SHULE YA KIINGEREZA YA JAMII YA WAMAASAI WILAYANI HAI YAPIGA MAENDELEO MAKUBWA

Posted by Arusha by day and by night On 03:40 1 comment

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akijadili jambo na mfadhili wa shule ya O'Brien ya Hai,Bibi Kellie O'Brien(katikati) na kulia ni diwani wa kata ya kia,Sinyoki Ole Nairuko
 Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga na Bibi Kellie O'Brien wakimkabidhi zawadi mke wa Leiyo ambapo familia hiyo ni miongoni mwa familia zilizotoa eneo la ujenzi wa shule hiyo
 Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga na mfadhili wa shule ya O'Brien Bibi Kellie O'Brien wakimkabidhi zawadi mke wa Julius Zakayo Mollel ambapo familia hiyo ni miongoni mwa familia mbili zilizotoa eneo la ujenzi wa shule hiyo bure.
Sehemu ya akinamama wa Kimaasai waliohudhuria shule ya siku ya shule ya The O'Brien School for the Maasai

 Wazee wa jamii ya Kimaasai wakishuhudia sherehe za siku maalumu ya The O'Brien School for the Maasai
Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akihutubia wazazi,wanafunzi na wageni waalikwa katika siku ya shule ya The O'Brien School for the Maasai.
 Sehemu ya wageni kutoka nchini Marekani waliohudhuria sherehe za siku ya shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza ya O'Brien ya Hai
 Diwani wa kata ya Kia,Sinyoki Ole Nairuki akiwatambulisha wageni mbalimbali katika sherehe za siku ya shule ya O'Brien
 Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akizungumza na mfadhili wa shule ya O,Brien Bibi Kellie O'Brien
 Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga na mfadhili Bibi Kellie O.Brien wakishuhudia shughuli mbalimbali za siku ya shule ya msingi ya O'Brien
 Wanafunzi wa shule ya O'Brien wakitoa burudani
Buruduni mbalimbali za ngomba za asili zikiendelea

Morani wakitoa burudani      
Na Richard Mwangulube,Hai

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga amewaonya baadhi ya wazazi wa jamii ya wafugaji wa Kimaasai katika vijiji vya kata ya Kia wanaowakatisha watoto wao masomo muda uliotolewa kwa ajili ya kuwarejesha shule umemamilizika na hivyo kitakachofuata sasa ni kuanza kuwakamata na kuwasikisha katika vyombo vya sheria.

Mkuu huyo wa wilaya alitoa kauli hiyo wakati wa sherehe ya siku ya shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza ya jamii ya Wamaasai ya  O'Brien iliyopo katika kijiji cha Sanya Stesheni wilayan humo.

Makunga ameeleza kuwa uamuzi huo walikubaliana kwa pamoja na viongozi wa vijiji vyote vitatu vya kata hiyo ambavyo ni Sanya Stesheni,Tindigani na Mtakuja na baadaye waliweza kufanya mikutano katika vijiji hivyo kuwaeleza wananchi hatua ambazo sitachukuliwa kwa wazazi wa aina hiyo.

Amesema kuwa tatizo limekuwa sugu zaidi katika kijiji cha Tindigani ambalo baada ya mikutano hiyo zaidi ya watoto robo tatu wamesharudi shule ya msingi ya kijiji hicho na kwa upande wa waliofaulu na kwenda sekondari ya Kia tayari wameshapiga ripoti.

Hata hivyo Makunga ameeleza bado kuna wazazi ambao ni sugu kwa makusudi hawataki kupeleka watoto shule na wengine wamekuwa wakitumia mbinu ya kuwazuia kuwapeleka shule watoto katika baadhi ya siku na kuwarudisha baada ya muda na hivyo kushindwa kufuatilia masomo kwa mtiririko unaotakiwa.

Amewataka wazee wa kimila maarufu kama Malwaigwanan kuacha kutuma ujumbe katika ofisi za wilaya pale serikali kwa kushirikiana na viongozi wa serikali vijijini na katika kata watakapoanza kuchukua hatua.

Aidha kwa upande mwingine ameipongeza shule ya msingi ya mchepuo wa Kiingereza ya O'Brien kwa maendeleo makubwa iliyofikia ambapo vijana wa jamii hiyo ya Kimaasai wameanza kuonyesha mafanikio makubwa ya kimasomo na wamekuwa wakisoma kwa bidii.

Makunga aliahidi serikali kuendelea kutoa ushirikiano wote unaotakiwa kwa mfadhili wa shule hiyo,Bibi Kellie O'Brien ambaye mwaka jana alianzisha upandaji wa Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangia shule hiyo na kufanikiwa kukusanya dola za Marekani 38,000/=

Kwa upande wake mfadhili wa shule ya The O'Brien School for the Maasai,Raia wa Marekani Bibi Kellie O'Brien amewataka jamii hiyo kuendelea kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha watoto wanahudhuria kila siku katika masomo ili malengo la kuikomboa jamii hiyo yaweze kutimia

1 comments:

This is a great job in our District, lets hold these supporters for what they did and continuing to do. Big Up.

Post a Comment