa za kawaida pamoja na pombe kinyumbe na masharti ya leseni zao

2.      Wapo wafanyabiashara wengi zaidi wanaofanya biashara zao bila ya kuwa na leseni wakati huo huo wanauza bidhaa za kawaida kwa kuchanganya na pombe.Hali hii imeipotezea mapato mengi halmashauri ya wilaya.

3.      Wafanyabiashara wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu kuendesha biashara kwa kuzingatia masharti ya leseni

4.      Jamii bado haina uelewa wa kuwepo kwa sheria inayosimamia muda maalumu wa kuanza  kuuza pombe na muda wa mwisho wa kuuza pombe ambao unatofautiana katika maeneo ya mijini na vijijini