BONANZA LA PASAKA LA KITAMBI NOMA LILIVYOFANA JIJINI ARUSHA

Posted by Arusha by day and by night On 07:20 No comments

Wachezaji w timu ya Benson kampani  wakivuta kamba
Mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga akiwa anasalimiana na wachezaji wa timu   Mango Garden ya jijini Dar es salaam wakati walivyokuja kushiriki bonanza la kitambi noma lililofanyika katika kiwanja cha kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid ya jijini Arusha
 Kulikuwepo pia na mashindano ya kukimbia na magunia  ambapo katika mashindano haya mchezaji kutoka timu ya Mango Garden alishinda

Timu ya mavetenari ya Kitambi noma imefanikiwa kuwa mabingwa wa jumla wa bonanza la pasaka lililofanyika Jumapili iliyopita April 20,2014 katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Kaluta Abeid.
Timu ya Mango Garden ya Kinondoni ilifanikiwa kushika nafasi ya pili katika tamasha hilo la kusherehekea sikukuu ya pasaka kwa michezo mbalimbali .

Bonanza hilo lililoandaliwa na Klabu ya Kitambi noma yenye maskani yake jijini Arusha na kufadhiliwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Bonanza hilo liliwakusanya mamia ya wapenda michezo na kushudia michezo mbalimbali ikiwemo ya kukimbiza kuku,kukimbia na magunia,soka,Kunywa bia,kuvuta kamba na burudani ya muziki kwa siku nzima ya pasaka.

Akifungua bonanza hilo,Mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga aliwataka washiriki wa bonanza hilo kufahamu kuwa michezo ni afya na burudani na hivyo mashabiki wanatarajia kuona burudani kutoka kwa wachezaji na siyo kuonyeshana ubabe na umwamba uwanjani.
Kadhalika alisema kuwa amefarijika kuwaona baadhi ya wachezaji waliokuwa katika ligi za juu za soka nchini wakirukia katika soka la veterani akiwemo mlinda mlango aliyedakia Yanga ya Dar-es-Salaam Aldinad Hashimu pamoja na kwamba  kwa sasa vitambi vimewanyemelea hivyo michezo ni fursa nzuri ya kuvipunguza.

Makunga akawaka washiriki na watanzania kushiriki katika michezo baada ya shughuli zao katika suala zima la kujenga Afya zao na kuleta burudani hakika taswira hiyo itajenga taifa la watu wenye Afya na kuondoa magonjwa balimbali yanayoinyemelea jamii yetu.

Timu zilizoshiriki katika bonanza hilo ni pamoja na Arusha Coaches,kampuni ya Benson, Mango Garden ambao walikuwa wageni waalikwa kutoka jijini Dar es salaam na wenyeji Timu ya Kitambi Noma  zote za jijini Arusha ambapo katika soka timu zote zilicheza kwa mzunguko na kujikusanyia pointi na bingwa kupatikana.

Katika mechi ya kwanza kati ya Arusha coaches walifungwa bao moja bila majibu na timu ya mango garden ikifuatiwa na mechi ya wenyeji kitambi noma na timu ya bensons na kujikuta benson wakipigiliwa kwa bao mbili bila majibu mechi iliyofuata ni kati ya timu ya makocha wa mkoa wa Arusha na Benson mchezo ulioisha kwa Arusha Coaches kuwapigilia bila huruma benson kwa bao 3 bila majibu.
Kwenye mchezo wa kuvuta kamba timu ya kitambi noma iliibuka mshindi katika fainali yake na timu ya benson huku benson na kitambi noma wakiibuka washindi kwa kugawana kuku moja moja katika mashindano ya kukimbiza kuku huku bonanza hilo likifana na kuwapa burudani murua wakazi wa jiji hili na viunga wake.

0 comments:

Post a Comment