UJENZI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI UNAENDELEA KWA KASI WILAYANI HAI

Posted by Arusha by day and by night On 06:29 No comments

Mkuu wa wilaya ya Hai akikagua ujenzi wa maabara ya masomo ya sayansi katika shule ya Sekondari ya Lyasikika

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akikagua ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari ya Maili sita

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akipata maelezo ya umaliziaji wa maabara ya masomo ya sayansi

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akiangalia ubora wa moja ya beseni katika maabara ya masomo ya sayansi

Moja kati ya majengo ya maabara za sayansi katika wilaya ya Hai


Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga katika moja ya vyumba vya maabara vinavyoendelea kujengwa wilayani mwake


TEMBO WANAOBEBA BINADAMU SASA WAHAMISHIWA HIFADHI YA TAIFA YA ARUSHA

Posted by Arusha by day and by night On 05:23 No comments

Wananchi wakimshangaa mmoja kati ya Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha waliohamishwa kutoka Ndarakwai
Mmoja kati ya waangalizi wa Tembo waliotoka Ndarakwai
Mwangalizi wa Tembo akimzuia mmoja ya Tembo hao kwa kutumia mgongo
Mlezi wa Tembo katika Ndarakwai akiwa na Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha
Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ni miongoni mwa waliowashuhudia Tembo hao mara tu baada ya kuwasili Arusha National Park
Picha inayoonyesha Tembo hao kabla ya kuondoshwa Ndarakwai na kupelekwa Arusha National Park
Moja kati ya vyumba vya Ndarakwai kabla ya kuchomwa moto



Na Richard Mwangulube,Arusha

Tembo wawili ambao wamekuwa kivutio kikubwa kwa wageni hususani watalii kwa kuruhusu kuguswa na kupiga picha na hata kubeba binadamu katika kambi ya kitalii ya Ndarakwai iliyopo wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro wamehamishiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha Moshi. 

Kuhamishwa kwa tembo hao kulikofanyika jumamosi iliyopita Novemba 15,2014 kumetokana na kitendo cha wafugaji wa Kabila la Wamasai kuteketeza kwa moto kambi hiyo ya kifahari ya watalii ya Ndarakwai siku hiyo jioni.

Katika tukio hilo vibanda 16 vyenye hadhi sawa na vyumba vya hoteli ya nyota nne viliteketezwa kwa moto huo.

Hata hivyo wataalamu wa wanyamapori katika hifadhi ya ya Taifa ya Arusha wameeleza kuwa tembo hao watahitaji matunzo maalumu kwa kipindi kabla hawajaweza kuishi peke yao kwa kuwa walishazoea maisha ya kutunza katika eneo la Ndarakwai.

Wameeleza katika matunzo hao itawabidi waendelee kuishi na timu iliyokuwa inawatunza kwa zaidi ya miaka kumi na tano akiwemo kijana mmoja wa Kitanzania.

"Sisi tunasubiri maelekezo kutoka ngazi ya juu ya wizara ya maliasili na utalii kwa hatua inayofuata kama ni kurejeshwa Ndarakwai ama kuhifadhiwa hapa Arusha National Park,"alisema mmoja ya wafanyakazi wa hifadhi hiyo.

Vurugu katika kambi ya Ndarakwai zilizodhibitiwa na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), waliolazimika kutumia mabomu ya machozi  zilianza juzi mchana na hadi kufikia saa 12:00 jioni mali za bilioni ya shilingi zilikuwa zimeteketezwa kwa moto. 

Kambi hiyo yenye shamba la watalii lenye ukubwa wa hekari 11,000 likiwa na wanyama wote isipokuwa simba na faru, linamilikiwa na raia wa Uingereza, Peter Jones ambapo hapo awali eneo hilo lilikuwa shamba linalomilikiwa na kampuni ya Bia nchini kwa ajili ya kuzalishia kimea cha bia.

 Kabla ya kuanza kwa uvamizi huo, watalii waliokuwapo katika kambi hiyo waliondolewa na kuhamishiwa kambi jirani ya Olpoponyi huku wafanyakazi nao wakiondolewa. 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, alitembelea eneo hilo siku hiloyofata na kuagiza waarifu wa tukio hilo wasakwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria

Katika vurugu hizo, vyumba 17 vyenye hadhi yoyote ya hoteli ya nyota nne, nyumba ya mapokezi, duka na nyumba za kulala wafanyakazi ziliteketezwa katika uvamizi huo. 

Mpaka wa wilaya mbili za Longido na Siha upo mwisho wa shamba hilo ambalo mazingira yake yametunzwa vizuri na hivyo kuwavutia wafugaji hao kutaka kuingiza mifugo yao. 

Jones, aaliwaeleza waandishi wa habari kwamba polisi walikwenda kuondoa mifugo iliyokuwa imeingizwa katika shamba lao na ndipo wafugaji waliposhikwa na hasira. “Sio hapa kwetu tu, lakini mifugo imekuwa ikiingizwa katika mashamba mengi hapa West Kilimanjaro.Polisi walikuwa hapa tangu mwanzo wa vurugu hizi,” alisema Jones. 

Meneja wa kambi hiyo, Ifigenia Irafay  alisema tatizo hilo sio la mwekezaji na wafugaji hao bali ni eneo la malisho ya mifugo ya wafugaji na kwamba kwa muda mrefu wamekuwa na mahusiano mazuri na wafugaji.

 “Tutatoa taarifa baadae kwa sasa hivi tunahangaika kuwasafirisha wageni wetu ambao tuwahamishie kambi ya jirani na pia kusafirisha wafanyakazi maana itabidi eneo hili tulifunge kwa muda,”alisema. Dalili za uvunjifu wa amani zilianza kujitokeza wiki tatu zilizopita ambapo kundi la wafugaji liliwashambulia maofisa wa ardhi waliokwenda kuweka mawe ya mpaka eneo hilo.

Tayari watuhumiwa kumi na saba wa tukio hilo wameshafikishwa katika mahakama ya wilaya ya Hai na kusomewa mashtaka ya kuharibu mali za thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 17 chini ya hakimu mkazi Dennis Mpelembwa na kesi yao itatajwa tena Desemba 7 mwaka huu.