MVUA YENYE UPEPO MKALI YALETA MAAFA WILAYANI HAI

Posted by MK On 00:52 No comments

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akimkabidhi misaada ya waathirika diwani wa kata ya Machame kusini ,Nasibu Mndeme(Kushoto)
Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akiwakabidhi  misaada ya chakula  madiwani wa kata ya Machame Weruweru, Mandrai na diwani wa kata ya Machame kusini Nassibu Mndeme
Diwani wa kata ya Machame Weruweru ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai akipokea msaada wa chakula kutoka kwa mkuu wa wilaya ya hai,Novatus Makunga
Moja kati ya nyumba ambayo ilidondoshwa kabisa katika kijiji cha Kwatito
Mo
Moja kati ya nyumba zilizoathiriwa na Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali katika kijiji cha Kwatito
Moja kati ya nyumba zilizoathiriwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali katika kijiji cha Kwatito
Vijana wkijitolea kusaidia kurejesha paa la moja ya nyumba katika kijiji cha Shirimgungani




Na Richard Mwangulube,Bomang'ombe


Nyumba zaidi ya arobaini zimeezuliwa mapaa na ekari zaidi ya mia tatu ya mashamba ya mahindi na migomba zimeharibiwa vibaya wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kutokana na mvua kubwa iliyoandamana na upepo iliyopiga mwishoni mwa wiki.


Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga alitembelea kaya zilizoathirika na maafa hayo Ijumaa iliyopita ambapo waandishi wa habari walishuhudia baadhi ya wamiliki wa nyumba hizo wakiwa katika jitihada za kurejesha mabati yaliyoezuliwa.


Mbali na nyumba,mvua hiyo pia imezoa daraja dogo linalounganisha eneo la mji wa Bomang’ombe ambao ndiyo makao makuu ya wilaya ya Hai na vijiji vya Rundugai na Chemka


Vijiji vilivoathirika na maafa hayo ni pamoja na Kwatito na Shirimgungani vilivyoko katika kata ya Machame Weruweru pamoja na Kijiji cha Mijongweni kilichopo katika kata ya Machame kusini.


Diwani wa kata ya Machame kusini Nasibu Mdeme ameeleza kuwa katika kata yake jumla ya nyumba 23 zimeathirika na maafa hayo pamoja mashamba ya mahndi ekari 255 na ekari nyingine 170 za migomba.


Alisema kuwa mvua hiyo iliyoandamana na upepo mbali ya kuezua mapaa ya nyumba lakini pia iliweza kung’oa idadi kubwa ya miti katika eneo hilo.


Waandishi wa habari walishuhudia nyumba nne zilizojengwa kwa udongo zikiwa zimeanguka kabisa katika kijiji cha Kwatito na nyingine moja katika kijiji cha Shirimgungani wakati katika kijiji cha Mijonweni athari kubwa zaidi imeonekana katika mashamba.


Kwa upande wake,mkuu wa wiaya ya Hai alitoa wito kwa wasamaria wema kutoa misaada ya hali na mali kwa kaya zilizoathirika katika maafa hayo ili kuziwezesha kurudi katika maisha ya kawaida.


Ameziomba taasisi na watu binafsi kuzisaida kwa misaada ya hali na mali kaya hizo kwa mahitaji mbalimbali yakiemo ya chakula pamoja na vifaa va ujenzi kama mabati,saruji,mbao,misumali na nondo.


Makunga amesema kuwa katika hatua ya haraka serikali imetoa chakula ambacho ni pamoja na  unga kilo mia mbili na maharage kilo mia pamoja na mafuta ya kupikia kwa ajili ya kaya ambazo zimeonekana hazina uwezo kabisa.


Ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha wananchi kutopuuzia kampeni ya upandaji wa miti baada ya kubainika kwamba katika sehemu kubwa ya maeneo ambayo nyumba zimeezuliwa mabaa hazikuwa na miti kabisa.

0 comments:

Post a Comment