JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI
YA RAIS
SEKRETARIETI
YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb.
Na EA.7/96/01/G/24 27 Juni, 2014
TANGAZO
LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi
wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma
Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu
29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo
hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa
jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi
zinazotokea katika Utumishi wa Umma
kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika
Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
Watanzania wenye sifa na uwezo wa
kujaza nafasi 877 za kazi kwa ajili ya Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Katibu
Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu
Tawala Mkoa wa Arusha, Katibu Tawala Mkoa wa
Shinyanga na Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
NB: MASHARITI YA
JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa
Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti
cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni
watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti
na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao
na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa
iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili
kutasababisha maombi
ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo
binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika
pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti
vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita
kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho
hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa
uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional
certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni
iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Testmonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati matokeo za
kidato cha nne na
sita (FORM
IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma
nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na
Mamlaka husika (TCU na NECTA).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika
Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu
Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni
waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko
katika utumishi wa
umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo
yaliyo katika Waraka
Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa
za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za
maombi ni tarehe 11 Julai, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua
kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
xiv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa
Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
AU Secretary,
Sekretariati
ya Ajira katika Public Service Recruitment
Utumishi
wa Umma, Secretariat,
SLP.63100,
P.O.Box 63100
Dar es
Salaam. Dar es Salaam.
1.0 MHANDISI KILIMO
DARAJA LA II (AGRO – ENGINEERS) – NAFASI 17
1.1 MAJUKUMU YA KAZI.
· Kuandaa program za
mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo,
· Kushiriki katika
kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana,
· Kushiriki kutengeneza
michoro/ramani za umwagiliaji,
· Kushiriki katika
ujenzi wa miradi ya umwagiliaji,
· Kushirikiana na
mafundi sanifu kuwafunindisha wakulima uendeshaji wa skimu
za umwagiliaji,
· Kukusanya takwimu za
miradi ya umwagiliaji,
· Kushiriki kuratibu na
kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji
pamoja na matumizi ya maji,
· Kuandaa
mafunzo/maonyesho ya matumizi ya za za kilimo,
· Kufuatilia program za
mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na
wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta,
· Kuwafundisha wakulima
ujenzi wa vihengo bora na
· Kushughulikia ubora
wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji
ipasavyo.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
shahada ya kwanza (Bachelor Degree) ya uhandisi yenye
mwelekeo mkubwa katika fani ya Kilimo cha umwagiliaji na cha zana kutoka
Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.
1.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia
viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS E Kwa
mwezi.
2.0 AFISA KILIMO DARAJA
LA II (AGRO – OFFICERS) – NAFASI 14
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa, Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro,
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya
Wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Mtendaji
Halamashauri ya Wilaya ya Liwale,
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya
Wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Iramba,
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya
ya Sumbawanga.
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuthibiti visumbufu
vya mazao na mimea,
· Kukusanya takwimu za
bei za mazao kila wiki na kila mwezi,
· Kukusanya takwimu za
upatikanaji wa mazao katika masoko kila wiki/kila mwezi,
· Kuendesha mafunzo ya
wataalam wa kilimo,
· Kufanya ukaguzi wa
ubora na matumizi ya pembejeo na zana,
· Ufuatiliaji wa
mwenendo wa soko la mazao ya biashara,
· Kuendesha mafunzo juu
ya hifadhi bora ya udongo na maji,
· Kutoa habari juu ya
teknolojia mpya kwa wadau,
· Kuandaa/kuandika
taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao,
· Kusimamia/kuendeleza
taaluma ya uzalishaji mboga, matunda, maua na mazao
mengine,
· Kusimamia/kuendeleza
uzalishaji wa mbegu bora,
· Kuandaa, kutayarisha
kufunga na kusambaza mbegu bora,
· Kufanya majaribio ya
magonjwa kwenye mbegu,
· Kufanya ukaguzi wa
mbegu mpya kwa kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla
ya kupitishwa,
· Kuendesha mafunzo ya
kuzalisha mboga, matunda, maua na viungo,
· Kuhamasisha
uzalishaji wa mazao ya bustani,
· Kufanya utafiti mdogo
mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya
kilimo cha umwagiliaji,
· Kufanya utafiti wa
udongo,
· Kuhamasisha
uanzishaji wa vikundi vya wakulima/wamwagiliaji,
· Kuzalisha mbegu za
msingi baada ya kuzalishwa na watafiti,
· Kuendesha/kusimamaia
vishamba vya majaribio vya mbegu na uchunguzi
maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
shahada ya kwanza (bachelor degree) ya kilimo au shahada ya
sayansi waliojiimarisha katika mchepuo
wa kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo
Sokoine au Vyuo vingine
vinavyotambuliwa na Serikali.
2.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia
viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D Kwa
mwezi.
3.0 MKUFUNZI KILIMO
DARAJA LA II (AQUACULTURE) – NAFASI 3
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na
Uvuvi.
3.1 KAZI NA MAJUKUMU
· Kusoma na kuelewa
vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.
· Kuandaa mtiririko na
mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa
upande wa nadharia na vitendo.
· Kufundisha kozi za
Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
· Kuandaana kufundisha
kozi za Wakulima.
· Kuandaa na kupanga
somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa
kujifunza.
· Kupima maendeleo ya
wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote
kinachohusika na kutunza alama zao.
· Kupima maendeleo ya
wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa
Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).
· Kutekeleza shughuli
nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa
kazi.
3.2 SIFA ZA KUINGILIA
MOJA KWA MOJA
· Kuajiriwa wenye
Shahada ya kwanza ya AQUACULTURE kutoka Chuo Kikuu
cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali,
waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology).
3.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali
yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
4.0 AFISA KILIMO MSAIDIZI
DARAJA LA II (AGRICULTURAL FIELD OFFICERS)
– NAFASI 131
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Mamlaka za
Serikali za Mitaa.
4.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kushirikiana na
watafiti kuendesha vishamba vya majaribio,
· Kukusanya/kuhifadhi
takwimu za majaribio,
· Kuwafundisha wakulima
mbinu za kilimo bora,
· Kuwafikishia wakulima
matokeo ya utafiti,
· Kuwafundisha wakulima
mbinu bora za kilimo, matumizi ya mbolea na madawa,
pembejeo za kilimo,
· Kukusanya na kutunza
takwimu za mazao na bei kwa wiki mwezi, robo na
mwaka ngazi ya halmashauri,
· Kukusanya takwimu za
mvua,
· Kushiriki katika
savei za kilimo,
· Kushirikiana na
vikundi vya wakulima kuhusu matatizo na teknolojia sahihi za
kutumia,
· Kupanga mipango ya
uzalishaji,
· Kupima uotaji wa
mbegu na kusimamia taratibu za ukaguzi,
· Kuwatambua
wasambazaji wa pembejeo,
· Kutoa mafunzo ya
lishe kwa wakulima,
· Kufanya vipimo vya
ubora, unyevunyevu na uotaji wa mbegu,
· Kudhibiti visumbufu
vya mazao na mimea,
· Kusimamia shughuli za
kila siku za majaribio ya kilimo,
· Kuwaelimisha wakulima
juu ya matumizi bora ya udongo na maji,
· Kutoa ushauri wa
kilimo mseto,
· Kuandaa sheria ndogo
za hifadhi ya mazingira na
· Kutoa taaluma ya
uzalishaji wa mboga, matunda, maua na viungo.
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa
Kidato cha Sita (VI) wenye stashahada (Diploma) ya
kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
4.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia
viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B Kwa
mwezi.
4.4 DAKTARI WA MIFUGO
DARAJA LA II (VETERINARY OFFICERS) – NAFASI 14
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga,
Mkurugenzi wa Jiji Halmashauri ya Jiji la Tanga,
Mkurugenzi wa Mji Halmashauri ya
Wilaya ya Korogwe, Katibu Tawala Mkoa wa
Dodoma, Katibu Tawala Mkoa wa
Kilimanjaro, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya
Wilaya ya Nyangw’ale, Katibu Tawala
Mkoa wa Dar es Salaam, Mkurugenzi
Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya
Ileje, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya
Wilaya ya Sikonge
.
4.5 MAJUKUMU YA KAZI
· Kutoa huduma za afya
ya mifugo
· Kufanya uchunguzi wa
magonjwa ya mifugo katika eneo au sehemu alipo.
· Kutayarisha na
kusimamia mipango ya kuzuia, kudhibiti na kutokomeza
magonjwa ya mifugo katika eneo lake.
· Kushiriki katika
uchunguzi wa magonjwa ya wanyama pori katika eneo lake.
4.6 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
Shahada ya kwanza (bachelor degree) ya Tiba ya Mifugo
kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa
na Serikali na wawe wamesajiliwa na
Bodi ya Madaktari wa Mifugo nchini.
4.7 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali TGS E kwa mwezi.
5.0 DAKTARI UTAFITI
MIFUGO DARAJA LA II (VETERINARY RESEARCH OFFICER II)
– NAFASI 7
Nafasi hizi ni Kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya
Wilaya ya Songea.
5.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kujifunza na kumudu
mbinu na taratibu za utafiti wa afya na maradhi ya mifugo
· Kuweka kumbukumbu za
utafiti
· Kusaidia kuendesha
semina na maonyesho ya ufugaji bora.
· Kuandaa mapendekezo
ya utafiti (“research proposal”) kwa kushirikiana na
Daktari Utafiti Mifugo anayemsimamia.
· Kufanya utafiti chini
ya usimamizi wa Daktari Utafiti Mwandamizi
· Kukusanya na
kuchambua takwimu za utafiti unaoendelea.
· Kuchapisha taarifa na
makala za utafiti
· Kuendesha semina na
maonyesho ya ufugaji bora.
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
Shahada ya kwanza (bachelor degree) katika fani ya Sayansi
ya Tiba ya Mifugo (“Veterinary
Science) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo au chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali. Wawe wamesajiliwa na
Bodi ya Madaktari wa Mifugo nchini.
5.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali TGS E kwa mwezi.
6.0 DAKTARI MIFUGO
MKUFUNZI DARAJA LA II (VETERINARY TUTOR II) – NAFASI 1
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kutafsiri mihutasari
ya mafunzo kwenye masomo
· Kuandaa mtiririko wa
kila somo (lesson plan) kwa upande wa nadharia na
vitendo
· Kufundisha kozi za
stashahada na astashahada kwa upande wa nadharia na
vitendo.
· Kuandaa na kupanga
somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa
kujifunza
· Kupima maendeleo ya
wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote
kinachohusika na kutunza alama zao.
· Kupima maendeleo ya
wanachuo kwa kushirikiana na madaktari /maofisa mifugo
wa wilaya, wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practicals).
· Kufanya kazi nyingine
zozote kadri atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.
6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Tiba ya Mifugo kutoka Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au chuo
kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Wawe wamesajiliwa na Bodi ya Madaktari
Tanzania.
6.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali TGS E kwa mwezi
7.0 MKUFUNZI MIFUGO
DARAJA II (ANIMAL SCIENCE) – NAFASI 3
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kutafsiri mihutasari
ya mafunzo kwenye masomo.
· Kuandaa mtiririko wa
kila somo (Lesson Plan) kwa upande wa nadharia na
vitendo.
· Kufundisha kozi za
stashahada na astashahada kwa upande wa nadharia na
vitendo.
· Kuandaa na kupanga
somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa
kujifunza.
· Kupima maendeleo ya
wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote
kinachohusika na kutunza alama zao.
· Kupima maendelo ya
wanachuo kwa kushirikiana na maofisa mifugo wa wilaya,
viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo.
· Kufanya kazinyingine
zozote za fani yake atakavyopangiwa na mkuu wake wa
kazi.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
shahada ya kwanza (bachelor degree) ya Sayansi ya Mifugo
kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo au chuo kingine kinachotambuliwa na
Serikali.
7.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali TGS D kwa mwezi.
8.0 AFISA MIFUGO DARAJA
LA II (LIVE STOCK OFFICER II) – NAFASI 5
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,
Msajili Bodi ya Nyama Tanzania,
Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Wilaya ya
Nkasi, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri
ya Wilaya ya Sumbawanga, Mkurugenzi
Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya
Sikonge.
8.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atabuni mipango ya
uzalishaji mifugo wilayani.
· Ataratibu uzalishaji
wa mifugo katika mashamba makubwa ya mifugo.
· Atasaidia kuratibu
mipango ya ugani kuhusiana na uzalishaji wa mifugo wilayani.
· Ataratibu na
kuendesha mafunzo ya ufugaji bora, usindikaji wa mazao ya mifugo
kwa wataam wa mifugo na wafugaji.
· Atafanya mapitio na
marekebisho ya miundo ya masoko ya mifugo wilayani
kwake na mkoani.
· Atabuni, kuanzisha na
kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo wilayani.
· Atafanya soroveya ya
rasilimali (resource survey) kama vile mifugo, vyakula vya
mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la kazi.
· Ataendesha mafunzo
kwa Mawakala, wauzaji na wataalam juu ya njia salama
katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo.
· Atatafiti maeneo
mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali
· Atafanya utafiti juu
ya uharibifu wa mazingira katika wilaya.
· Atashiriki katika
shughuli za kudhibiti milipuko ya wanyama/viumbe waharibifu wa
malisho.
· Ataandaa taarifa ya
jumla juu ya maendeleo ya mifugo.
· Atafuatilia, kuweka,
kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo.
· Atafanya kazi
nyingine zinazohusiana na fani yake kama atakavyoelekezwa na
mkuu wake wa kazi.
8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
shahada ya kwanza (bachelor degree) ya sayansi ya Mifugo
(Animal Science) kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali au sifa
inayolingana nayo.
8.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi
9.0 AFISA UTAFITI MIFUGO
DARAJA LA II (LIVESTOCK RESEARCH OFFICER II) –
NAFASI 8
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
9.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kujifunza kumudu
mbinu na taratibu za utafiti wa mifugo/ndorobo
· Kufanya utafiti chini
ya usimamizi wa Afisa Utafiti Mwandamizi.
· Kuandika na Kuweka
kumbukumbu za utafiti.
· Kusaidia kuendesha
semina na maonyesho ya ufugaji bora.
· Kuandaa mapendekezo
ya utafiti (Research Proposals) kwa kushirikiana na
Afisa Utafiti Mifugo anayesimamia.
· Kufanya kazi zozote
kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.
9.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
Shahada ya kwanza (bachelor degree) ya Sayansi ya Mifugo
kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine
kinachotambuliwa
na Serikali.
9.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.
10.0 AFISA UTUMISHI DARAJA
LA II (HUMAN RESOURCES OFFICER GRADE II)
– NAFASI 101
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara,
Mikoa na Halmashauri za Wilaya.
10.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kutunza Kumbukumbu
sahihi za watumishi wote katika Wizara, Mikoa, Wilaya na
Idara zinazojitegemea kulingana na
mahali alipo.
· Kutafsiri na
kushughulikia utekelezaji wa miundo ya utumishi.
· Kutafiti, kuchanganua
na kukadiria idadi ya watumishi wanaohitaji mafunzo.
· Kuandaa na kupanga
mipango ya mafunzo ya muda mfupi na mrefu.
· Kukadiria na kupanga
mahitaji ya vifaa vya mafunzo kwa kushirikiana na vyuo
vilivyopo chini ya sekta zinazohusika.
· Kukusanya, kuchambua
na kupanga takwimu na kumbukumbu zote zinazohusu
mipango ya watumishi.
10.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
Shahada ya kwanza ya Sayansi Jamii au Sanaa kutoka katika
Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali ambao wamejiimarisha (major)
katika
mojawapo ya fani zifuatazo:-
· Menejimenti ya
Raslimali Watu (Human Resources Management).
· Elimu ya Jamii
(Sociologly).
· Utawala na Uongozi
(Public Administration).
· Mipango ya Watumishi
(Manpower Planning).
· Awe na ujuzi wa
kutumia kompyuta
10.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
11.0 AFISA ARDHI MSAIDIZI – NAFASI 1
Nafasi hii ni kwa ajili ya Mkurugenzi
Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Iringa.
11.1 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa
Kidato cha Nne au Kidato cha Sita, waliofuzu mafunzo ya
miaka miwili ya Umiliki Ardhi na Uthamini kutoka Vyuo vya Ardhi au Vyuo
Vikuu
vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
11.2 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS C Tsh: 201,870/= na
kuendelea hadi Tsh: 250,930/= kwa mwezi.
11.3 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuingiza kumbukumbu
katika kompyuta
· Kutoa ushauri kwa
wateja.
· Kupokea, kukagua na
kusambaza majalada kwa maafisa kwa utekelezaji.
· Kusaidia Maafisa
Ardhi katika ukaguzi na kuchukua kumbukumbu, picha taarifa,
vipimo vya majumba na michoro.
· Kujumuisha na kuandaa
taarifa za ukaguzi.
· Kuandaa rasimu za
Hati na uingizaji wa plani ya Hati (deed plan)
· Kuagiza plani za Hati
(Deed Plan)
12.0 DEREVA DARAJA LA II
(DRIVER II) – NAFASI 3
Nafasi hizi ni kwa ajili yaMkurugenzi
Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa.
12.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuendesha magari ya
abiria, magari madogo na malori
· Kuhakikisha gari na
vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya
uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji
matengenezo,
· Kufanya matengenezo
madogo madogo katika gari,
· Kutunza na kuandika
daftari la safari “Log-book” kwa safari zote.
12.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Cheti
cha Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C”
ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa
kuendesha magari kwa muda usiopungua
miaka mitatu bila kusababisha ajali na
wenye Cheti cha Majaribio ya ufundi
Daraja la II (Trade test II).
12.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali yaani TGOS.A kwa mwezi.
13.0 AFISA UTALII DARAJA
LA II – NAFASI 1
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu
Tawala Mkoa wa Arusha.
13.1 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
Shahada/stashahada ya juu katika fani ya Utalii kutoka katika
vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
13.2 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS D
13.3 MAJUKUMU YA KAZI
· Kukusanya taarifa za
maeneo mapya yenye vivutio vya utalii kwa kushirikiana na
wadau wote.
· Kutoa Leseni za
utalii kwa mahoteli na wakala wa utalii.
· Kukusanya na kuweka
takwimu za watalii na safari za kitalii.
· Kutafuta na kupanga
nafasi za masomo ya utalii ndani na nje ya nchi.
· Kujibu malalamiko
kutoka kwa watalii.
· Kutoa ushauri wa
kitaalam kwa wadau katika uendeshaji wa Biashara ya utalii.
· Kuandaa kaguzi
mbalimbali za Wakala wa utalii.
· Kuchambua miradi ya
wakala wa utalii na hoteli.
· Kukagua hoteli, loji
na migahawa.
· Kujibu na kufatilia
malalamiko yanayoletwa na watalii.
· Kutoa ushauri wa
kitaalam kwa wakala wa utalii.
· Kukusanya taarifa za
maeneo mapya yenye vivutio vya utalii kwa kushirikiana na
Washika dau wote.
· Kukusanya takwimu za
watalii kwenye sehemu/vituo nchini vya kuingilia/kutoa
wageni.
· Kutunza kumbukumbu za
vitabu/majalada ya Maktaba ya Utalii.
· Kutayarisha taarifa
ya kila mwezi ya takwimu za watalii waliongia nchini na
mapato yaliyopatikana.
· Kufanya tafiti ngo
“Survey” kwenye Hifadhi za Taifa na maeneo tengefu ili kupata
idadi kamili ya Hoteli au Loji zinazotoa huduma kwa watalii.
· Kufuatilia kwa karibu
na kushirikiana na VETA juu ya maendeleo ya vyuo
vinavyotoa mafunzo ya utalii nchini.
· Kuratibu miradi yote
inayohusiana na utoaji wa mafunzo ya utalii.
· Kutayarisha ripoti za
mwezi, robo mwaka, na za mwaka mzima.
· Kufuatilia kwa karibu
maendeleo ya Sekta kwa kufanya suervey.
· Kuitisha mikutano ya
Tourism Facilitation Committee.
· Kutayarisha ripoti na
kusambaza kwa wajumbe na kukufuatilia utekelezaji wa
maazimio.
· Kupitia miongozo
inayohusu “Tourism Facilitation Committee”.
· Kuratibu shughuli za
kubuni vivutio vya utalii na mienendo mipya ya kuendeleza
utalii.
· Kutayarisha kuhakiki
vivutio vya utalii nchini.
· Kuitisha
mikutano/semina za uhamasishaji kuhusu uendelezaji utalii.
· Kushiriki katika
kupitia ripoti za EIA kuhusu miradi ya utalii.
· Kushirikiana na
Mashirika/taasisi mbalimali za mazingira katika shughuli
zihusuzo utalii na mazingira.
· Kukusanya rasilimali
za uendeshaji katika vyanzo vya ndani na nje.
14.0 AFISA USHIRIKA DARAJA
LA II (COOPERATIVE OFFICER GRADE II) –
NAFASI 1
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu
Tawala Mkoa wa Shinyanga.
14.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kukagua vyama vya
Ushirika vya Msingi vinavyoendesha miradi ya pamoja (
Jointy Venture )
· Kuhamasisha
uanzishaji wa vyama vya Ushirika vya Msingi.
· Kukusanya na
kuchambua takwimu zinazohusu Masoko katika Mkoa.
· Kutoa ushauri juu ya
uendeshaji wa Vyama vya Ushirika vya Msingi
· Kuratibu/kushiriki
katika Elimu ya Ushirika Shirikishi katika vyama vya ushirika
vya Msingi.
14.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
Shahada ya kwanza au Stashahada ya Juu (Advanced
Diploma) katika fani ya Ushirika
(Cooperative management and accounting)
kutoka vyuo vinavyotambulika na
Serikali.
14.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
15.0 AFISA SERIKALI ZA
MITAA II (LOCAL GOVERNMENT OFFICER GRADE II) –
NAFASI 1
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Tawala Mkoa wa Shinyanga.
15.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kutoa ushauri katika
utekelezaji wa Sheria za Serikali za Mitaa
· Kutoa ushauri juu ya
uanzishaji na uendeshaji wa mamlaka mpya Serikali za
Mitaa
· Kutoa ushauri juu ya
makadirio ya mapato ya mapato na matumizi ya Seriakali
za Mitaa
· Kusimamia na kushauri
juu ya matumizi bora ya matumizi bora ya fedha
Seriakali za Mitaa
· Kutayarisha taarifa
za robo mwaka na mwaka zinazohusu mwenendo wa Serikali
za Mitaa
· Kufanya kazi nyingine
zitakazoagiwa na Watendaji, Wasimamizi wa masuala ya
Serikali za Mitaa
15.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
Shahada ya kwanza ya Sanaa (/Management &
Administration), Sheria (LLB) toka
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au chuo
chochote kinachotambuliwa na Serikali AU
· Kuajiriwa wenye
Stashahada ya juu katika fani ya Serikali za Mitaa au Utawala
(Local Government Administration or
Public Administration) toka Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.
15.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali
yaani ngazi ya Mshahara TGS D kwa
mwezi.
16.0 MHANDISI II UFUNDI
(MECHANICAL ENGINEER) – NAFASI 5
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
16.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya kazi chini ya
uangalizi wa Mhandisi aliyesajiliwa na bodi ya usajili wa
Wahandisi kama Professional Engineer
ili kupata uzofu unaotakiwa.
· Kufanya kazi kwa
vitendo katika fani ya Mekanika ili kumwezesha kupata sifa za
kutosha kusajiliwa na Bodi ya Usajili
wa Wahandisi.
· Kukusanya taarifa na
takwimu kuhusu magari na mitambo mbalimbali, bei za magari na
mitambo na vifaa vya umeme ndani na
nje ya nchi.
· Kupitia mapendekezo
ya miradi (project proposals) mbalimbali ya Ufundi .
16.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwawenye
Shahada/Stashahada ya juu ya Uhandisi (Mechanical Engineering)
kutoka vyuo vikuu vinavyotambulika na
Serikali.
16.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
17.0 MHANDISI II -
HAIDROJIOLOJIA (HYDROGEOLOGISTS) – NAFASI 4
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
17.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kukusanya takwimu,
kutafiti pamoja na kutayarisha taarifa za kihaidrojiolojia zenye
maelezo fasaha ya kitaalamu.
· Kujenga (installation)
na kukarabati vifaa vya utafiti wa maji chini ya ardhi na kukarabati
vituo vya kuratibu rasilimali za maji
chini ya ardhi.
· Kusimamia uchumbaji
wa visima vya maji na kuhakiki uwezo wa kisima kutoa maji
(pumping test)
· Kukusanya sampuli za
maji na udongo kwa ajili kufanya uchunguzi wa kimaabara
· Kutathimini
(monitoring) rasilimali za maji chini ya ardhi kwenye sehemu ya kidao cha
maji (sub –catchment).
17.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
shahada ya Jiolojia au Jiofizikia na Haidrojiolojia kutoka Vyuo Vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali.wawe na
ujuzi wa kutumia Kompyuta.
17.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
18.0 MHANDISI DARAJA LA II
(MAJI) – WATER RESOURCE ENGINEER –
NAFASI 50
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
18.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kushughulikia
upembuzi yakinifu, usanifu wa ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya
miundombinu midogo midogo ya
usambazaji maji na kushiriki shughuli za upembuzi
yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji
na matengenezo ya miundombinu mikubwa ya
ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa
mazingira.
· Kufanyia mapitio
taarifa za upembuzi yakinifu na sanifu za ujenzi wa miundombinu ya
miradi ya usambazaji maji na usafi wa
mazingira.
· Kufanyia ukaguzi wa
utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na utengenezaji wa
miundombinu ya uzalishaji na
usambazaji maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya
kupata ubora unaokusudiwa.
· Kushiriki katika kazi
ya kupendekeza miradi na kupitia mapendekezo ya miradi (project
proposal) ya usambazaji maji na usafi
wa mazingira.
· Kufanya uchunguzi
kuhusu uharibifu wa miundombinu au ajali zinazojitokeza wakati wa
utekelezaji wa miradi ya maji na usafi
wa mazingira.
· Kutayarisha bajeti ya
utekelezaji wa shughuli za sekta za maji.
· Kusimamia kuratibu na
kufuatilia utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo ya
miundombinu ya miradi ya maji na usafi
wa mazingira.
· Kukusanya na
kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za sekta ya
maji kwa ajili ya matumizi ya sekta na
kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya Wahandisi.
18.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
Shahada/Stashahada ya juu ya uhandisi wa Maji (Water Resource
Engineering) kutoka vyuo vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali.
18.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
19.0 MHANDISI DARAJA LA II
(MAJI) – WATER RESOURCE WITH GIS ENGINEER –
NAFASI 5
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
19.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kushughulikia
upembuzi yakinifu, usanifu wa ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya
miundombinu midogo midogo ya
usambazaji maji na kushiriki shughuli za upembuzi
yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji
na matengenezo ya miundombinu mikubwa ya
ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa
mazingira.
· Kufanyia mapitio
taarifa za upembuzi yakinifu na sanifu za ujenzi wa miundombinu ya
miradi ya usambazaji maji na usafi wa
mazingira.
· Kufanyia ukaguzi wa
utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na utengenezaji wa
miundombinu ya uzalishaji na
usambazaji maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya
kupata ubora unaokusudiwa.
· Kushiriki katika kazi
ya kupendekeza miradi na kupitia mapendekezo ya miradi (project
proposal) ya usambazaji maji na usafi
wa mazingira.
· Kufanya uchunguzi
kuhusu uharibifu wa miundombinu au ajali zinazojitokeza wakati wa
utekelezaji wa miradi ya maji na usafi
wa mazingira.
· Kutayarisha bajeti ya
utekelezaji wa shughuli za sekta za maji.
· Kusimamia kuratibu na
kufuatilia utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo ya
miundombinu ya miradi ya maji na usafi
wa mazingira.
· Kukusanya na
kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za sekta ya
maji kwa ajili ya matumizi ya sekta na
kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya Wahandisi.
19.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
Shahada/Stashahada ya juu ya uhandisi wa Maji (Water Resource with
GIS) kutoka vyuo vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali.
19.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
20.0 MHANDISI DARAJA LA II
(UMEME) – NAFASI 5
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
20.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya kazi chini ya
uangalizi wa Mhandisi aliyesajiliwa na bodi ya Usajili wa
Wahandisi kama “Proffesional
Engineers” ili kupata uzoefu unaotakiwa.
· Kufanya kazi za
vitendo katika fani zinazomhusu ili kumwezesha Mhandisi kupata sifa
za kutosha kusajiliwa na Bodi ya
Usajili wa Wahandisi.
· Kukusanya taarifa za
Magari na Mitambo mbalimbali, kuhusu vifaa vya Umeme ndani
na nje ya nchi.
· Kupitia mapendekezo
ya miradi (Project proposals.) mbalimbali za Ufundi na Umeme.
20.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
Shahada/Stashahada ya Juu ya Uhandisi kutoka Vyuo Vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali katika
mojwapo ya fani ya Umeme (Electrical
Engineering).
20.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
21.0 MHANDISI II MAZINGIRA
(ENVIRONMENTAL ENGINEER II) – NAFASI 5
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
21.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kutoa ushauri wa
namna ya kulinda mazingira kutokana na shughuli za Binadamu
kama Kilimo,uvuvi,ufugaji nk
· Kufanya Tathimini ya
Mazingira (Environmental Impact Assesment) kwa miradi
inayoanzishwa hasa ya Umwagiliaji na
Uwekezaji katika Kilimo
· Kutoa ushauri wa
namna ya kupunguza uharibifu wa Udongo utokanao na kemikali za
madawa ya Kilimo, Pembejeo za Kilimo
au Kemikali zingine za Viwandani zihusianazo
na kilimo.
· Kubuni vifaa na
mikakati ya kuhakikisha kuwa maji taka na uchafu utokanao na kemikali
zitokazo na Kilimo haziathiri
Mazingira.
· Kubuni mikakati
itakayohakikisha kuwa Binadamu anaishi katika mazingira yenye Afya
na Rafiki kimazingira.
21.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
Stashahada ya juu au Shahada ya Uhandisi Mazingira kutoka Vyuo
Vikuu au Taasisi nyingine
zinazotambuliwa na Serikali. Wawe na ujuzi wa kutumia
compyuta.
21.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
22.0 FUNDI SANIFU DARAJA
LA II – UFUNDI (TECHNICIAN GRADE II MECHANICS) –
NAFASI 25
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
22.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya ukaguzi wa ubora
wa magari ya Serikali na kurekebisha ipasavyo.
· Kufanya upimaji wa
Mitambo kufuatana na Maelekezo ya Mhandisi.
· Kufanya kazi za
kutengeneza mitambo na magari.
· Kufanya usanifu wa
miradi midogo midogo ya ufundi.
· Kusimamia jinsi ya
kufunga mashine mpya zinazowekwa kwenye karakana za ufundi.
22.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Waliohitimu kidato
cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali katika
moja ya fani za ufundi.
Au
· Waliohitimu kidato
cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya
Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali
katika mojawapo ya fani za ufundi,
Au
· Wenye Cheti cha
Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi
kinachotambuliwa na Serikali,
Au
· Wenye Stashahada ya
Kawaida katika fani za ufundi kutoka Chuo kinachotambuliwa na
Serikali.
22.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
23.0 FUNDI SANIFU DARAJA
LA II - UMEME (TECHNICIAN GRADE II ELECTRICAL) –
NAFASI 25
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
23.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya ukaguzi wa
ubora wa mitambo ya Serikali na kurekebisha ipasavyo.
· Kufanya upimaji wa
Mitambo na Umeme kufuatana na Maelekezo ya Mhandisi.
· Kufanya kazi za
kutengeneza mitambo na vifaa vya Umeme
· Kufanya usanifu wa
miradi midogo midogo ya umeme
· Kusimamia jinsi ya
kufunga mashine mpya zinazowekwa kwenye karakana za ufundi na
Umeme.
23.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Waliohitimu kidato
cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali katika
moja ya fani za ufundi umeme.
Au
· Waliohitimu kidato
cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya
Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali
katika mojawapo ya fani za ufundi umeme,
Au
· Wenye Cheti cha
Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi
kinachotambuliwa na Serikali,
Au
· Wenye Stashahada ya
Kawaida katika fani za ufundi umeme kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali.
19
23.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
24.0 FUNDI SANIFU – (WATER
WORKS TECHNICIAN) DARAJA II – NAFASI 124
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
24.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kumsaidia Fundi
Sanifu Daraja I katika kazi ili kuapata uzoefu wa;
· Kutafsiri ramani za
ujenzi wa miundombinu ya maji au ya ufungaji wa mitambo ya miradi
ya maji
· Kujenga miundombinu
ya aina mbalimbali au kufunga mitambo ya miradi ya maji na
usafi wa mazingira;
· Kufanya matengenezo
ya kawaida ya vipindi na ya kuzuia uharibifu wa miundo mbinu
kwa kufuata ratiba na inapohitajika
kwa dharura;
· Kusimamia ukusanyaji
na utunzaji wa takwimu za uendeshaji na matengenezo ya
miundo mbinu au mitambo ya miradi ya
maji;
· Kuwaongoza mafundi
sanifu wasaidzi kutekeleza kazi zao
· Kutoa taarifa za
utekelezaji wa miradi kwa Mhandisi
24.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Awe na Cheti cha
Stashahada ya Maji (Water Works Technician) toka Chuo cha Maji au
Chuo chochote kinachotambuliwa na
Serikali.
24.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
25.0 FUNDI SANIFU MAABARA
– (WATER LABORATORY TECHNICIAN) DARAJA II –
NAFASI 25
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
25.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kumsaidia Fundi
Sanifu Daraja I katika kazi ili kuapata uzoefu wa;
· Kutafsiri maelezo ya
matumizi ya madawa mbalimbali kwa kwa ajili ya kazi mbalimbali
za maabara
· Kusimamia uchukuaji
wa sampuli za maji na udongo kwa ajili ya upimaji
· Kufanya na kusimamia
matengenezo ya vifaa vya maabara ya kawaida na ya dharura
yanapohitajika;
· Kufanya upimaji wa maji
na udongo wa maeneo ya miradi na kuandaa maelekezo ya
matibabu yanayohitajika.
· Kusimamia ukusanyaji
wa takwimu za hali ya maji na udongo zinazohitajika kwenye
maeneo ya miradi
· Kuwaongoza mafundi
sanifu wasaidzi kutekeleza kazi zao
· Kutoa taarifa za hali
ya maji na udongo wa maeneo ya miradi kwa Mhandisi.
25.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Awe na Cheti cha
Stashahada ya Maji (Water Laboratory) toka Chuo cha Maji au Chuo
chochote kinachotambuliwa na Serikali.
25.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
26.0 FUNDI SANIFU DARAJA
LA II - MAJI - (TECHNICIAN GRADE II - WATER) –
NAFASI 1
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu
Wizara ya Maji.
26.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Ukusanyaji na
ukaguaji wa takwimu za maji
· Kutunza takwimu za
maji
· Kuingiza takwimu za
maji kwenye fomu Na: H: 12 tayari kwa kutumiwa kwenye
michoro
· Kuchora hydrograph za
maji
· Utengenezaji visima
vya rekoda, stendi za winchi, sinia za maji ‘cable way post”
n.k.
· Kufanya matengenezo
ya vifaa vyote vya kupimia maji na hali ya hewa
· Kuingiza takwimu
kwenye kompyuta
· Kufundisha wasoma
vipimo
26.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa Wahitimu wa
vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao
wana cheti cha ufundi ( FTC) au
Stashahada ya Rasilimali za Maji na wenye
ujuzi wa kutumia kompyuta.
26.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
27.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI
(UFUNDI BOMBA) - (ASSISTANT WATER WORKS
TECHNICIAN PLUMBING)
– NAFASI 36
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
27.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya kazi kwa
kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
· Kufunga mitandao ya
bomba za aina mbalimbali ya miradi ya maji na usafi wa
mazingira;
· Kufanya usafi na
ukaguzi wa mitandao ya bomba ya miradi ya maji na usafi wa
mazingira kwa ajili ya kukidhi
uendeshaji nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
· Kuwezesha uzalishaji
na usambazaji wa maji na utoaji wa majitaka kwa kupitia
mitandao ya bomba za miradi ya maji na
usafi wa mazingira.
· Kufanya matengenezo
ya kawaida ya vipindi nay a kuzuia uharibifu wa mitandao ya
bomba kwa kufuata ratiba na
inapohitajika kwa dharura.
· Kunakili,
kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na
matengenezo ya mitandao ya bomba za
miradi ya maji na usafi wa mazingira;
· Kumsaidia Fundisanifu
kazi za kiufundi.
27.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa
kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo
chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III
(Plumbing).
27.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
28.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI
(UPIMAJI ARDHI) - (ASSISTANT WATER WORKS
TECHNICIAN GEOMETRIC)
– NAFASI 25
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
28.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya kazi kwa
kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aoyesajiliwa ili
aweze;
· Kushirikiana na
Wahandisi wa Maji na kuwaongoza walengwa katika kuchagua njia za
kupitisha bomba kwa ajili ya miradi ya
maji na usafi wa mazingira;
· Kupima hali ya
kijiografia ya maeneo ya inayokusudiwa kujengwa au yenye miradi ya
maji na usafi wa mazingira ili
kuwezesha usanifu wa miundo mbinu miradi;
· Kupima uwekaji wa
vifaa vya miundo mbinu kwenye ardhi wakati wa ujenzi wa miradi ya
maji na usafi wa mazingira;
· Kunakili na kutunza
taarifa za upimaji wa ardhi kwa ajili ya miundo mbinu ya miradi ya
maji na usafi wa mazingira kwa namna
inayokubalika kwa mchoraji wa ramani za
usanifu wa miradi kufanya kazi yake
kwa unadhifu;kuchora ramani za maeneo ya
miradi ya maji na usafi wa mazingira
kwa namna zote zinazokubalika kwa ajili ya
kuwezesha usanifu wa miundo mbinu ya
maji na usafi wa mazingira;
· Kumsaidia Fundi
Sanifu katika kazi za upimaji ardhi.
28.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa
kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo
chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III
(Water Works Technician Geometric).
28.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
29.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI
MITAMBO YA MAJI (PAMPU) – NAFASI 25
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
29.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atafanya kazi kwa
kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
· Kufunga pampu na
injini za aina mbalimbali za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
· Kufanya usafi na
ukaguzi wa pampu na injini za miradi ya maji na usafi wa mazingira
kwa ajili ya kukidhi uendeshaji
nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
· Kuhudumia uendeshaji
wa pampu na injini za miradi ya maji;
· Kufanya matengenezo
ya kawaida, ya vipindi na ya kuzuia uharibifu wa pampu na injini
kwa kufuata miongozo ya uendeshaji na
matengenezo na inapohitajika kwa dharura;
· Kunakiri,
kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na
matengenezo ya pampu na injini za
miradi ya maji;
· Kumsaidia Fundi
Sanifu katika kazi za kiufundi.
29.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa
kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo
chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III
(Mitambo Ya Maji (Pampu).
29.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
30.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI
MITAMBO YA MAJI (UMEME) – NAFASI 25
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
30.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya kazi kwa
kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
· Kufunga mfumo wa
umeme unaohitajika kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ya miradi
ya maji na usafi wa mazingira;
· Kufunga mota na vifaa
vingine vya umeme vya aina mbalimbali vya miradi ya maji na
usafi wa mazingira;
· Kufanya usafi na
ukaguzi wa mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine umeme vya
miradi ya maji na usafi wa mazingira
kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu wa pampu
na kuzuia uharibifu;
· Kuendesha mitambo
inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
· Kufanya matengenezo
ya kawaida, ya vipindi na ya kuzuia uharibifu kwenye mfumo wa
umeme, mota na vifaa vingine umeme kwa
kufuata miongozo ya uendeshaji, na
inapohitajika kwa dharura.
· Kunakili,
kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na
matengenezo ya mitambo inayotumia
umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
· Kumsaidia Fundi
Sanifu katika kazi za kiufundi.
30.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa
kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo
chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III
(Plants Technician Electrical).
30.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
31.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI
- (ASSISTANT TECHNICIAN WELDING) NAFASI 5
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji.
31.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya kazi kwa
kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
· Kufunga pampu na
injini za aina mbalimbali za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
· Kufanya usafi na
ukaguzi wa pampu na injini za miradi ya maji na usafi wa mazingira
kwa ajili ya kukidhi uendeshaji
nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
· Kuhudumia uendeshaji
wa pampu na injini za miradi ya maji;
· Kufanya matengenezo
ya kawaida, ya vipindi nay a kuzuia uharibifu wa pampu na injini
kwa kufuata miongozo ya uendeshaji na
matengenezo na inapohitajika kwa dharura;
· Kunakili,
kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na
matengenezo ya pampu na injini za
miradi ya maji;
· Kumsaidia Fundi
Sanifu katika kazi za kiufundi.
31.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa
kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo
chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III
katika fani ya Welding na fiter turner.
31.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi
za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
32.0 MHANDISI DARAJA LA II
- UJENZI (ENGINEER GRADE II – CIVIL) – NAFASI 125
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi na Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
32.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atafanya kazi chini
ya uangalizi wa Mhandisi aliyesajiliwa (Professional engineer)
na bodi ya usajili ya Wahandisi ili
kupata uzoefu unaotakiwa.
· Kufanya ukaguzi wa
Barabara, Madaraja na Majengo mbalimbali
· Kuchunguza vyanzo vya
ajali barabarani
· Kufuatilia utekezaji
wa Sheria, Kanuni za ujenzi wa Barabara na Majengo
· Kutayarisha bajeti ya
mwaka ya Ujenzi na matengenezo ya Barabara, Madaraja
na Majengo
· Kusimamia na kuratibu
kazi za Barabara, Madaraja na Majengo zinazotolewa na
makandarasi
32.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
Shahada/Stashahada ya Juu ya Uhandisi kutoka Vyuo Vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali katika
fani ya Uhandisi Ujenzi.
32.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
33.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI
( UJENZI – CIVIL TECHNICIAN ) – NAFASI 36
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Wizara ya Maji na Mkurugenzi
Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga.
33.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya kazi za
ujenzi wa kuta za nyumba na kupaka rangi na kufunga mabomba,
· Kuchonga vifaa vya
nyumba za serikali ikiwa ni pamoja na samani “furniture”,
· Kufanya kazi za
upimaji ( Survey ) wa barabara,majengo na mifereji kama
atakavyoelekezwa,
33.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa waliomaliza
kidato cha IV katika masomo ya Sayansi na kufuzu mafunzo ya
mwaka mmoja katika Fani ya Ufundi wa
Ujenzi (Civil Technician ) kutoka katika chuo
kinachotambuliwa na serikali,
Au
· Kuajiriwa waliomaliza
kidato cha IV wenye cheti cha Majaribio ya ufundi hatua ya II
(Civil Technician) kutoka chuo cha
ufundi katika mojawapo ya fani ya ufundi wa Ujenzi.
33.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya
Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
34.0 FUNDI SANIFU DARAJA
II – RAMANI (TECHNICIAN GRADE II - (MAPPING)
– (NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Mkurugenzi
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa
34.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kushughulikia
madaai/malalamiko ya hati za viwanja, kuweka na kutunza
kumbukumbu zake
· Kutunza kumbukumbu za
“cadastrals surveys” na mahesabu yake
· Kuandaa nakala za
“cadastral site plans”
· Kutunza miongozo ya
ramani (maping guides) na viwanja
34.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye
wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye cheti cha mafunzo ya
ufundi ya miaka miwili katika fani ya
Ramani (Mapping)
34.3 MSHAHARA
· . Kwa kuzingatia
Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
35.0 MPIGA CHAPA MSAIDIZI
(ASSISTANT PRINTER) - NAFASI 10
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu.
35.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kukunja karatasi
ngumu na kutengeneza ‘covers’ za vitabu, majarida, madaftari
katika mahitaji mbalimbali kwa
kugandisha, kuweka pamoja au kushona katika
hali mbalimbali za ubora.
· Kukarabati vitabu,
kumbukumbu mbalimbali au majarida kwa kuyawekea gamba
jipya, au kurudisha katika hali yake
ya mwanzo kutegemea na kifaa hicho
kilivyoharibika.
· Kupanga vifaa
vilivyotengenezwa katika makasha kwa vipimo vyake au katika
seti.
· Kuendesha mashine za
kukata karatasi/kupiga Chapa/Mashine za Composing,
kushona au kugandisha vitabu,
majarida, madaftari na vifaa vingine vinavyokuwa
vimetakiwa kwa mtindo na ubora wake.
· Kupanga karatasi
zitakazochapwa kwa hesabu ya kila kitabu, jarida, daftari na
vinginevyo kwa kushonwa au kugandishwa
pamoja.
35.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa
Kidato cha IV au VI katika masomo ya Sayansi, au Sanaa,
wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi
Daraja la I (Trade Test Grade I) katika
Lithography/Composing/Binding/Machine
Minding, au waliohitimu mafunzo ya
miaka miwili ya Kupiga Chapa.
35.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali
yaani ngazi ya Mshahara TGS.B kwa mwezi
X.M.
DAUDI
Katibu
Sekretarieti
ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
0 comments:
Post a Comment