MATOKEO YA CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA NCHI NZIMA DESEMBA 2014

Posted by bomang'ombe On 07:58 No comments

Na Augusta Njoji,Dar-es-Salaam 25th December 2014

Matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 14 na 21, mwaka huu, yalitangazwa jana yakionyesha kwamba vyama vya upinzani vimeng’ara zaidi kulinganisha na uchaguzi wa mwaka 2009.

Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini hapa wakati wa kutangaza matokeo hayo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kharist Luanda, alisema kwa mwaka huu ushiriki wa vyama vya siasa umekuwa mkubwa kutokana na vyama 15 kushiriki.


Aidha, Luanda alisema kuwa mwaka huu kulikuwapo na hamasa kwa wananchi katika uchaguzi huo ikilinganishwa na miaka iliyopita ambayo ulikuwa ukifanyika kienyeji na bila mvuto.


Luanda alisema licha ya vyama vya upinzani kupata viti vingi vya mitaa, vitongozi na vijiji ambavyo miaka iliyopita vilikuwa vinashikiliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama hicho tawala, kimeongoza.


Alisema katika nafasi ya wenyeviti wa vijiji,  CCM kimepata  9,378 (asilimia 79.81) wakati kwa vitongoji 48,447  (asilimia 79.83) na kwa mitaa  2,583 (asilimia 66.66.).


Kwa upande wa wajumbe serikali za vijiji na mitaa, CCM kimepata 100,436 (asilimia 80.24) na wajumbe wa viti maalum 66,147 (asilimia 82.13).

 
UKAWA
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi vimefuatia kwa kuzoa viti vingi ambavyo vilikuwa vinashikiliwa na CCM hadi baada ya uchaguzi wa mwaka 2009.


Chadema kimeshika nafasi ya pili kwa kupata wenyeviti wa vijiji 1,754 (asilimia 14.93), vitongoji 9,145 (asilimia 15.07) huku kikipata mitaa 980   (asilimia 25.29).

Katika nafasi za wajumbe serikali za vijiji na mitaa kimepata 18,527 (asilimia 14.80) na wajumbe viti maalum  10,471 (asilimia 13).


Kilichofuatia ni CUF ambacho kwa nafasi ya wenyeviti wa vijiji kimepata viti 516 (asilimia 4.39), wenyeviti wa vitongoji 2,561 (asilimia 4.22) na  wenyeviti wa mitaa 266 (asilimia 6.86).

Katika nafasi ya wajumbe serikali za vijiji na mitaa  kimepata 5,395 (asilimia 4.31) na viti maalum  kimepata wajumbe 2,676 (asilimia 3.32).

 
NCCR-Mageuzi katika nafasi ya wenyeviti wa vijiji kimepata 67 (asilimia 0.57), wenyeviti wa vitongoji 339 (asilimia 0.56) na wenyeviti wa mitaa 28  (asilimia 0.72).Chama hicho kwa wajumbe serikali za vijiji na mitaa kimepata 598 (asilimia 0.48) na viti maalum 455 (asilimia 0.56).


VYAMA VINGINE
Aidha, Luanda alivitaja vyama vingine kuwa ni TLP ambacho kwa wenyeviti wa vijiji kimepata viti 10 (asilimia 0.09), NLD wawili (asilimia 0.02), ACT wanane  (asilimia 0.07), UDP 14 (asilimia 0.12), NRA mmoja (asilimia 0.01) na kwamba vyama vilivyobaki havikupata uwakilishi.


Kwa upande wa wenyeviti wa vitongoji  TLP kimepata 55 (asilimia 0.09), NLD wawili (asilimia 0.00), ACT 72 (asilimia 0.12), UDP 54  (asilimia 0.09), APPT Maendeleo watatu (asilimia 0.00), NRA watatu (asilimia 0.00) na vyama vingine havikupata uwakilishi.


Luanda alisema kwa wenyeviti wa mitaa TLP kimepata mmoja (asilimia 0.03), ACT 12 (asilimia 0.31), UDP watatu (asilimia 0.08), NRA mmoja na UMD mmoja (asilimia 0.03).

Katika nafasi ya wajumbe serikali za vijiji TLP kimepata 62 (asilimia 0.05), NLD watatu (asilimia 0.00), ACT 106 (asilimia 0.08), APPT Maendeleo mmoja, Chaumma mmoja na NRA wanne (asilimia 0.00).


Mkurugenzi huyo alisema kwa upande wa wajumbe wa viti maalum, TLP 63 (asilimia 0.08), NLD mmoja (asilimia 0.00), ACT 57 (asilimia 0.07), UDP 43  (asilimia 0.05), APPT Maendeleo mmoja na Chaumma mmoja (asilimia 0.0).


Hata hivyo, Luanda  alisema matokeo hayo ni sawa na asilimia 99 ya maeneo yaliyofanya uchaguzi na kwamba bado kuna maeneo ambayo hayajafanya uchaguzi kutokana na changamoto mbalimbali ikiwamo mapingamizi, karatasi kuchomwa moto, vifo na kuongeza kuwa hayawezi kubadilisha asilimia za kichama zilizopatikana kwa sasa.


Wiki iliyopita, CCM kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, baada ya kutangazwa matokeo ya kwanza kabla yaw a marudio, alikiri kwamba ushindi wa chama hicho umepungua kwa asilimia 12 kutoka asilimia 96 za mwaka2009 hadi asilimia 84 zamwaka huu.

Nnauye alisema kuwa ingawa wapinzani wameshinda kwa asilimia 16, lakini ushindi huo siyo kigezo cha kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu wa mwakani.


KAULI YA TAMISEMI
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Tamisemi, Jumanne Sagini, amewataka viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo kuwajibika ipasavyo na iwapo mtu atashindwa kufanya hivyo, ajue hatoshi.
CHANZO: NIPASHE

HABARI ZA NYONGEZA KUTOKA VYANZO MBALIMBALI

ARUSHA, Luanda alisema Halmashauri ya Arusha yenye vijiji 64, CCM imeshinda 56, huku Chadema ikipata vijiji 8, wakati Halmashauri ya Meru yenye vijiji 79, CCM imeshinda 51 na Chadema 28. Karatu,CCM imepata vijiji 27 na Chadema 26 huku kwa upande wa vitongoji 246,CCM ikipata 119 huku Chadema ikipata vitongoji 128 wakati vitongoji sita havijafanya uchaguzi.Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ambayo ina vijiji 62, CCM imeshinda vyote, wakati Halmashauri ya Wilaya ya Longido ambayo ina vijiji 49, CCM ilipata 48 na Chadema kimoja. Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro yenye vijiji 72 vyote vimechukuliwa na CCM.Halmashauri ya Jiji la Arusha,CCM imezoa mitaa 78 na Chadema mitaa 75

 DAR ES SALAAM,Katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni yenye mitaa 188, CCM imepata 139, Chadema 34 na CUF 15. Luanda alisema Halmashauri ya Temeke yenye mitaa 172, CCM imepata 115, Chadema 27, huku CUF ikipata 30.

DODOMA, Alisema Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma yenye mitaa 17, CCM imeshinda yote. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa yenye vijiji 92, CCM imepata 71, Chadema viwili na CUF 19, wakati Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa yenye vijiji 96 vyote vimechukuliwa na CCM. Kwa upande wa Kongwa yenye vijiji 82, CCM imeshinda vyote na huko Chemba yenye vijiji 107, CCM imepata vijiji 73, Chadema 9 na CUF 14. Katika Wilaya ya Chamwino yenye vijiji 39, CCM imeshinda 38 na Chadema kimoja wakati Bahi yenye vijiji 59, CCM imepata 53, Chadema 5 na ADC kimoja.

GEITA ,Huko mkoani Geita katika Halmashauri ya Bukombe yenye vijiji 48, CCM imeshinda 29, Chadema 18 huku Halmashauri ya Chato yenye vijiji 115, CCM imepata 88, Chadema 27, wakati Halmashauri ya Geita yenye vijiji 142, CCM imepata 99 na Chadema 32. Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe yenye vijiji 18, CCM imeshinda 17 na Chadema kimoja. Katika Halmashauri ya Nyang’wale yenye vijiji 18, CCM imepata 17 na Chadema kimoja.

IRINGA, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa yenye mitaa 181, CCM imepata 126, Chadema 54 na CUF ikipata mmoja, wakati Mufindi yenye vijiji 39, CCM imepata 35 na Chadema kimoja. Halmashauri ya Kilolo ambayo ina vijijini 81, CCM imepata 78 na Chadema vitatu.

KAGERA,Katika Halmashauri ya Biharamulo yenye vijiji 77, CCM imepata 41 na Chadema 36, wakati katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba yenye vijiji 94, CCM imepata 79 na Chadema 10. Katika Manispaa ya Bukoba yenye mitaa 66, CCM imeshinda 34, Chadema 30 na CUF miwili. Karagwe yenye vijiji 77, CCM imepata 53 na Chadema 19 na huko Kyerwa yenye vijiji 95, CCM imeshinda 51 na Chadema 14. Misenyi yenye vijiji 77, CCM imepata 64, Chadema 12 na Muleba yenye vijiji 166, CCM imeshinda 91 Chadema 70, wakati Halmashauri ya Ngara yenye vijiji 66, CCM imeshinda 61 na Chadema vinne.

KILIMANJARO, Manispaa ya Moshi yenye mitaa 6, CCM imeshinda 29, Chadema 31; Hai vijiji 54, CCM imeshinda 33, Chadema 21; Siha yenye vijiji 60, CCM imeshinda 52, Chadema 8; Same vijiji 96, CCM imeshinda 78, Chadema 17; Mwanga yenye vijiji 72, CCM imeshinda 66, Chadema 6 na Rombo kati ya vijiji 55, CCM imeshinda 33 na Chadema 22.

MBEYA Halmashauri ya Mbeya yenye mitaa 179, CCM imeshinda 103, Chadema 74 na NCCR-Mageuzi mitaa miwili; Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya yenye vijiji 72, CCM imepata 52, Chadema 20; Chunya yenye vijiji 69, CCM imepata 66 na Chadema vitatu; Mbarali yenye vijiji 93, CCM imepata 78 na Chadema 15; Kyela vijiji 92, CCM imepata 79 Chadema 13, wakati Ileje yenye vijiji 70, CCM imepata 53, Chadema 15 na TLP kijiji kimoja. Halmashauri ya Wilaya ya Momba yenye vijiji 86, CCM imevuna 77 na Chadema 9 na Busokelo yenye vijiji 56, CCM imepata 51 na Chadema 5.

MWANZA Jiji la Mwanza lenye mitaa 174, CCM imepata 97, Chadema 70 na CUF 7; Ilemela yenye mitaa 168, CCM imeshinda 106, Chadema 62; Kwimba yenye vijiji 31, CCM imepata 26 na Chadema 5, wakati Magu yenye vijiji 82, CCM imeshinda 51 na Chadema 27. Misungwi yenye vijiji 74, CCM imeshinda 63 na Chadema 10; Ukerewe yenye vijiji 76, CCM imeshinda 27 na Chadema 47; Sengerema yenye vijiji 36, CCM imeshinda 33 na Chadema 3.

TABORA MJINI
Taarifa kutoka Manispaa ya Tabora ambayo ina mitaa 130, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kupata mitaa 86, sawa na asilimia 66, CUF mitaa 28 asilimia 21, Chadema mitaa 14 asilimia 14, huku vyama vya NCCR-Mageuzi na UDP kila kimoja vikishinda kiti kimoja.


MTWARA
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Limbakisye Shimwela, ametangaza matokeo ya jumla na kusema kuwa manispaa hiyo ina mitaa 111, ambako CCM imeshinda mitaa 54, sawa na asilimia 48.6, CUF 36 asilimia 32.4, Chadema 16 asilimia 14.4, NCCR-Mageuzi mitaa minne asilimia 3.6 na TLP kiti kimoja, asilimia 1.


MASASI
Msimamizi wa Uchaguzi wa katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Beatrice Dominic, alisema wilaya hiyo ina vijiji 159, ambako CCM imeshinda vijiji 150, Chadema 4, CUF 4 na NLD kimoja, ambacho awali hakikuwa na kiti hata kimoja wilayani humo.
Alisema kuwa mitaa miwili haijafanya uchaguzi kutokana mgombea kufariki dunia na wengine wanarudia leo.




SHINYANGA
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Manispaa ya Shinyanga kimeibuka kidedea baada ya kujizolea viti katika mitaa 29 huku CCM ikipata viti katika mitaa 26.


Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Shinyanga Mjini, Festo Kang’ombe, alisema kati ya vijiji 17, CCM kilishinda vijiji 14 na Chadema iliambulia ushindi katika kijiji kimoja.


Kang’ombe alisema kati ya vitongoji 84 katika Manispaa hiyo, CCM imeshinda katika vitongoji 65 na Chadema ilipata ushindi katika vitongoji 18.


Alisema uchaguzi utarudiwa kesho katika Mtaa wa Katunda katika Manispaa hiyo, baada ya kushindwa kufanya uchaguzi kutokana na picha na majina ya wagombea kuchanganywa katika fomu na kuhitilafiana na nembo za vyama.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Felix Kimaro, alisema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepata mitaa 18 kati ya 32 na CCM ikishinda mitaa 14. Kutokana na idadi hiyo ipo mitaa ambayo inaongozwa na CCM lakini bado imejikuta ikiwa nyuma ya vyama vya upinzani ambavyo vipo mbele kwa kupata mitaa 57 dhidi ya CCM yenye mitaa 54.


TANGA
Taarifa kutoka mkoani Tanga zinaeleza kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi katika mitaa 118, huku CUF ikishinda mitaa 60 na Chadema mitaa miwili.
Katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2009, CUF ilikuwa na mitaa 42 na kwa sasa kimeongeza mitaa mipya 18, huku Chadema ikiongeza mtaa mpya mmoja tofauti na ule wa awali waliokuwa nao.


Kwa mujibu wa Msimamizi wa Jiji la Tanga ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji hilo, Juliana Mallange, kwa upande wa wajumbe mchanganyiko CCM imepata wajumbe 356 na viti maalumu 230, CUF wajumbe 117 na viti maalumu 62, ambapo Chadema imepata wajumbe 3 na viti maalumu viwili.


Malange alisema wananchi wengi hawakujitokeza kupiga kura ingawa walikuwa wamejiandikisha.


“Tuliandikisha watu 163,999, lakini kati ya hao waliojitokeza ni asilimia 48 pekee,” alisema.
Alisema watalazimika kufanya uchaguzi katika maeneo ya Ndumi na Ngamiani Kaskazini kutokana na uchaguzi kuingiliwa na dosari, ikiwemo wagombea kuwekewa pingamizi.


HANDENI
Msimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Thomas Mzinga, alisema katika vijiji 60, CCM imeshinda 50 kwa kupita bila kupingwa na kati ya hivyo, vijiji 10 pia ilipata vijiji 7 na Chama cha CUF kikipata vijiji vitatu.


Hata hivyo, kata 20 kati ya 33 wilayani Muheza zilishindwa kufanya uchaguzi kutokana na ucheleweshaji wa karatasi za kupiga kura.


PWANI
Matokeo ya Uchaguzi katika Mkoa wa Pwani upande wa Wilaya ya Kibaha mitaa yote ni 73, ambako Chadema wamechukua mitaa 10, CCM mitaa 62, mtaa wa Kilimahewa kura zilizopigwa ziligongana kwa wagombea wa CCM na CHADEMA na hivyo utaratibu wa kurudia uchaguzi unapangwa.
Kibaha Vijijini vijiji vilivyopo ni 32, ambako CCM ilishinda mitaa 31, mitaa 10 ilishinda bila kupingwa, sawa na asimilia 96.9, upinzani ulishinda kijiji kimoja sawa na asilimia 13.1.
Wilaya ya Bagamoyo vijiji vilivyopo ni 75, CCM ilishinda vijiji 67 sawa na asilimia 90.5, lakini vijiji 8 kati ya vilivyopo havijafanya uchaguzi, vitongoji vipo 610, CCM ilishinda 540, sawa na asilimia 88.5, vitongoji 45 havijafanyiwa uchaguzi, wapinzani walishinda vitongoji sawa na asilimia 4.1.
Kisarawe Vijiji vilivyopo 66, CCM ilishinda vijiji 57, sawa na asilimia 86.4, wapinzani vijiji tisa sawa na asilimia 13.6, vitongoji 234 CCM 206, sawa na asilimia 88, Chadema vitongoji 2, CUF 26.


CHALINZE
Katika jimbo hilo idadi ya vijiji ni 75 na CCM imefanikiwa kupita bila kupingwa ni vijiji 38 wakati vijiji vilivyofanya uchaguzi ni 29.


CCM pia imepata ushindi katika vijiji vyote 10 vilivyopiga kura huku matatizo yakiwa yametokea katika vijiji vinane ambako uchaguzi utarudiwa.


Jimbo la Chalinze lina vitongoji ni 610 na CCM imepita bila kupingwa katika vitongoji 303.
Idadi ya vitongoji vilivyofanya uchaguzi ni 262 na CCM imeshinda 242, sawa na asilimia 90 ya vitongoji vyote wakati chama cha CUF kimepata vitongoji 10 na Chadema vitongoji 10.


TABORA MJINI
Taarifa kutoka Manispaa ya Tabora ambayo ina mitaa 130, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kupata mitaa 86, sawa na asilimia 66, CUF mitaa 28 asilimia 21, Chadema mitaa 14 asilimia 14, huku vyama vya NCCR-Mageuzi na UDP kila kimoja vikishinda kiti kimoja.


   Luanda alisema mikoa iliyofanya vizuri katika uchaguzi huo ni Lindi, Mtwara, Iringa, Njombe, Ruvuma, Dodoma, Katavi, Arusha, Kagera, Mbeya na Singida. Hata hivyo, alisema uchaguzi huo ulikuwa na dosari katika mikoa ya Kigoma, Tabora na Pwani ambayo kuna maeneo katika baadhi ya wilaya zake hayajafanya uchaguzi na kwingine utarudiwa.

0 comments:

Post a Comment