Na Richard
Mwangulube,Bomang’ombe
Wakazi wa kata 8 na
vijiji 21 wilawayani Hai mkoani Kilimanjaro walio kumbwa na maafa
ya kuezuliwa mapaa ya nyumba zao kutokana na upepo mkali ulio ulioambatana
na mvua wameshauriwa kujenga nyumba
imara ambazo zitaweza kuhimiri hali kama hiyo endapo itajitokeza
tena.
Rai
hiyo imetolewa katika vijiji vya Kwatito,Mijongweni na Ngosero vilivyopo
wilayani Hai mkoani Kilimanjaro na mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga
wakati wa kukabidhi msaada wa mabati yenye thamani ya shilingi milioni 5.2.
Msaada
umetolewa na Kampuni ya Megatrade Investment Limited ya Arusha baada ya
kuguswa na maafa hayo,ambapo Makunga amesema , kutokana na maafa ya namna hiyo
kujirudia kila mwaka ni vyema sasa wakazi wa vijiji hivyo wakajenga nyumba
imara kwa kutumia matofali ya kuchoma.
Ameeleza
kuwa eneo la vijiji hivyo vina udongo mzuri unaofaa kwa matofali ya kuchoma na
kwamba sasa wakati umefika wa viongozi kuanza kampeni ya kuhamasisha wananchi
kuyatumia matofali hayo kwa ujenzi.
Amesishukuru
kampuni hiyo kwa kukubali kutoa msaada kwa waathirika hao ambao wengi wao
itawachukuwa muda mrefu kurejesha nyumba zao na kurudi kwenye makazi yao
kutokana na hivi sasa kujihifadhi kwa majirani.
Makunga
ameeleza kuwa serikali imeshatoa msaada wa chakula tani 45.7 ambapo kila mtu
aliyeathirika na maafa hayo amepatiwa kilo 35 ambaz zitamtosheleza kwa kipindi
cha miezi mitatu.
Amesema
kuwa awali walitoa kilo ishirini wa unga wa sembe na kilo tano za Maharage kwa
kila kaya kutokana na msaada kutoka kampuni ya Bonite Bottles ya Moshi,kiwanda
cha unga cha Monaban cha Arusha na makampuni ya mahoteli ya Serena.
Kwa
upande wake meneja masoko wa Kampuni ya Megatrade,Gudlack Kway amesema
wameguswa na maafa hayo na kwa kuwa kampuni yao hufanya kazi Zaidi katika
jamii ndio maana wameamua kutoa msaada wa mabati hayo ambayo yatawasaidia
waathiriwa katika ujenzi wanaotarajia kuuanza muda si mrefu.
Mwishoni
mwa mwezi Februari wilaya ya Hai kwa nyakati tofautitofauti ilikumbwa
na upepo mkali ulio ambatana na mvua kubwa iliyo sababisha maafa
katika vijiji 25 ikiwemo kuezuliwa kwa mapaa ya nyumba,kubomoka kwa kuta za
nyumba kuharibika kwa mazao shambani na kifo cha mtu 1 katika kijiji cha
Kwatito
0 comments:
Post a Comment