MKAKATI WA MWANZA KUKOMESHA MIGOGORO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA NCHINI

Posted by Arusha by day and by night On 07:42 No comments














MAAZIMIO YA MKUTANO WA WADAU WA SEKTA YA MIFUGO ULIOFANYIKA TAREHE 5 – 7 SEPTEMBA 2014:- MALAIKA BEACH RESORT - MWANZA.
MADA
HOJA
AZIMIO
MUDA WA UTEKELEZAJI
MHUSIKA

Kutenga, kupima na kumilikisha maeneo na hifadhi mazingira
Kubainisha na kutenga maeneo yanayofaa kwa ufugaji na uwezo wa malisho kulingana na mifugo na kumilikisha maeneo hayo kwa wafugaji kwa kufuata modeli ya Handeni na Bagamoyo kwa kuanza na maeneo pembezoni mwa mapori ya hifadhi.

Wizara ya Ardhi (NLUPC), OWM TAMISEMI (MSM), Wizara ya  Mifugo na Sekta Binafsi


Serikali iimarishe na kusimamia matumizi ya njia za mifugo

OWM TAMISEMI (MSM), Wizara ya Mifugo


Kujenga uelewa wa kutosha kwa wafugaji juu ya teknolojia sahihi za kuwezesha wafugaji kuzalisha malisho na hifadhi yake kwa matumizi ya baadaye.

 OWM -TAMISEMI (MSM), Wizara ya  Mifugo na Sekta Binafsi


Kuweka miundo mbinu muhimu ya mifugo katika maeneo ya wafugaji na kufanya sensa ya mifugo kitaifa, pamoja na kufanya usajili ili kutambua mahitaji yao hasa utoaji huduma, kuzuia wizi, kutoa elimu na kutafuta masoko.

 OWM TAMISEMI (MSM), Wizara ya  Mifugo na Sekta Binafsi


Kuimarisha mabaraza ya ardhi ya Kata na Vijiji, ili kujenga uwezo wa utatuzi wa migogoro karibu zaidi na wafugaji.

OWM TAMISEMI (MSM)


Kuunda timu ya wataalam wa wizara za mifugo, kilimo, maliasili, maji, ardhi, TAMISEMI na mazingira ili kufanya tathmini yenye mgawanyo sawia wa matumizi ya ardhi nchini, ikiwa ni pamoja na kushauri kurejesha ardhi iliyohodhiwa na wawekezaji na kuachwa bila kuendelezwa kwa muda mrefu ili kuwamilikisha wafugaji na wakulima.

Wizara za Kisekta (LSLM)

Kuongeza tija na mchango wa sekta ya mifugo katika pato la Taifa
Kuelimisha wafugaji kupitia chama cha wafugaji Tanzania juu ya ufugaji wenye tija na kueneza teknolojia ya uhimilishaji, unenepeshaji mifugo na uboreshaji malisho.

OWM TAMISEMI (MSM), Vyama vya wafugaji na wazalishaji Wizara ya  Mifugo na Sekta Binafsi


Kuanzisha na kuimarisha viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya mifugo.

Wizara ya Viwanda na Biashara, TIC, Sekta Binafsi


Kuandaa “Livestock Lab” ili kuchambua kwa kina changamoto za mifugo na ufugaji, kutafuta majawabu na kuainisha vipaumbele vya utekelezaji.

Wizara ya Ardhi (NLUPC), OWM Wizara ya  Mifugo


Kuendelea kutekeleza mpango wa maendeleo wa Sekta ya Mifugo ambao utazingatia vipaumbele vyote muhimu na aina zote za mifugo na mazao yake.

Wizara ya  Mifugo


Tasnia za mazao ya mifugo ziandae mpango mkuu (Master plan) unaoonesha kanda za vipaumbele vyake na aina ya ufugaji.

Wizara ya  Mifugo


Kufufua na kuimarisha Folk Development Centers (FDCs) ili zitumike kufundisha wafugaji juu ya ufugaji na mnyororo wa thamani ya mifugo

Wizara ya Mifugo, Wizara ya Maendeleo ya Jamii JInsia na Watoto


Kuendelea kutenga  maeneo huru “Disease Free Zone” katika mipaka ya nchi ili kuzuia kuenea kwa magonjwa kutoka nchi jirani.

Wizara ya  Mifugo, OWM- TAMISEMI


Serikali kupitia TVLA iimarishe usimamizi na udhibiti wa ubora wa pembejeo za mifugo zinazotengenezwa na zinazoingizwa nchini kutoka nje.

Wizara ya  Mifugo


Mamlaka ya serikali za mitaa zitekeleze agizo la kutenga asilimia 15% ya mapato yatokanayo na mifugo na mazao yake kwa ajili ya kuendeleza sekta ya mifugo

OWM – TAMISEMI (MSM)


Kuongeza idadi ya wataalamu wa ugani wa mifugo ili kuondoa pengo la upungufu lililopo kwa kuruhusu wahitimu wote wa mifugo kuajiriwa moja kwa moja na serikali. 

Wizara ya  Mifugo, Ofisi ya Rais -Menejimemnt ya Utumishi wa Umma, OWM TAMISEMI


Kuweka mkakati wa kuhakikisha kuwa matokeo ya tafiti yanawafikia wadau haraka ili kuongeza tija katika uzalishaji kwa kuimarisha uhusiano wa kiutendaji (linkage) kati ya mgani, mfugaji na mtafiti.

Wizara ya  Mifugo, OWM - TAMISEMI

Upatikanaji wa masoko ya mifugo na bidhaa zake
Kuhamasisha uundwaji wa mitandao na ushirika wa wazalishaji wa mazao ya mifugo.

Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Wizara ya  Mifugo, Vyama vya Wafugaji


Kutoa elimu ya uzalishaji kibiashara wa mifugo na mazao yake kuhusu kuongeza ubora na uwingi ili kukidhi soko la nje.

Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya  Mifugo


Kujenga na kuimarisha minada ikiwemo mizani na kuboresha taratibu za uendeshaji wa minada/masoko ya mifugo ya ndani na mipakani ili kuwezesha wafugaji kunufaika na soko zuri la mifugo na mazao ya mifugo.

Wizara ya  Mifugo, OWM - TAMISEMI

Kuimarisha na kuboresha biashara ya mazao ya mifugo
Kujenga machinjio za kisasa na kuboresha zilizopo ili kupata nyama bora kwa walaji wa ndani na nje.

Wizara ya  Mifugo, OWM – TAMISEMI, Sekta Binafsi


Kuboresha, kuimarisha na kusimamia miundombinu ya ukusanyaji, usambazaji na usindikaji maziwa na nyama.

Wizara ya  Mifugo, OWM – TAMISEMI, Sekta Binafsi


Mpango wa unywaji maziwa shuleni utekelezwe nchi nzima ili kuongeza soko la ndani na kuongeza afya na ufaulu.

Wizara ya  Mifugo, OWM – TAMISEMI, Sekta Binafsi


Kusimamia kikamilifu Sheria ya Biashara ya ngozi namba 18 ya mwaka 2008,na sheria ya magonjwa ya mifugo ili kupata ngozi yenye thamani kubwa.

Wizara ya  Mifugo, OWM – TAMISEMI


Serikali kuridhia uundwaji wa chombo kitakachosimamia biashara ya ngozi ili kuwezesha ngozi nyingi kuuzwa kwenye viwanda vya kuchakata vya ndani ya nchi.

Wizara ya  Mifugo,


Uandaliwe Mkakati wa kuongeza thamani ya zao la ngozi (value addition) ili kuvifanya viwanda visindike ngozi hadi hatua ya mwisho.

Wizara ya Viwanda na Biashara


Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa, Wilaya na vijiji za pembezoni, TRA, POLISI na Vyombo vya Usalama (Mwanza, Kagera, Mara, Simiyu, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Kigoma na Manyara) zidhibiti utoroshwaji wa ngozi ghafi kwenda nje ya nchi.

KUU – Mikoa na Wilaya


Serikali itazame jinsi ya kurekebisha bei ya ngozi kwa soko la ndani ya nchi ikilinganishwa na bei itolewayo na nchi jirani



Upatikanaji wa mitaji na Mikopo kwa wadau wa sekta ya mifugo
Kuanzisha na kuimarisha vyama vya wafugaji vya ushirika wa akiba na mikopo

WKCU


Kurasimishashughuli za uzalishaji, biashara na raslimali za mifugo na mazao yake, ili taasisi za fedha kuweza kukopesha kwa urahisi

Wizara ya Mifugo, Viwanda na Biashara


Serikali iandae na kutekeleza mkakati wa kuwainua wazawa walio na nia ya kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya sekta ya mifugo kwa kuwawekea dhamana kwenye vyombo vya fedha hatimaye kuwa na Benki ya wafugaji.

Wizara ya Mifugo, Viwanda na Biashara, Taasisi za Fedha
wafugaji

Uwekezaji na vivutio vya uwekezaji katika sekta ya mifugo
Serikali isimamie kodi zilizopo kwa mazao yote ya mifugo yanayoagizwa kutoka nje ili kulinda soko la ndani la mazao hayo.

Wizara ya Viwanda na Biashara, Fedha

Uboreshaji wa mfumo wa ufugaji asili
Kuandaa sera ya ufugaji wa asili itakayolenga mabadiliko ya hatua kwa hatua kuboresha ufugaji wa asili kuwa wa kibiashara na kuzingatia uwezo wa nyanda za malisho uliopo.

Wizara ya Mifugo,


Kuboresha mfumo wa usambazaji taarifa kwa wafugaji zikiwemo taarifa za masoko na magonjwa kwa kuimarisha mfumo wa Livestock Marketing Information System (LMIS) uliopo.

Wizara ya Mifugo,


Kuwa na wiki ya wafugaji kila mwaka (Lini na nani atagharamia)


NB: maazimio yote haya yawekwe katika Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Mifugo uliopo na Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano ili kuepuka utegemezi wa wafadhili kutoka nje na kuuacha mpango huo kuwa katika makabrasha tu.
·         Serikali idhamini ufugaji wa samaki
·         Kuwe na Sheria za Haki ya Malisho kwa Mifugo
·         Katiba ijayo itambue Haki za wafugaji na Wakulima

HITIMISHO LA MH. WAZIRI WA MIFUGO
*      Ipo Sheria ya Malisho na vyakula vya mifugo na Sheria ya Haki za wanyama zenye ufafanuzi wa kina kuhusu haki ya malisho na haki za wanyama.

0 comments:

Post a Comment