MWONGOZO WA UPITISHAJI WA SHERIA NDOGO KATIKA NGAZI YA KIJIJI

Posted by Arusha by day and by night On 03:45 No comments


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

Dibaji 
Mwongozo huu wa upitishaji wa Sheria Ndogo katika ngazi ya Kijiji umetokana na Sheria za Serikali za Mitaa Mamlaka za Wilaya Sura 287 toleo la 2002 pamoja na Sera ya Serikali ya kugatua madaraka kwa kukabidhi kazi, haki, wajibu pamoja na rasilimali fedha kwa wananchi kupitia Serikali za Mitaa.

Aidha, changamoto mbalimbali zilizoko vijijini kupitia program mbalimbali kama vile Mipango ya Maendeleo ya Elimu ya Msingi na Sekondari, Mfuko ya Maendeleo ya Jamii(TASAF), hifadhi ya Mazingira na Kilimo kwanza, zimetoa msukumo mkubwa kuwa na haja ya kuwa na mwongozo kama huu unaowezesha vijiji kuandaa sheria zake ndogo zitakazosaidia kukabiliana na changamoto hizo mfano kuhimiza watu kushiriki na kuchangia kwenye shughuli za maendeleo na kushiriki kwenye ulinzi shirikishi katika maeneo yao.

Mwongozo huu umetolewa ili kuelekeza mambo muhimu ya kufuatwa katika kupitisha Sheria Ndogo za Vijiji na utasaidia katika:-
§  Kufahamu madhumuni ya kupitisha Sheria Ndogo za vijiji;
§  Kujua mahitaji muhimu ya kisheria wakati kuandaa Sheria Ndogo za Vijiji;
§  Kuelewa masharti yanayohusiana na usimamizi wa Sheria Ndogo;
§  Kuelezea utaratibu za kupitisha Sheria Ndogo za Vijiji;
§  Kuwa na mfano wa aina moja wa Sheria Ndogo katika ngazi zote za Vijiji hapa nchini.

Licha ya kuwasaidia Watendaji wa Vijiji na Halmashauri za Ujiji katika kusimamia masuala muhimu katika Kijiji, Mwongozo huu pia una umuhimu kwa vile unalenga katika:-
 
§  Kuwa na Sheria Ndogo zilizopitishwa na Wananchi wenyewe kwa lengo la kulinda Usalama wa mali na rasilimali za Vijiji;
§   Kuelezea umuhimu wa Jamii kushiriki katika kuamua mambo yao wenyewe kulingana na vipaumbele vyao;
§  Kuwezesha Halmashauri ya Kijiji kuwa na Sheria Ndogo zinazoelekeza na kudhibiti mambo mbalimbali katika Kijiji kulingana na mazingira ya Kijiji husika;
§   Kuwa na mwongozo wa kisheria utakaosimamia
§  Utekelezaji wa sera mbalimbali ikiwemo Kilimo, Elimu, Ufungaji, hifadhi ya Mazingira, Afya, Ulinzi, Usalama na masuala ya Kijamii na Kiutamaduni.
Mwongozo huu umeandaliwa kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Serikali za Mitaa, na maelezo ya mwongozo huu yametolewa kwa lugha nyepesi ili kuwawezesha
watumiaji wasio na uelewa wa taratibu za kutunga Sheria Ndogo za Vijiji kuuelewa, kuufuata na kutekeleza.

Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb)
WAZIRI WA NCHI OWM – TAMISEMI

SHUKRANI
Shukrani za dhati ziwaendee wote waliotoa michango yao katika uandaaji wa mwongozo huu hususan Bwana Norbert Feige na Bwana Jan Schrankel kutoka German International Cooperation (GIZ) ambao waliandaa rasimu ya mwongozo huu na kupitia Sheria Ndogo za mfano.

Shukrani hizi pia ziwaendee Bw. Selestine Nchimbi, Bw. Edwin Mgendera, Bw. Eustard Athanace Ngatale na Bw. Seleman Lukanga wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ambao walitoa maoni na mapendekezo yao katika rasimu ya mwongozo huu.

Shukrani za pekee zimuendee Bi Rehema Mdemu kutoka OWM – TAMISEMI ambaye licha yakutoa maoni pia alipitia kwa makini nakala ya mwisho ya mwongozo huu.
Nashukuru pia “German International Cooperation” (GIZ) kwa kusaidia kuandaliwa na kusambazwa kwa mwongozo huu.

Hussein A. Kattanga
KATIBU MKUU 

I. Utangulizi
Sheria Ndogo zimefasiliwa kama sheria zilizopitishwa na chombo chenye mamlaka au chombo cha shirika ambacho kinafanya kazi katika eneo fulani la kijiografia au kimamlaka. Kupitia Sheria Ndogo, serikali za mitaa ndipo zinapoweza kusimamia mambo yao. Kwa ujumla, Sheria Ndogo hupitishwa chini ya mamlaka ya sheria kuu nchini Tanzania chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 ambayo inafafanua mawanda ya masuala yatakayosimamiwa katika ngazi ya Serikali za Mitaa. Hata hivyo, ndani ya mamlaka yake na hususan katika maeneo yale kilichopewa mamlaka na chombo chenye mamlaka ya juu, Sheria Ndogo hazitofautiani na sheria nyingine na zinaweza kusimamiwa na chombo chenye mamlaka na kupitia mfumo wa mahakama.

Kwa mujubu wa kifungu cha 168 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 halmashauri ya kijiji inaweza kutunga Sheria Ndogo katika mawanda ya kazi ilizopewa na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287. Kutokana na sera ya ugatuaji wa madaraka, ambayo unalenga kuendelea kukuza utawala bora, demokrasia na uwajibikaji nchini Tanzania, mamlaka ya halmashauri za vijiji kutunga Sheria Ndogo ni wa umuhimu mkubwa. Hata hivyo, hadi leo hii vijiji vingi vimeacha kutunga Sheria Ndogo. Kwa kiasi fulani, hii inaweza kuwa imesababishwa na kukosekana kwa wanasheria au ushauri katika ngazi ya serikali za mitaa na vilevile kutojua mambo yanayoweza kuwa katika Sheria Ndogo na utaratibu wa kuzipitisha.

Mwongozo huu umekusudia kuamsha ufahamu kuhusu fursa za hatua za kisheria zinazoweza kuchukuliwa katika ngazi ya Serikali za Mitaa na kuzisaidia halmashauri za vijiji zitakazohitaji msaada wa maandalizi na upitishaji wa Sheria Ndogo. Tofauti na miongozo mingine, mwongozo huu hauangalii masharti yanayopasa tu, bali unazingatia kutoa mwongozo kwa vitendo. Hii inajumuisha, pamoja na mambo mengine, kubainisha mahitaji muhimu ya kisheria, kufafanua mahitaji ya kisheria na vikomo na vilevile mapendekezo mbalimbali ya jumla kwa ajili ya mchakato wa kuandaa mswada na kuupitisha. Mwongozo huu unahitimisha kwa mifano, ambayo kimsingi inaonyesha masharti muhimu ya Sheria Ndogo za vijiji.

II. Madhumuni ya Kupitisha Sheria Ndogo
Kwa ujumla, maisha ya amani ya kijamii ndani ya jamii ya wenyeji yanawataka wanajamii wake kuheshimu haki na mahitaji ya wanajamii wengine. Kwa kuangalia umma na vilevile watu binafsi, uhuru wa jumla wa kuchukua hatua ni mdogo ama wa kanuni zilizoandikwa au zisizo katika maandishi. Hata hivyo, chini ya utawala wa kisheria, vikwazo vyovyote vya uhuru wa wananchi, pamoja na kupiga marufuku wakati wote tabia mbaya, vinahitaji kuwa na msingi wa kisheria. Ni muhimu sana kwa wananchi kujua shughuli gani kwa ujumla zimepigwa marufuku na hivyo zinahitaji kupatiwa leseni au badala yake zinatozwa faini.

Ugumu na wingi wa masuala ya umma katika mikoa mbalimbali ya Tanzania unahitaji kuwekewa kanuni za kina katika ngazi ya serikali za mitaa. Sheria Ndogo zinatokana na mchakato shirikishi ambapo halmashauri ya kijiji, chombo kilichochaguliwa moja kwa moja, kwa kushauriana na wakazi wote wa kijiji husika, kupanga kanuni zinazoweza kutekelezeka. Vilevile, wanakijiji watasaidia kupanga Sheria Ndogo ambazo zitaongeza hali ya kukubalika kwa ujumla kwa kanuni ndani ya jamii. Zaidi ya hayo, Sheria Ndogo, tofauti na sheria za kitaifa au sheria za mkoa, zinaweza kuzingatia tofauti za maeneo husika ambazo pia huongeza ufanisi na kukubalika kwa ujumla.

Kupitia Sheria Ndogo, jamii ya kijijini inaweza kuweka kikamilifu kanuni kwa ajili ya masuala mbalimbali yenye maslahi kwa umma, hivyo kuweza kupunguza vitendo vya kuvunja sheria zinazohusiana na haki na wajibu wa wanakijiji wake. Kimsingi zinatoa nguvu za kisheria kwa watu ambao wameathirika vibaya na tabia fulani, kama Sheria Ndogo ambazo jamii ilikubaliana hapo awali, zilikuwa zinazuia wazi tabia hizo. Ili kulinda matumizi sahihi ya Sheria Ndogo na bila upendeleo, adhabu na njia za udhibiti zinaweza kuwekwa.

Zaidi ya hayo, mchakato wa kupitisha Sheria Ndogo unatoa fursa ya kusimamia matumizi ya bidhaa na huduma za umma, ili kuzuia matumizi mabaya, kulinda matumizi yao na kukipatia kijiji uwezo wa kifedha au kiutawala kuhusiana na utoaji wa huduma hizo. Licha ya hayo, jamii ya kijijini inaweza kubuni chanzo chake cha mapato kwa kupanga ada na malipo kwa ajili ya kulipia bidhaa na huduma za umma kupitia Sheria Ndogo hizo.

Kwa kuhitimisha, uwezo wa kusimamia masuala ya kijiji kupitia Sheria Ndogo huziwezesha jamii za vijijini kushughulikia na kusimamia kikamilifu mambo yenye maslahi kwa umma. Hivyo, sababu kuu za kupitisha Sheria Ndogo ni kukuza mazingira ya kisheria, kupunguza migogoro miongoni mwa wananchi na kuongeza ustawi wa wanakijiji kwa ujumla.

III. Mfumo wa Kisheria
1. Uwezo wa Halmashauri ya Kijiji Kisheria
Halmashauri ya kijiji inaweza kutunga Sheria Ndogo ndani ya mipaka ya kazi ilizopewa chini ya Kifungu cha 168 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287. Huu ni uwanja mpana sana kwa kuwa unarejelea mambo yanayohusiana na masuala ya kijiji, kama vile masuala ambayo yanahusu kijiji tu na si Wilaya au nchi nzima. Kulingana na Kifungu cha 113, 114, 147 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287, halmashauri ya kijiji kwa ujumla inaweza:
§  Kutunza na kuwezesha kudumisha hali ya amani, utulivu na utawala bora ndani ya kijiji
§   kuzidisha maendeleo ya jamii na uchumi ya kijiji na vilevile ustawi wa wakazi wake·
 kulinda mali binafsi na mali ya umma
§   kudhibiti na kuboresha kilimo, biashara na viwanda
§   kuimarisha maisha ya watu katika afya, elimu na jamii, utamaduni na burudani
§  kupunguza umaskini na dhiki na kuwasaidia vijana, wazee na watu wenye ulemavu
§   kuanzisha na kudumisha vyanzo vya mapato vyenye uhakika na kuongeza uwajibikaji wa umma katika masuala ya fedha
§   kutambua na kukuza ufahamu wa masuala ya kijinsia
§  kulinda na kutumia kwa usahihi mazingira kwa ajili ya maendeleo endelevu
§  kupanga na kuratibu shughuli za kijiji na kutoa msaada na ushauri kwa wakazi wa kijijini wanaoshughulika na kilimo, kilimo cha maua, misitu au shughuli nyingine au viwanda
§  kuwahimiza wakazi wa kijijini kuendesha na kushiriki katika shughuli za kijamii.
§   Kushiriki, k.m. kwa njia ya ubia, katika shughuli za kiuchumi na halmashauri za vijiji vingine

2. Mahitaji Muhimu ya Kisheria
Katika mfumo wa mamlaka haya, halmashauri za vijiji zinaweza kubainisha mahitaji mbalimbali ya kisheria. Mifano ifuatayo haikutajwa moja kwa moja na haizuii maamuzi yao ya kisheria. Ndani ya mamlaka iliyoelezwa hapo juu, halmashauri za vijiji zinaweza kusimamia mambo yote wanayoona kuwa muhimu kupitia Sheria Ndogo.

a) Usimamizi wa Matumizi ya Ardhi
Mashaka kuhusu kanuni na vikwazo vya matumizi ya ardhi yanaweza kusababisha migogoro mikubwa ndani ya jamii kijijini. Sheria Ndogo zinaweza kuwekwa kama mipango ya kupanga maeneo na maendeleo, hivyo kutenga maeneo mbalimbali au viwanja, miongoni mwa mambo mengine, kwa ajili ya ujenzi au kilimo. Sheria Ndogo hizo pia zinaweza kutaja aina na ukubwa wa majengo na matumizi ya ardhi katika maeneo haya. Zaidi ya hayo, inawezekana ikawepo haja ya kusimamia matumizi na malipo kwa ajili ya mifumo ya umma ya umwagiliaji au kushughulikia masuala ya usafi. Sheria Ndogo zinaweza pia kuweka mfumo wa kisheria kwa ajili ya kuhakiki na kusimamia malipo ya umiliki na matumizi ya ardhi kwa madhumuni fulani.

b) Kanuni kwa Watumiaji wa Mali za Umma
Ili kuendeleza mali za umma, halmashauri ya kijiji inaweza kuhitaji kuweka kanuni za watumiaji. Kwa mfano, inawezekana kukawa na mitazamo tofauti ndani ya jamii ya kijijini kuhusu shughuli zipi ziruhusiwe au zipigwe marufuku kuhusiana na matumizi ya kisima cha umma. Baadhi ya watu huacha kisima kikiwa kichafu, huwapeleka ng’ombe wao kisimani au kufua nguo zao chafu. Wengine wanachukizwa na tabia hiyo na wanahofia kuwa maji ya kunywa yanaweza kuchafuka.

Ili kuhakikisha kuwa kila mtu anaweza kutumia kisima bila maudhi, halmashauri ya kijiji inaweza kusimamia matumizi ya kisima kwa kutumia Sheria Ndogo.

c) Taratibu za Kupata Vizimba Sokoni
Sheria Ndogo zinaweza kusimamia upatikanaji wa vizimba sokoni na kueleza mambo gani yatazingatiwa (kama vile aina ya bidhaa, kuaminika, uwezo wa kifedha, nk.) kwa ajili ya kuvigawa. Zaidi ya hayo, Sheria Ndogo zinaweza kupanga kiasi cha ada ya kiingilio. Chini ya kanuni hizo, maafisa wa kijiji wataweza kufikia maamuzi yasiyo na upendeleo wakati waombaji mbalimbali watakaposhindania idadi ndogo ya vizimba sokoni. Hii huongeza uwazi na inaweza kupunguza rushwa kwa kuwa mafisa hao wanatakiwa kuwa na uwezo wa kutetea uamuzi wao kwa kufuata masharti yaliyowekwa na Sheria Ndogo.

d) Masuala ya Mazingira
Maendeleo endelevu ya kijiji yanahitaji wakazi wake kulinda maliasili kama vile upatikanaji wa maji safi, maeneo ya uvuvi, ufugaji na misitu. Kupitia Sheria Ndogo, halmashauri ya kijiji, miongoni mwa mambo mengine, hufanya kazi ya kusimamia maeneo ya uvuvi na ukubwa maalum wa nyavu za kuvulia, kupiga marufuku uvuvi wa kutumia baruti, inakataza ukataji wa miti michanga na kufyeka na kuchoma moto ili kusafisha ardhi.

e) Masuala ya Usafi
Ili kuendeleza afya ya umma, halmashauri za vijiji zinaweza kusimamia masuala ya usafi kupitia Sheria Ndogo. Kwa mfano, Sheria Ndogo zinaweza kubainisha maeneo ya kutupa taka na kusimamia namna ya kushughulikia maji taka na taka ngumu. Hasa, shughuli fulani zenye madhara kama vile uchomaji wa taka usio na udhibiti au kumwaga maji taka katika maeneo yaliyo karibu na visima ni mambo yanayoweza kupigwa marufuku.

3. Kanuni ya Usawa
Usimamizi wa suala lolote kupitia Sheria Ndogo kwa kawaida hupanga vikwazo vya haki za msingi na uhuru wa wananchi walioathirika, ambazo zimeelezwa katika ibara ya 12 ya Katiba ya Tanzania. Sheria Ndogo kama zilivyo huweka msingi unaotakiwa kisheria. Hata hivyo, ili viwango

vilivyowekwa havitakiwi kusababisha uvunjaji wa haki za msingi na uhuru, Sheria Ndogo pia zinahitaji kufuata kanuni ya usawa.

Hivyo, masharti ya Sheria Ndogo yanatakiwa kwanza kuwa ya kufaa na muhimu ili kufanikisha malengo ya kisheria, kama vile kudumisha amani na utulivu au kutoa hifadhi ya maliasili za kijiji. Kwa mfano, kanuni za utumiaji wa visima vya umma zinaweza kuzuia migogoro baina ya watumiaji na vilevile uchafuzi wa maji na hatimaye kuhatarisha afya ya wanakijiji.

Sheria Ndogo zinazozuia uuzaji wa chakula katika mitaa fulani na kufanya uuzaji ufanyike kwa kupata leseni inaweza kufanya mzunguko wa magari kuwa salama na mzuri. Hairidhishi, hata hivyo, kama watu wengi kijijini wanachukizwa na tabia fulani kama za wanaume na wanawake kushikana mikono, wanawake kuendesha baiskeli au kuvuta sigara sehemu zenye watu wengi.

Zaidi ya hayo, kanuni inataka kuwepo na ulinganifu kati ya uharaka wa kufikia lengo halali kwa upande mmoja na kiwango cha kuingilia haki na uhuru wa wananchi kwa upande mwingine. Hivyo, badala ya kupiga marufuku shughuli fulani, inaweza kutosha kuifanya shughuli hiyo ihitaji kutolewa kibali au leseni.

4. Kutogongana na Sheria Ndogo Nyingine
Sheria Ndogo au sheria zilizowekwa. Hivyo, msingi wa kisheria wa Sheria Ndogo zozote za kijiji umetolewa na bunge kupitia masharti husika ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287. Mamlaka ya kutunga sheria kwa halmashauri za vijiji umewekewa mipaka na Kifungu cha 169 (3) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) sura ya 287, ambacho kwanza kinaeleza kuwa Sheria Ndogo za vijiji hazitakiwi kupinga sheria yoyote iliyo katika maandishi. Hususan hii inajumuisha haki za msingi na uhuru uliotolewa na Katiba ya Tanzania na mamlaka ya kisheria iliyowekwa katikaSheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287.

Kijiji hakitakiwi kusimamia vitu vyovyote ambavyo hakina uwezo, k.m. kuhusiana na matumizi ya ardhi, ambayo ni mali ya wilaya. Pia hairuhusiwi kubadili masharti yaliyowekwa na sheria za bunge kama vile sheria ya ndoa au kanuni ya adhabu, hata kama halmashauri ya kijiji inafikiri hili litasaidia kudumisha amani na utulivu. Hata hivyo, kijiji kinastahili kurekebisha huduma za ustawi wa jamii kijijini alimradi haiendi kinyume na sheria za bunge kuhusu utoaji wa huduma za jamii.

Kifungu cha 169 (3) ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 kinaendelea kueleza zaidi kuwa Sheria Ndogo pia zinatakiwa kufuata Sheria Ndogo zozote zilizowekwa na Halmashauri ya Wilaya. Halmashauri ya kijiji kimsingi, inaweza kusimamia kupitia Sheria Ndogo masuala ambayo kwa ujumla imepangiwa na Halmashauri ya Wilaya kama ilivyoorodheshwa katika jedwali la kwanza kwenye Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287. Hata hivyo, kama Halmashauri ya Wilaya tayari imeshapitisha Sheria Ndogo kuhusiana na jambo hili, Sheria Ndogo za kijiji hazitakiwi kupingana na Sheria Ndogo hizo. Suala la Sheria Ndogo za kijiji kufuata sheria kuu linalindwa na mchakato wa ithibati, ambao umefafanuliwa hapo chini.

Ili kuzuia kueleweka vibaya au kwenda kinyume na sheria kuu, halmashauri za vijiji pia hazitakiwi kuingiza vipengele katika Sheria Ndogo zinazoandaliwa, ambavyo vinarudia masharti yoyote ya sheria kuu au hata kuongeza hatua zozote za kisheria katika jambo lolote ambalo tayari linasimamiwa katika ngazi ya juu. Kwa mfano, Sheria ya Ardhi ya Kijiji inatoa adhabu kwa kuhodhi ardhi kinyume na sheria na masuala yanayohusiana na elimu na uzuiaji wa ndoa za utotoni ni masuala yanayoangwaliwa na Sheria ya Elimu na Sheria ya Ndoa, kwa pamoja. Vilevile, masuala haya hayatakiwi kuangaliwa na Sheria Ndogo za kijiji.

5. Ada na Malipo
Sheria Ndogo zilizopitishwa na halmashauri ya kijiji zinaweza kutaja ada au malipo kwa ajili ya leseni au kibali chochote kinachotolewa na halmashauri ya kijiji, alimradi malipo hayo yawe yanalingana na viwango vilivyowekwa na sheria iliyo katika maandishi au viwango vilivyopangwa na Halmashauri ya Wilaya husika (kifungu cha 9 (2), (3) cha Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa. Kifungu cha 9 (1) (b) cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa inaendelea kufafanua kuwa mapato, fedha na raslimali za halmashauri ya kijiji ni pamoja na fedha zote zilizotokana na leseni, vibali, kodi, ada, malipo au ushuru uliobainishwa na Sheria Ndogo zozote zilizowekwa na halmashauri ya kijiji.

Vilevile, Sheria Ndogo lazima zitaje wazi kiasi cha ada na malipo yanayotakiwa kulipwa ili kupata bidhaa au huduma za umma zinazoangaliwa na masharti yake. Hili linaweza kufanyika kupitia jedwali lililoambatishwa kwenye Sheria Ndogo. Jedwali hilo linatakiwa kuorodhesha bidhaa na huduma zote zinazotakiwa kulipiwa. Mchakato ulio wazi na usio na upendeleo wa kupanga ada na malipo utasaidia kuongeza kukubalika miongoni mwa wanakijiji, kurahisisha usimamizi wake na kupunguza rushwa. Mapato yaliyokusanywa yanaweza kutumiwa katika kudumisha na kulinda bidhaa za umma na kukipatia kijiji fedha kwa ajili ya matumizi au kuendeshea shughuli za kiutawala zinazohusiana na utoaji wa huduma za umma zinazotozwa.

Ada na malipo lazima yatofautishwe na kodi. Hii ni michango ya lazima, ambayo kwa kawaida hutozwa, miongoni mwa mambo yote, katika mapato au mali za watu binafsi au mashirika au katika gharama za uzalishaji au mauzo ya bidhaa na huduma. Kodi haijumuishwi kama fidia kwa ajili ya mauzo ya bidhaa au huduma za umma kama vile leseni au vibali na inawezekana, isipokuwa kama zimetajwa na sheria kuu1, zisikusanywe na kijiji.

Zaidi ya hayo, kijiji hakiwezi kutoza kwa ajili ya shughuli ambazo ni chanzo cha mapato kwa serikali au mamlaka nyingine ya serikali za mitaa. Hivyo, kama halmashauri ya wilaya inatoza fedha kwa ajili ya huduma za basi linalohudumia eneo la kijiji, halmashauri ya kijiji haiwezi kutoza ushuru au malipo ya ziada. Mifano zaidi ya vyanzo vya mapato ya halmashauri ya wiliaya ni ushuru wa mazao ya kilimo na ada kutokana na ukaguzi wa nyama na matumizi ya machinjio.

Ada na ushuru zinatakiwa kuwa za wastani. Hii ina maana kuwa kiasi cha ada na ushuru unaotozwa kinatakiwa kuwa kinalingana na faida binafsi au za kiuchumi mlipaji anazopata kutokana na shughuli husika. Pia inatakiwa kuzingatia juhudi za kirasimu za wanakijiji kulingana na shughuli hiyo. Ada na malipo hayatakiwi kuwa mzigo mzito kwa mlipaji kwa kuchukua faida yote inayoweza kupatikana kupitia shughuli hiyo.

Kwa hali hii, halmashauri za vijiji zikumbuke kuwa ada na malipo yana athari za kiuchumi. Kulingana na kiasi kinachotozwa, ada na malipo yanaweza kusababisha shughuli za kiuchumi zisiwe zenye mvuto. Hivyo, umuhimu wa shughuli hizi kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya kijiji na wilaya unahitaji kufikiriwa. Ada na malipo kawaida yanaleta athari ambazo bidhaa au shughuli zinazotozwa ada zinakuwa na gharama kubwa zaidi kwa wananchi kwa kuwa mlipa ada anaweza kuongeza asilimia fulani ya ada katika bei ya rejareja. Hata hivyo, inatakiwa bidhaa na huduma muhimu ziwe za gharama nafuu ili kila mtu aweze kumudu kuzilipia. Ada na malipo yanaweza kusababisha hali mbaya sana kiasi cha watu kushindwa kumudu kulipia tena leseni au bidhaa za umma (kama maji). Hii itasababisha kuwanyima haki zao za msingi za kibinadamu za ushiriki na maendeleo. Ili kuepuka hili, halmashauri ya kijiji inaweza kuweka ada ndogo kwa watu wenye kipato kidogo zaidi.

6. Masharti Yanayohusiana na Usimamizi wa Sheria Ndogo
Sheria Ndogo zitabaki bila kufanya kazi kama hautafanyika mpango wa udhibiti ili kuhakikisha kuwa wananchi wanazifuata. Hivyo, kifungu cha 183 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 inampa mamlaka afisa yeyote wa Serikali za Mitaa kwa maandishi, miongoni mwa mambo yote, kuingia, wakati wote unaofaa, katika ardhi, jengo, nyumba au chombo chochote ndani ya eneo la mamlaka yake ili kufanya ukaguzi, kuhoji au kufanya kazi chini ya masharti ya Sheria Ndogo. Hivyo, kinadharia Sheria Ndogo si lazima zisimamie haki halisi za udhibiti.

Hata hivyo, inawabidi kufanya hivyo kwa madhumuni ya kutafuta ukweli kwa kuwa idadi kubwa ya wananchi walioathirika waweza kuwa hawajui kanuni za kisheria. Haki za udhibiti zilizowekwa kwenye mswada huu hazitakiwi kuzidi zile zilizotajwa na kifungu cha 183 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 lakini wanaweza kumbainisha afisa aliyeidhinishwa kuwa mkuu wa ukaguzi na kubainisha haki za udhibiti alizopewa ndani ya mfumo wa kisheria ulioelezwa. Kwa mfano, Sheria Ndogo zinaweza kumpa mamlaka afisa mtendaji wa kijiji

kudhibiti matumizi ya majengo ya umma kwa kukagua eneo husika, kuingia kwenye ardhi binafsi na kuwahoji wakazi.

Vivyohivyo utaratibu huu unahusu udhibiti wa makosa katika Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287, ambapo pia ni lazima uingizwe kwenye Sheria Ndogo kwa ajili ya kutoa ufafanuzi. Kuhusu hili, kifungu cha 182 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 inaeleza kuwa uvunjaji wa Sheria Ndogo unachukuliwa kuwa kosa. Iwapo kosa hilo limefanywa na kampuni au wabia, chini ya kifungu cha 189 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 linaelekezwa kwa mtu mwenye mamlaka au cheo, isipokuwa kama kosa lilifanyika bila yeye kujua. Kulingana na kifungu cha 187 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287, adhabu kwa kila kosa, kama haikuelezwa vingine, itakuwa adhabu ya faini isiyozidi TSH. 20,000/= au kifungo cha muda usiozidi miezi mitatu au zote mbili kwa pamoja.

Licha ya hayo hapo juu, Sheria Ndogo za kijiji zinaweza kuongeza adhabu tofauti kutokana na kuvunja masharti fulani. Kulingana na kifungu cha 172 (1), (2) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 faini hizo zinazopangwa na halmashauri ya kijiji zisizidi TSH 50,000 na hazitahusisha adhabu ya kwenda jela. Vilevile, kutokana na hali ya kifedha, Sheria Ndogo zinaweza kutaja faini kali zaidi kuliko zile zilizowekwa mapema na kifungu cha 187.

Kwa mtazamo wa jumla faini zimepangwa kama adhabu kwa wakosaji na kama kivutio kwa wakazi kuheshimu sheria, kuwekwa kwa faini kali inawezekana ikawa sahihi chini ya mazingira fulani. Hasa inafaa faini za kuvunja Sheria Ndogo ziwe za kukatisha tamaa kifedha, ikiwa na maana kuwa lazima ziwe zinazidi faida ya moja kwa moja au kwa njia nyingine inayopatikana kwa kufanya shughuli zisizo halali. Vinginevyo, wananchi watapata vishawishi vya kudharau Sheria Ndogo.

Watu wasipoheshimu Sheria Ndogo wanaweza kusababisha uharibifu. Ufyekaji na uchomaji ovyo mashamba, kwa mfano, wanaweza kusababisha moto ambao unaharibu maeneo makubwa ya misitu, kisima kikichafuka kinaweza kuhitaji kufanyiwa usafi. Hivyo, kulingana na kifungu cha 172 (3) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287, mbali na faini, adhabu chini ya Sheria Ndogo za kijiji zinaweza kuwa pamoja na “hatua zitakazoonekana kuwa zinafaa zaidi kwa mfano au kuwazuia wahalifu, kuhakikisha zinawafidia kwa uhalifu uliofanywa na mhusika na kurejesha usawa katika ulinganifu wa kijamii uliovurugwa kutokana na utendaji wa makosa.” Maneno haya yanaipa halmashauri uamuzi wa kubainisha na kusimamia hatua madhubuti za kudhibiti makosa ya kutoheshimu Sheria Ndogo.

Vilevile, halmashauri za vijiji zina uhuru wa kutumia njia za kawaida na kimila za kutoza malipo.Hata hivyo, njia hizi zihakikishwe hazigongani na sheria zilizo kwenye maandishi, hususan haki za msingi na uhuru uliotolewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mfano, Sheria Ndogo zinaweza kueleza kuwa gharama zilizosababishwa na uvunjaji wa masharti yake zitalipwa zote na mtu aliyetenda kosa au mtu atakayesababisha hasara itambidi kufidia kijiji kwa kufanya shughuli za huduma za jamii. Pia inaweza kueleza njia zisizo za fedha za kuwarekebisha wahalifu kama vile kueleza umma kuhusu kosa lake.

IV. Utaratibu wa Kupitisha Sheria Ndogo
Mapendekezo yafuatayo yanakusudiwa kuongoza halmashauri za vijiji katika kupitisha Sheria Ndogo na kutoa muhtasari wa hatua za kuchukua.

1. Maandalizi ya Mswada wa Sheria Ndogo na Mapendekezo ya Jumla
Iwapo halmashauri ya kijiji inakusudia kutunga Sheria Ndogo, inabidi imteue mtu au kamati ya kuandaa mswada wa pendekezo. Mwandishi au kamati inatakiwa kuzingatia mahitaji ya kisheria na vilevile mfumo wa kisheria ulioelezwa hapo juu. Hasa, mapendekezo haya ya jumla yazingatiwe.

a) Kutumia Mifano ya Sheria Ndogo
Mifano ya Sheria Ndogo, kama zile zilizoambatishwa katika kitini hiki, au Sheria Ndogo zilizopo zilizopitishwa na mamlaka nyingine za Serikali za Mitaa zinaweza kutumiwa kama mfano. Mwandishi au kamati inaweza kuangalia mfano wa Sheria Ndogo ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa [imeambatanishwa ], ambayo ina Sheria Ndogo za Halmashauri ya Wilaya zinazotumika kutoka Wilaya zote nchini Tanzania. Hii ni njia nzuri ya kuangalia jinsi Serikali za Mitaa zinavyoshughulikia masuala husika.
Sheria Ndogo zilizopo zinaweza kunakiliwa kwa sasa au kurekebishwa kulingana na mahitaji ya kisheria yaliyopo. Mfano wa Sheria Ndogo hizo unaweza kufikiwa kupitia intaneti, lakini pia inapatikana katika CD-Rom, ambayo inaweza kuagizwa kupitia Wanasheria wa Halmashauri za Wilaya.

b) Kufanya Mashauriano Mapema na Vikundi vya Kijamii na Wanasheria
Watu watakaoathirika na utungwaji wa Sheria Ndogo kama vilevile vikundi vya kijamii, mashirika yanayotoa huduma za kisheria yanaweza kufikiwa katika hatua za awali ili kupata mchango wao kuhusu Sheria Ndogo zinazokusudiwa kutungwa ili kuelewa upinzani uliopo kwa Sheria Ndogo. Mashauriano hayo yakifanyika mapema yatasaidia kushughulikia masuala yote muhimu na kuongeza kukubaliwa kwa ujumla kwa Sheria Ndogo zilizokusudiwa ndani ya jamii ya kijijini.

Iwapo mwandishi au kamati itakuwa na mashaka kuhusu mfumo wa kisheria ulioelezwa hapo juu, wamwone Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya. Mashauriano ni muhimu sana ili kuhakikisha kuwa Sheria Ndogo hazigongani na sheria za Bunge au Sheria Ndogo za Halmashauri ya Wilaya.

c) Muundo wa Jumla wa Sheria Ndogo
Kimsingi, ni juu ya halmashauri ya kijiji kuamua jinsi ya kuunda Sheria Ndogo. Hata hivyo, mapendekezo ya jumla yafuatayo na mfano wa Sheria Ndogo ulioambatishwa unatakiwa kuzingatiwa ili kuwa na muundo wenye mantiki. Sehemu ya kwanza ya Sheria Ndogo kwa kawaida hubainisha kichwa cha habari kutokana na jina, mamlaka inayopitisha na mwaka. Sehemu ya pili inafafanua eneo la matumizi ikiwa na maana kwamba Sheria Ndogo hizo zitatumika ndani ya eneo la mamlaka ya halmashauri ya kijii husika tu. Katika sehemu ya tatu, mwandishi au kamati inatakiwa kutoa tafsiri ya maneno yaliyotumika.

Baada ya kutoa tafsiri ya maneno yaliyotumika yanafuata masharti ya Sheria Ndogo, kama vile shughuli ambazo zinapigwa marufuku au zinatakiwa kukatiwa leseni au kulipiwa ada. Mwishoni, kuna haja ya kuweka masharti ambayo yakivunjwa yatasababisha kupewa adhabu, iwapo kama viongozi wa kijiji wana haki maalum ya kufanya ukaguzi na kama iwapo njia za ziada za kupata malipo ya fidia zitapangwa mapema. Ada, shughuli na au mahali au maeneo yanaweza kutajwa katika kiambatisho.

d) Maneno na Masharti ya Faini, Tarehe za kulipa, nk.
Wananchi wote watakaoathirika wanatakiwa kuwa na fursa ya kuelewa kikamilifu madhara ya Sheria Ndogo. Hivyo, mwandishi au kamati ihakikishe kuwa inatumia maneno yaliyo wazi na rahisi. Sheria Ndogo zinatakiwa kutamka kwa maneno yasiyokuwa na maana nyingi shughuli ambazo zinaruhusiwa, zimepigwa marufuku au zinazohitaji leseni na au ada. Chini ya utawala wa sheria, mashaka yoyote kuhusu mawanda na maana ya sheria yoyote yatakayojitokeza yataigharimu mamlaka iliyoipitisha na hayatatafsiriwa kumkandamiza mwananchi aliyeathirika.
Hasa, iwapo Sheria Ndogo zimeandaliwa ili kutoa adhabu kutokana uvunjaji wa masharti fulani kwa kupanga faini, shughuli zote zilizopigwa marufuku na kiasi cha faini vinatakiwa kutamkwa wazi. Wakati wa kupanga tarehe, mwandishi au kamati ikumbuke kuwa Sheria Ndogo zitafanya kazi kwa miaka kadhaa. Hivyo, ada hazitalipwa hadi tarehe fulani kama vile 1 Januari 2011 lakini “kila wiki/mwezi/mwaka” au “hadi siku ya kwanza/mwisho ya kazi ya wiki/mwezi/mwaka”.

e) Athari za Kiuchumi na Kutobagua
Iwapo mswada unatakiwa kuingiza mapema ada na malipo, mwandishi au kamati inatakiwa kukumbuka athari zake kiuchumi. Kama ilivyojadiliwa hapo juu, ada na malipo yanatakiwa kuwa ya wastani ili yasiathiri vibaya uchumi wa wenyeji au hata kufanya bidhaa au shughuli zinazotozwa ziwe ghali sana kwa wananchi.

Zaidi ya hayo, mwandishi au kamati iangalie tena kama iwapo mswada unafuata masharti yote ya kisheria. Kwa kuzingatia kanuni ya kutobagua, Sheria Ndogo lazima zihakikishwe haziathiri vibaya vikundi au watu fulani zaidi ya wengine. Hasa, athari mbaya zinazohusiana na masuala ya jinsia lazima zizuiwe.

2. Upitishaji na Uthibitishaji wa Sheria Ndogo
Baada ya kukamilisha mswada wa Sheria Ndogo, mwandishi au kamati itaripoti kwenye halmashauri ya kijiji ambayo itaanza mchakato wa kuipitisha.

a) Mkutano wa Kijiji
Kwanza, pendekezo la Sheria Ndogo linatakiwa kutolewa kwenye mkutano wa kijiji (kifungu cha 169 (1) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287). Hili linaweza kufanyika katika mkutano wa kawaida wa kijiji, ambao, kulingana na kifungu cha 105 (2) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287, unatakiwa kufanyika angalau mara moja katika kila miezi mitatu. Hata hivyo, kufuatia kifungu cha 169 (1); 105 (3) cha, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 halmashauri ya kijiji inaweza pia kuitisha mkutano wa dharura wa kijiji ili kuharakisha mchakato huo.

Kwa hali yoyote, mswada utatakiwa kuwekwa wazi kwa wananchi wote kwa kuubandika kwenye ubao wa matangazo ya kijiji kwa muda wa kutosha kabla ya mkutano kufanyika. Iwapo wananchi hawakubaliani na mswada huo, watakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuukosoa ipasavyo na vya kutosha kama watakuwa wamepata muda wa kufikiri kabla ya mkutano. Mchakato wa mashauriano ni muhimu ili kushughulikia vipengele vyote vinavyoweza kuwa havikushughulikiwa vya kutosha na mswada.

Katibu wa halmashauri ya kijiji anatakiwa kuandaa kwa makini kumbukumbu za mkutano wa kijiji kwa kuwa zinatakiwa kuambatishwa pamoja na mswada wa Sheria Ndogo kwa ajili ya hatua inayofuata ya kupitisha Sheria Ndogo. Kumbukumbu zinahitaji kueleza kwa muhtasari masuala yote yaliyojadiliwa wakati wa mkutano na lazima zieleze bila kuacha maoni yaliyotolewa na wajumbe wa mkutano wa kijiji.

b) Mkutano wa Halmashauri ya Kijiji
Kulingana na kifungu cha 169 (1) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 pendekezo la Sheria Ndogo linahitaji kujadiliwa katika mkutano wa halmashauri ya kijiji. Halmashauri ya kijiji inatakiwa kuzingatia mawazo ya wakazi kama yalivyotolewa wakati wa mkutano wa kijiji, lakini hailazimiki kufuata mawazo hayo. Wakati wa mkutano huu akidi chini ya kifungu cha 107 ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 inatakiwa kutimia, ikiwa na maana kuwa angalau nusu ya wajumbe wa halmashauri ya kijiji wanatakiwa kuwepo.

Halmashauri ya kijiji bado inaweza kurekebisha pendekezo katika hatua hii, bila kujali kama marekebisho hayo yanaangalia masuala yaliyoibuliwa wakati wa mkutano wa kijiji au yamebainishwa na halmashauri yenyewe ya kijiji.

Mwisho wa mkutano, Halmashauri ya kijiji inatakiwa kuamua kuhusu kupitisha Sheria Ndogo na marekebisho yanayoweza kufanyika. Katika hatua hii, ihakikishwe kuwa maneno yaliyotumika yanaakisi masharti yaliyokusudiwa. Licha ya kupitishwa kwa pendekezo hilo na halmashauri ya kijiji, Sheria Ndogo bado hazitaanza kutumika.

c) Kuidhinishwa na Halmashauri ya Wilaya, Kuanza Kutumika na Kuchapishwa
Kulingana na kifungu cha 169 (1) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287, halmashauri ya kijiji inatakiwa kuwasilisha Sheria Ndogo zilizopitishwa kwenye Halmashauri ya Wilaya kwa ajili ya kuthibitishwa. Hili linaweza kufanyika kupitia kwa katibu ambaye anatakiwa kuambatanisha kumbukumbu za mkutano wa kijiji, ambao pendekezo liliwasilishwa kwa ajili ya kutolewa maoni. Halmashauri ya kijiji pia inatakiwa kutoa mapendekezo kuhusiana na kuanza kutumika kwa Sheria Ndogo.

Ingawa mawanda ya kitini hiki hayaruhusu kutoa maelezo ya kina ya utaratibu wa uthibitishaji katika ngazi ya Wilaya, halmashauri ya kijiji lazima ikumbuke kuwa Halmashauri ya Wilaya inatakiwa kujiridhisha kuwa Sheria Ndogo za kijiji hazigongani na masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au sheria nyingine yoyote iliyo katika maandishi ikiwa ni pamoja na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287. Katika kuidhinishwa Halmashauri ya Wilaya pia huamua kuhusu tarehe ya kuanza kutumika kwa Sheria Ndogo, kifungu cha 169 (2) ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287.

Baada ya kuidhinishwa kwa Sheria Ndogo hizo, Halmashauri ya Wilaya itazirudishia kwa Halmashauri ya kijiji ili zianze kutumika. Iwapo Halmashauri ya Wilaya itakataa kuidhinisha Sheria Ndogo, itaitaarifu halmashauri ya kijiji kwa maandishi kuhusu sababu za kufanya hivyo. Halmashauri ya kijiji inaweza kurekebisha Sheria Ndogo kwa kuzingatia maoni ya Halmashauri ya Wilaya na kuziwasilisha tena kwa ajili ya kuidhinishwa. Iwapo halmashauri ya kijiji, kwa sababu za kisheria, haikukubaliana na sababu zilizotolewa na Halmashauri ya Wilaya inaweza kupinga kukataliwa huko mbele ya mahakama. Hata hivyo, hadi sasa hapajawahi kutokea tukio kama hilo.

Baada ya kuidhinishwa, Sheria Ndogo zinatakiwa kuchapishwa na halmashauri ya kijiji. Kulingana na kifungu cha 201 (1) (b) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287., Sheria Ndogo zitachukuliwa kuwa zimechapishwa ipasavyo kama zitabandikwa kwa muda wa kutosha mahali panapoonekana waziwazi kwenye au karibu na mlango wa nje wa mamlaka inayozipitisha zitumike au zimefanywa zijulikane kwa njia kama za jadi katika eneo la mamlaka. Hivyo, Sheria Ndogo lazima zibandikwe kwenye ubao wa matangazo ya kijiji. Nakala za ziada zinaweza kutolewa katika ofisi ya halmashauri ya kijiji kwa wananchi wanaotaka.

3. Urekebishaji na Ubatilishaji wa Sheria Ndogo
Ili kubadili masharti ya Sheria Ndogo, halmashauri ya kijiji inatakiwa kupitisha Sheria Ndogo zinazorekebishwa, ambazo zinatamka wazi masharti yanayotakiwa kurekebishwa, kuongezwa au kufutwa. utaratibu uliotumika kupitisha Sheria Ndogo ndio utatumika. Hii ina maana, marekebisho yaliyopendekezwa yanatakiwa kujadiliwa na mkutano wa kijiji, kupitishwa rasmi na halmashauri ya kijiji na kuthibitishwa na Halmashauri ya Wilaya kama ilivyoelezwa hapo juu.

Ili kutengua Sheria Ndogo zilizopo na zinazofanya kazi halmashauri ya kijiji itatakiwa kutangaza uamuzi rasmi wa kufanya hivyo. Zaidi ya hayo, Sheria Ndogo zinaweza kutenguliwa kwa amri ya mahakama au Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.

V. Mifano ya Sheria Ndogo
Tafadhali kumbuka:
Mifano ifuatayo inatokana na Sheria Ndogo halisi za vijiji na zinaonyesha mahitaji maalum ya kisheria kama yalivyobainishwa na halmashauri husika za vijiji. Mahitaji haya hayahusu jamii zote za vijijini nchini kote na mawanda ya kanuni yanaweza, baadaye, yasionekane wakati wote kuwa sahihi. Hasa, viwango vya faini na ada vinaweza kutofautiana sana kwa kutegemea viwango vya kijamii na mitazamo ya kimila au kidini ndani ya jamii. Vilevile, utoshelevu wa kiasi cha ada na faini hizo inategemea wastani wa ustawi wa wakazi. Vilevile, mifano ya mada zilizopo zisichukuliwe kama muundo sanifu ambao halmashauri nyingine lazima ziifuate. Mifano hii imechukuliwa kama mifano ya msingi, kuonyesha jinsi masuala fulani yenye maslahi kwa umma yanavyoweza kusimamiwa katika ngazi ya kijiji. Kila halmashauri ya kijiji ina uhuru wa kuangalia kama kanuni kama hizo zitafaa na kutosheleza kwa eneo lao hilo la mamlaka au hapana na, kukubali, kupitisha kanuni hizi au sehemu yao kwa ajili ya mahitaji maalum.

SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA)
(SURA YA 287)
HALMASHAURI YA KIJIJI CHA………………………………..
SHERIA NDOGO


Zimetungwa chini ya kifungu cha………
SHERIA NDOGO ZA (MAENDELEO YA JAMII) ZA HALMASHAURI YA KIJIJI CHA………., 2010

Jina na mwanzo wa kutumika

Sheria Ndogo zitajulikana kama Sheria Ndogo za (Maendeleo ya Jamii na Usalama wa Raia) za Halmashauri ya Kijiji cha……….. za [mwaka] na zitaanza kutumika baada ya kutidhinishwa na Halmashauri ya Wilaya [wilaya].

Eneo la matumizi

Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote lililo chini ya mamlaka ya Halmashauri ya Kijiji cha [kijiji].

Tafsiri
Kifungu cha172 (3) sura ya 287

Katika Sheria Ndogo hizi, isipokuwa itakapoelezwa vinginevyo;-
"Chakula" maana yake ni vitu vinavyoliwa na binadamu;
“Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Kijiji cha [kijiji];
“Huduma za Ulinzi wa Jadi” maana yake ni utekelezaji wa majukumu chini ya Mpango wa Usalama;
“Huduma za Umma” maana yake ni njia mbadala au ya ziada ya malipo ambayo inahusisha kazi zenye manufaa kwa jamii ya Kijijini kama vile kupanda miti au kusafisha mazingira;
“Kazi za Maendeleo ya Jamii” maana yake ni kazi zozote ambazo Halmashauri ya Kijiji itakazowaomba wakazi kuzifanya kwa pamoja ili kuboresha au kutunza Majengo ya Umma Kijijini;
“Kijiji” maana yake ni Kijiji [kijiji];
“Majengo ya Umma” maana yake ni majengo ya umma yanayotumiwa na umma ndani ya eneo la Kijiji;
“Mifugo” maana yake ni ng’ombe, mbuzi, kondoo, punda, mbwa na wanyama wengine muhimu
kiuchumi wafugwao na binadamu;
“Maliasili” maana yake ni maliasili yoyote inayopatikana kijijini, hususan mbao, miti, mchanga, miamba, madini au aina nyingine yoyote ya bidhaa inayopatikana katika eneo la kijiji;
“Mpango wa Usalama” maana yake ni mpango ambao Halmashauri inaupitisha chini ya Sheria Ndogo hizi unaowataka wakazi washiriki katika shughuli zinazohakikisha ulinzi wa watu na mali zao kijijini kwa muda utakaopangwa na Halmashauri;
“Saa za Kazi” maana yake ni mkuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 9 alasiri katika siku zote isipokuwa [Ijumaa/Jumapili] na siku za sikukuu;
“Usiku” maana yake ni muda kati ya saa 4 usiku na saa 12 asubuhi;
Kazi za maendeleo

(1)Halmashauri inaweza kuwaomba wakazi wa Kijiji watu wazima kushiriki katika Kazi za Maendeleo ya Jamii.
(2)Wito wa Kazi za Maendeleo ya Jamii ni halali endapo:
(a) ni muhimu kwa ajili ya maendeleo sahihi ya Kijiji na unaangalia upungufu wa miundombinu fulani;
(b) kazi zilizopangwa zinaleta mabadiliko ya ustawi wa wakazi wote wa Kijiji bila kuleta athari;
(c) kazi zilizopangwa zinapita majukumu na uwezo wa viongozi wa Kijiji; na
(d) ratiba za kazi zinazingatia ipasavyo vikwazo vya kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa Kijijini.
(3)Mtu yeyote ambaye, bila sababu ya msingi, amekataa kushiriki kwenye shughuli yoyote inayohusiana na Kazi za Maendeleo ya Jamii au anawashawishi watu wengine wasishiriki katika Kazi za Maendeleo atakuwa ametenda kosa na atatozwa faini isiyozidi Tsh 10,000/- au kulazimika kufanya kazi za Huduma za Jamii kwa muda usiozidi [siku/saa] au adhabu zote kwa pamoja faini na kufanya Kazi za Huduma ya Jamii
Ulinzi wa jadi
(1)Halmashauri inaweza kupitisha Mpango wa Ulinzi na kuwaomba Wakazi wa Kijiji watu wazimakushiriki katika Huduma za Ulinzi wa Jadi ndani ya mfumo wa mpango uliopitishwa.
(2)Wito kwa ajili ya Huduma za Ulinzi wa Jadi utakuwa halali endapo:
(a) shughuli zinazofanyika chini ya Mpango wa Usalama zipo nje ya majukumu na uwezo wa viongozi wa Kijiji;
(b) Viongozi wa Kijiji hawawezi kuhakikisha usalama ndani ya Kijiji bila kutoa mwito wa Huduma za Ulinzi wa Jadi; na
(c) Mpango wa Ulinzi unataka kuwepo na mgawanyo wa majukumu bila upendeleo na kwa usawa ndani ya jamii kijijini.
(3)Mpango wa Ulinzi unaweza kutoa amri ya kutotembea ovyo, alimradi kwamba usalama ndani ya Kijiji hauwezi kulindwa vinginevyo.
(4)Mtu yeyote ambaye;-
(a) bila sababu yoyote, anakataa kushiriki katika shughuli yoyote inayohusiana na Ulinzi wa Jadi au akiwashawishi watu wengine kufanya hivyo atastahili kutozwa faini isiyozidi Tsh 10,000/- au kupangiwa kazi za Jamii kwa muda usiozidi [siku/saa] au kutozwa faini na kufanya kazi.
(b) atazuia au kuhujumu shughuli za Mpango wa Ulinzi au kuwashawishi wengine kufanya hivyo atatozwa faini ya Tsh 20,000/- au atawajibika kufanya kazi za kijamii kwa muda usiozidi [siku/saa] au kutozwa faini na kufanya Kazi za kijamii.
(c) bila sababu za msingi anadharau amri halali iliyotolewa ya kutotembea ovyo atatozwa faini ya Tsh 1,500/-.
Maliasili

(1)Mtu yeyote atakayetaka kukusanya au kuvuna maliasili ndani ya eneo la Kijiji atatakiwa
(a) kuomba leseni kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Kijiji.
(b) kulipa ushuru kwa kila kipande cha Maliasili kwa viwango vilivyoainishwa kwenye jedwali la Sheria Ndogo hizi
(2)Leseni itolewayo chini ya kifungu kidogo cha (1) (a) hakitaruhusu kukata miti au mimea ambayo inalindwa chini ya Sheria ya Tanzania.
(3)Leseni hiyo itatolewa kwa kwa watu ambao
(a) wamelipa ada ya mwaka inayotozwa kwa ajili ya kibali kwa kiwango kilichopangwa kwenye Kiambatisho cha Sheria Ndogo hizi; na
(b) hawana madeni ya ada au ushuru chini ya Sheria Ndogo hizi au madeni mengine ya kodi kwa Serikali.
(4)Mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kukusanya au kuvuna Maliasili kinyume na masharti ya Sheria Ndogo hizi atatozwa faini ya 50% ya ada aliyopaswa kulipa au atatakiwa kufanya kazi za kijamii kwa muda usiozidi [siku/saa] au kulipa faini pamoja na kufanya kazi za kijamii.
Mifugo

(1)Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuingiza mifugo yake, kuilisha au kuiacha bila uangalizi kwenye ardhi ya umma au kuipitisha ndani yake au kwenye mali ya mtu binafsi bila ruhusa ya mmiliki.
(2)Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi kutoa tarifa juu ya uwepo dalili za ugonjwa wa wanyama kwa Mwenyekiti wa Kijiji.

Usafi wa mazingira
(1)Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi kuhakikisha kuwa nyumba yake ina mashimo ya kutupia taka na vyoo imara na vya kudumu.
(2)Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kutupa taka ovyo katika eneo lote la Kijiji
(3)Itakuwa ni marufuku kutumia mbolea ya samadi au ya viwandani, kumwaga majitaka, kukata miti na kufanya shughuli nyingine yoyote ambayo italeta athari mbaya katika ubora na wingi wa maji ndani ya mita 50 kutoka katika chanzo cha maji.
(4)Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu hiki atalipa faini isiyozidi Tsh 3,000/- kwa kila kosa au kutakiwa kufanya kazi za kijamii kwa muda usiozidi [siku/saa] au kulipa faini na Kufanya kazi za kijamii.

Uuzaji wa chakula
(1)Mtu yeyote atakayetaka kuuza chakula katika eneo la kijiji atatakiwa kuomba kibali kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji.
(2)Kibali hicho kitatolewa kwa mtu ambaye
(a) amelipa ada zote zinazotozwa kwa ajili ya kibali kwa kiasi kilichopangwa kwenye

Jedwali la Sheria Ndogo hizi;
(b) hadaiwi ada nyingine zozote au ushuru chini ya Sheria Ndogo hizi au madeni ya kodi kwa serikali,
(c) anaendesha biashara kwa usafi.

(3)Afisa Afya wa Wilaya anaweza kufuta kibali kilichotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1) au kuzuia uuzaji wa chakula katika maeneo fulani ndani ya Kijiji.
(4)Mtu yeyote ambaye atakwenda kinyume na masharti ya kifungu hiki atakuwa ametenda kosa na atatozwa faini isiyozidi Tsh 1,000/- kwa kila kosa au atatakiwa kufanya kazi za kijamii kwa muda usiozidi [siku/saa] au kutozwa faini na kufanya kazi za kijamii.
Moto

(1)Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuwasha moto ambao unaweza kusababisha hasara ya mali ya umma au binafsi
(2)Mtu yeyote ambaye anajitoa katika juhudi kubwa za kuzima moto ambao unaweza kusababisha madhara kwa jamii ya au kufanikiwa kuzuia juhudi hizo atastahili kupewa kiasi cha shilingi 50,000/- kama motisha.

SHERIA YA FEDHA ZA SERIKALI ZA MITAA
(SURA YA 290)
HALMASHAURI YA KIJIJI CHA………………………………..
SHERIA NGODO
Zimetungwa chini ya kifungu cha 9(1) na 16(1)
SHERIA NDOGO ZA (ADA NA USHURU) ZA HALMASHAURI YA KIJIJI CHA………., 2010

Jina na mwanzo wa kutumika

Sheria Ndogo zitajulikana kama Sheria Ndogo za (Ada na Ushuru) za Halmashauri ya Kijiji cha……….. za [mwaka] na zitaanza kutumika baada ya kutidhinishwa na Halmashauri ya Wilaya [wilaya].
Eneo la matumizi

Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote lililo chini ya mamlaka ya Halmashauri ya Kijiji cha [kijiji].
Tafsiri

“Ada na Ushuru” maana yake ni malipo yanayotolewa kwa Halmashauri kwaajili ya shughuli mbalimbali zinazoendeshwa ndani ya Halmashauri.

“Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Kijiji cha………..
“Wakala” maana yake ni mtu, kampuni binafsi au asasi ya umma au binafsi iliyoteuliwa na Halmashauri kukusanya ada na ushuru kwa niaba yake.
Ushuru

(1)Kutakuwa na ushuru utakaotozwa kutoka katika vyanzo vya mapato vilivyoainishwa katika jedwali la Sheria Ndogo hizi.
(2)Ada na Ushuru utakaokusanywa chini ya Sheria Ndogo hizi utatumika kwa Majengo ya Umma, elimu au miundombinu au hatua za maendeleo ambazo zinanufaisha jamii ya Kijijini kwa ujumla
(3)Ada na ushuru uliokusanywa chini ya Sheria Ndogo hizi utakusanywa na Halmashauri au kumteua wakala.
(4)Ada na ushuru utozwao chini ya Sheria Ndogo hizi unaweza kulipwa kwa:
(a) jumla kwa ajili ya shughuli au kitengo cha Maliasili katika siku ambayo shughuli hiyo inafanyika au kitengo hicho kinakusanya;
(b) kila wiki siku ya Jumatatu ya wiki husika;
(c) kila mwezi katika siku ya kwanza ya kazi ya mwezi husika;
(d) kila mwaka katika siku ya kwanza ya mwaka husika.

Wajibu wa wakala

(1)Itakuwa ni wajibu wa wakala;-
(a) kumpatia risiti mtu yeyote aliyelipa ada au ushuru
(b) kuandaa ripoti za kila mwezi kuipeleka Halmashauri akionyesha kiasi cha mapato aliyokusanywa.

(2)Wakala yeyote ambaye;-
(a) atashindwa kukabidhi kiasi chochote cha fedha alizokusanya kama ushuru kwa Halmashauri;
(b) kwa kujua akimdai mtu yeyote kiasi kinachozidi kiwango cha ushuru kilichowekwa; au
(c) kwa uzembe au makusudi akitoa taarifa za mapato zenye makosa, iwe kwa mdomo au
kwa maandishi, kuhusu idadi ya walipa kodi au jumla ya malipo aliyokusanya au kupokea;
atakuwa ametenda kosa.
(3)Halmashauri itawasilisha ripoti kuonyesha mapato na matumizi ya kila mwezi kwenye mkutano mkuu wa kijiji.
(4)Iwapo wakazi watatoa malalamiko kuhusu mwenendo mbaya kwa upande wa wakala, Halmashauri itaanza kufanya uchunguzi.
(5)Sheria Ndogo hizi hazizuii au vinginevyo hazimwondolei mtu yeyote kosa la jinai chini ya sheria za nchi mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya uzembe, kutoa au kupokea rushwa.
(6)Endapo Halmashauri ya Wilaya au Serikali Kuu itaongeza kiwango cha ushuru katika kitu chochote kilichoorodheshwa kwenye kiambatisho, Halmashauri itarekebisha viwango hivyo kwa kuzingatia marekebisho yaliyofanyika.

(1)Mtu yeyote hataaadhibiwa chini ya Sheria Ndogo hizi endapo ameshafunguliwa mashtaka na kusikilizwa chini ya Sheria Kuu au Sheria Ndogo za Halmashauri ya Wilaya kwa kosa hilo.
(2)Uendeshaji wa mashtaka ya makosa chini ya Sheria Ndogo utasimamishwa, mara mashtaka ya jinai chini ya sheria kuu au Sheria Ndogo za wilaya yatakapofunguliwa.

Kiambatisho – Ada na Ushuru
I. Vibali
Kibali cha kukusanya Maliasili Tsh 10,000/- kwa mwaka
Kibali cha kuuza chakula Tsh 1,000/- kwa mwezi
II. Maliasili
Mchanga Tsh 1,000/- kwa kila lori au trekta
Udongo wa mfinyanzi Tsh 1,000/- kwa kila lori au trekta
Mbao Tsh 100/- kwa gogo la 1 m³
Mbao za ubora wa hali ya juu, k.v. mpingo, mpera Tsh 1,500/- kwa gogo la 1 m³
III. Vyanzo vya Mapato
Biashara ya rejareja Tsh 15,000/- kwa mwaka
Usagaji Tsh 20,000/- kwa mwaka
Ukoboaji Tsh15, 000/- kwa mwaka
Biashara ya mkaa Tsh 15,000/- kwa mwaka
Mauzo ya mbao Tsh 20,000/- kwa mwaka
Uuzaji wa nyama Tsh 10,000/- kwa mwaka
[Vipengele vingine vyovyote vya Halmashauri vinavyoonekana kufaa vinaweza kuongezwa, isipokuwa kama ni chanzo cha mapato ya Halmashauri ya Wilaya au Serikali Kuu. Kwa hali hii, hakuna nafasi zaidi kwa ajili ya ushuru kama chanzo cha mapato.2]

SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA)
(SURA YA 287)
HALMASHAURI YA KIJIJI CHA………………………………..
SHERIA NGODO
Zimetungwa chini ya kifungu cha………
SHERIA NDOGO ZA (USIMAMIZI WA MISITU) ZA HALMASHAURI YA KIJIJI CHA………., 2010

Jina na mwanzo wa kutumika

Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria Ndogo za (Usimamizi wa Misitu) za Halmashauri ya Kijiji cha............ za mwaka......... na zitaanza kutumika baada ya kuidhinishwa na Halmashauri ya Wilaya ya...................

Eneo la matumizi

Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote lililo chini ya ya mamlaka ya Halmashauri ya Kijiji cha..........
Tafsiri
Katika Sheria Ndogo hizi, isipokuwa kama itakapoelezwa vinginevyo:
“Afisa Mtendaji” maana yake ni Afisa Mtendaji wa Kijiji au afisa mwingine wa umma anayekaimu kwa niaba yake;
“Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Kijiji [kijiji] ambayo iliundwa kulingana na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Wilaya);
“Kijiji” maana yake ni Kijiji cha [kijiji].
“Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya…………pamoja na afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi;
“Msitu” maana yake ni eneo la msitu ndani ya Kijiji cha [kijiji] isipokuwa maeneo ambayo yaliyo na barabara na maeneo ya hifadhi ya maji yanayotambulika;
“Maliasili” maana yake ni mkusanyiko wa aina mbalimbali za mimea, wanyama na viumbe hai vyote, mabaki ya viumbe hai wote, udongo, maji, mawe, miamba na vitu
vyote vinavyochukuliwa kuwa muhimu kwa ajili ya ekolojia ya msitu;
“Mkazi” maana yake ni mtu yeyote ambaye ana umri usiopungua miaka 18 na ana akili timamu na mkazi wa asili wa kijiji;
Kamati ya Mazingira
(1)Halmashauri inaanzisha Kamati ya Kudumu ya Maliasili ambayo itafanya kazi kama chombo cha ushauri.
(2)Halmashauri itamteua Afisa Maliasili baada ya kupata mapendekezo kutoka kwa Kamati ya Maliasili.
(3)Afisa Maliasili atakuwa na mamlaka ya kuamua kitu gani kipandwe kwenye msitu.
(4)Mtu yeyote atakuwa na haki ya kupinga uamuzi wa Afisa Maliasili kwa maandishi ndani ya siku 30 tangu kutolewa kwa maamuzi ya Afisa Maliasili.
(5)Afisa Maliasili atabandika na kurekebisha mabango pembezoni mwa msitu yanayoonyesha:
(a) aina za miti iliyo katika eneo la msitu;
(b) ukubwa wa eneo la msitu;
(c) jina la programu ya hifadhi ya msitu;
(d) shughuli za kiuchumi ndani ya eneo la msitu.

(6)Afisa Mtendaji kwa kushirikiana na Kamati ya Maliasili na Afisa Maliasili, wataandaa programu ya hifadhi ya msitu, ambayo itaanza kufanya kazi baada ya kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji.
Programu ya hifadhi ya misitu

(1)Programu ya ulinzi wa misitu itaandaa mapema hatua za ulinzi wa pamoja zinazohitaji ushiriki wa Wakazi wote.
(2)Afisa Mtendaji atapeleka kwa maandishi ombi la utekelezaji wa hatua hizo za pamoja kwa wakazi wa Halmashauri.
(3)Programu ya ulinzi wa misitu inaweza kutamka mwisho wa uendelezaji na matumizi ya msitu au bidhaa za misitu.

Umiliki na uendelezaji
(1)Misitu itakuwa mali ya pamoja ya wanakijiji wote.
(2)Misitu haitatumiwa kwa ajili ya shughuli nyingine yoyote zaidi ya zile
zilizoainishwa chini ya Sheria Ndogo hizi au zilizoelezwa chini ya programu ya ulinzi wa misitu.
(3)Mtu yeyote au vikundi vidogo vya Wakazi watakaotumia misitu watatakiwa kulipa ada ya Tsh 10,000/- kwa mwaka fedha ambazo zitaingizwa kwenye akaunti ya Kijiji na kutumiwa kwa kufuata maamuzi yatakayotolewa na Mkutano Mkuu wa Kijiji.
(4)Vikundi au watu walioruhusiwa kufanya shughuli za kiuchumi ndani ya msitu wataorodheshwa kwenye rejesta ambayo:
(a) itakuwa chini ya usimamizi wa Afisa Mtendaji;
(b) itaonyesha shughuli zilizoruhusiwa kufanywa msituni na maeneo husika; na
(c) itaonyesha ukubwa wa shughuli katika mradi husika.

Mifugo
(1)Mifugo yoyote itakayoonekana katika eneo la msitu bila uangalizi itakamatwa na kuachiliwa baada ya mmiliki kulipa faini ya kiasi cha shillingi (500/-) kwa kila kichwa cha mfugo.
(2)Endapo mmiliki wa mifugo hiyo atakuwa hajalipa faini iliyotajwa kifungu kidogo cha (1) ndani ya siku 7 tangu kukamatwa kwa mifugo hiyo, mifugo iliyokamatwa itauzwa kwa mnada.
Fedha zitakazopatikana kutokana na mnada ukitoa faini chini ya kifungu cha (2):
(a) atapewa mmiliki wa mifugo;
(b) zitawekwa kwenye sefu ya kijiji, endapo mmiliki hatajitokeza ndani ya siku 7 baada ya mnada.

Kutembea na kukagua msitu

(1)Itakuwa ni wajibu wa Afisa Mtendaji kuhakikisha kuwa eneo la msitu ni salama na hakuna mtu anayeingia eneo hilo bila kufuata Sheria Ndogo hizi pamoja na programu ya hifadhi ya msitu.

(2)Mkurugenzi au afisa yeyote wa serikali anaweza kutembelea na kukagua msitu huo
(3)Mtu yeyote anaweza kutembelea na kukagua msitu baada ya kupata kibali kutoka kwa Afisa Mtendaji kwa lengo la kufanya utafiti, kujifunza au kueleza mbinu bora za kuendeleza na kutunza misitu au shughuli nyingine zozote zinazohusiana na misitu na maliasili nyingine yoyote.
(3)Saa za kawaida za kutembelea misitu zitakuwa kila siku kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni.

Kuripoti na Kupokea Maagizo ya Mkurugenzi
Itakuwa ni wajibu wa Afisa Maliasili kuandaa ripoti ya kila robo mwaka kuhusu utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi na kuiwasilisha kwa Mkurugenzi ndani ya siku 14.
Halmashauri ya Wilaya itakuwa na mamlaka ya kutoa maagizo kwa maafisa wanaohusika na utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi kwa ajili ya kuboresha shughuli za hifadhi ya msitu, isipokuwa kama maelekezo hayo:
(a) yanataka yafanyike marekebisho au kufuta sentensi au kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mkosaji chini ya Sheria Ndogo hizi; au
(b) yana maslahi binafsi.

Makosa
Mtu yeyote ambaye;-
(a) atakataa au kuwashaawishi wengine kukataa, kushiriki katika hatua za pamoja za hifadhi ya msitu, bila sababu ya msingi, kama ilivyoombwa kwa maandishi na Afisa Mtendaji;
(b) ataingilia au kuhujumu shughuli za hifadhi ya msitu;
(c) atakata ovyo miti, matawi au majani, kuchimba mizizi, kuchuma uyoga, kuwinda wanyama au vinginevyo kuendeleza au kutumia maliasili ya msitu kinyume na Sheria Ndogo hizi au programu ya hifadhi ya msitu;
(d) atawaacha wanyama wake kupita ndani ya msitu au kushindwa kudhibiti mifugo yake isiharibu maliasili ya msitu;
(e) atafanya sherehe, matambiko,

mikutano, mazishi, kujenga makazi au kufanya shughuli za kijamii na kiuchumi bila kuwa na kibali kwa maandishi kutoka kwa Afisa Mtendaji;
(f) atachoma majani au miti msituni, kutumia moto katika kurina asali au vinginevyo kufanya shughuli zinazoweza kusababisha msitu kuwaka moto atakuwa ametenda kosa chini ya Sheria Ndogo hizi.

Adhabu
(1)Mtu yeyote atakayepatikana na hatia chini ya kifungu cha 10:
(a) atatozwa faini isiyozidi Tsh 20,000/- iwapo ni kosa la mara ya kwanza na Tsh 50,000/- kwa makosa mengine; na
(b) atatlipa fidia kwa uharibifu uliotokana na vitendo vyake kama itakavyokadiriwa na Afisa Maliasili isipokuwa fidia hiyo haitazidi kiwango cha faini kilichoainishwa chini ya kifungu (a).

Endapo mkosaji atashindwa kulipa faini na fidia kama ilivyoelezwa chini ya kifungu kidogo cha (1), atatakiwa kufanya kazi kwenye mradi wa umma kwa muda ambao utakuwa unalingana na kiasi cha faini au fidia anachodaiwa.
(3)Halmashauri ya Kijiji inaweza kuwasamehe waliofanya makosa kwa mara ya kwanza baada ya kupata mapendekezo ya Kamati ya Maliasili.

SHERIA KUHUSU TARATIBU ZA UENDESHAJI WA VYOMBO VYA SERIKALI ZA MITAA KATIKA NGAZI ZA JAMII

TANGAZO LA SERIKALI NA. 451 LA TAREHE 25/8/95
SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA)
YA 1982

(NA. 7 YA 1982)
SHERIA NDOGO
Zimetungwa kwa Mujibu wa Kifungu cha 110
TARATIBU ZA UENDESHAJI WA SERIKALI YA KIJIJI
Jina
1.Taratibu hizi ziitwe Taratibu za Uendeshaji wa Serikali ya Kijiji za Mwaka 1995
Ufafanuzi

2. Katika taratibu hizi, maneno yafuatayo yatakuwa na maana ile iliyoonyeshwa kwa kila neno:-
“Sheria” maana yake ni Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Wilaya) ya mwaka 1982
“Waziri” maana yake ni Waziri Mwenye Dhamana ya Serikali za Mitaa
“Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ambayo Kijiji kinachohusika kimo ndani ya eneo lake;
“Kijiji” maana yake ni Kijiji kilichoandikishwa kwa Mujibu wa Sheria;
“Rejesta” maana yake ni rejesta ya Wakazi wote wa Kijiji
“Halmashauri ya Kijiji” maana yake ni Serikali ya Kijiji kilichoandikishwa.
Matumizi ya Taratibu
3.Bila kuathiri masharti ya Kanuni nyinginezo zozote zitakazowekwa kwa mujibu wa Sheria, taratibu hizi zitatumika na kila Kijiji kilichoandikishwa kwa Mujibu wa Sheria.
Rejesta ya Kijiji
4.Kila Kijiji kitaweka na kutunza rejesta ya Wakazi wa Kijiji, ambayo itaonyesha habari muhimu zinazohusu wanakijji, kama itakavyoelekezwa mara kwa mara na Waziri.

Serikali ya Kijiji
5.1:Kila Kijiji kilichandikishwa, kitatakiwa kufanya Uchaguzi wa Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji kwa kufuata Kanuni za Uchaguzi zitakazowekwa na Waziri
5.2:Halmashauri ya Kijiji ndiyo itakuwa Serikali ya Kijiji
5.3:Halmashauri ya Kijiji itakuwa na uhai wa Kisheria, na hivyo itakuwa na uwezo wa kushitaki na kushitakiwa
5.4:Afisa Mtendaji wa Kijiji atakuwa Katibu wa Halmashauri ya Kijiji na Mtendaji Mkuu wa shughuli za Kijiji

Vikao vya Serikali ya Kijiji

Kutakuwa na vikao vifuatavyo vya Serikali ya Kijiji
(i) Mkutano Mkuu wa Kijiji
(ii) Halmashauri ya Kijiji
(iii) Kamati ya Halmashauri ya Kijiji
Mkutano Mkuu wa Kijiji
7.1:Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kijiji watakuwa ni wakazi wote wa Kijiji, ambao wamefikia umri usiopungua miaka kumi na nane (18)
7.2:Mkutano Mkuu wa Kijiji utafanyika mara moja katika kila miezi mitatu lakini Mkutano wa dharura unaweza kuitishwa wakati wowote kama itaonekana inafaa
Kazi za Mkutano Mkuu wa Kijiji

8.Kazi za Mkutano Mkuu wa Kijiji zitakuwa ni hizi zifuatazo, ambazo ndizo zitakuwa agenda za kawaida za vikao vyake
8.1:Kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Kijiji, itakayotolewa na Serikali ya Kijiji
8.2:Kupokea na kujadili taarifa ya Mapato na Matumizi ya fedha za Kijiji, ya tangu Mkutano uliopita
8.3:Kupokea taarifa ya makusanyo ya fedha ya ushuru, na mapato mengineyo yanayopaswa kulipwa na kila mkazi wa Kijiji
8.4:Kupokea na kujadili mapendekezo yatakayotolewa na Serikali ya Kijiji, ya kutunga Sheria Ndogo kwa Manufaa ya Kijiji
8.5:Kupokea na kujadili, taarifa ya watu walioomba ardhi na kupewa au kunyimwa katika Kijiji. (Kutokana na 30)
Kifungu 8(5) cha Sheria Na. 5 ya 1999* sasa (toka 1.5.2001) Serikali ya Kijiji haina uwezo wa kugawa au kuwanyima watu ardhi.
Ikipokea maombi ya ardhi inapaswa kupeleka mapendekezo kwa Mkutano Mkuu wa Kijiji ambao ndio utaamua nani apewe au anyimwe
8.6:Kuzungumzia mambo mengine yanayohusu maendeleo ya Kijiji
8.7:Kupokea maagizo (Kama yapo) kutoka ngazi za juu ya Serikali na kuweka mkakati wa utekelezaji wake

Halmashauri ya Kijiji
9.1:Halmashauri ya Kijiji itakuwa na wajumbe waliotajwa katika sheria
9.2:Halmashauri ya Kijiji itafanya Mikutano yake mara moja kila mwezi, lakini mikutano ya dharura inaweza kuitishwa wakati wowote, kama itaonekana inafaa
Kazi za Halmashauri ya Kijiji

Kazi za Halmashauri ya Kijiji zitakuwa ni hizi zifuatazo:
1. Kusimamia shughuli za Ulinzi na Usalama katika Kijiji
2. Kupokea na kujadili taarifa kutoka kwenye Kamati mbalimbali za Kudumu za Serikali ya Kijiji
3. Kupokea na kujadili taarifa ya Mapato na Matumizi ya fedha Mtendaji wa Kijiji, ikiwa ni pamoja na taarifa za makusanyo ya fedha za Halmashauri ya Wilaya katika Kijiji hicho.
4. Kupokea taarifa ya mambo yaliyojadiliwa katika mikutano ya Vitongoji mbalimbali vya Kijiji hicho, kutokana na kumbukumbu za mikutano hiyo ziliowasilishwa kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji.
5. *kujadili maombi ya watu wanaoomba ardhi katika Kijiji
*kifungu 8(5) cha Sheria Na. 5 ya 1999
A village council shall not allocate land or grant a customary right of occupancy without a prior approval of the village assembly Kifungu 8(6) A village council shall:-

(a) At every ordinary meeting of the Village Assembly, report to and take account of the views of the Village Assembly on the management and administration of the Village land; and
(b) Brief the Ward Development Committee and the District Council, having jurisdiction in the area where the village is situated, on the management of the village land
6. Kuzungumzia mambo mengine yoyote ambayo ni muhimu kwa Maendeleo ya Kijiji na Wilaya kwa ujumla
7. Kupokea maagizo (kama yapo) kutoka kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata na Halmashauri ya Wilaya
Majukumu ya jumla ya Halmashauri ya Kijiji

Majukumu ya jumla ya Halmashauri ya Kijiji
(a) Kubuni na kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa madhumuni ya kuinua hali ya maisha ya Wanakijiji
(b) Kufanya jambo jingine lolote linaloweza kuleta maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii kwenye Kijiji
(c) Kutunga Sheria Ndogo ndogo kwa manufaa ya Kijiji, kwa kufuata utaratibu uliowekwa
(d) Kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa amani katika Kijiji;
(e) Kuwa Wakala wa Serikali Kuu kadri itakavyoamuliwa na Waziri
Kamati za Kudumu za Halmashauri ya Kijiji

1.Kutakuwa na Kamati za Kudumu zifuatazo za Halmashauri ya Kijiji
(a) Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango;
(b) Kamati ya Huduma za Jamii na shughuli za kujitegemea;
(c) Kamati ya Ulinzi na Usalama

2. Lakini Halmashauri ya Kijiji zinaweza kuunda kamati nyinginezo zozote kwa ajili ya kushughulikia jambo maalum
Kazi na Wajibu wa Kamati

Kamati ya fedha, Uchumi na Mipango itakuwa na wajibu kama ifuatavyo:-
(a) Kubuni miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Kijiji;
(b) Kupendekeza matumizi bora ya ardhi ya Kijiji kwa shughuli mbalimbali za Kilimo, Ufugaji, Ujenzi, Viwanja vya Michezo n.k;
(c) Kuunganisha mipango yote ambayo itatokana na Kamati nyingine Kijijini au Mipango ya Kiwilaya au Kitaifa ambayo inatekelezwa Kijijini hapo;
(d) Kutayarisha makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Miradi na shughuli zote zinazohitaji matumizi ya fedha za Kijiji;
(e) Kuweka hesabu sahihi za shughuli zote Kijijini na kuhakikisha kuwa fedha za Kijiji zinatumika kihalali na zile ambazo hazijatumika zinawekwa benki katika akaunti ya Kijiji;
(f) Kusimamia ukusanyaji wa kodi na ushuru wowote uliowekwa na Halmashauri ya Wilaya au na Serikali ya Kijiji katika eneo la Kijiji;
(g) Kutafuta njia mbalimbali za kuongeza mapato ya Kijiji kama inavyoruhusiwa na Sheria ya fedha za Serikali za Mitaa;
(h) Kuhakikisha kuwa kanuni za kilimo bora, na malengo ya kilimo, ufugaji bora au na uvuvi bora zinafuatwa na kutekelezwa yaani:-;
- Kutayarisha mashamba mapema;
- Kuchagua mbegu bora na kuweka mbolea mashambani;
- Kupanda mapema na kufuata mazingira na hali ya hewa;
- Kuhifadhi mazao ghalani;
- Kusafisha mashamba baada ya mavuno;

- Uvuvi bora unaohakikisha hifadhi ya mazalio ya Samaki na Mazingira.
(i) Kuhakikisha kila Mwanakijiji anajishughulisha na kupiga vita umaskini
2. Kamati ya Huduma za Jamii na shughuli za Kujitegemea itakuwa na kazi na wajibu ufuatao:-
(a) Kuona kuwa watoto waliofikia umri wa kwenda shule wanaandikishwa na kuhudhuria shule hadi kumaliza elimu ya msingi;
(b) Kuona kuwa watu wazima wasiojua kusoma na kuandika wanahudhuria kisomo cha Watu Wazima;
(c) Kuhamasisha ujenzi na ukarabati wa madarasa, visima, zahanati, majosho n.k na kushirikisha wataalamu mbalimbali wanaoshughulika na mambo haya;
(d) Kuhamasisha wanakijiji kuhudhuria kwenye mikutano yote ya Kijiji iliyotamkwa katika Sheria;
(e) Kusimamia utekelezaji wa masharti ya kuzuia mlipuko wa magonjwa pamoja na masharti ya kuweka mazingira ya Kijiji katika hali ya usafi;
(f) Kuweka taratibu zinazofaa za utekelezaji wa kazi za kujitegemea;
(g) Kuwahamasisha wakazi wa kijiji kuhudhuria Sherehe za Taifa, Mikutano ya hadhara inayoitwa na Serikali, Halmashauri Mbunge au Diwani
3. Kamati ya Ulinzi na Usalama
(a) Itakuwa na Wajibu wa jukumu la kuona kuwa Mafunzo ya Mgambo na Sungusungu yanaendeshwa pamoja na kuhakikisha kuwa Sungusungu na Mgambo wanaendesha shughuli za Ulinzi na Usalama katika Kijiji
(b) Kushirikiana na Kamanda wa Ulinzi na Usalama wa Wilaya katika kupeana taarifa mbalimbali za uhalifu na nyingine zenye manufaa kwa usalama wa Taifa
(c) Kuhakikisha kuwa hakuna magendo au biashara ya magendo inayofanyika katika Kijiji
4. Kamati zote za kudumu za Serikali ya Kijiji zinatakiwa kukutana kabla ya kila mkutano wa Halmashauri ya Kijiji ili kila Kamati iweze kutoa taarifa yake katika Mkutano huo wa Halmashauri ya Kijiji
Kazi za Mwenyekiti wa Kijiji
Mwenyekiti wa Kijiji atakuwa na majukumu yafuatayo:-
1. Atakuwa ndiye Mkuu wa Serikali ya Kijiji;
2. Atakuwa na wajibu wa kuitisha na kuongoza mikutano yote ya Halmashauri ya Kijiji pamoja na mikutano Mikuu ya Kijiji. Lakini endapo Mwenyekiti hayupo katika Mkutano wowote, Mkutano unaohusika unaweza kuchagua Mwenyekiti wa muda wa Mkutano huo;
3. Kwa jumla, Mwenyekiti wa Kijiji atakuwa na majukumu mengine yote kama aliyonayo Mwenyekiti wa Kitongoji katika Ngazi ya Kitongoji;
4. Atakuwa Mwakilisha wa Kijiji kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata;
5. Atawahudumia kwa usawa wanakijiji wote bila kujali tofauti za Kisiasa za Kijinsia au za Kidini;
6. Atakuwa mfano wa Uongozi bora na Utendaji bora wa kazi kwa kuwa na shughuli zake mwenyewe za kujitegemea ambazo zaweza kuigwa na Wanakijiji wenzake
Kazi za Afisa Mtendaji wa Kijiji
14.Afisa Mtendaji wa Kijiji ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya lakini anawajibika kwa Halmashauri ya Kijiji katika Utendaji wake
1. Mjukumu ya Afisa Mtendaji wa Kijiji yatakuwa ni haya yafuatayo:-
(a) Atakuwa ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli zote za Kijiji;
(b) Atakuwa mwandishi na Mtunzaji wa kumbukumbu zote za Vikao vya Kijiji pamoja na rejesta ya Kijiji na nyaraka nyingine muhimu za Kijiji;
(c) Atakuwa kiongozi wa Watendaji wengine wote waliopo Kijijini;
(d) Atakuwa mshauri Mkuu katika kubuni na kutekelza miradi ya Maendeleo Kijijini; na Msimamizi Mkuu wa utekelezaji wa Miradi iliyokubaliwa na Serikali ya Kijiji pamoja na miradi mingine yote ya Serikali inayotekelezwa katika eneo la Kijiji chake;
(e) Atakuwa kiungo muhimu kati ya Serikalid ya Kijiji na Kamati ya Maendeleo ya Wadi (WDC). Halmashauri ya Wilaya na pia atakuwa Kioungo muhimu baina ya Serikali ya Kijiji na Wenyeviti wa Vitongoji wa Kijiji hicho;
(f) Atatakiwa kuwa mfano wa Kiongozi bora Kijijini kwa kujiheshimu na kufanya kazi kwa bidii
Mapato ya Kijiji
16.Mapato ya Halmashauri ya Kijiji yatatokana na maeneo yote yaliyoruhusiwa kwa mujibu wa Ibara ya 9 ya Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Na. 9 ya 1982.
2. Mapato mengine yaweza kutokana na shughuli mbalimbali zitakazofanywa na Kijiji chenyewe;
3. Halmashauri ya Kijiji itakuwa wakala pekee wa kukusanya mapato ya Halmashauri ya Wilaya na itapewa ada ya Uwakala isiyopungua kiasi cha asilimia kumi na saba ya mapato yote yatakayokusanywa na Kijiji hicho, au zaidi kama itakavyoamuliwa na Halmashauri;
4. Halmashauri ya Kijiji paia inaweza ikawa wakala wa Serikali Kuu katika kukusanya mapato yake na italipwa ada ya Uwakala itakavyoamuliwa na Wizara ya Fedha kwa makubaliano na Waziri
Utaratibu wa Kutunga Sheria Ndogo

17.Halmashauri ya Kijiji ina uwezo wa kisheria wa kutunga Sheria Ndogo kwa madhumuni ya kuhimiza utekelezaji wa kazi na majukumu yake
2. Utaratibu wa kutunga Sheria Ndogo za Halmashauri ya Kijiji ni kama ifuatavyo:
(a) Halmashauri ya Kijiji itapendekeza aina ya Sheria Ndogo inayotakiwa kutungwa. Kwa mfano kwa ajili ya kuzuia uchaomaji moto

hovyo, Hifadhi ya Mazingira, kuhimiza Elimu ya Msingi, kuzuia ukataji Miti n.k
(b) Mapendekezo ya sheria hiyo ndogo yatawasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Kijiji ili kupata mawazo na maoni ya Wanakijiji wote;
(c) Halmashauri ya Wilaya ikiridhika na mapendekezo ya Sheria Ndogo ya Halmashauri ya Kijiji itaidhinisha Sheria hiyo ndogo na baada ya hapo itakuwa tayari kutumika;
(d) Mfumo wa Sheria Ndogo ya Kijiji utakuwa kama inavyoonyeshwa katika mfano ulioonyeshwa kwenye Jedwali la Taratibu hizi.
Kufuta Taratibu za Uendeshaji wa Serikali ya Kijiji za Mwaka 1975 G.N 1975 No. 161
18.Taratibu hizi zinachukua nafasi ya Taratibu za Uendeshaji wa Serikali ya Kijiji za mwaka 1975 ambazo sasa zimefutwa

TANGAZO LA SERIKALI NA. 451 LA TAREHE 25/8/95
SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA)
YA 1982
(NA. 7 YA 1982)
SHERIA NDOGO
Zimetungwa chini ya Kifungu cha 163
SHERIA NDOGO (……………………………………) ZA HALMASHAURI YA KIJIJI CHA ……………………………………………………….200…………………….
1. Sheria Ndogo hizi zitaitwa Sheria Ndogo (…………………….) za Halmashauri ya Kijiji…………………….. za 200 ………………
2. Sheria hizi Ndogo zitaanza kutumika kuanzia tarehe zitakapoidhinishwa na Halmashauri ya Wilaya ya …………………………………….
3. Sheria hizi ndogo zitatumika katika eneo la Kijiji cha…………………………..
4. Madhumuni ya Sheria hii ndogo yatakuwa:-
(a)………………………………………………………………………………..
(b) ………………………………………………………………………………...
5. Masharti yafuatayo yatahusu Sheria hii ndogo:-
(a) …………………………………………………………………………………
(b) …………………………………………………………………………………
(c) …………………………………………………………………………………..
6. Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na Sheria hii ndogo atakuwa anatenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini ya Sh………………………………. Au kifungu cha miezi…………………….. Jela au adhabu zote mbili, faini na kifungo.
38
Muhuri rasmi wa Halmashauri ya Kijiji cha …………………ulipigwa kwenye Hati ya Sheria hizi ndogo kufuatana na azimio la Halmashauri lililopitishwa kwenye Mkutano uliofanyika…………………… tarehe………………………19…………….. muhuri wa Halmashauri uliowekwa mbele ya:-
……………………………………..
………………………………………
Tarehe na Muhuri rasmi wa Afisa Mtendaji wa Kijiji
Halmashauri ya Kijiji
ZIMEIDHINISHWA
………………………………………….
Mwenyekiti wa Halmashauri
……………………………………… Mkurugenzi wa Halmashauri
……………………………………..
Tarehe ya Muhuri rasmi wa
Halmashauri ya Wilaya
NAKUBALI
Cleopa David Msuya
Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais
Dodoma
10 Julai, 1995