KITUO CHA MABASI CHA BOMANG'OMBE CHAANZA KUWEKWA LAMI

Posted by MK On 11:09 No comments




Na Richard Mwangulube,Hai

Kituo kikuu cha mabasi cha wilaya ya Hai kilichopo katika mji wa Bomang'ombe kimefungwa kwa muda  ili kupisha matengenezo makubwa ya kuweka lami.

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga amewaeleza waandishi wa habari kwamba matengenezo hayo yanatokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010.

Ameeleza kuwa matengenezo hayo ya kipande cha urefu wa kilometa 0.85 utachukuwa siku 45 kwa gharama ya shilingi milioni 90.

Amefafanua kwamba matengenezo hayo yataunganisha barabara inayoingia kituoni hapo na ile ya Moshi hadi Arusha pamoja na kukiwekea lami.

Makunga ameeleza kuwa wakati kituo hicho kikiwa kimefungwa,hivi sasa kinatumika kituo cha muda katika eneo la Double road

Ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha wa 2012/2013,Halmashauri ya wilaya ya Hai ilitengewa na serikali jumla ya shilingi 460,810,000.

Wilaya ya Hai ina barabara zenye urefu wa kilometa 466.2 ambapo kati ya hizo,kilomeya 32 ni barabara kuu,kilometa 42 ni za mkoa,kilometa 175.93 ni za wilaya na kilometa 150.27 ni za vijiji na barabara za Hai ni kilometa 66.

Amesema kuwa barabara zinazopitika nyakati zote ni kilometa 235.53 ambazo ni sawa na asilimia 50.82

0 comments:

Post a Comment